Yaliyojiri katika kesi ya Freeman Mbowe: Jaji aahirisha kutoa uamuzi mpaka tarehe 17/11/2021 saa tatu asubuhi

Mbona Kama jaji kashatoa uamuzi maneno yake kuwa upande wa mashtaka mtamleta shaidi na atakaa kizimbani kuendelea kutoa ushahidi si tayari anashiria kukataaa pingamizi
Na mimi nimeshangaa au labda sijaelewa vizur kuhusu mapingamizi ya jana.
 
Upande wa mashtaka mutamleta shahidi atakaa kizimban na ataendelea kutoa ushahidi wake, mbona sasa kama tayari ameshatoa uamuzi kwa namna yake fulani hivi
 
Jaji ameingia Mahakamani Muda huu

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani

Wakili wa Serikali Robert Kidando anatambulisha Jopo la Mawakili wa Serikali

Jenitreza Kitali
Abdallah Chavula
Pius Hilla
Nassoro Katuga
Esther Martin
Tulimanywa Majige
Ignasi Mwinuka

Wakili Peter Kibatala anatambulisha Jopo la Mawakili wa Utetezi


Jeremiah Mtobesya
John Malya
Seleman Matauka

Wakili wa Serikali Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Uamuzi Mdogo

Wakili Peter Kibatala Mheshimiwa Jaji nasisi tupo tayari Kupokea Malekezo

Jaji Jana nilihairisha Shauri Jana Jioni, Nikasema Nitasoma Uamuzi leo.

Lakini Kutokana kwa Wingi wa Hoja naomba Muda zaidi Mpaka Kesho


Nikakamilishe Kuandika Uamuzi

Naomba Radhi kwa Hairisho hili ambalo hatukulitarajia

Mawakili wa pande zote mbili Wanasimama Kukubaliana


Jaji kama nilivyosema kwamba nahairisha Shauri Mpaka Kesho, Upande wa Mashitaka Mtamleta Shahidi atakaa Kizimbani Na ataendelea Kutoa Ushahidi

Nahairisha Mpaka Kesho Saa 3 Asubuhi

Jamani

Huyu siyo jaji, Sasa anawaambia wamlete shahidi kesho aje kuendelea kutoa ushahidi wa Nini Sasa ,huku hujatoa rulling (hukumu/maamuzi/maelekezo) halafu unaahirisha mpaka kesho ili iweje Sasa???? Aiseeeeee Hakuna kitu hapo ,,,,ni upumbavu tu, hatuna haki taifa hili, unaahirisha mpaka kesho ,ko ni pingamizi gumu lakini utalitupilia ,Jaji Tiganga ni Kama ndugai tu Hakuna kitu hapo.
 
Mbona Kama jaji kashatoa uamuzi maneno yake kuwa upande wa mashtaka mtamleta shaidi na atakaa kizimbani kuendelea kutoa ushahidi si tayari anashiria kukataaa pingamizi
Hili hata mimi sijaelewa, kama hakuna typing errors, basi jaji kashatoa maamuzi, ila tuu haja yaandika.

Ndiomana kasema shahidi aje, atakaa kizimbani na ataendelea kutoa ushahidi.
 
Usiku wa kuamkia leo nimeota; nimemuona kiumbe la kutisha sana likidondoka toka mawinguni kwa kasi sana na kudondokea juu ya mawe na lilichanika vipande vipande na gafla tazama moto wa ajabu ukashuka toka mawinguni na kuunguza kwa kasi yale mabaki ya lile jitu bila hata mfupa kubakia.
 
Upande wa mashtaka mutamleta shahidi atakaa kizimban na ataendelea kutoa ushahidi wake, mbona sasa kama tayari ameshatoa uamuzi kwa namna yake fulani hivi
Huyu Jaji anafanya makusudi kuharibu kesi. Anataka asilaumiwe na waliomtuma ili maamuzi yake yakatiwe rufaa.
 
Yaani unawaambia watu kesho shahidi apande kizimbani aendelee kutoa ushahidi wakati bado hujatoa uamuzi wa mapingamizi ya upande wa utetezi?

Bado watu wasubiri uamuzi gani wakati huyo shahidi utetezi wanapiga kua hana sifa?😂😂😂

Huyu Jaji ana matatizo gani?

Nitawashangaa sana mawakili wa upande wa upande wa utetezi kama mtaendelea na huyu Jaji.
 
Salaam Wakuu,

Leo tarehe 16/11/2021 kesi ya Mwenyekiti wa CHEDEMA Freeman Mbowe inaendelea.

Kujua jana kesi ilipoishia, soma: Yaliyojiri kesi ya Freeman Mbowe na wenzake Nov 15,2021

Ungana nami katika uzi huu ili kujua kila kinachojiri Mahakamani.
Jaji anawapa muda mawakili wa Serikali kwenda kumfunda vizuri shahidi wao ambaye akili yake ni ndogo.sana kuweza kushika uongo anaofundishwa kuja kuutoa mahakamani.

Wakati huo huo Jaji naye anaenda kupigwa msasa na mamlaka ya uteuzi ili ahakikishe Mbowe anafungwa.Hakika mhimili wa Mahakama na tasnia ya sheria kwa ujumla wake imenajisiwa vibaya sana.
 
Mbona Kama jaji kashatoa uamuzi maneno yake kuwa upande wa mashtaka mtamleta shaidi na atakaa kizimbani kuendelea kutoa ushahidi si tayari anashiria kukataaa pingamizi
Nafikili wakati wa kutoa mahamazi, shaidi anatakiwa awepo kizimbani, na vile vile unavgofikiria pia Inawezekana
 
Jaji anamwambia shahidi kesho awepo aendelee kutoa ushahidi!?!? Hapo si tayari katoa uamuzi kwamba nshahidi ataendelea kuwa shahidi licha ya ushahidi wake ni wa kutazamia?
 
Dunia inabadilika sana. Inawezekana ikatokea huyu jaji siku moja akampigia magoti huyu Mbowe. Ya Mungu mengi.
 

Attachments

  • VID-20210811-WA0028.mp4
    1.9 MB
Back
Top Bottom