Yaliyojiri Bungeni: Usomaji Bajeti ya Serikali 2015/16

Yaliyojiri Bungeni: Usomaji Bajeti ya Serikali 2015/16

hiyo PAYE wangefanya below 10%,mfanyakazi analipa kodi kubwa kuliko mfanyabiashara
 
Fedha zote zitakazopatikana kwenye nyongeza ya tozo zinaenda REA. Ni jambo jema sana. Hata hivyo nyongeza imekuwa kubwa mno. Serikali iangalie jinsi ya kubalance ili wananchi wa kawaida wasibebeshwe mzigo huu
 
Kwa wale waliozoea "Pororo" za maduka ya jeshi na migahawa mwisho mwaka huu wa fedha, serikali itafute utaratibu mwingine kwa walengwa,nchi wanachama wa jumuia ya Afrika Mashariki walishafunga utaratibu huo.
 
Mashirika ya uma hilooo linakuja..... gharama za matumizi kutozidi asilimia sitini, 60% ya mapato , na bakaa ( faida baada ya kodi), asilimia sabini , 70%, kurudishwa hazina.

Tozo ya mapato ghafi yaongezeka toka asilimia 10% mpaka asilimia 15%.

Viwango vya posho kutazamwa upya.
 
Biashara ya Hati Fungani kicheko kwa mabenki na wawekezaji wakubwa , serikali kukopa takribani trilioni nne na ushee ndani, biashara saafi isiyokuwa na hatirisho ( Risk-Free)!,kuliko kukimbizana na wakopaji sugu mitaani,
 
mwaka wa fedha wa 2015/2016 serikali inatarajia kukusanya mapato yenye thamani ya tsh. Tril. 22.4
Acha uongo....haina uwezo wa kukusanya kiasi hicho....hapo kuna mikopo na misaada....matonya yuko kuaga na kutembeza bakuli, kuna nchi wamemshtukia wamemfukuza asiingie
 
Bajeti ya Tanzania ni Tzshs trillion 22.4, Bajeti ya Kenya ni Tzshs trillion 47, tutafika wabongo? Idadi ya watu Tanzania ni 50 million Kenya 38 million eneo ni km za mraba Tanzania ni 945 000 kwa makadirio na Kenya ni 540,000 kwa madirio. Je unaweza kukubaliana na maneno ya waziri wa fedha kwamba Tanzania inaweza kuwa nchi ya kipato cha kati 2016/2017, huo sio muujiza? Kama deni la taifa ni zaidi ya trilioni 35 na 2016/2017 litakuwa zaidi ya trillion 41? Kama ccm itaendelea kubaki madarakani kwa miaka 5 deni litakuwa sh trilioni 65 na kwa miaka kumi litakuwa trillion zaidi ya 100. Kama PAYE imeshuka kutoka 12% - 11% na ushuru wa bei ya mafuta diesel 50%, petrol 100%, mafuta ya taa 150% hilo sio ombwe? Tuliosoma mathematics tunaiita msawazo linganifu (balanced equation). Je unapoacha kuongeza kodi ya pombe na sigara unataka watanzania tuendelee kulewa ili mtukashifu kama mlivyowakashifu watu wa Rombo? Hamjui kwamba ongezeko la kodi ya mafuta litaathiri sector zote? Hayo ni mazonge! Je shilingi ya Tanzania itaporomoka kwa kiasi gani? Je kama 40% ya bajeti ya 2014/2015 haikufikiwa kuna maendeleo yatakayofikiwa? Je hii iliyoongezeka itafikiwa? Huu sii muujiza? Ikiwa bajeti ya maendeleo (development expenditures) imepungua kutoka trillion 6 mpaka trillion 5 na ile ya matumizi ya kawaida (recurrent expenditures) imeongezeka kutoka trillion 13 mpaka trillion 16 je tutafika?Tafakari chukua hatua, nusuru taifa. Nenda kajiandikishe 25/10/2015 ndio suluhu, Shahada mkononi, nusuru Taifa."MABADILIKO NI WEWE, ANZA SASA, CHUKUA HATUA"Imeandikwa na JUVENAL SHIRIMA D. (BSc. LMV ARDHI UNIVERSITY) (Mwanamabadiliko)
 
speed inatosha sana.kama mwaka 2010 umeme vijijini ilikua 17% leo miaka mitano baadae ni 34%,hebu rudi nyuma hadi 2005 utajaji kama haikua hata 5%.

then rudi nyuma 1995 utakuta ilikua 0.5%.
kwa miaka kumi speed kubwa munoo

Sasa umeme vijijini ndugu halafu hauwaki ndo nini
 
hii bajeti ya serikali ya ccm haina jipya kwani kupanda bei ya mafuta ndo wameharibu kila kwani nauli za magari zitapanda ,vyakula ,vitapanda kutokana na usafirishaji .hii ndo bajeti ya mwisho kwa utawala wa ccm .
 
Unaongeza kodi kwa petrol then unashusha PAYE unasema umemsaidia mwananchi kweli si Ile idea ya bulicheka kuhamisha bahari katk kidimbwi...
 
Sasa umeme vijijini ndugu halafu hauwaki ndo nini

Hawa ccm ni wasanii kama huku kwetu wameleta nguzo tuu sijui hizo nguzo wanafikiri zitawaka zenyewe.
 
Hawa ccm ni wasanii kama huku kwetu wameleta nguzo tuu sijui hizo nguzo wanafikiri zitawaka zenyewe.

Zipo sehemu nyingi nguzo zinaangushwa hata mashimo hawachimbi Mpaka miaka na miaka nguzo zimelala chini,hii serikali ya ccm isiongee mafanikio yoyote kwenye sekta ya umeme
 
mbona serikali waseme mradi umeshakamilika au wametudanganya .

Kwani serikali imeanza kudanganya leo, waulize plant za gas zinaendeleaje uko msimbati? wazungu wanafanya mpaka matambiko, hali teteee
 
Back
Top Bottom