Yafuatayo ni majibu Mujarab ( Sahihi ) ya Ali Mayai wa BMT kwa wanaohusisha Rangi za Mkapa Stadium na Ushoga ( LGBTQ )

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,573
108,929
"Walioliibua hili ( GENTAMYCINE nawataja kuwa ni wana Yanga SC ) wana Uelewa mdogo mno wa Mambo. Rangi zote zilizopo zinawakilisha Uafrika Wetu pamoja na Rasilimali zinazopatikana na ukiangalia Kiumakini katika Rangi hizi utaona nyingi ziko hata katika Bendera yetu ya Tanzania ambao tumepewa Heshima ya Uenyeji na Ufunguzi wa Mashindano haya mapya zikiwakilisha Uhalisia wa Mtanzania na Tanzania kama nchi"

"Nikisema walioliibua hili ( GENTAMYCINE nawataja ni wana Yanga SC tu ) wana Uelewa mdogo wa Mambo ni kwamba Total Energy ambao ndiyo Wadhamini Wakuu wa Mashindano ya AFCON, CHAN na hata CAFCC, CAFCL na hata hili Jipya la AFL wanatumia Rangi hizi hizi zilizopo hapa mbona hatuoni wakisema Vilabu vyao vitoke au vijitoe huko? au mbona Timu zetu za Taifa zinashiriki na hawatuambii Serikali tuzitoe huko Mashindanoni?"

"Watu wajikite zaidi kutafuta Maarifa ( GENTAMYCINE nakuhakikishia Ali Mayai Tembele siyo kwa wana Yanga SC ) kwani kama Mdhamini Mkuu wa hili Shindano Jipya la AFL ni nchi ya Saudi Arabia ambayo Wanapinga sana Vitendo vya Ushoga ( LGBTQ ) na hata katika Michuano ya Kombe la Dunia mwaka Jana waliizuia Ndege ya Ujerumani iliyokuwa na Rangi pamoja na Bendera zinazounga mkono Ushoga na haikutua Kweli leo hii wanaweza Kweli kuruhusu Uchafu huu wa Kimaadili ufanyike katika Shindano Kubwa, Jipya na la Kitajiri ambalo Wao ndiyo Wadhamini Wakuu?"

Nukuu zote hizi GENTAMYCINE nimezitoa kwa Kumsikia Kaimu Mkurugenzi wa Michezo ( BMT ) Ali Mayai Tembele ( ambaye si ni mwana Yanga SC lia lia bali pia ni Mwanachama na ameshaichezea Timu hiyo na kuwa Nahodha wake alipokuwa Akihojiwa na Mtangazaji wa EFM Radio Israeli Mwakyeja Lugano jana ( Jumanne ) ndani ya Uwanja wa Benjamin Mkapa Temeke Dar es Salaam Tanzania.

Kudadadeki hampo na mnaumia tu.
 
Kawapa ukweli...acheni upuuzi...basi mjitoe club bingwa maana ndo rangi zake...ushoga uko akilini kwa mtu anaewaza 24/7 ushoga...
Ila wewe Tate Mkuu sidhani kama una hizo akili...
Mna sababu za msingi za kuihusisha Yanga/mashabiki wa Yanga na upingaji wa hizo rangi?

Je, kuna tamko lolote lile rasmi la Klabu ya Yanga, viongozi wake, mashabiki wake; kuzihusisha hizo rangi na ushoga kama huyu ndugu yenu Popoma anavyotaka kupotosha?
 
Mna sababu za msingi za kuihusisha Yanga/mashabiki wa Yanga na upingaji wa hizo rangi?

Je, kuna tamko lolote lile rasmi la Klabu ya Yanga, viongozi wake, mashabiki wake; kuzihusisha hizo rangi na ushoga kama huyu ndugu yenu Popoma anavyotaka kupotosha?
Mi nachojua mashabiki wa Yanga wale wasiokua na akili ndo wanaoshabikia mitandaoni...
 
Kama hawa Mazembe hawataki kushiriki hii nafasi yao wapewe Yanga maana mayowe,matusi,kejeli na manung'uniko kila kona ya nchi yamezidi kwa wao kutoshirikishwa.
FB_IMG_1697623683508.jpg
 
Back
Top Bottom