Yafuatayo hunitokea mara baada ya kunywa pombe

Mpyena

JF-Expert Member
Apr 3, 2015
904
1,083
Wakuu poleni na majukumu ya kulijenga taifa letu pendwa la Tanzania. Pia poleni sana na mfumko wa bei uliopo nchini na dunia ni kwa ujumla.

Ndugu zangu wana JF, mimi ni mtumiaji wa masanga(pombe) japo mara chache chache. Na siku ambayo hutumia kinywaji hiki huwa ni Jumamosi kwa maana ya kwamba ndiyo siku ambayo nakuwa mapumziko.

Na pombe nazokunywa ni hizi hizi bia za kawaida yaani za watu wenye uchumi wa kati (Kilimanjaro, Serengeti, Castle) na wakati mwingine napiga hizi ngumu nyeupe.

Baada ya kunywa balaa huwa ni kesho yake napatwa na:
1. Huzuni
2. Simanzi
3. Wasiwasi
4. Kutojiamini
5. Majuto ( kujiona mkosefu)
6. Majonzi
7. Pia nakuwa mwingi wa huruma.
Kwa wataalam naombeni mawazo yenu yote hayo husababishwa na nini?

Maana kwa kuhofia kupatwa na niliyoyaeleza hapo juu, najikuta naogopa kutumia pombe tena

20210104_143709.jpg
 
Haya mambo huwa yanaenda kiukoo kama kwenye ukoo hakuna historia ya mtu yeyote kunywa pombe au kuvuta bangi utakapotumia jiandae kudhalilika kwa sababu umetumia vitu ambavyo kwenye ukoo wenu havipo. Mimi ile Konyagi kubwa napiga nusu na bado natembea vizuri na siyumbi. Zile ambiance nagonga vichupa vitatu ndio kidoogo naweza kuzima wakati kuna wengine akinywa nusu tu anaanza kuongea pumba tu.
 
Tafuta pombe inayokufaa na usipende kuchanganya, kuna watu wakinywa dompo hawalali wanaota kukabwa ila wakinywa vant hata mizinga mitano fresh tu, chagua unayokufaa uendelee kumwagilia moyo.

Ila ukumbuke kunywa kwa kiasi na ukiona huelewielewi mshukuru Muumba achana nayo itakuja kukupa matatizo. Kila mtu na starehe yake
 
Tafuta pombe inayokufaa na usipende kuchanganya, kuna watu wakinywa dompo hawalali wanaota kukabwa ila wakinywa vant hata mizinga mitano fresh tu,chagua unayokufaa uendelee kumwagilia moyo.
Ila ukumbuke kunywa kwa kiasi na ukiona huelew elew mshukuru Muumba achana nayo itakuja kukupa matatizo. Kila mtu na starehe yake
Ni kweli mkuu kila mtu na starehe yake
Mfano mimi naenjoy sana kupiga chabo na nyeto
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom