Ya Polisi na vyama vya siasa Tanzania

Ya Polisi na vyama vya siasa Tanzania

nna masisikitiko makubwa sana kwa yaliotokea na ambayo yanaendelea kutokea Arusha kwa sasa.

haya yote yasingetokea kama viongozi wa chadema wangeweka mbele maslahi ya Umma na wanachama wao. Ungangari si sera ya Chadema lakini sijui ilikuwaje ikarithi sera hii mbovu


wao wameruhusiwa kufanya mkutano, na wameambiwa wasifanye mandamano iko simple wao walikuwa wafanye huo mkutano, na kama kweli walikuwa na mazito ya kuyasema wangeyasema na ujumbe ukafika bila ya kutokea yaliyotokea.

baada ya kikao ingekuwa kazi ya viongozi kufuatilia kwa nn kibali chao kufutwa, na hii ingekuwa ni vita kati ya Viongozi wa chama na Uongozi wa polisi.


lakini ukiangalia kwa kina utagundua kuwa ni kweli aliyoyasema Rais kuwa ajenda si kufikisha ujumbe bali wanaamini kwa kutumia strategies kama hizi ndio kitawasaidia chama chao kusikika nje ya nchi.


ni ufinyu wa mawazo na masikitiko kwa wanachama ambao kwa bahati mbaya wanapelekeshwa na viongozi hawa wasiowatakia mema bila ya kutafakari


nnaamini ndani ya chadema kuna viongozi ambao hawakuliunga mkono hili, na tutajua baadae kuwa ni Mbowe na Slaa tu

Acha porojo zisizo na maana kma huna cha kuongea kwa nini uanzishe thread.
Unajaribu kuainisha wazo lilinje ya uwezo wako wa kufikiri unaishia kuchekesha.
 
Ikithibitika kuwa umeathirika kwa HIV Serikali inahaki kabisa ya kuzuia ngono kati yenu ili kuepusha kumuathiri mwenzako ambae bado hajaathirika!!!!!

Siyo kweli mnapewa ushauri nasaha wa jinsi ya kuishi pamoja bila kuambukizana na ziko njia salama za kufanya mapenzi bila kuambukizana, vivyo hivyo nayo serekali ingeangalia jinsi ya kusimamia maandamano hayo ili hizo tetesi zao za kiintelijensia kuhusu vurugu wazizuie maana ndio kazi yao sio kuzuia maandamano, yani wao polisi wanataka kusema hawana manpower ya kusimamia maandamano ya 7km ili yasilete vurugu ila wan uwezo wa kutanda mji mzima kuzuia usiandamane, polisi wanazungumza siasa badala ya kufanya kazi yao.
 
Wewe kama sio Kichaa ni mwehu, unajua waliopigwa au hata kuuwawa ni watanzania wenzetu, Jamani put awat ur vyama and tudai haki za watanzania wenzetu, damu yao imemwagika katika ardhi ya what we claim nchi ya amani think about it as a calamity that is coming in our country
Waliandamana CUF mkawabeza. WAHUNI WALE WAVAA BUIBUI NA VIBALAGHASHIA. waliuawa watu wengi kule pemba mkazidi kubeza. Leo mnasema CUF ni CCM-B. Mlisahau historia ya mapambano na DIRA ya siasa na uzalendo wa kitaifa. Aliwahi kuvunjwa mkono Profesa wa UCHUMI mkabeza eti Profesa uchwara. SASA ONJENI SHUBIRI HIYO NA MJUE SERIKALI IPO. NGOMA IKILIA SANA MWISHOWE HUPASUKA.
Sifurahii ila nakumbushia!! viva Dr. Slaa dr wa ukweli
 
Waliokufa ni watanzania wenzetu na ndugu zetu, hao walinzi wako wanaona makosa waandamanaji wasio na silaha nguvu wala chakula, Ila hawaoni EPA, Meremeta, Downs,bei ya umeme! Acha kichaa
Mchungaji Slaa na Mbowe lazima wawe responsible kwa vifo vya wananchi wasio na hatia, kila nchi inakuwa na ulinzi usipofuata sheria lazima sheria ufuate mkondo wake.

Hakukuwa na sababu hawa wachungaji walazimishe maandamano yasiyo kuwa na dira yoyote, either wangeomba kibali na kufuata utaratibu uliokuwepo, TZ haktokuwa na mtu yoyote kuwa above the law. Mchungaji lazima aadhibiwe bila kujali
 
Siyo kweli mnapewa ushauri nasaha wa jinsi ya kuishi pamoja bila kuambukizana na ziko njia salama za kufanya mapenzi bila kuambukizana, vivyo hivyo nayo serekali ingeangalia jinsi ya kusimamia maandamano hayo ili hizo tetesi zao za kiintelijensia kuhusu vurugu wazizuie maana ndio kazi yao sio kuzuia maandamano, yani wao polisi wanataka kusema hawana manpower ya kusimamia maandamano ya 7km ili yasilete vurugu ila wan uwezo wa kutanda mji mzima kuzuia usiandamane, polisi wanazungumza siasa badala ya kufanya kazi yao.

kama yule asieathirika akikataa kufanya ngono na muathirika nae analazimisha ngono kwa nguvu then Serikali inahaki ya kumzuia huyo mgonjwa kufanya ngono kwani hapa Serikali inataka kulinda uhai wa mtu!!!
 
Moto huu wa uvunjifu wa Amani ni mipango thabiti na ya makusudi kutoka Chadema.
Chadema, kabla ya uchaguzi, wakati wa kampeni za uchaguzi, waliashiria kumwaga damu na kuanzisha vurugu pindi watapo pata fursa na sasa fursa waliokuwa wanaitafuta wameipata. Jee, ni kwa faida ya nani?

Ni kwa uchu wa madaraka wa watu wachache ambao kura kidogo sana walizopata hazikuwatosha kuingia madarakani.

Na haya yote ni shinikizo la dhati kabisa linaloanzia kanisani. Si tumeona huko Sumbawanga? Mpaka waumini wametengwa na kanisa, eti kwa sababu tu, wamewapigia kura CCM.

Chadema, leo mnadhani mnapigania haki, la hasha, hakuna haki inayopatikana itayopatikana katika uvunjifu wa amani. Na hilo ndio mlilofanya leo. Na ndilo mlilolikusudia.

Mlitangaziwa kuwa msifanye maandamano, lakini kwa makusudi kabisa mkayafanya na kuanza kuchoma moto magari, mkaanza kuiba, mkaanza kupora na mkaanza kufanya fujo bila ya sababu maalum au msingi.

Kma kweli mnadai haki, ni vipi, muibe, mpore, muwashe moto magari na mali za raia?

Serikali ichukuwe hatua kali na thabiti kabisa kudhibiti hili wimbi la fujo, la sivyo, Tanzania patakuwa hapakaliki na huu moto uliowashwa na kanisa na wafuasi wa kanisa, matokeo yake yatakuwa zaidi ya Rwanda.

Ni matumaini yangu, nguvu za dola tena za ziada, zitatumika kuwadhibiti na kuwachukulia hatua kali na zisizo na huruma viongozi wote wa Chadema na washabiki wao wachache wanaoanzisha vurumai hapa nchini.

Wa Tanzania tunaopenda amani na kuitakia mema Tanzania tulaani kwa nguvu zetu zote hivi vitendo vya Chadema wakisaidiwa na makanisa.
 
Ndugu wananchi tuache jazba na hamaki!! damu ya watanzania wenzetu Polisi na Raia imemwagika!!! wakati huu si wakati wa kuchochea chuki na kuropoka kila kinachotoka mdomoni matokeo yake ni kupalilia chuki na kuzidisha machafuko huku wanaoathirika ni binaadamu wezetu!!

Huu ni wakati wa kutuliza bongo na kupunguza hamasa ili hasira za wananchi zisizidi mipaka na tuiombee nchi yetu Amani kwani hakuna kitu muhimu zaidi kwa sasa kuliko utulivu! tukizidi kuchochea chuki na hasira ndugu zangu tutajikuta tunaingia ktk kapu waliloingia majirani wenzetu wa Kenya, Rwanda, Burundi, Somalia nk!!!

Hasa JF great thinkers nawaomba tuache JAZBA na Katu tusichochee moto! wengi wa JF hawako Bongo wako Ulaya na Marekani! kauli zenu zitasababisha machafuko ya kisiasa na mwisho wake ni mbaya kwani utabadilika kuwa wa kisiasa na kuwa wa kidini na kikabila!!!

Mimi nalaani mauaji haya bila kujali alieuwawa ni Polisi au Raia lakini kwa sasa natanguliza Amani kwanza halafu sheria ije baadae!!!
 
Watanzania Tunatoa Machozi kwa Watanzania Waliopigwa Risasi na JK Kisa Uroho wa Uongozi na Kutaka Kuwatetea Mafisadi. Mashujaa Hawa Walikuwa Hawana Siraha Kama Siku Zote Tulivyo na Waliondoka Majumbani Kwao Jumatano Asubuhi na Kwenda Kuandamana Kuunga Mkono na Kuwawakilisha Watanzania Wote Nchini. Sababu za Maandamano ni Hizi Kupinga Wizi wa Kura Nchi Nzima na Hasa Maamuzi ya JK Kuwalipa Dowans. Jk Akamtuma Mwema Apeleke Polisi Wengi Kuzuia Hatari ya Amani. JK Anaamweleza Mwema Kwamba Chadema Inahatarisha Amani? Hivi Nani Anashikiria Siraha na Risasi? Historia ya Tanzania Tunaona Hakuna Watanzania Hata Mara Moja Wanaopenda Kuchafua Amani Zaidi Kutaka Maisha Bora. Kuishi Kwetu Tanzania Kila Mtanzania Amechoshwa Kuonewa na Kutosikilizwa na Tumepiga Kelele na Tunachoka Sasa. Wananchi Tunadharauliwa Wazi Kabisa Hasa Huu Uamuzi wa Dowans wa Kuwalipa Kampuni Hewa, Watanzania ni Wajinga Kiasi Gani? Uchaguzi Wanajiwekea Tume Zao na Kura Wanaiba, Maana ya Kupiga Kura nini? Sasa Tunaona Chaguzi za Udiwani Zinaibiwa Hivi Machoni Mwetu? Hii ni Mwisho Sasa. Hizi Ndizo Sababu CCM Hawataki Wananchi Waandamane na Ndicho Kimewauwa Mashujaa Wote Jana (Tarehe 05-01-2011).
  1. Tunaomba Majina na Familia Zao Tuwape Heshima za Mashujaa Tanzania
    [*]Tunaomba Arusha Tupeni Video ya Mauwaji, Duniani Waone Uuwaji wa CCM
    [*]Wananchi Tuwape Misaada Familia za Mashujaa - Michango Jinsi Gani ya Kutoa Heshima
    [*]Wananchi Tupeleke Hili Swala "Hague na UN Human Rights" Dunia Ipate Habari Kamili ya JK
    [*]Wananchi Kote Tanzania Tunaandamana Tanzania Nzima, Tepembeza Habari kwa Kote

"Kikwete Afiki 2015 Muda wa Kuondoka Umefika. Mwizi ni Mwizi Siku Zote"
 
watu wengine bwana.. serikali ikikuambia usilale na mke wako/mume wako hutalala naye?

Watu kama wewe ndio wenye fikra finyu na mnaofurahi mkiona amani imevunjika na watu kuuwana. Fitna, chokochoko na uzabizabina umekukaa hata kwenye haya maandishi yako. Watu wankufa wewe unaleta mfano wa kulalana na mkeo? Hauna unachofikiri ila huo upuuzi tu.

Na Serikali sasa ndio mtaijuwa kuwa ina mkono mrefu.
 
Ndugu wananchi tuache jazba na hamaki!! damu ya watanzania wenzetu Polisi na Raia imemwagika!!! wakati huu si wakati wa kuchochea chuki na kuropoka kila kinachotoka mdomoni matokeo yake ni kupalilia chuki na kuzidisha machafuko huku wanaoathirika ni binaadamu wezetu!!

Huu ni wakati wa kutuliza bongo na kupunguza hamasa ili hasira za wananchi zisizidi mipaka na tuiombee nchi yetu Amani kwani hakuna kitu muhimu zaidi kwa sasa kuliko utulivu! tukizidi kuchochea chuki na hasira ndugu zangu tutajikuta tunaingia ktk kapu waliloingia majirani wenzetu wa Kenya, Rwanda, Burundi, Somalia nk!!!

Hasa JF great thinkers nawaomba tuache JAZBA na Katu tusichochee moto! wengi wa JF hawako Bongo wako Ulaya na Marekani! kauli zenu zitasababisha machafuko ya kisiasa na mwisho wake ni mbaya kwani utabadilika kuwa wa kisiasa na kuwa wa kidini na kikabila!!!

Mimi nalaani mauaji haya bila kujali alieuwawa ni Polisi au Raia lakini kwa sasa natanguliza Amani kwanza halafu sheria ije baadae!!!
Tumechoka na message yako ya kinafiki huku unajifanya unataka amani sehemu nyingine mwenyewe unachochea fu......off.
 
kama yule asieathirika akikataa kufanya ngono na muathirika nae analazimisha ngono kwa nguvu then Serikali inahaki ya kumzuia huyo mgonjwa kufanya ngono kwani hapa Serikali inataka kulinda uhai wa mtu!!!

Matokeo yake kwa kutumia nguvu zilizopitiliza hawajalinda bali wamesababisha TZ kuweka image mbaya kwenye siasa na pia uhuru na amani wa wananchi, kumbuka waliokuwepo maandamanoni hawakushikiwa bakora.
 
Ndugu zangu tusisahau kwamba hata Ivory Cost, Kenya, Sudan or anywhere were people are slaughtering each other mambo ya kijinga jinga ndio yalifikisha nchi hizo hapo zilipo.

Jeshi la polisi kama litaendelea na huu upuzi wake na ujinga usio na kichwa wala miguu basi Tanzania inaweza kuingia kwenye zile nchi ambazo watu walichinjana wenyewe kwa wenyewe. Ieleweka ya kwamba hakuna hata Mtanzania mmoja anaeyetaka kuchinja mwingine, lakini upuzi huu wa Polisi hauwezi kuvumiliwa, ujinga wa kudhania kwamba Tanzania inamilikiwa na raisi nadhani inabidi ukomeshwe.

Tunaitaji Katiba itakayo zungumzia kabisa kwamba role ya Polisi ni kulinda wananchi na mali zao, na sio kuwalinda viongozi walio madarakani.
 
Mashujaa? Ushujaa wa nini? Hao ni waporaji, vibaka na wafanya fujo. Na nna uhakika wote ni wafuasi wa kanisa fulani kama ulivyo wewe.
 
kama yule asieathirika akikataa kufanya ngono na muathirika nae analazimisha ngono kwa nguvu then Serikali inahaki ya kumzuia huyo mgonjwa kufanya ngono kwani hapa Serikali inataka kulinda uhai wa mtu!!!

Asiyeathirika akikataa ni sawa ila siyo serekali imwamulie kukataa kufanya ngono, na ndio maana yakaitwa maandamano ya amani, na wao ndio wametaka, Amref(serekali) walitakiwa kutoa ushauri nasaha sio kuwaamulia, polisi wametreat yale maandamano ya amani kama riot, yani wameyafanya yawe riot ili waweze kutimiza adhma yao, but still what people want to say will be said again and again until when they will listen.
 
Jamani kwani mtu akiandamana aka kuvunja sheria kwani lazima apewe kisago....mbona nchi zilizoendelea wanafunzi waliandamaana na kudiriki kulitupia mapipa na hata kuligusa na kutingiza gari la Prince Charles juzi hakufa mtu wala kupigwa kisago.....yaani utadhani hayo maandamano yalikuwa ya kilomita ngapi sijui.....hata huko kwneye mkutano wangefika vipi kama sio kwenda kwa vikundi au Polisi walitaka watu watue kwa helikopta hapo mkutanoni??

Hawa polisi hawajui kuna mwisho...hawaoni boss wao Lau Masha yupo ubaoni...hawaoni kina Tiba wapo ubaoni...wewe subiri...tutaanza kuzaa nao mmoja mmoja...!!
 
Mtu wa Pwani,
Sina muda wa kusoma upupu wako. All I can say is go to hell!
 
Ndugu wananchi tuache jazba na hamaki!! damu ya watanzania wenzetu Polisi na Raia imemwagika!!! wakati huu si wakati wa kuchochea chuki na kuropoka kila kinachotoka mdomoni matokeo yake ni kupalilia chuki na kuzidisha machafuko huku wanaoathirika ni binaadamu wezetu!!

Huu ni wakati wa kutuliza bongo na kupunguza hamasa ili hasira za wananchi zisizidi mipaka na tuiombee nchi yetu Amani kwani hakuna kitu muhimu zaidi kwa sasa kuliko utulivu! tukizidi kuchochea chuki na hasira ndugu zangu tutajikuta tunaingia ktk kapu waliloingia majirani wenzetu wa Kenya, Rwanda, Burundi, Somalia nk!!!

Hasa JF great thinkers nawaomba tuache JAZBA na Katu tusichochee moto! wengi wa JF hawako Bongo wako Ulaya na Marekani! kauli zenu zitasababisha machafuko ya kisiasa na mwisho wake ni mbaya kwani utabadilika kuwa wa kisiasa na kuwa wa kidini na kikabila!!!

Mimi nalaani mauaji haya bila kujali alieuwawa ni Polisi au Raia lakini kwa sasa natanguliza Amani kwanza halafu sheria ije baadae!!!

Hizi ni taarifa za kusikitisha.
Ni kitendo cha kinjama kwa polisi kuua raia ilhali ilipaswa kuwalinda.
Ni vitendo vinavyopaswa kulaaniwa kwa nguvu kubwa, na katika kulaani vitendo hivi..maneno mazito na ya ukali na pengine hata vitendo huambatana.

Usituambie tuache kulaani vitendo hivi eti kwa sababu tunapalia chuki na hasira. Kinachopalia chuki na hasira si michango katika thread hii bali ni mauaji ya raia yaliyotoke jana Arusha. Kama ni amani ilishatokomea mbali katika uso wa nchi hii..kilichobaki ni utulivu ambao nao sasa serikali imeamua kuufuta kwa kuprovoke hasira na chuki katika jamii kotokana na unyanyasaji, ukandamizaji na uonevu wa waziwazi dhidi ya raia.

Nchi hii si mara ya kwanza kuona serikali ikiua raia...nani ameshuhudia sheria ikichukua mkondo wake?...kwa ufupi hakuna haki Tanzania na hivyo sheria haiwezi kufanya kazi tena kama inavyokusudiwa. Usifikiri wale waliondamana na kuuwawa walifanya hivyo ili kuisaidia CHADEMA...Wananchi wanayo machungu yao dhidi ya serikali kutokana na unyanyasaji uliokithiri. Walituua, wametuua na wanaendelea kutuua..LAKINI siko inakuja na siku ipo ambapo nao wataonja uchungu wa Kifo na ndipo watakapotambua thamani ya Uhai...UKOMBOZI wetu u karibu.

Rest in peace our comrades.
 
Asiyeathirika akikataa ni sawa ila siyo serekali imwamulie kukataa kufanya ngono, na ndio maana yakaitwa maandamano ya amani, na wao ndio wametaka, Amref(serekali) walitakiwa kutoa ushauri nasaha sio kuwaamulia, polisi wametreat yale maandamano ya amani kama riot, yani wameyafanya yawe riot ili waweze kutimiza adhma yao, but still what people want to say will be said again and again until when they will listen.

Nasaha ilishatolewa kuwa CDM wasiandamane kwani kutatokea uvunjifu wa amani na tumeona yaliyotokea! ni uporaji, kuchoma magari na maduka moto! sasa sidhani kama ingekuwa sawa Serikali kuachia maandamano hayo yaendelee!!! wao waliruhusiwa kufanya mkutano lakini maandamano hayakuruhusiwa sasa nani wa kubeba lawama?
 
Watu kama wewe ndio wenye fikra finyu na mnaofurahi mkiona amani imevunjika na watu kuuwana. Fitna, chokochoko na uzabizabina umekukaa hata kwenye haya maandishi yako. Watu wankufa wewe unaleta mfano wa kulalana na mkeo? Hauna unachofikiri ila huo upuuzi tu.

Na Serikali sasa ndio mtaijuwa kuwa ina mkono mrefu.

Sasa unalaumu waliokufa au walioua,sheria inasema ukiandamana wakati umekatazwa uuwawe?
 
Back
Top Bottom