WanaJF,
Jeshi la polisi hapa Tanzania linaongozwa na nani ?
Wakuu wa mikoa ? wakuu wa wilaya ? au wakuu na maofisa wa jeshi hili ?
Wamepata mafunzo wapi? Kivukoni? Au vyuo vya Polisi?
Kazi ya jeshi la polisi ni nini ? Kubambikia raia kesi ? Kulinda usalama wao na mali zao?
Je chombo hichi ni cha umma au ni miliki ya chama fulani cha siasa ?
Mimi sijawahi kusikia hata siku moja kuwa imetokea mkutano wa Chama Cha Mapinduzi kimezuiliwa kufanya mkutano, au « hakikupewa kibali ».
Je wewe msomaji unakumbukumbu ya CCM kuzuiliwa wasifanye mkutano ? Au kutokupewa kibali cha mkutano ?
Hili la kibali ,ni dhana potofu, any way, Chama cha siasa hakiombi kibali cha kufanya mkutano, bali wanatakiwa kutoa taarifa in advance, ili polisi iweze kujiandaa kulinda usalama katika mkutano.
Sasa nikuulize wewe msomaji. Mara ngapi umeshasikia kuwa mkutano wa CHADEMA, NCCR, CUF umezuiliwa au haujapewa kibali ?
Hutokea vyama ambavyo vilikwishatoa taarifa ya kufanya mkutano na kuambiwa kuwa polisi haina askari wa kutosha kulinda tukio siku hiyo. Lakini inapotokea Chama hicho kikisema « sisi tutafanya mkutano wetu hivyo hivyo »
Utashangaa ! Polisi hii iliyosema haina askari wa kutosha kulinda mkutando, huanza mapema kufunga barabara zinazoelekea sehemu ya tukio. Polisi hii hii inaazima askari kutoka sehemu za jirani kuhakikisha wana askari wa kutosha kuzuia mkutano usifanyike lakini hawana askari wachache wa kulinda mkutano.
Je Polisi wana maelezo ya kutosheleza kueleza ni kwa nini ni mikutano ya vyama vya upinzani tu ndio wao huwa hawana askari wa kulinda tukio ?
Ni kwa nini mara nyingi « hawatoi kibali » cha mkutano kwa vyama vya upinzani ?
Je Polisi yetu inafanya kazi kwa msukumo wa kisiasa ?
Kama ni hivyo, Tendwa ana nafasi ipi katika kuuondoa uoza huu ?