Ya Mbagala Na Bedui Aliyekojoa Msikitini... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ya Mbagala Na Bedui Aliyekojoa Msikitini...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Oct 18, 2012.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Oct 18, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,057
  Likes Received: 320
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,

  Moja ya hadithi za Mtume Muhammad S.A. W ni pale Mtume Muhammad alipokuwa msikitini na maswahaba wake. Mara akaingia msikitini mtu wa kabila la Mabedui na kuanza kukojoa. Maswahaba wa Mtume wakasimama kwa hamaki kutaka kumwadhibu Bedui yule.

  Mtume akawasihi maswahaba wake wasifanye jambo lolote litakalomdhuru Bedui yule. Hapo ikavutwa subira. Bedui yule akakojoa na akamaliza. Mtume Muhammad alipomuhoji Bedui yule ikabainika kuwa alikuwa ni mtu wa hovyo na wala hakujua kuwa alimokuwa ni msikitini. Bedui yule akaelimishwa, akaelewa. Akarudi kwenye ustaarabu.

  Ndio mkojo ule ulifutwa kwa maji na amani ikawepo. Wahenga walinena; Subira yavuta heri. Siku zote, hamaki si jambo jema. Kwa kutanguliza subira na kutumia hekima Mtume Muhammad aliivuta heri na kuepusha shari.

  Maana, kama Mtume alisingewaasa maswahaba wake kuvuta subira, basi, makubwa matatu yangetokea ndani ya msikiti ule; Mosi, zingezuka vurugu na watu kuumizana na hata kutoana roho. Pili, mkojo wa Bedui yule ungesambaa msikitini kwa vile alishaanza kukojoa na isingekuwa rahisi kwake kukatisha mkojo wake. Tatu, Mkojo una madhara ya kiafya pia.

  Naam, kwa mwanadamu, ni muhimu kuwa na subra na kutafakari kabla ya kufanya maamuzi. Kwa ndugu zangu Waislamu, tunaona Mtume Muhammad ameweza kuonyesha hilo. Na kwa ndugu zangu Wakristo, kuna mifano pia ya Yesu Kristo kuonyesha subra.

  Ndio, Uislamu, kama ilivyo kwa Ukristo na dini nyingi za humu duniani, msingi wake ni amani na upendo. Kitendo cha mtoto yule wa Mbagala kukojolea korani kitazamwe kwa sura ya kitendo kilichofanywa na mtoto .

  Na kama ilivyokuwa kwa Bedui yule, kama pale Mbagala subira na hekima vingetangulizwa, basi, yumkini tungebaini kuwa mtoto yule hakujua madhara ya kitendo chake. Naye angekanywa kama tuwakanyavyo watoto wetu. Na hata kitendo hicho kingefanywa na mtu mzima, bado tulikuwa na haja ya kutanguliza subira na hekima kumhoji aliyetenda, yaweza akawa kama Bedui yule kwenye msikiti alimosali Mtume na maswahaba wake.

  Na kwa kuangalia picha zile za Mbagala naiona hatari iliyopo sasa, kuwa tuna vijana wengi wasio na kazi; Wakristo kwa Waislamu. Vijana wasio na dogo. Ni kama moto uliofifia. Akipatikana kwa kuchochea kuni wanalipuka.

  Ni vijana wanaopatikana wakati wowote na mahali popote. Hata jambo likianza saa tatu asubuhi wao wapo. Hawana ofisi wala bosi wa kumwomba ruhusa ya kwenda kuandamana na kurusha mawe. Ndio hawa wanaonekana wamevaa ' Kata kiuno' na wengi wao hawajahi hata kuingia misikitini au makanisani.

  Inakuawaje kijana wa kweli wa Kiislamu achome kanisa na kuiba kompyuta. Inakuawaje kijana na muumini wa kweli wa Kiislamu aonekane saa mchana wa jua kali akivamia baa na kukimbia na kreti za bia? Ni maswali yanayotutaka tutafakari kwa makini.

  Maana, ninavyoamini mimi, uchumi na elimu duni ndio hasa vinavyochochea vurugu za kijamii, iwe za kidini au kisiasa, na hususan inapohusisha vijana. Vijana wetu hawana misingi mizuri ya elimu, na wengi hawana ajira pia. Haya ni sawa na makombora yasiyo na gharama kubwa kuweza kutumiwa na wanasiasa wasio waadilifu na hata viongozi wa kidini wenye mitazamo mikali. Ni makombora yaliyoanza kutulipukia. Tuliziona ishara, tukazipuuzia.

  Leo Kuna vijana watakaotumiwa au kutumia fursa hiyo kutenda maovu kwa kisingizio cha dini. Ni hawa wataoshiriki kuchafua taswira za dini husika pia. Tujiadhari, kabla ya hatari kubwa inayotujia. Hatujachelewa.

  Na hilo ni Neno La Leo.

  Maggid Mjengwa,

  Iringa.

  0788 111 765
   
 2. Mwitongo

  Mwitongo JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2012
  Joined: Jan 30, 2009
  Messages: 311
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  TUngekuwa na Waislamu japo 10 ya Mjengwa hapa Tanzania, hakika nchi ingekuwa ya maana sana. Huyu ana akili. Si hawa wanaoleta vurugu. Swali kwa Mjengwa: Yule aliyekojolea Kuran kafikishwa mahakamani, je, yule aliyempelekea Kuran mbona kaachwa?
   
 3. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 41,927
  Likes Received: 9,789
  Trophy Points: 280
  Safi sana maggid kwa neno jema na la kujenga! Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu.
  Dini zetu ni nzuri sana kama tukizitumia vyema.

  Sisi sote ni ndugu!
   
 4. Facilitator

  Facilitator JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 703
  Trophy Points: 280
  Nimependa sana hii red text. Hebu tusome wote tuelewe kwa pamoja
   
 5. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,631
  Likes Received: 1,662
  Trophy Points: 280
  Lowasa aliwahi kuonya kuhusu suala hili la vijana. Ni bomu la hatari sana. Tusubiri.
   
 6. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #6
  Oct 18, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kwahiyo maswahaba huwa hawana subra!
   
 7. Philipo Kidwanga

  Philipo Kidwanga Verified User

  #7
  Oct 18, 2012
  Joined: Jul 12, 2012
  Messages: 2,063
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  pamoja na yote hekima ya mtume ndio ilyotumika pale ingali maswahaba walitaka kuanzisha fujo,kwa kuchukua mfano wa masswahaba inamaanisha waislam huwa hawana subira maana maswahaba ni watu wa karibu sana na mtume lakini hawakua na hekima,hivyo basi mtume na uislamu hawana matatizo isipokuwa baadhi ya waislamu uchwara ndio wanaoutia doa waislam.asante maggid kwa somo zuri.
   
 8. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #8
  Oct 18, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 0
  Nikiungana na Mjengwa kwenye hili, moja ya hadithi za mtume Muhammad SAW aliwaambia maswahaba zake kuwa Uislamu ni usafi (al islam nadhif)hapa haku maanisha kuwa unadhifu wa uislamu uko kwenye kuvaa kanzu safi, bagharashia na kikoi au nguo safi pekee! Bali usafi wa muislamu uko mpaka kwenye matendo, moyo na mazingira yanayomzunguka.

  Hivi karibuni kumetokea mambo kadhaa ambayo baadhi ya vijana/watu kwenye makundi ya yaliyojumuisha waislamu wamekuwa wanafanya vitendo ambavyo ni kinyume na maadali na utamaduni wa kiisalamu na hivyo kuchafua jina na taswira ya uislamu.

  Uislamu ni dini ya amani kama zilivyo baadhi ya dini nyingine, matendo maovu ya wachache yanaharibu taswira ya uislamu, na hii inapelekea waislamu na uislamu kuingizwa na kujumuishwa kwenye kapu moja la mambo mabaya. Kwa neno hili la leo na haya machache ninayo andika, naamini waumini wengine watavaa hekima na busara zao kuuona uislamu na waislamu kwa ujumla kuwa sio dini ya fujo na vurugu, bali ndani ya dini hiyo wapo waumini wachache wenye hulka zenye mhemko kinyume na ustaarabu na hekima za uislamu kama jinsi walivyo kwenye dini nyingine.

  Tuungane pamoja kukemea ovu litakalo sababisha kutugawa kwa dini zetu na madhehebu yetu. Tukikaa kimya tutaharibikiwa wote.
   
 9. P

  Paul J Senior Member

  #9
  Oct 18, 2012
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kama tukielewa mitume wetu waliishije na kuyaelewa maandiko matakatifu katika vitabu vyetu amani na upendo vitatawala na upuuzi tunaoushuhudia hautakuwepo. Nje ya hapo ni kujidanganya eti tunawatetea mitume! Mjengwa nakuomba uwaelimishe wengi nje ya jamii forum labda watakuelewa maana mbali na kutokuwa na kazi wengine mioyo yao ni migumu mno, ukweli hawautaki kama ambavyo umetoa mfano wa bedui na badala yake wamegeuka kuwa watumwa!
   
 10. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #10
  Oct 18, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,898
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  na mimi nashauri tuwalee watoto wetu kwa kuwaambia ukweli,waislamu kwa wakristo.
  watoto wa siku hizi ni wadadisi na akili zao hazikubaliani na vitu vya kufikirika.
  ukimwambia mtoto kuwa mtoto ananunuliwa hospitalini ujue akili yake haitatulia mpaka amedhibitisha.
  ukimwambia ukichana biblia utakuwa wa bluu na kwa sababu hajawahi kusikia wala kuona mtu wa bluu atajaribu.

  TUWE MAKINI NA WATOTO.
   
 11. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #11
  Oct 18, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,782
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mtoi na kundi lako, nadhani umemezeshwa propaganda zinazoenezwa na maadui juu ya lile tukio. Waislamu si wajinga kama mnavyotaka watu wafikri. Issue ni kuwa baada ya mama mmoja wa kiislamu kuripoti hii habari ya kokojelea masahafu kwa mama wa ' bedui'. Yule mama alijibu kwa jeuri 'si makaratasi tu hayo'

  Hiki ndicho chanzo cha kadhia nzima ambacho watu hawataki kukizungumza badala yake wanalilia guitar na 'whisky' zilizomwagwa altereni!

  Dharau za hawa ndugu zako hazivumiliki, hata humu JF unaona mwenyewe, wako hivyo!
  Endelea nao, lakini ufahamu walivyo!
   
 12. 1

  1992 New Member

  #12
  Oct 18, 2012
  Joined: Oct 17, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  hapa sasa nimeanza kupata picha kwamba si Waislamu wote ni waumini wa hizi fujo. na hata mafundisho ya kiislamu hayapendekezi fujo na ghasia. ni kweli ni tatizo la ajira na elimu
   
 13. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #13
  Oct 18, 2012
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Maggid,

  As much as I agree na unachokizungumza pia uelewa yule Bedui alikuwa amelewa. Hivyo basi hujaelezea uhalisia wa jambo lilivyokuwa. Binafsi yangu I do not believe in violence but rather busara na hekima. Ndio maana nasema hivi suala la waislamu na wakristo ni vema likaangaliwa kwa macho mawili na uangalifu mkubwa. Niliwahi kushauri zamani kuwa iwepo TRUTH AND RECONCILIATION COMMITTEE. Watu wakanibeza but ukweli wa mambo ni kwamba waislamu wana joto lao moyoni linawauma. Waislamu wengi wanaamini Nyerere alitumika kuukandamiza uislamu (refer to Mohamed Said books). Vile vile baadhi ya mambo yanayofanywa na wakristo kukandamiza waislamu mfano wanapokejeli ati wao wamepeleka mwanzo MOU wakati sio kweli waislamu walipeleka mwanzo MOU ikapigwa chini (refer to Mohamed Said books), kunapelekea kuona waislamu wanaonewa.

  Tukirejea suala la huyu kijana nadhani maggid you are misleading kwa sababu huyu ni kijana wa miaka 14 (inamaana ana fahamu zake na akili timamu kwasababu umri huo mara nyingi vijana wa kiume wanabelehe) hivyo basi anajua fika kitu anachokifanya na kwanini anafanya. Usimfananishe na mtoto wa miaka 7 ambaye hata kuoga hajui. Hapo Maggid unakosea. Vile vile mtume alitumia busara kuwaambia masahaba wamuachie yule bedui kwasababu alikuwa kwanza amelewa na pili hajui anafanya nini. Kisheria tunasema he is in the state of unsound mind. Hata kwenye macho ya kisheria ukiuwa katika hali hiyo unakuwa unapewa punishment pungufu kwasababu wanachukulia hukuwa unafahamu unachokifanya. Sasa huyu kijana alikuwa anajua fika analolifanya na sio kuwa alikuwa amelewa au hafahamu.

  Hivyo nakushauri siku nyengine unapogusa suala la waislamu kuwa na ufahamu kidogo wa kitu unachokizungumzia. Yes hekima na busara ni muhimu katika jambo hili but GET YOUR FACTS RIGHT !!!!!

  Nilikuwapo!!!!
   
 14. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #14
  Oct 18, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,787
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Mtume alijaaliwa hekima na busara! hawa wenzetu elimu dunia imewapita kando!
   
 15. m

  maswitule JF-Expert Member

  #15
  Oct 18, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,387
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Mjengwa umenena lililo jema, ndugu kuna any association ya waislam wasomi Tanzania? kama ipo ni wakati mwafaka kushughulika na kutoa elimu hiyo njema. Mimi si muislam lakini nitakuwa tayari kuchangia shughuli zenu. Maana wakristu kuna association kama Christian Professionals of Tanzania CPT. Kama haipo anzisheni mkuu
   
 16. Majita

  Majita JF-Expert Member

  #16
  Oct 18, 2012
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 602
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Mjengwa,naamini kama umepotoka kidogo.Tunafahamiana humu kwa muda mrefu japo hatujawahi kuonana Kwa macho.Kwa nini kijana wa watu kijana mdogo nimwite mtoto (kwa tafasili ya sheria ya tanzania)aliyekojolea kuran unamwita BEDUI?Hope unajua vizurii maana ya neno bedui.WHAT IF HUYO MTOTO HANA DINI?
   
 17. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #17
  Oct 18, 2012
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Ipo na inaitwa Tanzania Muslim Professional TAMPRO what is your point? Elimu gani unayoiita njema hebu fafanua.
   
 18. Rufiji

  Rufiji JF-Expert Member

  #18
  Oct 18, 2012
  Joined: Jun 18, 2006
  Messages: 1,693
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160

  Mdondoaji,

  Nimejaribu kufuatlia hoja yako lakini nimeshindwa kuelewa una maanisha nini! Kwa hiyo, wewe kwa mtazamo wako, unadhani kwa kuwa kijana ana miaka 14 basi ni sawa kwa hao waumini kureact kwa kuchoma makanisa? Na ni nani aliyesema kwamba mtoto mwenye miaka 14 ni mature enough kuweza kujua impact ya lile alilolifanya? Ni wangapi kati yetu tushawahi vitu vingi vya kijinga katika umri kama wa huyo kijana.
   
 19. w

  wikolo JF-Expert Member

  #19
  Oct 18, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 801
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hapo kwenye nyekundu ndo suala la subira linapozungumziwa. Kama walikuwa wamevumilia kitendo cha kukojolea kitabu ilishindikana vipi kuvumilia jibu la huyo mama hata kusababisha yote yaliyotokea? Cha msingi hapa ni kwamba kukitokea machafuko hakuna atakayeponywa na dini yake, tutaathirika wote kwa namna sawa. Uvumilivu ni kitu cha msingi sana.
   
 20. Domy

  Domy JF-Expert Member

  #20
  Oct 18, 2012
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 4,702
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Waislam fuateni ushauri huu wa maggid kwa faida yenu na watoto wenu,acheni kuendekeza fujo kwa vitu vidogo vidogo,Hivi kama mtoto wa kiislam angekojolea Biblia mnafikiri wakristo wangefanya mliyoyafanya? Vp leo itokee wakristo wachome msikiti na kuiba mazuria itakuwaje? Tuangalie mbele tutumie hekima na busara kama za maggid kuepusha machafuko.Kwa kifupi tujifunze kuvumiliana.
   
Loading...