Wazee wa kichaga wamtaka Dkt. Kimei kuomba radhi na kufuta kauli yake

Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
4,077
10,376
Mbunge wa jimbo la Vunjo Dk Charles Kimei amekalia kuti kavu kutokana na kauli yake yenye ukweli usiotia shaka aliyoitoa bungeni kuwa wachaga wanapenda biashara ya magendo na kukwepa kodi.

Kutokana na kauli hiyo wazee wa kichaga wameichukulia kama ni dharau na kejeli kwa wachaga wote na wamemtaka atoke hadharani kuomba radhi na kuifuta kauli hiyo kwenye kumbukumbu za bunge.

========

Kauli ya Mbunge wa Vunjo, Dk Charles Kimei kuwa Wachaga wanapenda biashara ya magendo inakiibua kikundi cha wazee jimboni humo na kutoa tamko kali dhidi yake.

Katika tamko hilo, wazee hao wa Kichaga wamelaani kauli hiyo na kwamba wanachukulia kauli hiyo kama matusi kwao na kumtaka Dk Kimei ajitokeza hadharani na kufuta kauli hiyo katika kumbukumbu rasmi za Bunge.

Mbali hilo, wazee hao wameitaka CCM itafakari juu ya kauli hiyo na kumchukulia hatua za kinidhamu mbunge huyo wakidai kuruhusu kauli hizo ni kutawafanya watilie shaka umakini katika kuwapata viongozi.

Hata hivyo, Dk Kimei alipotafutwa alipatikana kwa njia ya Whatsapp hakutaka kuzungumzia suala hilo.

“Una matatizo wewe na mimi?” alihoji Dk Kimei. Alipoelezwa umuhimu wa yeye kueleza upande wake alijibu kwa kifupi, “achana nao” na aliposisitiziwa akasejibu “achana nami”.

Kauli iliyoleta mtafaruku

Kauli iliyoleta mtafaruku Dk Kimei aliitoa bungeni wiki mbili zilizopita wakati akiuliza swali la nyongeza katika Wizara ya Mambo ya Ndani.

“Jimbo la Vunjo mheshimiwa spika ni jimbo lililo mpakani na majimbo yaliyo mpakani yanakuwa na changamoto tofauti kidogo. Kwa mfano magendo unajua Wachaga wanavyopenda magendo,” alisema Dk Kimei alipokuwa akiuliza swali.

“...la pili kule Vunjo unywaji wa gongo, ulaji mirungi, bangi na dawa za kulevya umekithiri kwa sababu watu wengi hawana ajira...nataka tuombe wizara iweze kutueleza inachukua mikakati gani,” alisema.

Wazee wamshukia

Kutokana na maelezo hayo katika swali, kundi la wazee wa Kichaga limeibuka likieleza kusikitishwa na kushtushwa na kauli hiyo na kumtaka mbunge huyo kujitokeza hadharani kuifuta na kuomba radhi.

Mbali na kauli ya “wachaga kupenda magendo”, wazee hao pia walilaani kauli ya mbunge huyo kuwa vunjo unywaji wa gongo, ulaji wa mirungi na matumizi ya dawa za kulevya vimekithiri.

Akizungumza mjini Moshi, mmoja wa wazee hao, Raymond Mushi ambaye alijitambulisha kama mwenyekiti wa wazee wa kabila la Wachaga, alisema kauli hiyo imewatafakarisha na kuwafanya wajiulize maswali mengi.

“Kauli hizi zimetupa mashaka dhidi ya umakini wake na kujiuliza yeye si sehemu ya Wachaga? Angewezaje kututhibitishia kuwa Wachaga tunapenda magendo?” alihoji Mushi aliyeambatana na wazee wengine wanne, wakisema wanawakilisha Wachaga.

“Magendo ni kinyume cha sheria za nchi anaweza kuthibitisha kauli hizo mbele ya vyombo vya dola na sheria?” Sisi kama wazee, kauli hizi zilitushtua sana lakini tulijipa muda tukiamini kwamba angetoa kauli za kutengua kauli hizo”

“Kwa mantiki hiyo kwa niaba ya wazee wote uchagani na jamii ya Wachaga wote, tunalaani vikali kauli hizo na kwamba sisi kama wahusika wa kabila alilolitaja, tunachukulia kauli hizi ni matusi dhidi yetu na kashfa kwetu,” alisisitiza.

Kuhusu unywaji wa gongo, matumizi ya mirungi na dawa za kulevya alisema hiyo si sifa ya jimbo hilo.

CCM Kilimanjaro nao watia neno

Hata hivyo, Katibu wa CCM mkoa Kilimanjaro, Jonathan Mabhiya alipoulizwa, alisema CCM inaheshimu utawala wa sheria ambao umeweka mihimili mitatu ya dola.

“Mimi kama katibu naona sitakuwa nimemtendea haki Dk Kimei kumjadili kutokana na kauli alizozizungumza kwenye moja ya mihimili ya dola.

Chanzo: Mwananchi
 

cariha

JF-Expert Member
Apr 9, 2015
20,698
41,382
Dah nilikuwa najuaga kimei ana akili kumbe hamnazo kiasi hicho, Yani anajizalilisha mwenyewe kama mchaga hafu watu walikuwa Wana mtaja eti Waziri wa fedha naye akajiona ana akili kumbe hamnazo
 

magu2016

JF-Expert Member
Oct 8, 2017
7,354
5,793
Dah nilikuwa najuaga kimei ana akili kumbe hamnazo kiasi hicho, Yani anajizalilisha mwenyewe kama mchaga hafu watu walikuwa Wana mtaja eti Waziri wa fedha naye akajiona ana akili kumbe hamnazo
Jibu hoja yake. Wachaga wanapenda magendo yaani ni wezi. Mimi nawajua kwa kuwa nimeoa dada yao alichosema Dr. KIMEI ni sawa kabisa.
 

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
19,618
33,772
Ni kweli alichosema. Niliishi Machame watu wengi wanaiba umeme wa Tanesco. Wamwjiunganishia kiwiziwizi karibu nusu ya kijiji
Mimi naishi Rombo.

Mpaka huko Vunjo nafika.

Alichokisema Kimei ndio ukweli na uhalisia na wao wanajua.

Kama huku Rombo vitu vingi vinavyotumika huku ni kutoka Kenya na ni kwa njia ya magendo.

Mafuta ya kula tu, yanatoka Kenya tena wanayaweka kwenye vikopo vidogo vidogo kukwepa TRA.

 
6 Reactions
Reply
Top Bottom