Yaliyojiri katika kesi ya Freeman Mbowe na wenzake, kesi imeahirishwa mpaka 15, Nov 2021

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,556
Salaam Wakuu,


Leo tarehe 12/11/2021 anatarajiwa kusikilizwa shahidi mwingine katika muendelezo wa kesi Mwenyekiti wa CHEDEMA Freeman Mbowe.

Kujua jana kesi ilipoishia, soma: Kesi ndogo ya Freeman Mbowe: Shahidi akamilisha ushahidi wake, Shahidi mwingine kuendelea tarehe 12/11/2021

Ungana nami katika uzi huu ili kujua kila kinachojiri Mahakamani.

FD-q4B6XwB0d7Ul

Picha: Watu mbalimbali waliohudhuria kesi Mahakama Kuu leo 12/11/2021
Mawakili wa Jamhuri walishafika mapema, waliomba dakika 10, wakapewa, zimefika 30. Wao wanataka kupinga uamuzi mdogo wa jana kuhusu kielelezo chao cha D.R (detention register) kukataliwa.

======
Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa

Wakili wa Serikali, Robert Kidando: anatambulisha Jopo la Mawakili wa Serikali

Jenitreza Kitali
Abdallah Chavula
Pius Hilla Esther
Martin Tulimanywa
Majige Ignasi Mwinuka

Wakili Peter Kibatala: anatambulisha Jopo la Mawakili wa Utetezi

Jeremiah Mtobesya
Paul Kaunda Fredrick
Kihwelo Dickson
Matata Idd Msawanga
John Mallya
Nashon Nkungu
Alex Massaba
Khadija Aron
Evaresta Kisanga

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa na Leo tuna shahidi Mmoja tupo tayari Kuendelea Wakili

Peter Kibatala: Nasisi tupo tayari Kuendelea

Jaji: Shahidi Wenu..?

Wakili wa Serikali: Robert Kidando Yupo amefuatwa

Jaji: Majina yako

Shahidi: anaitwa Askari namba H4323 Msemwa

Jaji: Miaka

Shahidi: 31

Jaji: Dini Yako

Shahidi: Mkrito

Shahidi: Mimi Askari namba H4323 D/ C Msemwa Naapa Kwamba yote nitakayo Sema ni ya Kweli

Wakili wa Serikali: Umesema Unaitwa Nani

Shahidi: naitwa Askari namba H4323 Msemwa

Wakili wa Serikali: Kazi yako nini

Shahidi: Askari Polisi

Wakili wa Serikali: Kituo cha kazi Upo wapi

Shahidi: Nipo Oysterbay

Wakili wa Serikali: Kabla ya Hapo ulikuwa wapi

Shahidi: Kituo cha Polisi Msimbazi na Baadae Kituo cha Polisi Central

Wakili wa Serikali: Central ya wapi

Shahidi: Central Ya Dar es Salaam

Shahidi: Anaweza Kuletwa na Mtu yoyote hata Kama wananchi au Maaskari watakao Kuwa Wamemkamata

Wakili Wa Serikali: Mtuhumiwa anapoletwa Je ni Vitu gani hufanyika

Shahidi: Kumpekua Mashtaka, Kwanza ni Kuona Kama ana viambatanisho Vya Reference namba Na siyo Mtuhumiwa lazima. Awe amefunguliwa kesi, Unaweza Kumfikisha Mtuhumiwa akafunguliwa Kesi pale pale WS: Mtuhumiwa ambaye Kesi imeshafunguliwa analetwa na nani

Wakili wa Serikali: Chumba cha Mashitaka Maana yake nini

Shahidi: Chumba Cha Mapokezi, Tunaita CRO pale ambapo Mteja anapokelewa

Wakili wa Serikali: Wateja wa aina gani wanaopokelewa

Shahidi: Wanakuja Kufungua Kesi na Watuhumiwa wote hao ni Wateja Kwa Polisi

Wakili wa Serikali: Majukumu yanayohusiana na Mashitaka (CRO)

Shahidi: Kufungua Kesi, Kupokea Watuhumiwa na Kutoa Au Kupokea Huduma Mbalimbali zinazohitaji Huduma za Kipolisi

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama sasa CRO inahusika Kupokea Watuhumiwa, Je Utaratibu Wa Kupokea Watuhumiwa Ukoje

Shahidi: Pindi Mtuhumiwa amepokelewa Polisi Pale Chumba Cha

Wakili wa Serikali: Tofauti na Mtuhumiwa Kueleza Mwenyewe, Je Taratibu Zingine ni zipi

Shahidi: Ukiondoa hiyo ya Yeye Kusema, Kama Mtu ni Kibaka wakati Unampekua unaweza Kuona Majeraha

Jaji: Kibaka ni Mtu gani

Shahidi: Mtu ambaye ameletwa baada ya Kupigiwa na Wananchi

Wakili wa Serikali: Hali ya Ki Afya ya Mtuhumiwa hapo Chumba Cha Mashtaka hutokea Vipi

Shahidi: Uelezwa na Yeye Mwenyewe wakati tunaandika Taarifa zake kama Nzuri tunaandika "Good" Kumaanisha Mzima na Kama ni Magonjwa tunaandila "Sick" Kumaanisha Mgonjwa.

Wakili wa Serikali: Kama Mlikuwa wengi tutajie hao wengi ni akina nani

Shahidi: Assistant Inspector Fatuma, PC Emanuel, PC Semeni na Constable Samweli

Wakili wa Serikali: Kazi yako Siku hiyo ilikuwa nini

Shahidi: Nilipangiwa Charge Room

Wakili wa Serikali: Ambapo kazi yake ni nini

Wakili wa Serikali: Zamu ya namna gani

Shahidi: Zamu ya Masaa 12, Kwa hiyo Robo saa Kabla Natakiwa Kuwa kazini

Wakili wa Serikali: Ukiwa Kama Askari za wa zamu, Siku hiyo Majukumu yako yalikuwa yapi

Shahidi: Tulikuwa Wengi na incharge anagawa Majukumu

Wakili wa Serikali: Kwani Dhumuni la Kuangalia Afya ni nini

Shahidi: Ni sababu ya Kutaka Kujua Kama hali ya Mtuhumiwa ni nzuri

Wakili wa Serikali: Endapo Mkaona hali yake Ki Afya siyo Nzuri Mnafanyeje

Shahidi: Tunajaza KWENYE Fomu ya PF3 na Tunampeleka Hospitali, Wale wenye Malaria tunawapeleka Hospitali na Bado Wakirudi tunajaza Mgonjwa

Wakili wa Serikali: Eleza Mahakama tukufu Kwamba 07 August 2020 ulikuwa wapi

Shahidi: Mnamo tarehe 07 August 2020 Alfajiri nilikuwa naingia Kazini, Central Dar es Salaam Kama Askari Wa Zamu Chumba Cha Mashtaka. Ni kafanya Utaratibu Wa Kawaida Upekuzi Kuwa andika Kwenye Detention Register

Wakili wa serikali: Baada ya kuwa Detain Ukafanya nini

Shahidi: Kuwachukua watuhumiwa na Kuwapeleka Mahabusu

Wakili wa Serikali: Mahabusu ya wapi

Shahidi: Ya Central palepale

Shahidi: Walifika Central Ilala Eneo la CRO wakiwa na Watuhumiwa na Moja kwa Moja Baada ya Kufika Afande Jumanne akauliza pale, Nani anahusika na Watuhumiwa Nikamwambia Mimi hapo, Akasema Hawa watuhumiwa Wamekamatwa Moshi na Reference Namba zao hizi hapa

Shahidi: Kuingiza na Kuwatoa Watuhumiwa Chumba cha Mahabusu

Wakili wa Serikali: Unakumbuka Siku hiyo ilikuwaje

Shahidi: Alifika Afande Kingai, Afande Jumanne Na Askari Wengine Wakiwa wameshikilia Bunduki Wakiwa Pamoja na Watuhumiwa Wawili

Wakili wa Serikali: Afande Kingai na Afande Jumanne ni akina nani hasa

Shahidi: Afande Kingai Kwa sasa ni RPC..

Wakili wa Serikali: Kipindi Hicho alichofika

Shahidi: Afande Kingai alikuwa RCO Arusha na Afande Jumanne alikuwa anatokea Polisi Makao Makuu, Ndiyo nilikuwa nafahamu hivyo

Wakili wa Serikali: Walifikia Eneo gani

Wakili wa Serikali: ikawaje

Shahidi: Afande Kingai alirudi Kumchukua Mtuhumiwa

Wakili wa Serikali: Mtuhumiwa Yupi

Shahidi: Adam Hassan Kasekwa

Wakili wa Serikali: Umesema Kwa Mujibu Wa Reference Ulizoluwa Umeletewa Hawa watu walikuwa na kosa Gani

Shahidi: akula Njama za Kufanya Vitendo Vya Kigaidi

Wakili wa Serikali Watuhumiwa Walioletwa ni akina nani

Shahidi: Walikuwa ni Watuhumiwa Wawili wa kiume

Wakili wa SerikaliJe Kuwatambua Kwa Majina

Shahidi: Mohamed Abdilah Ling'wenya na Adam Hassan Kasekwa

Wakili wa Serikali: Kingai na wenzake baada ya Kuwapeleka Mahabusu wote walikwenda wapi

Shahidi: Baada ya Kuwapeleka Mahabusu Watuhumiwa Wote na Kuwajaza Majina yao, Umri wao, Afya zao na Kosa wanalotuhumiwa nalo Baada ya Hapo nikawapeleka Mahabusu, Wao wakina Kingai Wakaondoka

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Kwamba Baada ya Kuwa wamerejeshwa Mahabusu, lini tena ulishughulika nao

Shahidi: Mimi Ndiyo nilikuwa Mtunza Mahabusu, Niligawanya Muda wa kuwatembelea. Muda wa Asubuhi Wakatikuwapelekea Uji kwa Watuhumiwa Wote na Kushusha Chai za Ndugu wengine

Shahidi: Niliwauliza hali yao ya Kiafya na Majina yao, Wakasema Nzuri na nikawajazia Kwamba ni Good

Wakili wa Serikali: Majina ya Washtakiwa Uliyapata wapi

Shahidi: Walinipatia Wao wenyewe, Nilimuuliza Wa Kwanza akasema anaitwa Adam Kasekwa na Wapili Mohamed Ling'wenya

Shahidi: Baada ya Kingai Kuja Kumchukua Adam Kasekwa, alifika Afande Jumanne Kumchukua Mohamed Abdilah Ling'wenya

Wakili wa Serikali: Afande kingai alimchukua kwenda wapi

Shahidi: alipandisha naye kwenda Juu Ofisi ya RCO Nikaenda Naye

Wakili wa Serikali: Huyu Jumanne alimchukua Mohammed Akaenda naye wapi

Shahidi: Alimchukua akiwa na Karatasi Mkononi akasema nitoleeni Mtuhumiwa akaenda naye kwenye Chumba cha OCS

Wakili wa Serikali: alimrudisha Saa ngapi

Shahidi: Baada ya Muda alimrudisha Baada ya Kingai Kumrudisha wa kwake

Wakili wa Serikali: Sasa Hali zao Ki Afya zikoje

Shahidi: Baada ya Kingai Kuja Kumchukua Adam Kasekwa, alifika Afande Jumanne Kumchukua Mohamed Abdilah Ling'wenya

Wakili wa Serikali: Afande kingai alimchukua kwenda wapi

Shahidi: alipandisha naye kwenda Juu Ofisi ya RCO Nikaenda Naye

Wakili wa Serikali: Huyu Jumanne alimchukua Mohammed Akaenda naye wapi

Shahidi: Ilibaaki Palepale CRO

Wakili wa Serikali: Ni lini tena Ulishughulika nayo

Shahidi: Wakati Wa January Mwaka huu, nimehamia Kinondoni, Nilipokea Samansi ya Kuja Kutoa Ushahidi hapa

Wakili wa Serikali: Vitendea kazi Kwa Maana ya D.R vyenyewe Mnapeleka wapi

Shahidi: Zinabaki CRO kwa ajili ya Kuendelea Kujaza Taarifa za Watuhumiwa Wengine. Lakini Kama Imejaa Unaipeleka Kwa OCS anakupa D.R Nyingine

Wakili wa Serikali: Ile uliyowaingiza Adam na Mohammed Ulienda wapi Baada ya Kujaza

Shahidi: Na Mchana niliwatembelea na Jioni Wakati wa Kukabidhiana. Mbali na Kuwaona Wakati Afande anawarudisha Watuhumiwa, Niliwaona tena Muda wa Chai, Mchana na Jioni

Wakili wa Serikali: wakati Unawaona Mchana na Jioni Hali zao Zilikuwaje

Shahidi: Nzuri. Walivyo ingia Hapakuwa na Mgonjwa

Shahidi: Kutoa Ushahidi

Wakili wa Serikali: Ushahidi Wa Kesi gani

Shahidi: Shauri namba 16 la Uhujumu Uchumi

Wakili wa Serikali: Ilikuwa ni Lini

Shahidi: 20 September Mwaka 2021, Wakati nilipo takiwa Kuonyesha Kielelezo Kama Niliwapokea Watuhumiwa Nikiwa Central Wakati Ule, Ilitoa Kma Kielelezo na Ikapokelewa hapa Mahakamani

Wakili wa Serikali: Ilipolewa na Nani Shahidi: Na Mahakama, Akiwepo Mheshimiwa Jaji Siyani WS: Baada ya Kielelezo hicho Kupokelewa na Mahakama, Shahidi: Baadae Nikaruhusiwa Kuondoka

Shahidi: Nikaandika Barua ya Movements Order, Na baada ya Kuandika Movement Order Kule Central Nilimkabidhi D. R Mahakamani Kama Kielelezo baada Kutoa Ushahidi

Wakili wa Serikali: Unasema Ulimkabidhiwa Kwa MADHUMUNI gani

Shahidi: Kuja nayo Kama Kielelezo

Wakili wa Serikalkalii: Mahakamani Kwa ajili gani

Shahidi: Naomba Mahakama Ipokee Barua hii Kama Uthibitisho kwamba Mimi ndiye niliyepokea Kielelezo Cha Detention Register Kutoka Kwa Msajili wa Mahakama Mawakili wa Utetezi wanaingalia na Kuijadili kwa Pamoja kama Jopo, Wamemaliza.

Wakili wa Serikali: Shahidi hebu Tizama Nyaraka hii, Elezea Mahakama Nyaraka hiyo ni nini

Shahidi: Nyaraka hii Ndiyo Iliyonipa Kielelezo, Ina Force Namba zangu H4323 DC Msemwa Na Pia Ina sahihi Ya Msajili Wa Mahakama

Wakili wa Serikali: Unaiomba nini sasa Mahakama Kuhusiana na Barua hiyo

Wakili wa Serikali: Kielelezo Ulikiacha Mahakamani Je ni lini tena Ulishughulika nacho

Shahidi: Nilipokea tena Samansi kwamba Natakiwa Kutoa Ushahidi Kwenye kesi namba 16 ya Mwaka 2021 ya Uhujumu Uchumi, Nikamwambia Sina Kielelezo Akasema Kwamba fika Mahakamani utatakikuta huko huko

Nilifika Kwa Msajili wa mahakama Kumwambia Nimekuja Kutoa Ushahidi Mahakamani Akanikabidhi kile Kielelezo na Barua, na Baada Ya Kupokea Kielelezo akanisainisha Kwenye Kitabu Kwamba nimepokea

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Barua ambayo Ametumia Msajili Wa Mahakama Kukukabidhi Kielelezo. Utaitambuaje

Shahidi: Barua ina Force Namba zangu H4323 ambazo DC Msemwa

Wakili wa Serikali: Kingine

Shahidi: Ni sahihi ya Msajili wa Mahakama

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shahidi anaonyesha Uwezo Wa Kukitambua

Mtobesya: Kwa Niaba ya Mshtakiwa wa 1 tunapingamizi ya Upokeaji wa hii Barua kwa Sababu Zifuatazo 1. Ukisoma Inaonekana Kwamba Mlengwa ni NATIONAL PROSECUTION SERVICE Huyu si Mtumishi wa Ofisi ya NATIONAL PROSECUTION SERVICE na Hakujitambulisha hivyo wakati wa Utambulisho wake

Mtobesya: Lakini Shahidi Alitumia Maneno hayo Kujenga Misingi Ya Ushahidi wake Kwa kuzingati Kesi ya FARID MOHAMMED Vs DPP na CHARLES ABEL GEZILAHABO Vs JAMHURI zimeshasema Kwamba Shahidi anatakiwa Kuwa na Ufahamu na Ushahidi anayotaka Kutoa.. Anasimama John Mallya.

Fact kwamba ametajwa kwenye Barua haitoshi kwa sababu hata Mshitakiwa Wa tatu ametajawa humu, awezi kutoa Barua hii kwa Sababu Haimuhusu. Kwa sababu hiyo Mheshimiwa Jaji tunapinga Kupokelewa Kwa Nyaraka hii.

Mallya: Mh Jaji Naunga Mkono Pingamizi lililoletwa na Mtobesya Kama alivyosema Mlengwa wa Barua ni NATIONAL PROSECUTION SERVICE wanaohusika ni DPP na Wanafanya huduma hizo za Mashtaka, na Shahidi siyo mmojawapo angalau kwa Ushahidi wake, na Mmiliki wa Barua (Maker) Siyo Yeye

FREDRICK KIHWELO: wakati Shahidi anaomba Barua hii Ipokelewe alisema Kwamba Yeye Ndiye aliyepewa Barua hii, Lakini Barua hii Inakwenda Ofisi ya mashtaka Ya Taifa, Kwa hiyo Naungana na Mawakili Wa Mshtakiwa Wa Kwanza na Wapili Kupinga Kupokelewa kwa Barua hii..

Kibatala: Na sisi Kwa niaba ya Mshtakiwa wa Nne tunapinga Kwa Nguvu 1. Shahidi siyo Competence, na Competence Inagawanyika MAKUNDI Mawili (a) In ISOLATION Kwamba haja' lay Foundations Kwamba inamuhusu, Kama Mimi Ningekuwa Ndiyo Wakili wa Serikali, Kwa kuwa Shahidi alidai Kwamba. Alisainishwa Mahala fulani, ilikuonyesha NEXUS kati ya Ofisi ya Msajili na Shahidi, Kwamba Barua Isingemfikia Kwa kuelea Hewani, Wameweka toroli Mbele ya Farasi na Hiyo Ndiyo inaondoa Competence ya Shahidi ambayo pia ni R Prequisite ya Tendering.

Hapo pia Wameweka toroli Mbele ya Farasi.. Shahidi anasema Kwamba Amewasiliana yeye Mwenyewe na Msajili Kwa Ushahidi Wake Mwenyewe, Ilitakiwa sasa ionekane Kwa namna gani Imemfikia Kutoka NPS...

Kibatala: Hajaogozwa Kwa Namna yoyote ile kwamba NATIONAL PROSECUTION SERVICE Tena WA P.O BOX 1733 DODOMA Wamempatiaje hii Barua

Shahidi, Ilipaswa Barua hii Ipokelewe na Agent wao wa NATIONAL PROSECUTION SERVICE DODOMA ambaye anatambulika na Mahakama Afikishe Kwa Shahidi,

KIBATALA: Hatari ambayo Tusingependa Kufika huko, Ni Naibu Msajili N.N Ntandu Kuja kuwa Shahidi Kwenye kesi hii, Mahakama itahusishwa Kuja Kuziba Gap Fulani aje Kuulizwa Ulimkabidhi Shahidi Kwa Madhumuni Gani wakati Shahidi Siyo Muhusika.

Kibatala: Sijasikia Shahidi akisema Kwamba Barua hii ni Nakala Kwake na Kwa Mamlaka yapi.. Lakini Pia Barua Kama ambayo Ina Purport Kupokea Exhibit Kwenye Mahakama, Ilitakiwa iwe preceded na Law, It's Jurisdiction Issue.. Ni hayo tu... Anaketi chini..

Mawakili wa Serikali Wanateta Pamoja hapa..

Wakili wa Serikali Abdallah Chavula:
Ikupendeze Mheshimiwa Jaji, Tumesikikiza Mapingamizi Kutoka kwa Wenzetu Wa Utetezi Kuhusu Upokelewaji wa Kielelezo hiki.. Kiujumla sisi Hatukubaliani nao... hayana Muunganiko na Kilichopo.. Na Kwamba tulichokifanya, Kwa Maoni yao hatujui tunafanya nini na Kwa Maoni yao tumetanguliza toroli Mbele ya Farasi na Kwamba wangekuwa wao Werevu wasingefanya hivyo.....

Na Pia Hakuna Ushahidi Kwamba NATIONAL PROSECUTION SERVICE au Wakala Wake Dar es Salaam ambaye amethibitishwa Kumkabidhi shahidi. Kwa hali hiyo Shahidi hana Uwezo, na Haitoshi Kwamba Shahidi Majina yake Yameonekama kwemye Kielelezo hicho na Wenzetu Wanadai Kwamba Majina hayo

Hoja ya Kwanza Imejengwa kwamba Barua Kwa Maana Ya Kielelezo hiki hakikuelekezwa Kwa Shahidi Na Badala yake, Kielelezo HIKI kimelezwa Kwa NATIONAL PROSECUTION SERVICE yenye anuani yao DODOMA na Ni Hoja zao Kwamba Shahidi yeye siyo Mhusika wa NATIONAL PROSECUTION SERVICE..

Wakili wa Serikali Abdallah Chavula: Ndiyo yaleyale tuh+ Mheshimiwa Jaji

Kibatala: MHESHIMIWA JAJI Naona Wakili yupo Emotional Sana, Na Hii siyo Vita Vya Mtaani, Hebu ajielekeze Kwenye Kujenga Hoja tu...

Wakili wa Serikali: Abdallah Chavula Ndiyo sasa Uchague cha Kusema sasa, Sisi tumeelewa hivyo

Jaji: Hakusema wao Werevu, amesema angelikuwa yeye angefanya...

Kibatala: Basi Mheshimiwa Jaji, tumuache aendelee kuelewa anayotaka, Tutapata muda wa Kujibu..

Wakili wa Serikali: Wenzetu Wanajaribu Kusema Kwamba Shahidi Hakuwahi Kutaka Nakala hiyo Ya Barua haikulekezwa Kwenda Kwake na Kwa sababu hiyo Ushahidi Haupo na Hivyo Kupata Barua hii ni Haramu Kumfikia Kwake bila Kupita kwa NATIONAL PROSECUTION SERVICE

Ni Maswala ya kufikirika tu, Yasiyokuwa na Uhalisia, Na Kama tunaamini sote kwamba Nyaraka inajizungumza Yenyewe, Ni Maoni yetu Kwamba Tuache Hii Barua ijisemee Yenyewe

Wakili wa Serikali: Sisi tunaona Barua Ipo Sawa Kwasababu inamtaja Shahidi Dhidi Ya Kielelezo, Inamuhusisha Yeye Shahidi Na Kielelezo ambacho Shahidi anakileta Kingine kwamba Barua hii haikupaswa kwenda Kwa Shahidi Bali Kwa NATIONAL PROSECUTION SERVICE pekee nayo siyo Sahihi

Na haikuishia hapo, amesema anaitambua Barua hiyo kwa sahihi ya Msajili.. Hali ingelikuwa ni Tofauti kama anayeonekana katika Barua hiyo ni Mtu Mwingine na siyo Msajili.

Imemtaja kwa Force Namba Yake, Majina yake na Rank yake.. Hoja Ingekuwa Miongoni Mwa wanaopaswa Kupata Nyaraka Hii Shahidi Jina lake lipo.. Sisi tunasema ni Mambo ya Kufikirika Mheshimiwa Jaji Shahidi Katika ushahidi wake amesema aliyempa Barua ni Msajili

Wakili waSerikali: Je Iliandikwa kwa NATIONAL PROSECUTION SERVICE wenyewe DODOMA au Kuna watu Wengine Walikusudiwa kupata hii Barua Mheshimiwa Jaji Ukiangalia Ukurasa wa Nyuma Inaonyesha wakina nani wanapaswa Kupewa hii Nyaraka Na Miongoni Mwa watu waliotajwa Shahidi Ni oja wapo, Barua hii

Mheshimiwa Jaji sote tunafahamu Kwamba Barua imeandikwa halafu Ikaandikwa "Copy to" basi wamepata Watu wote.. Siye Maoni yetu tunaona hilo halikuwa la Msingi na halikuwa na lazima.. Hoja Nyingine ni ya Competence kwamba Shahidi hayupo Competent..

Wakili wa Serikali: Tungeanza kufikria kwamba Shahidi hajaweka Misingi, Hoja Ingekuwa aliye Saini Siyo Msajili, Basi tungesema Shahidi ameshindwa Kuweka Misingi.. Hoja Ingelikuwa Hicho kinachosemakena Kimekabidhiwa kwa Shahidi Sicho Shahidi anachokisema Kusingekuwa na Misingi...

Na haijaelezwa Mahakama Kwenye Issue ya Competence, Haijaelezwa Mahakama Kivipi Kielelezo hiki Siyo Competence.. Lililo elezea Kwa Urefu ni Moja tu, Competence ya Shahidi..

Maneno ni lazima Uwe Relevant, Imezungumzwa Jumla lakini Mahakama Haikuambiwa Kwamba Ushahidi Siyo Relevant na Kwa nini siyo Relevant Haikuelezwa hivyo Mahakamani.. Haikuelezwa kwa kigezo Cha Material na kwamba Ushahidi Siyo Material kwa kadha wa Ladha..

Wakili wa Serikali: Mahakama Ikarejewa a kwemye Maamuzi yake Iliyo fanya Jana, Pia Kwa Sharif Athuman na wenzake Sita, Shauri Lingine ni la Charles Gezilabo.. Ambapo Kwenye Mashauri hayo Mahakama ilikuwa inaongelea katika Upokelewaji wa Ushahidi Mahakamani, Yale ambayo ni Testimonial yaani wa

Na akaeleza kwamba Alipokutana na Msajili wa mahakama, Msajili akampatia Barua, Akaeleza Barua hiyo ina Force nmab zake pamoja na Majina, Na Barua hiyo ina Sahihi ya Msajili.... Shahidi ameonyesha Kwamba Baada ya kutoka Kwa Msajili Kielelezo hiki Kilikuwa Kwake Moja kwa moja

Shahidi Kushindwa Kulay Foundation Kabla ya Kutoa Kielelezo, Shahidi hana Uelewa, lacks Knowledge ya Kielelezo hiki, Mheshimiwa Jaji sisi tunasema Haya yote Shahidi Amezungumza, Utatizamwa ushahidi wake wa awali, Kabla alionyeshwa Nyaraka akaitambua..

Wakili wa Serikali: Abdallah Chavula ANASOMA

Wakili wa Serikali: Siyo lazima awe Custodian au Maker wa hiyo Document ndiyo aweze Kuitoa Nyaraka, Kinachoangaliwa anaufahamu, Ya Yaliyomo kwenye Nyaraka ya Ushahidi huo, Amewahi Kumiliki Kwa wakati Fulani Kielelezo hicho, Kimewahi Kumfikia Mikononi Kielelezo hicho

Naomba nielekeze Mahakama Yako Kwenye Shauri la DPP Vs Milzahi Bilibatish ama Jina lingine Haji na wenzake Watatu, Rufaa ya Jinai Namba 493 ya Mwaka 2016, Ni Mahakama ya Rufaa ya Tanzania Katika Ukurasa wa saba, Aya ya Mwisho Mpaka Aya ya Kwanza Ukurasa wa Nane

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji siye tunaona Kwamba Ushahidi huo ni Msingi Tosha, Foundation Tosha ya kumpa yeye Uwezo wa kutoa Kielelezo, Hoja ya kwamba Kigezo Pekee ni Knowledge, kwa mtu Kutoa Ushahidi Mahakamani sisi tunasema Siyo Sahihi, Si Msimamo wa Sheria,

Huu ndiyo Uthibitisho wa Kuonyesha Kwamba Tumefuata Utaratibu wa Kiutawala Kama Ilivyo zungumzwa na Mahakama..

Utaratibu wa Kiutawala Maombi yanafanywa kwa Kupeleka Katika Mahakama.. Hivyo basi Mheshimiwa Jaji Kwa Kuheshimu Uamuzi wa Mahakama Ukiosomwa Jana na Kwakufuata Uamuzi wa Mahakama Ukiosomwa Jana, Ambao Umetamka wazi wazi Kwamba Utaratibu wa Kiutawala Unaweza Kufuatwa

Wakili wa Serikali: Shahidi kaonyesha Ufahamu Walau kwenye Nyaraka hiyo ameonyesha Majina yake, Walau katika Nyaraka hiyo ameeleza aliye Saini, Ameeleza alikoitoa Nyaraka hiyo (Source yake), Shahidi ameonyesha ana Knowledge ameonyesha uwezo, Kwa Uchache tu siye tunasema ana taarifa ya kile alichoonyesha Ndani ya Nyaraka, Wenzetu Wanasema Eti Palipaswa yafanyike Maombi na Mahakama itamke, Jaji hawajasema hivyo, Walisema ingetangulia Amri ya Mahakama, Wakili wa Serikali Abdallah Chavula Sote tunafahamu kwamba ili Mahakama itoe Amri inapaswa Ipelekwa (MOVED).

Kwenye Maamuzi yaliyofanywa na Mahakama Yalisomwa Siku ya Jana, Mahakama Katika Uamuzi wake ilisema Kwamba Mambo ambayo yanapaswa Kufanywa na siye, Ni Pamoja na Kufanya Utaratibu wa Kiutawala katika Kuipata hiyo Nyaraka. Sasa Mahakama Imeelekezwa haya, Siye ni akina nani tutafute.

Njia tunayiijua Kuoata Hiyo Nyaraka, Na sote tunafahamu Kwamba Unaofuata Utaratibu wa Kiutawala Maombi yanafanywa kwa Kupeleka Katika Mahakama.. Sasa Mahaka Imeelekezwa haya, Siye ni akina nani tutafute Njia tunayiijua Kuoata Hiyo Nyaraka, Na sote tunafahamu Kwamba Unaofuata.

Wakili wa Serikali: Hivyo Mheshimiwa Jaji Hoja ya kwamba Tulipaswa Tufuate Amri ya Mahakama sisi tunasema Hapana hatukupawa Kwenda njia hiyo... Naomba Nimkaribishe Mwenzangu Wakili wa Serikali Pius Hilla,

WS Pius Hilla........

Kibatala: MHESHIMIWA JAJI tunaomba Tujirizishe kama Shahidi hana Diary na Kama Kwenye Diary anaandika Chochote.. Na Pia kama Shahidi ana simu pale kizimbani.... Na Kama ameingia na Vitu Visivyoruhusiwa kizimbani tunaomba aondolewe kuwa Shahidi..

Kibatala: Zitoke pande mbili za Mawakili Chini ya Mahakama tukamkague Kwanza Kabla Kesi haijaendelea...

Shahidi: ANAONYESHA DIARY, PENI, KARATASI NA SIMU JUUUUUU kabla hajakaguliwa...

Kibatala: Tunaomba vitu hivyo viwe chini ya uangalizi wa mahakama kabla hatujaendelea na kesi

Afisa wa Mahakama anaenda Kizimbani Kuchukua DIARY, PENI na SIMU kutoka kwa shahidi wa Jamhuri.. Shahidi anatikisa kichwa kama ishara ya kusikitika... WS Pius Hilla anaendelea

Kwa sababu Vigezo Vyote Vilivyowekwa kwenye Kesi ya SHARIF Shahidi amevifanya.. Na wakati anatambua Vielelezo akasema Hiyo Force Namba Yake ameiona.. Lakini pia Shahidi aka authonticate Barua hiyo kwa kusema kwamba amemkabidhi wa na Msajili wa Mahakama, kwa Maana Authentication of Material, Kwa Maana Nyaraka hiyo Imemfikia Kwa Kukabidhiwa na Msajili wa Mahakama,

Wakili wa Serikali: Kesi ya ROBISON MWANGISI Vs JAMUHURI TLR 213 ya 2003 Inahusiana na Kielelezo Cha Leo ambacho Shahidi alikuwa anaomba Kipokelewe

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Wakili Mtobesya aliongelea Kwamba Shahidi amefeli Ku authenticate Kielelezo ambacho alikuwa anakiomba, Hoja hii haina Mashiko

Mheshimiwa Document hii wala Siyo lazima, Kwa sababu Shahidi ame' lay Foundation Kwamba ameipataje.. Na Mheshimiwa haijaelezwa hata kidogo Iwapo shahidi haaminiki... aliyopewa na Kwamba Ndiyo Kitu alichopewa.. Na ameonyesha Kwamba alikuwa kwa ajili ya Kukabidhiwa Kielelezo, Kwa Maana yupo Knowledgeable.. Mheshimiwa Jaji nizungumzie Kuhusu Handover Documents ambayo Imezungumzwa kwamba Hajasainishwa na NATIONAL PROSECUTION SERVICE

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Itoshe Kusema Kwamba zile Kanuni za authentication of Documents alizifanya kikamilifu, Wakili Mallya alisema Kwamba Kutaja tu Kwenye Document hakutoshi Kufanya, Mheshimiwa Shahidi haikuishia Kutajwa tu. Yameonyesha Mengi na Shahidi Kwa Maana alivyoioata Madhumuni

Kwa Dhumuni la Kielelezo. Katika Mazingira hayo Mheshimiwa Jaji uhitaji Jambo Lingine, na wala hicho siyo Kigezo Cha hiyo Barua Kuingia Katika Ushahidi huo. Na lingine huwezi Barua Kama hiyo Ukasubject Kwenye Chain, Kwa sababu Barua Imetoka Kwa Msajili Kakabidhiwa Shahidi..

Wakili wa Serikali: Kwenye Shauri la Yusuf Massalu, Alliance na wenzake 3, Rufani ya Jinai ya 163 Mwaka 2017, Mahakama ilisema katika Uamuzi wake Kwamba Kinachotakiwa Kuangaliwa ni Assurance, Hakuna Ubishi Kwamba Barua ni ya msajili wa Mahakama na Wala hakuna Ubishi Kwamba Shahidi amekabidhiwa

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Wakili Kibatala Alielekeza Juu ya Prosecutorial arrangements, Hakuna Cha Prosecutorial Arrangements hapa, Ni Msajili Alimkabidhi Barua, Tunaomba hiyo hoja Itupiliwe mbali..

Wakili wa Serikali: Nimalizie kwa Kusema Kwamba, General Assessment Ya Kile ambacho Shahidi amekieleza na Barua ambayo Imetolewa Kwa Msajili haina Ukweli wowote kuhusu Kupokelewa Kwa Barua, Shahidi ni Competence, Material ni Relevance..
Na Pia Ime' pass Vigezo Vyote Vya Upokelewaji wa Ushahidi.. Tunaomba Mheshimiwa Jaji Mapingamizi yatupiliwe mbali na Kielelezo Kipokelewe.. Wakili wa Serikali Pius Hilla anamalizia na kukaa..

Jaji: Mmemaliza Upande wa Mashtaka?

Mawakili wa Serikali Wote wanaitika NDIYO

Mtobesya: Naomba Kuongezea Machache.. nisiichoshe Mahakama Yako kama Mwanahistoria, Nitajibu na naomba Kuongezea Machache..

Mtobesya: Kaka Yangu Chavula anasema Nyaraka inatakiwa ijisemee yenyewe na Kwamba hata Submission tusimgefanya.. Na Kwa Maneno Ya Mahakama ya Rufaa ya ROBINSON RWANGISI inasema Kwamba Nyaraka iwe Sahihi, Ndiyo Maana Tunafanya hili zoezi.. Aliyetakiwa Kuifanya Nyaraka ingie Siyo Mwingine Bali ni Shahidi....

Mtobesya: Na sisi tunasema Kwamba Kesi hii Inafanana Misingi ya Kesi ya SHARIF Vs DPP na Kesi ya CHARLES GAZILABO.. Sisi tunasema alichokisema haitoshi kwa sababu, Unique features Kama Tarehe na Anuani hakuvitaja..

Wakili wa Serikali, Robert Kidando: OBJECTION naona Kama Unique Features ni Kitu Kipya..

Jaji: Unique Features ni Moja ya Criteria ya authentication..

Mtobesya: Kaka Yangu Pius Hilla wakati anasema Kuhusu Kuna Force Namba sifikirii Kama alisema Just for Cosmetics.

Mtobesya: Kitu Pekee hapa ni FACTUAL EXPIDITION ni Namna Barua Ilivyo Mfikia Shahidi.. Na Njia pekee ya Ku Prove hiyo Fact ilikuwa ni Kwa wao Kuileta hiyo Dispatch Book kwa wao Kufuata Procedure.. Kwa ajili ya ku Prove Competence ya Shahidi Kupitia Knowledge Ilipaswa Iletwe hapa

Jaji: Nisaidie hizo unique features

Mtobesya: vipo kwenye Kesi ya CHARLES GAZILABO

Jaji: sawa

Mtobesya: Mimi na Malya hatukusema Kwamba Hakusema alipewa Nakala ya Barua, na Kwamba Mlengwa wa Barua siyo yeye, Kitu Pekee ambacho Kingeondoa Utata ni DISPATCH BOOK ambayo hajaileta

Mtobesya: Kwa Bahati Mbaya Hakuwepo Hapa Mahakamani Kusema Kama kweli alimpatia na Kwa Bahati Mbaya Sana Kaka yangu Pius Hilla Anasema Dispatch siyo Jambo Msingi... Na sisi Tunasema hajafika Viwango Vya authentication kama inavyopaswa....

Mtobesya: Alisimama Pia Kaka Yangu Chavula akasema Kwamba Content inatosha Kuonyesha Kwamba Ilikuwa inatosha..

Mtobesya: Kwa sababu za Kaka Yangu Pius Hilla Anasema Ilimradi Shahidi Anasema alipewa Inatosha na wala haihitaji Uthibitisho, Lakini Kwa Bahati Nzuri Shahidi akisema Alisaini Kwenye Dispatch..

Jaji: Hakusema Dispatch

Mtobesya: Alisema alisaini Kwenye Kitabu, Kwa Maana hiyo Sehemu Yoyote Ambayo nimesema DISPATCH isomeke Kitabu alichosaini..

Jaji: sawa

Mtobesya: Kwa Bahati Mbaya alizumgumzia suala la content kwa 75% ya Wasilisho lake wakati huo huo Pius Hilla Kaongelea kwamba Haturuhusiwi Kuiongelea Suala la Content Kama Ilivyo Kwenye Kesi Ya ROBISON RWANGISI.. Sasa Mheshimiwa Jaji hawawezi Kula Keki na Kuendelea Kuwa nayo,

Mtobesya: Waamue Jambo 1 Kama wanaijadili Content Wakubali wote tujadili, Kwa Bahati Mbaya Kaka Yangu Pius Hilla Alianza kuongelea Masiala ya Force Namba, Ambapo ndiyo Content yenyewe.. Ni Wasilisho letu Kwamba Mahakama Ipitie Barua hiyo na tunaomba Barua hiyo Isipokelewe.

Mallya: Kwa ufupi sana Mheshimiwa Jaji, Kwanza Naunga Mkono Wasilisho la Kaka yangu Mtobesya, Wakati Abdallah Chavula anafanya Wasilisho alisema Mtu Kumiliki tu Kwa Barua hiyo Kunatosha Kuonyesha Kama Yupo Competence..

Kwa Maana Nyingine ni kwamba Wao wakina Chavula Ndiyo waliondika Barua na Wao wakina Chavula Ndiyo waliojibiwa na Siyo Shahidi.. Na Pia Chavula anasema Kwamba Mahakama inapoenda Kufanyia Maamuzi iangalie Content Ya Barua hiyo na Kwa Maneno hayo Maana yake siyo Maneno Ya Shahidi

Sisi tunasema Kwamba Hakuonyesha aliipataje hasa Barua hiyo na Kwamba Pande zote Mbili tunakubaliana kwamba Shahidi Siyo Mlengwa wa Barua hiyo.. Chavula alisema Kwamba Wao ni akina nani wasifuate Maamuzi ya Mahakama Katika Kupata Barua hiyo

Fredrick Kihwelo: Barua anayosema alipewa siyo hii iliyopo hapa Mahakamani, Kwa sababu Barua Inaonyesha Mlengwa ni NATIONAL PROSECUTION SERVICE.. Kwa sababu hiyo sisi tunapinga Upokelewaji wa Barua hii, ahsante sana Mheshimiwa Jaji..

Fredrick Kihwelo: Naomba Kukubaliana na Wenzangu Mawakili Wa Upande wa Utetezi, Shahidi alisema Kwamba alikwenda Kwa Msajili yeye Mwenyewe na akapewa Barua na Kielelezo, Na Kwa Mara ya Kwanza shahidi alionana na Msajili

Wakili wa Serikali, Abdallah Chavula: OBJECTION naona Kama analeta Jipya

Kibatala: Asante Mheshimiwa Jaji, Nianze na Suala la hicho Kitabu, Tunasisitiza kwamba alichoongozwa Shahidi Kukizingumzia palikuwa na Jaribio la Authentication, Wao walikifanya Kitabu Kuwa Mchakato wa Barua, Huku kutengenishwa kulianza saa ngapi,

Ndiyo Maana Nilisema wameweka toroli Mbele ya Farasi Kitu ambacho Wamechukia, Lilikuwa Legal and not Ego.. Wenzetu wanasema Mheshimiwa Jaji sote hatubishani, Ukweli tunabishana, Kwa sababu Mimi sijui wala Wewe Mheshimiwa Jaji.. Hujui kama hiyo Barua Imetoka Kwa Msajili kweli

Sasa Usahihi wa Saini Ya Msajili.. Kuna Mazoezi Walitakiwa Wenzetu Kufanya na hawakufanya.. Na Ndipo suala la ku' Chagua Toroli likae wapi na Farasi akae wapi ni Jambo Muhimu... Maamuzi yalikuwa Criticism na Siyo Permissive ndiyo Maana Mahakama Ika' refuse...

Kibatala: Ndiyo Maana nikasema Je ni Sahihi Kwa sisi kitokutimiza Majukumu yetu na Kuanza Kumuingiza Msajili Kwenye Authentication ya Barua hiyo Hapa Mahakamani, Hicho ni Kielelezo na ni sehemu ya Ushahidi, Wenzetu wanasema Eti alitambua Shahihi Ya Msajili, Shahidi anatambuaje

Kibatala: Kwamba Mahakama iliwalekeza wao Waletwe Barua Bila Kitabu Walichosaini Kupokea hiyo Barua,.... Nimesikia Mtu anasema Kuhusu Assurance, Assurance Ambayo Mahakama inapata, Mahakama hii ni Tofauti na siyo sehemu ya Msajili wa Mahakama...

Mallya pia amesema Hapa kwamba Barua Imewataja washtakiwa mbona hawajapata? Kutajwa kwamba Unapewa Nakala haimaanishi Kwamba umepewa Nakala ya Barua hiyo, Kwa maana hiyo Barua hiyo inakosa Uthibitisho...

Kibatala: Assurance Ipo wapi Kama Hakuna aliposaini, Na Hapo Ndiyo Njia ya Chain inapoanzia na kama Njia Inakosekana Haiwezekani Kupokelewa.. Kuna argument kaleta Sijui Abdallah Chavula au Pius Hilla Kwamba Eti Kwakuwa Barua Imemtaja Shahidi Ndiyo Lazima awe amepata..

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Wenzetu pia walisema hatuja onyesha Lack of Competence ya Barua, Mbona Nimesema hapa Sasa hivi na Muda Ule, Kwamba Kuna fanya na Barua na Shahidi Juu ya Competence, Comptence inaangaliwa wamefanya nini Katika ushahidi wao..

Tunamalizia Kwa Kusema Competence Ya Shahidi Ni Muhimu na Competence ya Nyaraka ni Muhimu, Tunamalizia kwa Kusisitiza kwa Mapingamizi yetu.. Kwamba Kweli Kuna Maamuzi ya mahakama Kuhusu Nyaraka, lakini Mahakama haikusema Wenzetu Wasifuate taratibu Katika Kuleta Nyaraka Mahakamani

Na Kwamba isionekene Lawama ni za Kwako kwa Kuwaelekeza Kufanya hivyo, Haya ni Mambo 2 tofauti na wala Usijione Kwamba Umekosea Kuwaelekeza.. Na Mwisho Kesi ya MIZIRAHI sina la Kuzungumza kwa sababu Mambo yote ya MIZIRAHI Yapo kwenye kesi ya GEZILAHABO. Ahsante Mheshimiwa Jaji

Jaji: Kuhusu vitu ambavyo vimechukuliwa Kwa shahidi kizimbani,

Kibatala: Tungeweza kwenda mbali kwa sababu tunahisi kwamba mifukoni bado anavitu vingine ila kwa sababu ya utu tusifike huko.. Tunaomba malekezo yako kwamba shahidi amekiuka kiapo chake na uelewa wa kazi yake

Wakili wa Serikali, Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Kwa vyovyote Vile wakati Suala hilo linaibuliwa na wakili Msomi Kibatala, Ni wakati wa Mawasilisho ya Hoja za Mapingamizi, Lakini hatujasikia Wakati wowote Kwamba Vitu hivi Vimetumika wakati Shahidi anatoa Ushahidi.. hiyo Diary yake.. Na Zoezi analolialika Mahakama Kufanya naona ni tofauti na Sheria inavyotaka.. Jaji: Nilisikia Kibatala Kwamba umesema Kwamba Shahidi ana simu na ana Diary, Je ulisema kwamba Alikuwa anavitumia..?

Wakili wa Serikali: Sifa za shahidi tunafahamu zipo Chini ya Kifungu cha 127 cha Sheria ya Ushahidi Ambapo imeonyesha Shahidi anaweza Kukosa Sifa, Nilikuwa nadhani kwenye hilo tujiongoze Vizuri, Kwa sababu Kitu Kama simu ni Mali Binafsi ya Shahidi, Na Pia Mimi Nimeona tu Wakati Shahidi Anatoa

Jaji: Je Shahidi anapotakiwa Kuingia Kizimbani anatakiwa kukaguliwa, Nasema hayo Kwenye simu naona tunaongelea Privacy ya Mtu, Maana hatujui Kwenye simu tutaangalia wapi, Diary ni Rahisi Kwa sababu tunaweza Kupekua...

Kibatala: Leo Wakati Kesi inaendelea ProfessorJay aliniandika kwamba Shahidi anasoma, Tukasema tujiridhishe kwanza, Wakati tunaendelea na Hoja alikuwa na Pen na Diary akiwa bussy akiandika.. Na kabla hatuja Simama tulikuwa tayari tumeshajiridhisha kuanzia

Mtobesya: Je hiyo Diary sasa inakaaa kwa nani? Jaji: itakaa Mahakamani...

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Sasa haya Maombi haya semi kama ni Kwa Mujibu wa Sheria au Lah na Kwa sababu hiyo Hatujui ni zoezi la Kisheria..

Kibatala: Sheria Inakataza na Mpaka kesi zipo za Marejeo Vifungu Vya 127 Vya Sheria ya Ushahidi,

Jaji:
naomba Mkatumie Week end hii mkajidhirishe Kwa Kufanya Wasilisho Dogo Kuhusu Shahidi Kuwa na Diary Kizimbani.. Na Kuhusu simu tumrudishie...

Jaji: Ndiyo nimesema Jumatatu tutafanya Wasilisho hilo kwanza nini Madhara yake ya shahidi kuwa na Diary

Shahidi: anayoosha mkono kwa tahadhari

Jaji:
kuna Jambo Unataka Kuongea lakini hautoruhusiwa Kuiongelea Diary Kwa sababu nilisha Tolea Maamuzi

Shahidi
: Sawa Mheshimiwa Jaji

Jaji: Basi Shauri linahairishwa Mpaka Jumatatu Tarehe 15 November 2021 Shahidi Utatakiwa Kurudi Mahakamami Siku hiyo, Washtakiwa wataendelea Kuwa Rumande chini ya Magereza Mpaka Jumatatu saa 3 Asubuhi..

Jaji anatoka..
 
Tupo tupo pamoja najuwa hali itakuja kupatikana tu mwisho wa siku....
 
Kesi ndogo kwenye kesi kubwa siyo ok ok tupo gado - leteni uhondo wakuu.
 
Huyu haaminiki......nadhani huwaga anawahi kublock wenye spidi akina Roving Journalist ili tusiwe well informed. Uhuni.
Sidhani kama hoja yako ina ukweli , hii ni kwa sababu Mods wanaweza kusaidia ku update uzi huu bila shaka yoyote hata kama mletaji analenga kuhujumu .

Hata hivyo sometimes Mahakama inachelewa kuanza , sasa hakuwezi kuwa na Updates hadi kesi ianze
 
Asulubiwee asulubiwee..
Aliyesubiwa na wayahudi baadae alifufuka na kisha kujulikana kuwa ni mkombozi wa ulimwengu.

Mbegu ikipandwa ni lazima Ife ndipo iote.
Ndivyo ilivyo kwa mbowe,sasa ivi mnamsulubu kama haitoshi yeye ni mbegu ya ukombozi wa pili wa nchi hii kutoka kwa mkoloni ccm.
ATAOTA KWA USHUJAA

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Kweli maana mpaka akati huu mawakili wa serekali hawjaingia ili hali upande wa utetezi wapo muda mrefu
Sidhani kama hoja yako ina ukweli , hii ni kwa sababu Mods wanaweza kusaidia ku update uzi huu bila shaka yoyote hata kama mletaji analenga kuhujumu .

Hata hivyo sometimes Mahakama inachelewa kuanza , sasa hakuwezi kuwa na Updates hadi kesi ianze
 
Back
Top Bottom