Ya Mbagala Na Bedui Aliyekojoa Msikitini...

Ya Mbagala Na Bedui Aliyekojoa Msikitini...

hata kama angekuwa ni wa miaka 100, je msahafu unahalalisha kuchoma makanisa na kuiba mali za kanisa, je hilo ni suluhisho? kwani aliyefanya kitendo hicho ametumwa na makanisa yaliyovamiwa?
Mkuu wangu nitarudia kusema hivi yaliyotokea Mbagala ni mazao ya kile tulichopanda. Hawa watu wote ni maskini na wajinga ambao walipewa sababu ya kuvamia na kuchoma makanisa ilihali wao wenyewe wamejazwa ujinga kama yule mtoto alokojolea Msahafu.

Hekima haiwezi kutokea ktk kundi la wajinga sasa nyie wenye werevu na usikivu ndio mnaotakiwa kuitangaza kheri, amani na utumilivu lakini ikiwa nanyi mnashindwa kuelewa basi itakuwa kazi kubwa sana kuuondosha udini nchini. Mabadiliko huanza na sisi, wewe ulostaarabika mfunze mwenzako ustaarabu, wewe uloelimika mfunze yule ambaye hana elimu ili kesho naye akawafundishe wengine..

Leo hii ukianzisha lolote hata iwe kuua wahindi na matajiri basi sii waislaam wala wakristu watakaoshiriki maana tumewapa sababu ya kuwachukia wahindi na matajiri kwa kuwaweka wao ktk umaskini. Hivyo mnapokataa kosa la kukojolea msahafu hawa wenzenu hawatawaelewa na wala huwezi kupima kwa mtazamo wako, heshimuni imani yao ili nanyi mheshimiwe. Kifupi tuheshimiane kwanza.
 
Ndugu zangu,

Moja ya hadithi za Mtume Muhammad S.A. W ni pale Mtume Muhammad alipokuwa msikitini na maswahaba wake. Mara akaingia msikitini mtu wa kabila la Mabedui na kuanza kukojoa. Maswahaba wa Mtume wakasimama kwa hamaki kutaka kumwadhibu Bedui yule.

Mtume akawasihi maswahaba wake wasifanye jambo lolote litakalomdhuru Bedui yule. Hapo ikavutwa subira. Bedui yule akakojoa na akamaliza. Mtume Muhammad alipomuhoji Bedui yule ikabainika kuwa alikuwa ni mtu wa hovyo na wala hakujua kuwa alimokuwa ni msikitini. Bedui yule akaelimishwa, akaelewa. Akarudi kwenye ustaarabu.

Ndio mkojo ule ulifutwa kwa maji na amani ikawepo. Wahenga walinena; Subira yavuta heri. Siku zote, hamaki si jambo jema. Kwa kutanguliza subira na kutumia hekima Mtume Muhammad aliivuta heri na kuepusha shari.

Maana, kama Mtume alisingewaasa maswahaba wake kuvuta subira, basi, makubwa matatu yangetokea ndani ya msikiti ule; Mosi, zingezuka vurugu na watu kuumizana na hata kutoana roho. Pili, mkojo wa Bedui yule ungesambaa msikitini kwa vile alishaanza kukojoa na isingekuwa rahisi kwake kukatisha mkojo wake. Tatu, Mkojo una madhara ya kiafya pia.

Naam, kwa mwanadamu, ni muhimu kuwa na subra na kutafakari kabla ya kufanya maamuzi. Kwa ndugu zangu Waislamu, tunaona Mtume Muhammad ameweza kuonyesha hilo. Na kwa ndugu zangu Wakristo, kuna mifano pia ya Yesu Kristo kuonyesha subra.

Ndio, Uislamu, kama ilivyo kwa Ukristo na dini nyingi za humu duniani, msingi wake ni amani na upendo. Kitendo cha mtoto yule wa Mbagala kukojolea korani kitazamwe kwa sura ya kitendo kilichofanywa na mtoto .

Na kama ilivyokuwa kwa Bedui yule, kama pale Mbagala subira na hekima vingetangulizwa, basi, yumkini tungebaini kuwa mtoto yule hakujua madhara ya kitendo chake. Naye angekanywa kama tuwakanyavyo watoto wetu. Na hata kitendo hicho kingefanywa na mtu mzima, bado tulikuwa na haja ya kutanguliza subira na hekima kumhoji aliyetenda, yaweza akawa kama Bedui yule kwenye msikiti alimosali Mtume na maswahaba wake.

Na kwa kuangalia picha zile za Mbagala naiona hatari iliyopo sasa, kuwa tuna vijana wengi wasio na kazi; Wakristo kwa Waislamu. Vijana wasio na dogo. Ni kama moto uliofifia. Akipatikana kwa kuchochea kuni wanalipuka.

Ni vijana wanaopatikana wakati wowote na mahali popote. Hata jambo likianza saa tatu asubuhi wao wapo. Hawana ofisi wala bosi wa kumwomba ruhusa ya kwenda kuandamana na kurusha mawe. Ndio hawa wanaonekana wamevaa ' Kata kiuno' na wengi wao hawajahi hata kuingia misikitini au makanisani.

Inakuawaje kijana wa kweli wa Kiislamu achome kanisa na kuiba kompyuta. Inakuawaje kijana na muumini wa kweli wa Kiislamu aonekane saa mchana wa jua kali akivamia baa na kukimbia na kreti za bia? Ni maswali yanayotutaka tutafakari kwa makini.

Maana, ninavyoamini mimi, uchumi na elimu duni ndio hasa vinavyochochea vurugu za kijamii, iwe za kidini au kisiasa, na hususan inapohusisha vijana. Vijana wetu hawana misingi mizuri ya elimu, na wengi hawana ajira pia. Haya ni sawa na makombora yasiyo na gharama kubwa kuweza kutumiwa na wanasiasa wasio waadilifu na hata viongozi wa kidini wenye mitazamo mikali. Ni makombora yaliyoanza kutulipukia. Tuliziona ishara, tukazipuuzia.

Leo Kuna vijana watakaotumiwa au kutumia fursa hiyo kutenda maovu kwa kisingizio cha dini. Ni hawa wataoshiriki kuchafua taswira za dini husika pia. Tujiadhari, kabla ya hatari kubwa inayotujia. Hatujachelewa.

Na hilo ni Neno La Leo.

Maggid Mjengwa,

Iringa.

0788 111 765

Nukuu toka Quran

7_199.png
"Be tolerant, command what's right, pay no attention to foolish people" [7:199]

25_63.png

"And the servants of the Most Merciful are those who walk upon the earth easily, and when the ignorant address them [harshly], they say [words of] peace," [25:63]

16_125.png

"Invite to the way of your Lord with wisdom and good instruction, and argue with them in a way that is best. Indeed, your Lord is most knowing of who has strayed from His way, and He is most knowing of who is [rightly] guided." [16:125]
 
Dini hizi zitawafilisha mbali, at the end mtapigwa kebiriti wote.
 
Mkuu wangu sasa unaenda kusiko faa kabisa tunatoka ktk Mada. Hivi unataka kunambia Wakristu hawauwi?.. Mpaka mtu aue kwa jina la dini yake na ukatangaziwa ktk vyombo vya habari ndio unajua mtu mbaya lakini yule anayeua pasipo kuitumia dini wakati ni muumini wa dini hana hatia siyo.. What make the difference ikiwa leo Marekani ndio nchi iloshambulia nchi nyingine ili kusimika serikali wanayoipenda..lakini wao wazuri sana, Huko Marekani kuna vifo vya risasi kila siku kuliko sehemu yoyote duniani lakini wao ndio wazuri kuliko watu wote duniani..mbona mnataka kutuaminisha uongo jamani.. Hivi kweli unaweza kunipa hesabu ya mauaji ya Crusade ukilinganisha na vita yoyote ya kiimani?..

Mkuu wangu tulipofika leo hii hatuna sababu ya ku provoke watu ili wa react na mseme hii ndio dini ya shetani isipokuwa ushetani ni wa roho, unapopanga kufanya, yale ulokusudia rohoni ndio shetani hivyo kifo pekee sio dhambi maana hata Mungu mwenyewe katuandikia watu wote tutakufa...Na huwezi kusema Mungu ni Shetani kwa sababu katuandikia kifo..
Mkuu hukunielewa. Nimekuambia si kila kitu katika ukristo ni kizuri na naamini si kila kitu katika uislamu ni kizuri. Yaani mimi nakubaliana na criticisms za ukristo na nina criticisms zangu kwa huo ukristo. Kwa kifupi tu nikuambie madhara mengi ya dini yanaonekana pale inapokuwa na nguvu ya dola. Karne nyingi ukristo ilikuwa dola ya dunia. Katika kipindi hicho wamefanya unyama wa kutisha. Ile Vatican imejengwa kwa damu ya watu wengi ambao hawakuwa na hatia sawa sawa na Makkha ulivojengwa kwa damu nyingi za watu wasiokuwa na hatia kwa unyama wa kutisha ambao bado unatumiwa na wanadamu wanaonufaika na utawalala wa kisiasa kwa mgongo wa dini. Ndio maana nimekuambia si kwamba ukristo ni utakatifu. Mimi kwa uelewa wangu nnavochukulia dini na mwenendo wa historia inavyoonyesha dini zilitumika kusimika tawala za wanadamu. Ukianza kwa Musa, kwa Samwel, mpaka kwa Saul hadi Daudi na wafalme wengine waliofuata walijikita kwenye dini kili kutawala. Ambaye aliondoa dini kwenye utawala ni Yesu. Lakini alipoondoka tu watu wakajipachika uwakilishi wake na kuanza kutawala wanadamu wengine kwa mgongo wa dini. Hao ndio wanaitwa popes. Uislamu hausalimiki katika kosa hili mtume wake katumia dini kujijenga kisiasa na kupata umaarufu kisha kuwa mtawala.
Kwa hiyo mkuu mimi sisemi ukristo haujatenda dhambi. Marekani inasababu nyingi za kutokuwepo kwenye historia hiyo ya dini na utawala ndio maana Marekani kama nchi utasema ina hayo mabavu ya kukalia nchi nyingine lakini haina maana kuwa ni ukristo ila ni ufalme (yaani ni utawala) usiohusiana na dini.
Nilichotaka kusema ni kuwa Mungu hana vurugu, hana hasira za haraka, ni mvumilivu na hakurupuki, haui hovyo na vitendo vyovyote vinavyokinzana na hizo tabia za mwenyezi Mungu lazima tuzikatae. Kuhubiri chuki kati ya jamii zetu na kusema dini fulani ni maadui wetu tuzikatae na tuwaambie waziwazi viongozi wetu wa dini kama watakuja kutuhubiri hizi chuki misikitini au makanisani kwamba wanachokifanya ni ushetani na tuwakatae.
 
Mtoi na kundi lako, nadhani umemezeshwa propaganda zinazoenezwa na maadui juu ya lile tukio. Waislamu si wajinga kama mnavyotaka watu wafikri. Issue ni kuwa baada ya mama mmoja wa kiislamu kuripoti hii habari ya kokojelea masahafu kwa mama wa ' bedui'. Yule mama alijibu kwa jeuri 'si makaratasi tu hayo'

Hiki ndicho chanzo cha kadhia nzima ambacho watu hawataki kukizungumza badala yake wanalilia guitar na 'whisky' zilizomwagwa altereni!

Dharau za hawa ndugu zako hazivumiliki, hata humu JF unaona mwenyewe, wako hivyo!
Endelea nao, lakini ufahamu walivyo!

Lilikuwa ni suala la kuongea na mama yake au kuliripoti kwa mamlaka?

Makanisa ya madhehebu mbali mbali yamevunjwa, je huyo mtoto anasali kwote huko?
 
Naomba nikusahihishe,

Nimesoma kwenye gazeti moja na kwa mujibu wa watu walioko huko huyo kijana alikuwa ana miaka 14. Hata kama ana miaka 12 ni umri ambao vijana wengi wanakuwa washabaleghe na hivyo anajua fika anachokifanya.

Hata hivyo inawezekana baadhi yao ni waislamu na ukiangalia zaidi ni ufukara na chuki ya muda mrefu dhidi ya ndugu zetu wakristo ndio imepelekea hivi. Kwani wasichome masinagogi ya wahindi kule Temeke? Kwanini wasiharibu miti ya ibada ya wapagani bali wameenda makanisani? Haujiulizi why?
Mkuu na wewe una misimamo mikali sana na chuki sana,umepotea mida lakini naona umerudi.

Sasa ingelikuwa ni sharia,huyo mtoto aliyebalehe mngemfanya kitu gani?
 
Mkuu wangu nitarudia kusema hivi yaliyotokea Mbagala ni mazao ya kile tulichopanda. Hawa watu wote ni maskini na wajinga ambao walipewa sababu ya kuvamia na kuchoma makanisa ilihali wao wenyewe wamejazwa ujinga kama yule mtoto alokojolea Msahafu.
Watu wanasema eti tunakoelekea ni kubaya,mimi nasema tumeshafika kubaya.Wewe hupenda kumtetea Sheick Ponda.

Hayo unayoyasema hapo juu wewe na Mdondoaji kuhusu ukosefu wa ajira,ujinga na ukosefu wa elimu,munaandika tu bila kujuwa kwamba munasapoti misimamo ya Ponda kuhusu mfumo Kristo, hayo sijui ya Necta,kwamba waislam wanapenda shule ila wanazuliwa na wakristo.Kwamba hata kazi hawana kwasababu mfumo kristo ndiyo unawanyanyasa,hiyo ni chuki mbaya sana!Ni sawa na wale Hitler aliowaweka kambini ambao walikuwa hawajui wazazi wao,na baada ya kufundishwa jeshini,wakaambiwa wazazi wao waliuwawa na jews!

Mmesahawaonyesha hao vijana kuwa adui yao ni wakristo,na kwamba huo ufukara,ujinga na mengineyo,sababu ni wakristo.

Sasa mnataka kupakazia wengine.Chuki imepandwa na waislam wakiongozwa na kiongozi wa nchi.Hilo liko wazi.

Haijalishi maneno ya kwamba eti ni wahuni sijui eti mtoto aliyekojolea kuraan alijazwa ujinga.Ukweli ni kwamba mmezipanda hizo mbegu za chuki.Its a painfull truth.
 
Mkuu hukunielewa. Nimekuambia si kila kitu katika ukristo ni kizuri na naamini si kila kitu katika uislamu ni kizuri. Yaani mimi nakubaliana na criticisms za ukristo na nina criticisms zangu kwa huo ukristo. Kwa kifupi tu nikuambie madhara mengi ya dini yanaonekana pale inapokuwa na nguvu ya dola. Karne nyingi ukristo ilikuwa dola ya dunia. Katika kipindi hicho wamefanya unyama wa kutisha. Ile Vatican imejengwa kwa damu ya watu wengi ambao hawakuwa na hatia sawa sawa na Makkha ulivojengwa kwa damu nyingi za watu wasiokuwa na hatia kwa unyama wa kutisha ambao bado unatumiwa na wanadamu wanaonufaika na utawalala wa kisiasa kwa mgongo wa dini. Ndio maana nimekuambia si kwamba ukristo ni utakatifu. Mimi kwa uelewa wangu nnavochukulia dini na mwenendo wa historia inavyoonyesha dini zilitumika kusimika tawala za wanadamu. Ukianza kwa Musa, kwa Samwel, mpaka kwa Saul hadi Daudi na wafalme wengine waliofuata walijikita kwenye dini kili kutawala. Ambaye aliondoa dini kwenye utawala ni Yesu. Lakini alipoondoka tu watu wakajipachika uwakilishi wake na kuanza kutawala wanadamu wengine kwa mgongo wa dini. Hao ndio wanaitwa popes. Uislamu hausalimiki katika kosa hili mtume wake katumia dini kujijenga kisiasa na kupata umaarufu kisha kuwa mtawala.
Kwa hiyo mkuu mimi sisemi ukristo haujatenda dhambi. Marekani inasababu nyingi za kutokuwepo kwenye historia hiyo ya dini na utawala ndio maana Marekani kama nchi utasema ina hayo mabavu ya kukalia nchi nyingine lakini haina maana kuwa ni ukristo ila ni ufalme (yaani ni utawala) usiohusiana na dini.
Nilichotaka kusema ni kuwa Mungu hana vurugu, hana hasira za haraka, ni mvumilivu na hakurupuki, haui hovyo na vitendo vyovyote vinavyokinzana na hizo tabia za mwenyezi Mungu lazima tuzikatae. Kuhubiri chuki kati ya jamii zetu na kusema dini fulani ni maadui wetu tuzikatae na tuwaambie waziwazi viongozi wetu wa dini kama watakuja kutuhubiri hizi chuki misikitini au makanisani kwamba wanachokifanya ni ushetani na tuwakatae.
Nimekuelewa vizuri sana lakini haya sii mafundisho ya Ukiristu wala Uislaam. Ukisoma vitabu hivi viwili utanielewa vizuri naposema Ukirstu au Uislaam sio WATU ama mkusanyiko wa watu (jamii) isipokuwa wale wanaofuata mafundisho ndio huitwa wakristu au waislaam. Kwetu sisi vitabu hivi ni kama toleo ya agizo la Mungu hivyo hakuna mbora zaidi ya Mungu mwenyewe.

Kwa hiyo sisi wote tuliozaliwa ktk Uislaam na Ukristu halafu tukafikiri sisi ni waumini, tunajidanganya wenyewe kutokana na kwamba hatufuati mafundisho. Na bahati mbaya kuna watu wanafikiri wanaweza wao kuwa na uchungu na dini hizi kuliko Yesu au Muhammad ambao ndio viongozi wetu kwa fokra ya kwamba wanaweza kuilinda dini ya Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo wale wote wanaoyafanya mambo haya kwa faida zao na kwa minajiri ya kupanua wigo la utawala wao hawana Uislaam wala Ukristu maana tumearishwa tu KUJILINDA pale tunapoingiliwa na kukwazwa ktk imani zetu. Kama vile mwanamke anayetaka kuwa rapped akajitetea hivyo hata akiua itakuwa amejilinda yeye na makosa ni ya yule alotaka kumwingilia..

Nikuchekeshe kidogo:- Tatizo la Dunia ya leo kimfumo ni kwamba atalaumiwa yule mwanamke kwa kuua kwa sababu kitendo cha kuwa rapped watamuuliza kama yeye bikira kama sio bikira kwani taabu iko wapi hadi afikie kuua?
 
kwa hiyo huko Pakistani, Afghanistani, Sudan, Somali, Mombasa, na kwingineko wote wanalalamikia MOU?
Analytical, hapo pekundu, umenikumbusha kisa cha kale ka-binti kanaitwa MALALA kutaka kuuwawa, eti msahafu haururusu wanawake kwenda shule/kupata elimu dunia, kinacho nitisha jinsi hawa jamaa wanavyopenda kuiiga mambo hii staili nayo wanaweza kuileta hapa TZ.
 
Watu wanasema eti tunakoelekea ni kubaya,mimi nasema tumeshafika kubaya.Wewe hupenda kumtetea Sheick Ponda.

Hayo unayoyasema hapo juu wewe na Mdondoaji kuhusu ukosefu wa ajira,ujinga na ukosefu wa elimu,munaandika tu bila kujuwa kwamba munasapoti misimamo ya Ponda kuhusu mfumo Kristo, hayo sijui ya Necta,kwamba waislam wanapenda shule ila wanazuliwa na wakristo.Kwamba hata kazi hawana kwasababu mfumo kristo ndiyo unawanyanyasa,hiyo ni chuki mbaya sana!Ni sawa na wale Hitler aliowaweka kambini ambao walikuwa hawajui wazazi wao,na baada ya kufundishwa jeshini,wakaambiwa wazazi wao waliuwawa na jews!

Mmesahawaonyesha hao vijana kuwa adui yao ni wakristo,na kwamba huo ufukara,ujinga na mengineyo,sababu ni wakristo.

Sasa mnataka kupakazia wengine.Chuki imepandwa na waislam wakiongozwa na kiongozi wa nchi.Hilo liko wazi.

Haijalishi maneno ya kwamba eti ni wahuni sijui eti mtoto aliyekojolea kuraan alijazwa ujinga.Ukweli ni kwamba mmezipanda hizo mbegu za chuki.Its a painfull truth.
Mkuu wangu nimeandika hivi:- Mfumo Kristumaana yake ni pale serikali inaposhirikiana na kanisa kuendesha shughuli za AFYA na ELIMU... Je jambo hili halifanyiki nchini?.. Hili linafanyika sasa hivi na ndio uchcochezi ulipoanza kwa nini serikali isiliondoe, kun ugumu gani?.

Labda nikupe mfano mwingine serikali yetu ikitumia hukumu zinazoendana na Uislaam itakuwa kosa kwa Mkristu kusema tuna Mfumo wa Sharia law? halafu Waislaam wachukie wakati wanaona kweli unatumika?.. Mfano mwingine.. Leo hii serikali nyingi zina mfumo Dume mbona wewe mwanaume huchukii kusikia wanawake wanaposema tuna mfumo dume isipokuwa hapa kwenye Ukristu wakati unajua fika kwamba serikali yetu inashirikiana na makanisa kuhudumia wananchi ktk Afya na Elimu jambo ambalo waislaam hawalipendi..

Sasa ni nani anayeendeza udini na kuwapandisha waislaam chuki kama sio serikali. Hivi kuna tatizo gani ikiwa serikali haitashirikiana na kanisa? kwani nchi gani Makanisa walishindwa kuendesha shule na Hospital zao! kuna ulazima gani kuendeleza mfumo wa kikoloni ambao hata Nyerere aliupiga vita...
- Nasubiri majibu yako..
 
Sasa utasemaje hao waislam waliokosa elimu na ni mafukara wasiwashambulie wakristo kama msiamo wako ndo huo?Hivi unadhani ni kwanini wanachoma makanisa kwa sababu ya ukosefu wa elimu na ajira?
 
Sasa utasemaje hao waislam waliokosa elimu na ni mafukara wasiwashambulie wakristo kama msiamo wako ndo huo?Hivi unadhani ni kwanini wanachoma makanisa kwa sababu ya ukosefu wa elimu na ajira?
Nifikiri mimi tena au wewe ndio unatakiwa kufikiria na kunipa jawabu. Mkuu wangu ukisema Saudia Arabia au Iran wanatumia mfumo wa Sharia law na hatuutaki kabisa Tanzania, nitakubaliana na wee wala sintopinga wala kuona huwapendi Waislaam. Haya labda niulize miye kama napenda mfumo huo utumike nyumbani? -nitakujibu - Hell NO! Kwa sababu sisi ni taifa ambalo halina dini na wananchi wake ndio wanafuata imani za dini zao hakuna sababu ya kumlazimisha mtu imani, utaratibu ama sheria zako.

Sasa nashangaa sana wakristu wanajua fika kwamba mfumo huu uliopo nchini uliletwa na wakoloni kuja kuitawala Afrika wakitumia makanisa kuendesha shughuli za AFYA na ELIMU huku wao wakikwapua maliasili zetu. Wakiwanyima haki sawa Waislaaam na Waislaam wanajua madhara ya mfumo ule sasa wanapokuja kuilalamikia serikali mnashindwa vipi kuliona hili badala yake mnaitetea serikali ile ile mnayotaka kuindoa madarakani..

Hawa wa Mbagala ni matokeo ya kulea Mfumo kwa miaka 20 toka mwaka 1992 waislaam wamekuwa wakilalamika na wengine wachochezi wakimlalamikia Nyerere kwa sababu walifikiria wao ndio watakuwa na nguvu ya kuendesha nchi kwa sheria zao.. Hivyo binafsi yangu yanaona makosa pande zote mbili na nasema tuondokane na mfumo kristu tuweke mfumo bora zaidi wa ELIMU na AFYA nchini haya matatizo yataondoka laa sivyo jipu hili litaendelea kusambaa kesho litakuwa sehemu ambayo hatukutegemea kabisa..
 
hahahaha bahati mbaya MAJJID si mwislamu kama wengi wanavyofikiria, ni jina tu linashabihiana na majina ya kiislamu na kwa kuwa anao ndugu zake wengi waislamu maeneo ya kisarawe na kule iringa.
 
Mtoi na kundi lako, nadhani umemezeshwa propaganda zinazoenezwa na maadui juu ya lile tukio. Waislamu si wajinga kama mnavyotaka watu wafikri. Issue ni kuwa baada ya mama mmoja wa kiislamu kuripoti hii habari ya kokojelea masahafu kwa mama wa ' bedui'. Yule mama alijibu kwa jeuri 'si makaratasi tu hayo'

Hiki ndicho chanzo cha kadhia nzima ambacho watu hawataki kukizungumza badala yake wanalilia guitar na 'whisky' zilizomwagwa altereni!

Dharau za hawa ndugu zako hazivumiliki, hata humu JF unaona mwenyewe, wako hivyo!
Endelea nao, lakini ufahamu walivyo!

kwahiyo wewe pia ulienda kuchoma makanisa kwa kukasirishwa na hilo neno ni makaratasi.. wewe na wenzako ni watu wa ajabu sana.sasa kwa kuchoma makanisa unadhani kile ulichokusudia umepata????
 
Tofauti ni kuwa yule bedui alikuwa hafahamu kitu kuhusu uislam lakini hawa leo wanaujua vizuri uislam
 
Nifikiri mimi tena au wewe ndio unatakiwa kufikiria na kunipa jawabu. Mkuu wangu ukisema Saudia Arabia au Iran wanatumia mfumo wa Sharia law na hatuutaki kabisa Tanzania, nitakubaliana na wee wala sintopinga wala kuona huwapendi Waislaam. Haya labda niulize miye kama napenda mfumo huo utumike nyumbani? -nitakujibu - Hell NO! Kwa sababu sisi ni taifa ambalo halina dini na wananchi wake ndio wanafuata imani za dini zao hakuna sababu ya kumlazimisha mtu imani, utaratibu ama sheria zako.

Sasa nashangaa sana wakristu wanajua fika kwamba mfumo huu uliopo nchini uliletwa na wakoloni kuja kuitawala Afrika wakitumia makanisa kuendesha shughuli za AFYA na ELIMU huku wao wakikwapua maliasili zetu. Wakiwanyima haki sawa Waislaaam na Waislaam wanajua madhara ya mfumo ule sasa wanapokuja kuilalamikia serikali mnashindwa vipi kuliona hili badala yake mnaitetea serikali ile ile mnayotaka kuindoa madarakani..

Hawa wa Mbagala ni matokeo ya kulea Mfumo kwa miaka 20 toka mwaka 1992 waislaam wamekuwa wakilalamika na wengine wachochezi wakimlalamikia Nyerere kwa sababu walifikiria wao ndio watakuwa na nguvu ya kuendesha nchi kwa sheria zao.. Hivyo binafsi yangu yanaona makosa pande zote mbili na nasema tuondokane na mfumo kristu tuweke mfumo bora zaidi wa ELIMU na AFYA nchini haya matatizo yataondoka laa sivyo jipu hili litaendelea kusambaa kesho litakuwa sehemu ambayo hatukutegemea kabisa..
Mkuu,siyo kwamba ninapinga hayo unayosema,ila ninachosema ni kwamba hayo ndiyo yametufikisha huku tulipo.So ni lazima mchukuwe responsiblity.

Marekani,UK,Australia na Canada ambapo waislam wana thrive na kuishi vyema kwa amani na kusoma kuna mfumo gani?

Hilo la mfumo krsito ndo mzizi wa fitina,na hapo ndipo waislam na wakristo hawataweza kuelewana hata kidogo.Kwa mantiki hiyo,hakuna maneno yatakayoweza kutufanya tuishi pamoja kwa amani tena.
 
Mtoi na kundi lako, nadhani umemezeshwa propaganda zinazoenezwa na maadui juu ya lile tukio. Waislamu si wajinga kama mnavyotaka watu wafikri. Issue ni kuwa baada ya mama mmoja wa kiislamu kuripoti hii habari ya kokojelea masahafu kwa mama wa ' bedui'. Yule mama alijibu kwa jeuri 'si makaratasi tu hayo'

Hiki ndicho chanzo cha kadhia nzima ambacho watu hawataki kukizungumza badala yake wanalilia guitar na 'whisky' zilizomwagwa altereni!

Dharau za hawa ndugu zako hazivumiliki, hata humu JF unaona mwenyewe, wako hivyo!
Endelea nao, lakini ufahamu walivyo!

Hii siyo dini.Zanzibar washaua askari.Ndiyo wanayofundishwa misikitini,
 
Maggid,

As much as I agree na unachokizungumza pia uelewa yule Bedui alikuwa amelewa. Hivyo basi hujaelezea uhalisia wa jambo lilivyokuwa. Binafsi yangu I do not believe in violence but rather busara na hekima. Ndio maana nasema hivi suala la waislamu na wakristo ni vema likaangaliwa kwa macho mawili na uangalifu mkubwa. Niliwahi kushauri zamani kuwa iwepo TRUTH AND RECONCILIATION COMMITTEE. Watu wakanibeza but ukweli wa mambo ni kwamba waislamu wana joto lao moyoni linawauma. Waislamu wengi wanaamini Nyerere alitumika kuukandamiza uislamu (refer to Mohamed Said books). Vile vile baadhi ya mambo yanayofanywa na wakristo kukandamiza waislamu mfano wanapokejeli ati wao wamepeleka mwanzo MOU wakati sio kweli waislamu walipeleka mwanzo MOU ikapigwa chini (refer to Mohamed Said books), kunapelekea kuona waislamu wanaonewa.

Tukirejea suala la huyu kijana nadhani maggid you are misleading kwa sababu huyu ni kijana wa miaka 14 (inamaana ana fahamu zake na akili timamu kwasababu umri huo mara nyingi vijana wa kiume wanabelehe) hivyo basi anajua fika kitu anachokifanya na kwanini anafanya. Usimfananishe na mtoto wa miaka 7 ambaye hata kuoga hajui. Hapo Maggid unakosea. Vile vile mtume alitumia busara kuwaambia masahaba wamuachie yule bedui kwasababu alikuwa kwanza amelewa na pili hajui anafanya nini. Kisheria tunasema he is in the state of unsound mind. Hata kwenye macho ya kisheria ukiuwa katika hali hiyo unakuwa unapewa punishment pungufu kwasababu wanachukulia hukuwa unafahamu unachokifanya. Sasa huyu kijana alikuwa anajua fika analolifanya na sio kuwa alikuwa amelewa au hafahamu.

Hivyo nakushauri siku nyengine unapogusa suala la waislamu kuwa na ufahamu kidogo wa kitu unachokizungumzia. Yes hekima na busara ni muhimu katika jambo hili but GET YOUR FACTS RIGHT !!!!!

Nilikuwapo!!!!

Hapo kwenye red; Unataka kusema leo hii mlevi akiingia msikitini akawa anakojoa na mpo waislamu kadhaa ndani, mtamuacha kwa sababu amelewa na hajui anachokifanya?
 
Back
Top Bottom