Yahusu kufuta kauli

Nusu ya wabunge ni wapumbavu.....! Nafuta kauli nusu ya wabunge sio wapumbavu
nusu ya wabunge sio wapumbavu na nusu ya wabunge ni wapumbavu ni kauli ile ile tu.......isipokua tu sa hv kawataja wale nusu wasio wapumbavu kaachana na hawa nusu wapumbavu
 
Sio vzr kuwasema wenzenu .
Waacheni wale keki ya taifa kwa raha zao
Hivi mnadhani tunajilipaje pushap zetu na tunarudije feri 2020?
 
Tatizo lako Mshana Jr ndugu yangu unajua kila kitu ukianzia ulozi hadi uhasibu. Tofautisha masuala ya fraud (wizi, kutoonekana) na udhaifu wa mfumo simamizi (control weaknesses) ambayo hii ya pili ukija kwenye uhakiki kitu utakikuta ila hakijashughulikiwa katika utaratibu au mfumo unaosimamia kiasi kwamba udhaifu huo unaweza kuleta ubadhilifu.

Haya ni masuala ya kihasibu na ukaguzi wa vitabu vya uhasibu, utawala, na mfumo wa usimamiz wa shughuli za kihasibu.
Hizo 'control weaknesses' unazozieleza ni mawazo yako au ya CAG?
Zimeripotiwa kwenye ripoti kuwa 1.5t imehusika nayo??

Hivi sasa tumeingia katika mtego wa kubashiri, kila mtu anabashiri la kwake (with a benefit of doubt).
Lakini je tuko sahihi kuwasemea wengine??

Na hii tabia inakua..hivi karibuni mara tu baada za hotuba za JPM utasikia watu Rais alimaanisha hivi? Ndo alikuambia utufafanulie? Je mawazo yako ndio yake? Yeye mwenyewe alimaaanisha nini?

Tusiifafanulie serikali majibu kwa tasfiri zetu binafsi.
 
Mfumo uliotumika ulibadilika... Zamani tulikua tunatumia elimination method, kwa sasa tumebadilisha, tunatumia substitution ili kuleta ufanisi zaidi..
Ndiyo maana Majibu ya siieijii yanatofautiana na haya ya kwetu.
 
200 bil zimeenda zanzibar
Zilizobaki chukua karukureta ndugu
Huu utaratibu wa kuwakusanyia Zanzibar mapato umeanza mwaka 2016/2017? Miaka yote nani alikuwa anawakusanyia hapa Tanzania bara? Vyanzo vya mapato vya Znz vilivyopo bara ni vipi? Kwanini walipohojiwa na CAG hawakutoa vielelezo vyoyote hadi kawaumbua kwenye ripoti?
 
"Nusu ya wabunge wote humu ni wapumbavu" kisha akakanusha "Nusu ya wabunge wote humu si wapumbavu". haichekeshi lakini lazime ucheke kidogo. Kwamba pesa labda zimejenga madaraja , lakini hazikupitia bungeni kibajeti kupata idhini ya bunge kama sheria inavyoongoza. Uhalali uko wapi? Ikitokea miradi imechakachuliwa bunge litamuhoji nani? Kuna jambo, tena si dogo
Na hv siku hz mkandarasi mkuu wa miradi ya govt ni ya vichaa construction mzigo utakuwa unapita juu kwa juu
 
"Nusu ya wabunge wote humu ni wapumbavu" kisha akakanusha "Nusu ya wabunge wote humu si wapumbavu". haichekeshi lakini lazime ucheke kidogo. Kwamba pesa labda zimejenga madaraja , lakini hazikupitia bungeni kibajeti kupata idhini ya bunge kama sheria inavyoongoza. Uhalali uko wapi? Ikitokea miradi imechakachuliwa bunge litamuhoji nani? Kuna jambo, tena si dogo
Kwa mtazamo wangu kama hajakanusha vile maana nusu ni wapumbavu na nusu si wapumbavu nikama kasisitiza tu
 
Huu utaratibu wa kuwakusanyia Zanzibar mapato umeanza mwaka 2016/2017? Miaka yote nani alikuwa anawakusanyia hapa Tanzania bara? Vyanzo vya mapato vya Znz vilivyopo bara ni vipi? Kwanini walipohojiwa na CAG hawakutoa vielelezo vyoyote hadi kawaumbua kwenye ripoti?

Chanzo cha mapato kinachojulikana ni PAYE

Ambacho hakizidi 35 bilion kwa wakati huu
 
Back
Top Bottom