Yaliyojiri katika Mkutano wa CHADEMA - Iringa

Yaliyojiri katika Mkutano wa CHADEMA - Iringa

Mkuu maana yangu ni kwamba kama kua mtu ambaye ana ushahidi wa hivyo vipusa vinavyo mhusisha kigogo wa CCM , viwekwe hadharani.
Unadhirifu hata ukifanywa na nduguyo unakera na ni kosa.
Tatizo lililopo wengi wanalitumia hilo " tatizo la vipusa" kipropaganda na hakuna ushahidi wake.
Lakini wa China pia hautoshi mkuu?? au Lumumba iliridhia kauli ya "kampuni ni yangu lakini ndovu si wangu"??
 
Wanajua hali ikichafuka wataiba simu za watu ila kwa kuwa Mungu wetu wa Mbinguni ni mkubwa unakuta wanaoenda kwenye hiyo mikutano wote ni vibaka.
 
Wanajua hali ikichafuka wataiba simu za watu ila kwa kuwa Mungu wetu wa Mbinguni ni mkubwa unakuta wanaoenda kwenye hiyo mikutano wote ni vibaka.

usilitaje bure jina la Mungu,kisa unalipwa elfu saba!!
 
Wakuu.

Mtakumbuka kuwa leo wabunge wa Chadema walio fukuzwa kiuonevu bungeni wanafanya mkutano jimbo la Iringa mjini ili kushtaki kwa umma uonevu walio fanyiwa.

Hapa ni yanayojiri mkutanoni.

• Diwani wa Iringa mjini, Nyalusi, wananchi wa Iringa wana imani na viongozi wa CHADEMA, kuliko walioko madarakani. Kapanda Sugu

• Sugu: Tutaendelea kukomaa. Kiti kinamfukuza Lissu kwa kufanya kazi yake, wakati Serukamba mbunge wa FT, akiachwa! Tusi kubwa, hakuna mbunge katika jumuiya ya madola amewahi kutukana tusi baya kama hilo, limevunja rekodi Jumuiya ya Madola

• Sugu: Kauli ya WASSIRA, Kibanda ni nani? Ubinadamu na utu kwao ni cheo!

• Kiwia: Matusi kwa Wtz ni kufanywa maskini katika nchi tajiri, akina mama kwenda na nyembe na kila k2 kujifungua, kuzungumzia madawati miaka 50 ya uhuru wakati Kenya wanazungumzia kompyuta kwa kila mtoto.

• Kiwia: Ukiona mahali kuna amani ya kweli inayotokana na haki pamoja na demokrasia, ujue kuna watu wachache wamejitoa, ikibidi kwa jasho na tone la damu! Bunge sasa limegeuzwa kuwa rubber stamp ya masuala ya CCM!

• Mnyika anasema fedha za DECI zirudishwe. Wabunge wanazuiwa kujadili suala la Deci eti liko mahakamani, mbona Magufuli aliamua kuongelea suala la samaki wake kwani aliwagawa hao samaki wakati kesi ikiendelea.

• Mnyika anatuma salamu kwa Kamhanda kuwa alisababisha mauaji ya Mwangosi. Anasema kitendo hiki hakivumiliki na hawataliacha suala hili bila hatua kuchukuliwa

• Wenje anazungumzia suala la watoto kukaa chini kwa kukosa madawati wakati mbao zinasafirishwa kwenda nje kila siku kwa dili za wakubwa.

• Wenje anasema Maige aliwajibishwa kwa upotevu wa twiga wawili iweje kwa kawambwa ishindikane?

• Suala la mfumuko wa bei na kodi zisizo za lazima. Wenje "Kama akina Lusinde ndio washauri wa serikali hasa kupandisha thamani ya pesa zetu eti kwa kuondoa picha ya nyoka na kuweka ya Nyerere na Karume basi tumeruhusu akili ndogo kutawala akili kubwa".

• Dr Slaa Anasema wabunge wake hawatatafuna maneno inapofika suala kuiwajibisha na kuiagiza serikali kwa ajili ya maslahi ya Watanzania.

• Anasema Serikalii hii ni IMPOTENT kuanzia yule wa juu hadi walioko chini.

• Ameagiza; wabunge wa CHADEMA wakaze mwendo kuwa more focused na wakali zaidi kuliko sasa, kama kiti kinaendelea na tabia ya kuminya haki.

• Ameagiza kuanzia sasa hotuba zote za Kambi ya Upinzani Bungeni zitolewe nakala na kugawiwa hadi ngazi ya kata ya chama, kupeleka taarifa na maarifa kwa wananchi, Watanzania kila mahali nchi nzima.

• Mkutano umekwisha kwa amani, wananchi wanaandamaa kwa amani wakilisukuma gari la Dr Slaa na kuimba "Raisi, raisi, raisi, ....

====== Picha =======
attachment.php

attachment.php
Kaka mtoi nimekukubali sana, hapa uzalendo kwanza mafisadi kamwe, hii aibu ya kueneza propaganda za ugaidi, udini, ukabila na ukanda hakika umeirudi ccm, mwisho wa ubaya ni aibu.
Asante kwa updates nzuri sana,tuendelea kupigania haki chini ya CHADEMA, SIKU HIZI MIMI SI LALI NA WAZA NAMNA YA KUJENGA FIKRA MPYA KWA VIJANA ILI WAONDOKANE NA ANALOGIA YA MAJAMBAZI WA CCM.
BIG UP ALUTA CONTINUA.
 
Kaka mtoi nimekukubali sana, hapa uzalendo kwanza mafisadi kamwe, hii aibu ya kueneza propaganda za ugaidi, udini, ukabila na ukanda hakika umeirudi ccm, mwisho wa ubaya ni aibu.
Asante kwa updates nzuri sana,tuendelea kupigania haki chini ya CHADEMA, SIKU HIZI MIMI SI LALI NA WAZA NAMNA YA KUJENGA FIKRA MPYA KWA VIJANA ILI WAONDOKANE NA ANALOGIA YA MAJAMBAZI WA CCM.
BIG UP ALUTA CONTINUA.
 
Lakini wa China pia hautoshi mkuu?? au Lumumba iliridhia kauli ya "kampuni ni yangu lakini ndovu si wangu"??

Ndio maana mtu mwenye ushahidi ni muhimu kumwaga hadharani ku connect umiliki wa kampuni na umiliki wa vipusa.
 
maana kama usemi usikikavyo, "wakajizolea mamia na maelefu" namna hiyo watu wataelewa na kujielewa. Ila tatizo ni pale kiongozi wa watu anapowatamkia watu kuwa "FUJO BUNGENI HAZITAISHA HADI SPIKA AACHE UPENDELEO" tena ikasemekana wanaenda kuwashtaki Spika na Naibu wake kwa waliowachagua. Well naona busara hainipi maana wao ndio waliomchagua spika, sio wananchi wa Njombe mjini wala wa Kongwa, wananchi walimchagua Mbunge ambao kama wana akili timamu, watawasikiliza na watawaambia kwa njia ya wao kujieleza "JE HAMKUWACHAGUA WENYEWE?" NENDENI MKAMUONDOE. Maana siku moja nilisikia ilivyokuwa baada ya Mh. Mbowe na wenzake kwenda Mwembeyanga Tandika kuwapa wahuni wa kijiweni mwembeyanga namba za Spika na Naibu wake. Hapo unategemea nini, si kujisifia kufanya uhasi wa wazi?

Juzi niliangalia picha kwenye Luninga za Bwana Mmoja aliyejulikana kama Hitler wa Ujerumani (alikuwa Corporal Jeshini wakati huo), hakujua kusema na watu kwa karibu alikini alikuwa na mvuto wa kusema kwa nguvu sana na alitumia msemo wa "PEOPLES' POWER"ajabu na nguo alizozivaa zilifanana sana na baadhi ya uniform za Chama maarufu nchini. Sinema ilikuwa na kichwa "a criminal in making" tahadhari sana maana kama kiongozi wa watu anatamka kuwa Fujo hazitaisha, mtu huyo ni cha fujo, hayo ni maoni yangu

Alamsiki
 
CHADEMA? CHADEMA JAMANI CHADEMAAAAA TENA, TENA NA TENA MBEYA KAMA IRINGA???

Jamani kama kweli umati huo wote nao ni kwa hiari tu na ni kutokana na mkutano ulioitishwa chini ya masaa 72 tu basi kweli tukio hili si bure lazima kitu kama ka 'UGAIDI' hivi dhidi ya uamuzi tata wa Naibu Spika Mhe Job Ndugai kufukuza wabunge 6 wa CHADEMA bungeni majuzi na hali ya uchonganishi kwa kiongozi huyu kwa chama chake CCM ki-ajali tu bila kutarajiwa matokeo yote haya na mtu yeyote yule.

Kutokana na matukio haya tangu Mwanza, Dodoma, Iringa na sasa kule katika taifa la Mbeya, napendekeza tena kwa dhati kabi kwamba kijana mwenzetu Nape usikubali jambo hili hata kidogo; cha msingi hebu kamwite Mhe Mwigulu Nchemba ofisini Lumumba mara moja na upate kumpa maagizo ya kutayarisha HOJA BINAFSI kwenda bungeni wiki ijayo kwa madai ya 'Ugaidi Mpya wa CHADEMA dhidi ya Mheshimiwa sana Job Ndugai.

Ili kuweza kupata ushahidi zaidi wa kikatu hapa, hebu kamchomoe fasta jomba Ludo kule lupango na akamtembelee tena upya Maggid Mjengwa kisha video kuopolewa hapo hadi bungeni bila chenga.

Hili la wabunge 6 tu kutikisha nchi kiasi hiki kamwe haikubaliki maana maslahi ya chama tawala haipo salama huku mitaani licha ya Mama Makinda na Ndg Ndugai kuonyesha umahiri mkubwa kuchezea CCM nafasi zote muhimu za Full-beki namba 4 na 5 kwa kila kombora lichomokalo toka kambi ya upinzani pale sebuleni Dodoma.

attachment.php

MAELEZO YA PICHA YA PILI:

Picha hiyo hapo chini ni kumbukumbu muhimu kuhusiasa na mkutano uliofana sana na umati mkubwa wa WAPIGA KURA WA 2050 huku wakihiari kuhudhurishwa tamasha la muziki wa Bongo Flava na ubwabwa wa kukata na shoka kwenye mkutano wa kisiasa kwa watani zetu wa kijani uliofanyika kule Igunga kwenye uchaguzi mdogo jimboni hapo.

Kiongozi wa kampeni hizi kwa wakati huo alikua ni 'Mkuu wa Mawasiliano ya Kigaidi na Ulipaji Taifa', Mhe Mwigulu Nchemba ambaye pia alipata kuchokonolewa macho hapo Igunga kwa madai ya kushindwa kujizuia kujenga ujirani wa kindo na mwandani kwa kada mwingine wa CCM.

Wadadisi wa mambo ya kisiasa nchini walinakiliwa wakidai kwamba gharama iliotumika na CCM jimboni hapo ilikua ni zaidi ya gharama ya mtu kuweza kununua mabasi 25 yenye ubora wa Marcopolo Paradiso.

Basi moja ya aina hii siku hizi hukadirishwa kufikia dhamani ya Tsh 130,000,000/-
.

52fghv.jpg
 
Wakuu.

Mtakumbuka kuwa leo wabunge wa Chadema walio fukuzwa kiuonevu bungeni wanafanya mkutano jimbo la Iringa mjini ili kushtaki kwa umma uonevu walio fanyiwa.

Hapa ni yanayojiri mkutanoni.

• Diwani wa Iringa mjini, Nyalusi, wananchi wa Iringa wana imani na viongozi wa CHADEMA, kuliko walioko madarakani. Kapanda Sugu

• Sugu: Tutaendelea kukomaa. Kiti kinamfukuza Lissu kwa kufanya kazi yake, wakati Serukamba mbunge wa FT, akiachwa! Tusi kubwa, hakuna mbunge katika jumuiya ya madola amewahi kutukana tusi baya kama hilo, limevunja rekodi Jumuiya ya Madola

• Sugu: Kauli ya WASSIRA, Kibanda ni nani? Ubinadamu na utu kwao ni cheo!

• Kiwia: Matusi kwa Wtz ni kufanywa maskini katika nchi tajiri, akina mama kwenda na nyembe na kila k2 kujifungua, kuzungumzia madawati miaka 50 ya uhuru wakati Kenya wanazungumzia kompyuta kwa kila mtoto.

• Kiwia: Ukiona mahali kuna amani ya kweli inayotokana na haki pamoja na demokrasia, ujue kuna watu wachache wamejitoa, ikibidi kwa jasho na tone la damu! Bunge sasa limegeuzwa kuwa rubber stamp ya masuala ya CCM!

• Mnyika anasema fedha za DECI zirudishwe. Wabunge wanazuiwa kujadili suala la Deci eti liko mahakamani, mbona Magufuli aliamua kuongelea suala la samaki wake kwani aliwagawa hao samaki wakati kesi ikiendelea.

• Mnyika anatuma salamu kwa Kamhanda kuwa alisababisha mauaji ya Mwangosi. Anasema kitendo hiki hakivumiliki na hawataliacha suala hili bila hatua kuchukuliwa

• Wenje anazungumzia suala la watoto kukaa chini kwa kukosa madawati wakati mbao zinasafirishwa kwenda nje kila siku kwa dili za wakubwa.

• Wenje anasema Maige aliwajibishwa kwa upotevu wa twiga wawili iweje kwa kawambwa ishindikane?

• Suala la mfumuko wa bei na kodi zisizo za lazima. Wenje "Kama akina Lusinde ndio washauri wa serikali hasa kupandisha thamani ya pesa zetu eti kwa kuondoa picha ya nyoka na kuweka ya Nyerere na Karume basi tumeruhusu akili ndogo kutawala akili kubwa".

• Dr Slaa Anasema wabunge wake hawatatafuna maneno inapofika suala kuiwajibisha na kuiagiza serikali kwa ajili ya maslahi ya Watanzania.

• Anasema Serikalii hii ni IMPOTENT kuanzia yule wa juu hadi walioko chini.

• Ameagiza; wabunge wa CHADEMA wakaze mwendo kuwa more focused na wakali zaidi kuliko sasa, kama kiti kinaendelea na tabia ya kuminya haki.

• Ameagiza kuanzia sasa hotuba zote za Kambi ya Upinzani Bungeni zitolewe nakala na kugawiwa hadi ngazi ya kata ya chama, kupeleka taarifa na maarifa kwa wananchi, Watanzania kila mahali nchi nzima.

• Mkutano umekwisha kwa amani, wananchi wanaandamaa kwa amani wakilisukuma gari la Dr Slaa na kuimba "Raisi, raisi, raisi, ....

====== Picha =======
attachment.php

attachment.php

Chama chetu hicho dah niko right right side jamani
 
mabadiliko lazima yamekuja na usipokubali ukweli huu ukweli utakulazimisha.
 
Back
Top Bottom