Ya Mbagala Na Bedui Aliyekojoa Msikitini...

Mkuu wangu please umeenda shule na umeelimika sana kiasi kwamba haya sii maoni yako... Unaposema Marekani kwani sisi ni sawa na Marekani ambao wao wanaenzi Ukristu na kuwa msingi wa Utaifa wao. katiba yetu inafanana na yao mbona tunasema kila siku nchi yetu haina dini..

Hawa wenzetu wamefikia mahala hawana Ubaguzi, wameondokana na adha zote na wewe ndio unatakiwa ku fit in the system yao, halafu kila mwananchi anapewa nafasi sawa pasipo kulazimishwa. Tatizo letu tunalazimishana japokuwa ni kinyume cha katiba..Nitakwambia ukweli kwamba Waislaam Marekani au Canada wako Huru kuliko Tanzania iwe ktk swala la Elimu au Afya na serikali zao zinawalipia wagonjwa waliohudumiwa ktk Hospital ama shule sio serikali kutoa fungu la bajeti yake kuendesha Shule au Hospital za kanisa..Hawa wenzetu wanajali UTU sio sisi malimbukeni wa wonna be..

Kwa nini mnaona taabu shule na Hospital zenu ziwe Private? zijiendeshe zenyewe na kutoza ada ama gharama za matibabu ambapo serikali itawalipia wanafunzi au wagonjwa..Leo hii mbali na serikali kutoa mikopo kwa wananzi bado serikali inatoa fedha ktk bajeti yake kuendesha shule hizi. Tumeona migomo ya Madaktari na walimu wakiinyooshea kidole serikali wakati hizi nyingine ni Private owned..

katika mfumo wangu serikali will serve billions watalipia tu ada za wanafunzi na hakuna kutoa fedha ktk bajeti yake kugawana na makanisa na wala hakuna ruzuku. Wafanyabiashara jengeni mashule zenu na serikali itajenga yake hivyo mtoto atachagua shule anayotaka kwenda. hapo ushindani utakuwepo na shule za serikali zitaweza kupimwa ktk ushindani huo. Nyerere aliweza sana tukiona Shule za Private wakishindana na zile za serikali japokuwa zilikuwa chache, vita yetu kitaifa ni kupambana na Umaskini, Ujinga na Maradhi, haya mawili ya mwisho hayawezi kuwa kazi ya kanisa hata kidogo, ni mfumo wa mkoloni unao affect la kwanza..
 
Mjengwa unaujuwa Msikiti na unaijuwa Qur'an? au unajiandikia tu?
 
Mheshimiwa free world, naomba nikuulize swali; Kuambiwa kwamba hayo ni makaratasi tuu kunatosha kuchoma makanisa? Kunatosha kukusudia kuua? kama kuipa kisasi kwa usahihi kwanini nanyi waislamu msiseme tu kwamba Biblia ni makaratasi? Kwanini mnatoa adhabu kubwa kuliko kosa? Ninajua waislamu wengi ambao wametukana ukristo waziwazi kwenye miadhara, mnashauri wakristo wawafunze adabu pia? Najua ni ngumu kuelewa, lakini kwa upande wa ukristo wa ukweli, Mungu anawapigania watu wake, na sii watu wake wanampigania na kumtetea!
 
Hii siyo dini.Zanzibar washaua askari.Ndiyo wanayofundishwa misikitini,

Dini ni ipi, uhakikishe unapojibu unaleta na ushahidi.

Dini ni neno la Kiarabu, Jee unalijuwa maana yake? au unakurupuka tu?
 
Tofauti ni kuwa yule bedui alikuwa hafahamu kitu kuhusu uislam lakini hawa leo wanaujua vizuri uislam
kwa hiyo huyo mtoto aliyekojolea hiyo Quran alikuwa anaujua uislamu vizuri?
Kazi ipo.
 
Mkuu tatizo tulilonalo la kuhusiana na elimu na afya,ni la kimsingi kabisa kwa wananchi wa Tanzania.Kwahiyo let me assume kwamba unazijali afya za watanzania wote bila ya kujali dini zao,je serikali ambayo imeshindwa kuprovide adequate health services kwa wananchi wake,wakiacha kushirikiana na makanisa,je hao wananchi waislam wakatibiwe wapi?wakasome wapi?

Kwasababu mkuu solution ninayoiona,ni nyie waislam kufungua vituo vya afya halafu mushirikiane na serikali kuwapatia waumuni wenu huduma hiyo,whats wrong with that?

Kwenye mfumo wa sasa,unaweza kuniambia kuwa serikali peke yake inaweza kuzitoa huduma toshelezi za afya na elimu?Wataweza vipi na wakati hawawezi hadi hivi sasa licha ya kusaidiwa na hayo mashirika ya kidini?

Ama umeshasahau migomo ya madaktari na hata walimu?Wewe unadhani haya mnayoyafanya yana manufaa kwa muislam?ama hata mkristo mtanzania?

Kwasababu wivu wa kimaendeleo ni mzuri kuliko wivu wa kurudishana nyuma,wa chuki na wa kukwamishana.Badala ya kusema eti huduma za afya zinazotolewa na hayo makanisa,ambazo zinawasaidia waumini wote bila ya kujali dini zao,kwamba zisiwezeshwe kuendelea kufanya hivyo,basi ni kutokuwajali wananchi wenzako.

Ndipo hapo hata huwa ninashangazwa sana na ndugu zetu waislam,kwa mfano hata wale wanaojilipuwa,huwa hawajali hata kama kuna waislam wenzao kwenye maafa hayo kwasababu ya kuwekeza kwenye kifo badala ya kuwekeza kwenye uhai.Hivyo sishangazwi na hatua za kutokuwajali waislam wenzako ambao wananufaika na afya na elimu hizo just because azma yako ya kumpinga kafiri inatimia.

Ni lazima tujuwe kwamba kuna mamno ambayo yamechamgia sana haya ya chuki.Kuna mambo ya tamaduni za watu ambayo tumebugia tu na sasa hata ndugu na ndugu hakuna upendo wala kujaliana.
 
Mkuu wangu unatumia assumptions na hii sio sawa wala haki. Tulipopata Uhuru tulikuwa na Hospital hata moja, tulikuwa na wataalam wa kutosha mbona tuliupata Uhuru lna leo hii wewe na mimi tumepata elimu na kutosha..haya nayosema ni kwa ajili ya Kesho, maandalizi yoyote ya maendeleo hayataki mavuno leo. hata ya Udini tumeyapanda miaka 20 iliyopita kwa hiyo huwezi kunambia Waislaam watatibiwa wapi? Kwani wewe utatibuwa wapi?..Huu ndi udini naozungumzia maana tayari umeanza kama serikali haina uwezo.. Hizi ndizo mbinu walizotumia kurudisha Hospital na shule na ndizo walizotumia viongozi wetu kuuziana Meremeta, Kiwira na miradi ya serikali..

Serikali haiwezi kushindwa kuendesha Shule na Hospital isipokuwa matumizi yake ndio mabaya.. nadhani mkuu wangu ninatosha kwa leo nimejieleza vya kutosha na msg yangu imewafikia. Mtafakari sana maana swala sio uwezo wa serikali bali makanisa hayahitaji fedha ya serikali kujiendesha yanaweza kabisa kutokana na misaada wanayoipata kutoka wafadhili wa dini. Nchi yetu haina dini hivyo ni makosa makubwa ya Kikatiba serikali kuunda Ubia na kanisa ktk maswala muhimu sana kwa jamii yetu hasa ktk kuondoa Ujinga na maradhi hili ni jukumu la serikali na wafanyabiashara wote (binafsi) watatumia policies moja kwa wote ili waifanye kazi hii kwa ufanisi na faida kwa wote..
- Imetosha nadhani nimeeleweka vya kutosha.
 
Kwahiyo unataka kuniambia huwezi kuhudumiwa kwenye hospitali ya mission hadi uachane na uislam?

Hilo la shule kuwa private,ninakubaliana nalo,lakini kusema kwamba federal government haitoi misaada kwenye mashirika ama institutions za kidini marekani,utakuwa unanidanganya.Nyinyi mlichonacho ni chuki tu.

Sasa nani kasema hamruhusiwi kuiomba serikali iwasadie kwenye shule na hosptitali za waislam?Hapo ndipo kwenye mzizi wa fitna.

Ni wivu mbaya,kama ni wivu mzuri,fanya na wewe.Wenye private na uwezo wa kuoperate nao wafanye,lakini nchi yetu ni masikini na hatutakiwi kuwa na muda wa kurudishana nyuma.

Serikali ikitoa misamaha ya kodi kwa vifaa vya afya na elimu,tayari huo ni msaada.

Halafu una maana gani kusema kwanini hawakubali shule zao ziwe private!Una maana kuwa si private?Kwani hata institution za private hazitaweza kupatiwa misamaha ya kodi na other incentives kutoka serikalini na bado ikawa ni msaada wa serikali?Mkuu vipi tena?si unaona mwenyewe?

Kila mmoja atapata kuwezeshwa na serikali kutokana na nature yake,lakini serikali haiwezi kuwapangia eti siju wawe hivi ama wawe vile.Msaada wa serikali unaweza kupatikana kwa namna nyingi tu,lakini bado ni msaada.Sasa bado ninaomba unifafanulie maana halisi ya kusema hizo za mission ziwe private,maana si bado wanalipisha?
 
Unaona sasa tayari umesha anza kutuhukumu.. Chuki itoke wapi? Ni shule gani Private au ya kanisa huko Marekani ilijengwa kwa fedha za kodi ya wananchi? Mkuu ni shule gani za kanisa hutegemea bajeti ya serikali kuwalipa walimu ama madaktari wake. Acha hizo mkuu wangu acha maana hujui unalilitakia kw anchi yetu kazi kulalamika tu inapotokea uhasama kama huu..Hivi hao wanaoilalamikia Barricks, huwa hakuna watanzania wanafanya kazi wnasoma ama kutibiwa na Hospital zao?.. maswali mengine jamani hata siwaelewi..
 
Duh!Kwahiyo kumbe kusema serikali haina uwezo ni mbinu?Kama unaamini ina uwezo,kwanini musiwaambie wakusaidieni na nyie ili muendeshe shule na hospitali zenu badala ya kutaka kuharibu hata kile kidogo kilichopo?Unajuwa kabisa kuna tatizo sugu la afya na elimu,lakini umelifumbia macho hilo kwasababu gani zaidi ya udini?

Hilo la policy moja kwa wote ndiyo unakosea kabisa,ni sawa na kuitumia ile falsafa ya "one size fits all",hiyo haifanyi kazi kwenye dunia ya sasa.At least not on every issue.

Unaposema tulipopata uhuru tulikuwa na shule za kutosha na wataalam wa kutosha pia ni uongo mkubwa kabisa!

Anyways,ni sawa tu tukiishia hapa kwa leo.Baadae.
 

Kwa nini mtoto wa kiislamu ampe kuran mtoto wa kikristu ili aikojolee? Wa kumkemea hapa ni nani? mnachikera ndugu waislamu ni kuuma mchana na kupuliza usiku. Kiongozi wenu wa kitaifa aliyekemea hii kero ni nani? Saa nyingine nawaita wehu ila nshakula ban 2
MUNGU YUPO
 
Mkuu marekani kuna misaada ya federal,kuanzia hatua zote tu hadi za uendeshaji.Kama siyo directly,basi ni inderectly.

Federal hawatoi hiyo misaada kwa hizo instititutions specifically ili wawalipe wafanyakazi mishahara,ila inaweza kusaidia kwenye uendeshaji wa institutions hizo, ulipaji wa mishahara ikiwa ni mojawapo ya shughuli za uendeshaji.

Lakini kuna njia nyingi sana ambazo federal wanazitumia ikiwemo pesa nk.Na kama si pesa,zipo other forms za uwezeshwaji ie subsidies.

Kwa mfano hata private university bado serikali inachangia kwenye kumlipia mwanafunzi in many ways,inaweza kuwa through grants,federal loans,na hata scholarships.Wanafanya hivyo kwa utaratibu unaoitwa "matching"

Hospitals ni the same way.Tena siyo federal govenrment peke yake,hata State.Na hata wasiokuwa na insurance,sometime the govt pick up the tab depending on the situation.

Kwa namna moja ama nyingine,serikali inasaidia.Huo ndo ukweli,lakini wenzetu hawaibuki na chuki ama upuuzi wa kusema eti hawa ni wakristo ama waislam na hivyo wasisaidiwe.

Fuatilia mkuu,hadi misikiti ina subsidies kama ilivyo kwa other reiligious institutions,wenzetu wangekuwa wanaoperate kwa mentality hizo basi hata misikiti isingekuwepo kwao.

Wewe ni kama vile unasema serikali ndiyo inawalipa mishahara hao wafanyakazi wa hizo shule na hospitali za Tanzania,hapo ni lugha ya upotoshaji iliyosababishwa na chuki.

Hata hopstitali zinazofunguliwa na Barrick sidhani kwamba uendeshaji wake unategemea Barrick fully!

Nimekupa mifano ya subsidies za serikali,kwamfano vifaa vya hospitali kutokutozwa kodi,hilo tayari ni mfumo wa serikali kuwasiadia kwasababu ni mapato ambayo serikali ilikuwa iyakusanye kupitia utozaji wa kodi.

Kwahiyo pesa wanazosave(kwa msamaha wa kodi), ndizo wanazitumia kwenye shughuli za uendeshaji,ulipaji mishahara ikiwa ni mojawapo ya shughuli hizo,ndivyo mambo yanavyokwenda,there is no way the government wont be helping.

Ndivyo dunia ilivyo,na ndivyo mambo yanavyoendeshwa.

Sasa mkiwasikiliza wale wenye misimamo mikali hamtaweza kuishi kwenye taratibu za dunia hii ya sasa,ndo ukweli huo mkuu.
 
duuu ni kweli wawe na burara, pia kwanini waislam baathi ni wastaarabu wengine ni wachoze wa vurugu.
 
dini zenyewe mliletewa na wakoloni kwenye
Mitumbwi, leo hii hamna la maana mnalofanya
kutwa kuchwa ni kukashfiana na
kudharauliana...
Wenzenu waliowaletea wako makwaoo
wanafanya shughuli za maendeleo, nyie kila siku ni tafrani tu, uchumi wa nchi mbovu, maisha
yanazidi kuwa magumu kila kukicha aaaggh.... mbaaaav
 

Malizia tu, ukiwaambia ukichana au kukojolea Qur'an unakuwa chizi au unageuka kuwa mjusi, au paka hakuna atakayeamini bila kuprove!.
 

Shida hii inatokana na mafundisho Ya UONGO kuwa Koran ikikojolewa au kuchanwa mtu anageuka kuwa chizi au mjusi. Kama hili ni kweli kwa nini mtoto huyu hakuachwa ili ageuke kuwa chizi? Kukojolea karatasi za mgololo zilizo andikwa ujumbe wa MUNGU kunaathiri nini?
 
lakini kumbuka vita havina macho! unaweza kusema wewe una hasira lakini machafuko yakianza pengine wa kwanza kudhurika na machafuko hayo waweza kuwa ni wewe. subira ni kitu muhimu sana.
 

Join Date : 18th July 2012
Posts : 25
Rep Power : 319
Likes Received:3
Likes Given:1

wiki ya kwanza ni kujifunza about JF and its policy! Elimu dunia ndio msingi wa kila kitu.waislam wasomi wenye kazi zao hawawezi kusupport ujinga wa sheikh Ponda.Please Back to school wewe mburula mwenye fikra ubwabwa.
 
Mkuu big up. Mi nimekuelewa sana, ila shida kubwa naona uislamu unakosa who to control the non-civilized doctrines within uislam. Hii inasababisha emotions rulings na hatimaye kusababisha mobilized actions.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…