Mzee Mwanakijiji,
Mkuu bado unakwepa swali uloulizwa wewe. Unataka Chadema wafanye nini?.. maanake yaonyesha wewe unauliza swali ukiwa na jibu tayari kichwani. Chadema wameeleza itikadi yao sera zao ilani zao bado kitu gani haswa ambacho wewe kinakukwaza? Je hukubaliani na itikadi zao kama ndivyo nakumbuka ulishindwa kutueleza kule ktk mada iliyopita kuhusiana na sera za Chadema wapi unapingana nao pamoja na kwamba niliposoma sera za CCJ walichotofautiana zaidi ni kimaandishi tu.
Pili sidhani kama hao CCJ wengine waliojiunga na Chadema ni wajinga kiasi hicho, hawakutazama mapungufu uloyaona, wao wakaenda kukaa na viongozi wa Chadema wakjayaweza wazi maswala yao hadi imefikia wao kujiunga.Huu ndio ustraabu lakini kuja hapa JF ukaendelea kuuliza kitu ambacho hakieleweki ati Then What?
Kisha umetoa mfano wa KANU na Coalition, sijui kama unajua kwamba hata hiyo Kanu yenyewe ilikuwa coalition ya vyama vitatu kama tunavyoizungumza CCM leo hii. Kanu ilitokana na vyama vitatu - chama cha Jomo Kenyatta - KAU,Tom Mboya - NPCP na Oginga Odinga -KIM hawa ndio waliungana pamoja ku form KANU na kama unakumbuka vizuri..CCM pia haina tofauti toka TANU hadi CCM yenyewe ni coalition zilizowezesha umoja wa jumuiya zetu kutokana na WATU na MAZINGIRA tulokuwa nayo.
Huwezi kutumia mifano ya US ya kiitikadi kujenga UMOJA katika nchi ambayo wewe mwenyewe unakubali hakuna haki. Nitarudia kusema tazama South ANC na PAC hawa wote walikuwa na itikadi tofauti lakini ilipofikia swala la kumwondoa mkoloni na Apartheid that became priority number one..Tazama Zimbabwe, Zambia yenyewe wakati wa Kaunda mbinu zilizotumika ni sawa na hizi tunazotangaza hapa leo hii..
Mkuu wangu huwezi kuvuta umati wa kiafrika kwa kutumia itikadi isipokuwa kwa kumwondoa adui aliyepo madarakani na zipo nchi nyingi sana zimefanikiwa ikiwa unataka kutumia mifano kama hii.. South Afrika chini ya Mandela ni mfano mmoja mkubwa sana wa mafanikio ambao dunia nzima wanawapongeza hivyo hata hao Yankees walijiunga state hadi state kupambana na ukoloni wa Malkia wasijue itikadi gani wataitumia kutawala lakini baada ya kumwondoa Malkia ndipo fikra za itikadi zinakuja...
What next? haina mwisho mkuu wangu na kwahakika naweza kujibu kuwa -Tutahakikisha Mafisadi wanafikishwa mbele ya sheria na ukaendelea kuuliza what next?.. nikajibu Tutarudisha uhuru na haki mikononi mwa wananchi - what next? hivyo hivyo tukajaza kurasa na kurasa za maswali ya kufikirika kuandika hadithi ndefu kwa mkono wa Binadamu..
It's ONLY God knows mambo ya What next itazaa kitu gani, sisi tunapanga tunayoyaweza leo kulingana na mazingira tuliyopo. Hatuwezi panda mbegu zetu kwenye jiwe tukitegemea mavuno bora wala hatuwezi panda mahindi tukitegemea kuvuna mpunga sisi hatuko huko kabisa...isipokuwa tunachozungumza hapa ni kupata kwanza hati milki ya ardhi ambayo itatumika kwa kilimo. Kilimo ambacho kila mmoja wetu anakubali kwamba ndio uti wa mgongo wa uchumi wetu hayo ya kulima mpunga, mahindi au chochote unachofikiria wewe yatajulikana mbele ya meza kuu baada ya kupata haki miliki ya ardhi..
Hizo then what - tutalima kinachoweza kustawi - then what, then what - then what.. yoote itakuwa ktk historia ya nchi kama vile historia ya maisha yako ulitaka kuja Marekani -then what? - umefika US - then what?. haya maswali kweli tutafika!.
Leo hii hatuna hata kiwanja mkuu wangu unataka tufikirie kujenga maghorofa!