Ya Polisi na vyama vya siasa Tanzania

Ya Polisi na vyama vya siasa Tanzania

Naomba sana wanaCCM na hasa swahiba Kibs wasisahau kwamba when you fight with your son who is at the adolescent age, you are bound to be humiliated....

  1. Arusha is the Geneva of africa... they would have chosen the better battle field not arusha
  2. tourism industry is already damaged... while allowing the matching would have just ended with followers feeling fools of themselves
  3. EAF's hub is arusha, i cant imagine how Kenyans are smiling right now

While you think you are slapping your wife, just remember your neighbours are enjoying your degradation

How wrong did the government go on this? no one knows

Arusha kitu gani bwana mbona wakati yanatokea ZNZ hamkusema wakati hata ZNZ kuna wataliii suala hapo ni kwamba wamevunja sheria walitakiwa kufanya mkutano na sio maandamano
 
CUF wamefanya juzi maaaandamo sijaona ukiponda japo nao walikatazwa.... Ulishawahi ona CCM anakatazwa kufanya maandamano??? Ngozi ya kenge ina madoamadoa..... Kweli ngozi ya kitimoto huwezi kuwamba ngoma... Weee utabakia CCM wenzio tutaendelea kuipinga CCM mpaka tutakapozikwa kwa kuwa wezi usisubiri siku ya arobaini hata ya kumi na tano waweke pembeni...

UKWELI: Maandamano yaliruhusiwa na Andengenye masaa 48 kabla lakini JK kupitia Mwema kabla ya masaa kama nane tuu wakaamua kuibaka demokrasia na kuambukiza tiba badala ya ugonjwa...


MyTake::: Kama makamanda wa mikoani hawatakuwa na full control ya mkoa na kuripoti kwa mabosi kwa njia ya Simu basi iko siku watu tutachongoana ndani ya nchi hiii!!!


kwanza kubakia kwenye chama ukipendacho ni haki yako kisheria sioni tatizo

kuhusu la CUF tuliliongea hapa na wengi wetu tulisema walistahiki kichapo, maana ile ya kupeleka documents haikuhitaji maandamano, ingetosha kuita waandishi wa habari ili washuhudie kupeleka makabrasha yao


ama kuhusu kuruhusiwa kufanya maandamano na andanyenge haimaanishi kuwa ndio kibali tosha wakati mkuu wake wa kazi akikifuta, amri halali huwa hii ya mwisho na ambayo imetoka juu zaidi ya mwanzo

uungwana ni kuepusha shari na ukomavu wa uongozi ni kuwa na maono ya mbali na kuwa na uwezo wa kutoa maamuzi mema kwa speed ya ajabu ambayo hayatokuwa na athari kwa Taifa na wananchi unaodai unawatetea.


janja ya chadema imejulikana wao si kwa wananchi ni kwa maslahi yao binafsi
 
Angalau mkuu umeweka sababu za mauaji hayo.
Nikweli tunahitaji mabadiliko lakini tuwe makini na wanasiasa jamani, kulikuwa na sababu gani za msingi kulazimisha maandamano?
Wengine wanakufa ili wengine wajiongezee mitaji kisiasa.
Ugumu wa maisha usitufanye tuamini kila kitu tunachoambiwa na so called upinzani kuwa ni sahihi.
Wengine humu wanashabikia na kuita huu ni mwanzo mzuri wa ukombozi, wamepandikizwa vichwani mwao kuwa bila fujo na mauaji basi maisha kwao yataendelea kuwa hovyo.
Narudia kusema hatuna sababu ya kuendeshwa na wanasiasa kama rimoti kontro, tumepewa akili na utashi kuchambua, mwisho wa siku kura zetu na umoja wetu tukiamua hata wachakachue vipi wataondoka


Sababu gani ya kuua
Polisi wanatakiwa ku make sure maandamano yanaenda kwa amani ,sio kuzuia au kuua.
 
Yaani alipoamka tu Mtu wa pwani, akaamka na Kadogoo something fishy here eeh!!!!!! Kila la heri.
 
Dr Slaa aliomba mazungumo lakini ccm hawataki......

 
Last edited by a moderator:
Hata wale waliokuwa tayari wamefika na kukaa kwenye uwanja wa mkutano walivamiwa na kupigwa! kwa hiyo swala halikuwa kuandamana bali kuonyesha CDM kuwa wao ndo wanao power. Sheria inasema chama kinatakiwa kutoa taarifa 48hrs siyo kuomba kuandamana huko hapo.... viongozi wa viombo vya dola lazima wabadilike.
 
mbona wakati wa MKAPA msikiti wa mwembechai waliuwawa watu..? CDM wanacheza na nguvu ya dola, hapo kwenye habari inasema waliambiwa wasiandamane wakapewa maagizo waandamane lini
Kwa mujibu wa waandishi wa habari mjini Arusha, Polisi walikuwa wamewakataza viongozi wa CHADEMA na wafuasi wao kufanya maandamanao kabla ya mkutano wa kisiasa wa Jumatano, lakini mamia ya wafuasi wa chama hicho wakawafuata viongozi hao walipokuwa wanaelekea eneo la mkutano.

Mzee Slaa kwa uchu wa Madaraka anatamka maneno haya
pia akamtaka Rais Kikwete kujiuzulu.
anawatumia hana lolote, ona sasa wamepigwa risasi end of the day ye atarudi nyumbani kwake miguu juuu. It was simple instruction msiandamane subirini mpaka siku flani
 
Hata wale waliokuwa tayari wamefika na kukaa kwenye uwanja wa mkutano walivamiwa na kupigwa! kwa hiyo swala halikuwa kuandamana bali kuonyesha CDM kuwa wao ndo wanao power. Sheria inasema chama kinatakiwa kutoa taarifa 48hrs siyo kuomba kuandamana huko hapo.... viongozi wa viombo vya dola lazima wabadilike.


kuwa mkweli usispin, wapigwe kwenye mkutano ?
 
nna masisikitiko makubwa sana kwa yaliotokea na ambayo yanaendelea kutokea Arusha kwa sasa.

haya yote yasingetokea kama viongozi wa chadema wangeweka mbele maslahi ya Umma na wanachama wao. Ungangari si sera ya Chadema lakini sijui ilikuwaje ikarithi sera hii mbovu


wao wameruhusiwa kufanya mkutano, na wameambiwa wasifanye mandamano iko simple wao walikuwa wafanye huo mkutano, na kama kweli walikuwa na mazito ya kuyasema wangeyasema na ujumbe ukafika bila ya kutokea yaliyotokea.

baada ya kikao ingekuwa kazi ya viongozi kufuatilia kwa nn kibali chao kufutwa, na hii ingekuwa ni vita kati ya Viongozi wa chama na Uongozi wa polisi.


lakini ukiangalia kwa kina utagundua kuwa ni kweli aliyoyasema Rais kuwa ajenda si kufikisha ujumbe bali wanaamini kwa kutumia strategies kama hizi ndio kitawasaidia chama chao kusikika nje ya nchi.


ni ufinyu wa mawazo na masikitiko kwa wanachama ambao kwa bahati mbaya wanapelekeshwa na viongozi hawa wasiowatakia mema bila ya kutafakari


nnaamini ndani ya chadema kuna viongozi ambao hawakuliunga mkono hili, na tutajua baadae kuwa ni Mbowe na Slaa tu


Kama vile katiba yachelewa vile. JK anayo kazi hapo baadae.
 
Nakumbuka hotuba zake wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu 2010, Muheshimiwa Wilberd Slaa alikuwa akisisitiza kuwa yeye na chama chake hawako tayari kuingia Ikulu au kuwa kiongozi huku damu ya wa TZ inamwagika!!!!

Huko Arusha Serikali imeharamisha maandamano ya CDM lakini Dr. Slaa na uongozi wa CDM wamekataa kutii amri ya Serikali na kinyume chake amewaamrisha wananchi wavamie kituo cha Polisi matokeo yake ni Askari na wananchi wetu wamepoteza maisha kwa sababu ya kutaka Umeya wa Arusha!!!

Damu ya wa TZ imeshamwagika!! Nani awajibike? ni Serikali au ni uongozi wa Chadema?

Source: http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=13188

Kweli Wewe Maskini wa Nchi. Unachojua Kusema ni Kosa la Dr Slaa Kuundamana na Kufanya Mkutano wa Uhalali Nchini Kwake. Katika Nchi Yetu Majambazi na Wauwaji Unafikiri Kuna CCM Wala JK Wanahuruma na Watanzania? Kitu Gani Dr Slaa au Wanachama wa Chadema Arusha Kimehatarisha Maisha ya Watanzania Arusha? Tunataka Ushahidi wa Kila Kitu Kinachosababisha Kinaonyesha Chadema au Historia ya Watanzania Kuhatarisha Maisha ya Watanzania. Tunataka Ushahidi na Upelekwe Mahakama Hague Sio Mahakama za TZ-CCM. Wananchi Wangapi Wamekufa Mahospitalini na Mijini Kisa Mafisadi na Viongozi wa CCM Wawe na Maisha Mazuri? Msialete Kubadilisha Maneno na Waliokufa Wote Tunawapa Heshima Kubwa kwa Kutaka Mabadiliko na Kukataa Kulipwa kwa Dowans, EPA, na Wizi Bank Kuu. Tanzania Hakuna Amani na Haitakuwepo Mpaka Wananchi Wapewe Katiba na Kufukuza JK na Mafisadi.

"CCM ni Wauwaji na Hukumu Yao Ipo Karibu Sana Waangalie Kenya Nani Anaadhibiwa Sasa"
 
Mtu wa pwani, i think i once saw u somewhere snitching as usual.... I had the same feeling that u like the CCM fishy democracy in R-chugga... But u must know that Sombetini diwani wa CCM alimdisi live JK kwenye mkutano wa CHADEMA tena mbele ya Slaa... Wenzio wanabadilika lakini ww uko vilevile... SOURCE: Gazeti ulipendalo HABARILEO LA LEO..habarileo.co.tz

MYTAKE: U will change one day and see.... Tanzania tunaonewa saana.. Hivi ulishawahi kusoma boarding ya serikali... its a misery aiseeee..... lakini u ar still snitching your felllows...!!!
 
Mchungaji Slaa na Mbowe lazima wawe responsible kwa vifo vya wananchi wasio na hatia, kila nchi inakuwa na ulinzi usipofuata sheria lazima sheria ufuate mkondo wake.

Hakukuwa na sababu hawa wachungaji walazimishe maandamano yasiyo kuwa na dira yoyote, either wangeomba kibali na kufuata utaratibu uliokuwepo, TZ haktokuwa na mtu yoyote kuwa above the law. Mchungaji lazima aadhibiwe bila kujali

Sheria inasema kutoa taarifa kwa Polisi masaa 48 kabla ili Polisi watoe ulinzi siyo kuomba ruhusa kwa polisi. Hiyo sheria yako ni ipi? Kama polisi wanayo askari wa kutosha kuzuhiya maandamano hata kwa kuua watashindaje kupata askari wa kulinda na kuongoza maandamano kwa amani? Haya ni mauaji ya makusudi kwa dola ya kikatili ya ccm.
 
Kweli Wewe Maskini wa Nchi. Unachojua Kusema ni Kosa la Dr Slaa Kuundamana na Kufanya Mkutano wa Uhalali Nchini Kwake. Katika Nchi Yetu Majambazi na Wauwaji Unafikiri Kuna CCM Wala JK Wanahuruma na Watanzania? Kitu Gani Dr Slaa au Wanachama wa Chadema Arusha Kimehatarisha Maisha ya Watanzania Arusha? Tunataka Ushahidi wa Kila Kitu Kinachosababisha Kinaonyesha Chadema au Historia ya Watanzania Kuhatarisha Maisha ya Watanzania. Tunataka Ushahidi na Upelekwe Mahakama Hague Sio Mahakama za TZ-CCM. Wananchi Wangapi Wamekufa Mahospitalini na Mijini Kisa Mafisadi na Viongozi wa CCM Wawe na Maisha Mazuri? Msialete Kubadilisha Maneno na Waliokufa Wote Tunawapa Heshima Kubwa kwa Kutaka Mabadiliko na Kukataa Kulipwa kwa Dowans, EPA, na Wizi Bank Kuu. Tanzania Hakuna Amani na Haitakuwepo Mpaka Wananchi Wapewe Katiba na Kufukuza JK na Mafisadi.

"CCM ni Wauwaji na Hukumu Yao Ipo Karibu Sana Waangalie Kenya Nani Anaadhibiwa Sasa"

Kwa taarifa yako wale wote walioshiriki kuchochea machafuko huko Kenya kutoka pande zote za Chama tawala na wapinzani pia wanamashitaka ya kujibu ktk mahakama ta kimataifa! mfano ni Uhuru Kenyata aliekuwa upande wa Serikali!

Hivyo tusichochee machafuko kwani ni majuto baadae!!!
 
Ndugu wananchi tuache jazba na hamaki!! damu ya watanzania wenzetu Polisi na Raia imemwagika!!! wakati huu si wakati wa kuchochea chuki na kuropoka kila kinachotoka mdomoni matokeo yake ni kupalilia chuki na kuzidisha machafuko huku wanaoathirika ni binaadamu wezetu!!

Huu ni wakati wa kutuliza bongo na kupunguza hamasa ili hasira za wananchi zisizidi mipaka na tuiombee nchi yetu Amani kwani hakuna kitu muhimu zaidi kwa sasa kuliko utulivu! tukizidi kuchochea chuki na hasira ndugu zangu tutajikuta tunaingia ktk kapu waliloingia majirani wenzetu wa Kenya, Rwanda, Burundi, Somalia nk!!!

Hasa JF great thinkers nawaomba tuache JAZBA na Katu tusichochee moto! wengi wa JF hawako Bongo wako Ulaya na Marekani! kauli zenu zitasababisha machafuko ya kisiasa na mwisho wake ni mbaya kwani utabadilika kuwa wa kisiasa na kuwa wa kidini na kikabila!!!

Mimi nalaani mauaji haya bila kujali alieuwawa ni Polisi au Raia lakini kwa sasa natanguliza Amani kwanza halafu sheria ije baadae!!!

Damu kumwagika kwa sababu ya siasa ni jambo baya sana,lakini kwa upande mwingine siasa ndo kila kitu katika dunia hii.
Kwa nini CCM mng'ang'anie madaraka? Hivi mnafikiri Tanzania ni tofauti sana na nchi zingine kuwa damu haiwezi mwagika?
Ulilaani pale ambapo CCM malikiuka taratibu za uchaguzi na kujitangazia Meya?
CCM mnajua kabisa kuwa mtavunja sheria halafu mtapelekwa mahakamani,kesi itaburuzwa mpaka karibu uchaguzi 2015,muda wote huo Meya ni wenu.Kwa nini msiwe na ubinadamu???
 
watu wengine bwana.. serikali ikikuambia usilale na mke wako/mume wako hutalala naye?
 
Mtu wa pwani, i think i once saw u somewhere snitching as usual.... I had the same feeling that u like the CCM fishy democracy in R-chugga... But u must know that Sombetini diwani wa CCM alimdisi live JK kwenye mkutano wa CHADEMA tena mbele ya Slaa... Wenzio wanabadilika lakini ww uko vilevile...
SOURCE: Gazeti ulipendalo HABARILEO LA LEO..habarileo.co.tz


Leo umeliamini gazeti la Habari Leo?
 
Mambo ovyo kabisa.

ILA CCM wasubiri tu Mwanza waanze kazi. Hapo itabidi wapeleke JESHI.

ICC inamsubiri mtu. Naomba zichukuliwe Video na Picha pamoja na barua ya kuomba kuandamana, katiba ya Tz inayoruhusu kuandamana, na report ya tukio zima na apelekewe yule mama wa ICC.......

 
Last edited by a moderator:
Damu kumwagika kwa sababu ya siasa ni jambo baya sana,lakini kwa upande mwingine siasa ndo kila kitu katika dunia hii.
Kwa nini CCM mng'ang'anie madaraka? Hivi mnafikiri Tanzania ni tofauti sana na nchi zingine kuwa damu haiwezi mwagika?
Ulilaani pale ambapo CCM malikiuka taratibu za uchaguzi na kujitangazia Meya?
CCM mnajua kabisa kuwa mtavunja sheria halafu mtapelekwa mahakamani,kesi itaburuzwa mpaka karibu uchaguzi 2015,muda wote huo Meya ni wenu.Kwa nini msiwe na ubinadamu???

Kwa hiyo wewe unaona ni bora damu ya wananchi imwagige ili diwani wenu wa CDM apewe Umeya ?
 
Back
Top Bottom