Bila ya maswahaba utafika wapi?

Bila ya maswahaba utafika wapi?

OMKEIT 93

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2026
Posts
219
Reaction score
302
Uislamu haukuanza leo, wala Qur'an na Sunnah havikushuka kwa kizazi chetu. Allah Aliwachagua Maswahaba wa Mtume ﷺ kuwa mashahidi wa wahyi, wakajifunza moja kwa moja kutoka kwa Mtume ﷺ, wakauelewa, wakaufanyia kazi, na wakaupeleka kwa waliokuja baada yao.

Allah Amesema:
"Na wa kwanza waliotangulia miongoni mwa Muhajiri na Ansari na wale waliowafuata kwa wema, Allah Ameridhika nao na wao wameridhika Naye..." (Surat At-Tawbah 9:100)

Na pia Amesema:
"Na anayempinga Mtume baada ya kubainikiwa na uongofu, na akafuata njia isiyokuwa ya Waumini, tutamwacha katika alichokichagua na tutamuingiza Jahannam." (Surat An-Nisā' 4:115)

Wanazuoni kama Ibn Taymiyyah (rahimahullah) walisisitiza kuwa kuelewa Qur'an na Sunnah kwa usahihi ni kwa kufuata ufahamu wa Maswahaba. Hii ni kwa sababu wao ndio waliokuwa karibu zaidi na Mtume ﷺ, walijua sababu za kushuka kwa aya, waliona utekelezaji wa Sunnah kwa macho yao, na walifundishwa moja kwa moja.
Mtume ﷺ amesema:
"Kizazi bora ni kizazi changu, kisha wanaowafuata, kisha wanaowafuata." (Sahih al-Bukhari na Sahih Muslim).

Hivyo, mwenye kudai kuwa anaweza kuifasiri Qur'an na Sunnah kwa maoni yake binafsi huku akipuuza ufahamu wa Maswahaba, anajiweka katika hatari ya kupotea. Dini haijengwi juu ya hisia wala tafsiri za mtu mmoja, bali juu ya wahyi ulioeleweka na kutekelezwa na Mtume ﷺ na Maswahaba wake.

Qur'an na Sunnah ndiyo msingi wa Uislamu, lakini zinaeleweka kwa usahihi kupitia ufahamu wa Salaf wema, hususan Maswahaba wa Mtume ﷺ. Hapo ndipo kunapatikana usalama wa dini na kujiepusha na upotofu. Mwenyezi Mungu Atujaalie tushikamane na Kitabu Chake, Sunnah ya Mtume Wake ﷺ, na njia ya Maswahaba kwa uadilifu. Aamiin.
 
Allah kama yupo kweli ahakikishe ahadi yake Gambe haiharibu uaminifu wake popote alipo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom