Mkuu wangu please umeenda shule na umeelimika sana kiasi kwamba haya sii maoni yako... Unaposema Marekani kwani sisi ni sawa na Marekani ambao wao wanaenzi Ukristu na kuwa msingi wa Utaifa wao. katiba yetu inafanana na yao mbona tunasema kila siku nchi yetu haina dini..Mkuu,siyo kwamba ninapinga hayo unayosema,ila ninachosema ni kwamba hayo ndiyo yametufikisha huku tulipo.So ni lazima mchukuwe responsiblity.
Marekani,UK,Australia na Canada ambapo waislam wana thrive na kuishi vyema kwa amani na kusoma kuna mfumo gani?
Hilo la mfumo krsito ndo mzizi wa fitina,na hapo ndipo waislam na wakristo hawataweza kuelewana hata kidogo.Kwa mantiki hiyo,hakuna maneno yatakayoweza kutufanya tuishi pamoja kwa amani tena.
Hawa wenzetu wamefikia mahala hawana Ubaguzi, wameondokana na adha zote na wewe ndio unatakiwa ku fit in the system yao, halafu kila mwananchi anapewa nafasi sawa pasipo kulazimishwa. Tatizo letu tunalazimishana japokuwa ni kinyume cha katiba..Nitakwambia ukweli kwamba Waislaam Marekani au Canada wako Huru kuliko Tanzania iwe ktk swala la Elimu au Afya na serikali zao zinawalipia wagonjwa waliohudumiwa ktk Hospital ama shule sio serikali kutoa fungu la bajeti yake kuendesha Shule au Hospital za kanisa..Hawa wenzetu wanajali UTU sio sisi malimbukeni wa wonna be..
Kwa nini mnaona taabu shule na Hospital zenu ziwe Private? zijiendeshe zenyewe na kutoza ada ama gharama za matibabu ambapo serikali itawalipia wanafunzi au wagonjwa..Leo hii mbali na serikali kutoa mikopo kwa wananzi bado serikali inatoa fedha ktk bajeti yake kuendesha shule hizi. Tumeona migomo ya Madaktari na walimu wakiinyooshea kidole serikali wakati hizi nyingine ni Private owned..
katika mfumo wangu serikali will serve billions watalipia tu ada za wanafunzi na hakuna kutoa fedha ktk bajeti yake kugawana na makanisa na wala hakuna ruzuku. Wafanyabiashara jengeni mashule zenu na serikali itajenga yake hivyo mtoto atachagua shule anayotaka kwenda. hapo ushindani utakuwepo na shule za serikali zitaweza kupimwa ktk ushindani huo. Nyerere aliweza sana tukiona Shule za Private wakishindana na zile za serikali japokuwa zilikuwa chache, vita yetu kitaifa ni kupambana na Umaskini, Ujinga na Maradhi, haya mawili ya mwisho hayawezi kuwa kazi ya kanisa hata kidogo, ni mfumo wa mkoloni unao affect la kwanza..