Yaliyojiri katika kesi ya Freeman Mbowe: Jaji aahirisha kutoa uamuzi mpaka tarehe 17/11/2021 saa tatu asubuhi

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,813
4,544
Salaam Wakuu,

Leo tarehe 16/11/2021 kesi ya Mwenyekiti wa CHEDEMA Freeman Mbowe inaendelea.

Kujua jana kesi ilipoishia, soma: Yaliyojiri kesi ya Freeman Mbowe na wenzake Nov 15,2021

Ungana nami katika uzi huu ili kujua kila kinachojiri Mahakamani.

1637060281571.png

UPDATES;
- Jaji ameingia Mahakamani..

- Kesi inatajwa..


Wakili wa Serikali: Robert Kidando anatambulisha Jopo la Mawakili wa Serikali..
1. Jenitreza Kitali
2. Abdallah Chavula
3. Pius Hilla
4. Nassoro Katuga
5. Esther Martin
6. Tulimanywa Majige
7. Ignasi Mwinuka

Wakili Peter Kibatala anatambulisha Jopo la Mawakili wa Utetezi..
1. Jeremiah Mtobesya
2. John Mallya
3. Seleman Matauka

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Uamuzi Mdogo

Peter Kibatala Mheshimiwa Jaji na sisi tupo tayari Kupokea Malekezo

Jaji: Jana nilihairisha shauri Jana Jioni, nikasema Nitasoma uamuzi leo... Lakini kutokana na wingi wa hoja naomba muda zaidi mpaka kesho.. Nikakamilishe kuandika uamuzi... Naomba radhi kwa hairisho hili ambalo hatukulitarajia wote..

- Mawakili wa pande zote wanasimama kukubaliana

Jaji: kama nilivyosema kwamba nahairisha shauri mpaka Kesho, UPANDE WA MASHTAKA MTAMLETA SHAHIDI ATAKAA KIZIMBANI NA ATAENDELEA KUTOA USHAHIDI Nahairisha mpaka kesho saa 3 asubuhi.

- Jaji anatoka!

Kooooooooooortiiiiiiiiii..

===

Kesi ya ugaidi inayomkabili mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu imeahirishwa hadi kesho kutokana na kutokukamilika kuandikwa uamuzi kuhusu uhalali wa shahidi wa Jamhuri anayedaiwa kupanda kizimbana akiwa na diary, simu na kalamu

Akitoa uamuzi huo leo Jumanne Novemba 16, 2021 Jaji Joachim Tiganga amesema ameshindwa kukamilisha kuandika uamuzi huo kutokana na wingi wa hoja zilizotolewa na mawakili wa pande zote.

Jana yaliibuka malumbano ya kisheria katika mahakama hiyo kuhusiana na uhalali wa shahidi kupanda kizimbani akiwa na diary, simu na kalamu.

Upande wa utetezi unadai kuwa shahidi huo alikuwa anatumia vifaa hivyo wakati akitoa ushahidi wake Ijumaa, jambo wanalosisitiza kuwa ni kinyume cha sheria na utaratibu.

Chanzo: Mwananchi
 
Salaam Wakuu,

Leo tarehe 16/11/2021 kesi ya Mwenyekiti wa CHEDEMA Freeman Mbowe inaendelea...
Hiyo link uliyoiweka ili tujuwe kesi ilipoishia jana haijitoshelezi! Ni bora usingeiweka.

Imeishia jaji alipotoka na kusema atarejea saa nane na nusu, na hailezei kama alirudi hiyo saa nane na dakika ishirini, na kwamba ni nini kilichojiri mara baada ya kurejea kwake.

Hivyo basi hakuna muendelezo, labda ungetoa summary maamuzi ya jana yaliishia wapi?

Jaji: kwa kuwa Leo tunaishia Kwenye Jambo hili basi tupumzike Kidogo. Turudi hapa Saa 8 na Dakika 20

Jaji anatoka..
 
Salaam Wakuu,

Leo tarehe 16/11/2021 kesi ya Mwenyekiti wa CHEDEMA Freeman Mbowe inaendelea...
Acheni keherehere, kama hamwezi kufanya updates mpaka mwisho heri msianzishe Uzi kabisa kama yule mwenzako wa jana
 
Shukurani ya punda ni mateke! Jamaa ameweka bando kwa pesa yake ya ngama, lakini wajumbe hamridhiki tuu! Umewai hata kusema Asante kwa hizi taarifa?!
Mkuu, wabongo wengi tuna matatizo ya akili yasababishwayo na msongo wa mawazo, sonona, umasikini na ugumu wa maisha, kunakopelekea tuishi kihasirahasira na kikichaakichaa.

Wa humu ni kuwasamehe bure tu ila viongozi au wanaotarajiwa kuwa viongozi lazima tuchukue hatua mapema.
 
Back
Top Bottom