Lazima nikuoe wewe binti.Mmmhh! Muku
Mkuu,yaani hata siamini kama ni mimi na akili zangu timamu niliandika upupu huo,anyway ni pepo baya liliniingia bro.KARANJA 007 by then
KARANJA 007 usijali kabisa life gas so much to shareMkuu,yaani hata siamini kama ni mimi na akili zangu timamu niliandika upupu huo,anyway ni pepo baya liliniingia bro.
Mkuu,mimi nimezaliwa usukumani ndani kabisa(Ntuzu),na hiyo MUKU naifahamu sana,na nimeshuhudia vikongwe vikifanyiwa hilo zoezi la kuezua paa moja wapo la majani au lolote ili kikongwe akate roho haraka maana anateseka na roho haitoki,basi wanafanya hivyo na kweli kikongwe anafariki muda huo huo,sasa najishangaa ilikuwaje nikafanya madudu kupinga Mkuu.
Thanks bro,bravo kwa uungwana ubarikiwe.KARANJA 007 usijali kabisa life gas so much to share
Tuachane na yaliyopita tu focus yaliyopo na yajayo hili ndio la muhimu leo tupo hai tunapost na kureply JF, kesho hatupo lakini maandishi yapo hayafutiki yatadumu kadiri ya dunia itakavyodumu...kwa maana nyingine mileleMkuu,mimi nimezaliwa usukumani ndani kabisa(Ntuzu),na hiyo MUKU naifahamu sana,na nimeshuhudia vikongwe vikifanyiwa hilo zoezi la kuezua paa moja wapo la majani au lolote ili kikongwe akate roho haraka maana anateseka na roho haitoki,basi wanafanya hivyo na kweli kikongwe anafariki muda huo huo,sasa najishangaa ilikuwaje nikafanya madudu kupinga Mkuu.
Mkuu,hapo ndio nakupa hongera kwa roho yako ya kiungwana kabisa,ingekuwa mtu mungine mpaka leo ningepokea kashfa kila siku,lakini kwako napata nasaha na hekima ambayo na mimi inanijenga ndugu yangu.Tuachane na yaliyopita tu focus yaliyopo na yajayo hili ndio la muhimu leo tupo hai tunapost na kureply JF, kesho hatupo lakini maandishi yapo hayafutiki yatadumu kadiri ya dunia itakavyodumu...kwa maana nyingine milele
Nipo chumbageni,mwambie mtaalam aje bas tufanye mambo y MUKU,na upande ule wa mambo yetu ukoje,maan ndio nautaka haswa,maaan mtu akifuata buku kumi nyumbani mpka aone kero kuchukuaMuku hauhitaji professionalism sana sana hatapigwa kwa TKO kwakuwa ule ni ugomvi wa kusukwa
mshana jr test ya muku haiishii kwenye majambia tu,; ni visu, nyembe, sindano, misumari na risasi ya ukweli ukweli lazima idufue mwili wako tena inalengwa kifuani!
Hutakiwi kuwa muoga siku ya kuchanjwa na kwenye tukio la test vinginevyo ukitestiwa inaingia mazima na risasi itakuuwa!!
Huko kigoma hii kitu inaitwa "VIDONO"
Na wakaguru wanaipata kwa mtemi wao anaitwa "JENGA" inapatikana wilaya ya Gairo kijiji cha Idibo- hakatizi maasai hapo kijijini na ikitokea kakatiza huchinjwa kama kuku na jeshi kuu la "MWANO"
Kule kanda ya ziwa inaitwa "BHULABHUKA"
Ilishawahi kututesa hii kitu mwaka juzi bibi alipofikia kufa ktk umri wake wa miaka 100+ alitusubirisha mpaka wiki mbili hafi huku mwili ukiwa umeoza ila bado angali anapumua!!!
Mwishoni alikuja mdogo wake akaamuru tutoboe juu ya paa na mwiba wa nungunungu!!!
Dunia ina maajabu acha kabisa!!

Mkuu mi sijawahi kufa hivyo naweza nisielewe, hivi mauti yanapomfika mtu kuna ugumu pia? Unapimaje ugumu na uraisi wa kifo cha mtu?Hili neno laweza kuwa na tafsiri nyingine kwa wengine lakini kwa watu wa Tanga lina maana yake muhimu ya ugumu ujasiri na roho ngumu![]()
Hili nililishuhudia huko Lushoto kwa watu kadhaa waliochanjiwa muku ni wagumu kuugua kuumia na kiboko ya yote kufa aliyechanjiwa muku ni mtu mwenye roho ngumu hasa akikamatwa kwa mfano kwenye tukio la ujambazi au wizi na wananchi wenye hasira kali wanaweza kumpiga mpaka wakadhani wameua lakini siku inayofuta akakutwa bado anapumua.
Muku ni mzuri Unapokuwa hai lakini ni kitu kibaya kabisa unapokaribia kuachana na dunia hii kwa maana ya kifo...watu waliochanjiwa muku hufa kwa mateso makubwa sana kutokana na madawa aliyokunywa na kufanyiwa...akifanikiwa kufa mapema basi si chini ya siku tatu na hata akipata ajali mbaya kabisa au hata kuchomwa moto au kukatwa shingo mwili wake huchukua muda mrefu mno kupo.
Ninafahamu wengi wanapenda ujasiri na kuwa na kinga ya muku lakini kumbuka mateso siku roho yako ikitaka kuachana na mwili wako
Ukiweza kafanye lakini madhara yake ndio hayo
Kwahiyo huo muda ndio ugumu uliouongelea mkuu? Mi nilidhani uhai kutoka ndio kifo, na kwa namna yoyote utakavyokufa unakuwa umekufa. Au unaongelea muda wa kuugua hadi kufa?Kwenye kukata roho... Inachukua muda sana kuachana na mwili
Kuugua hadi kufa ni jambo la kwanza lakini jambo la pili ni kile kitu kinaitwa HARI ZA KIFO... ndio namaanisha hapaKwahiyo huo muda ndio ugumu uliouongelea mkuu? Mi nilidhani uhai kutoka ndio kifo, na kwa namna yoyote utakavyokufa unakuwa umekufa. Au unaongelea muda wa kuugua hadi kufa?