Ya Mbagala Na Bedui Aliyekojoa Msikitini...

Imekuwa kazi yangu kubwa hapa kijiweni kujaribu kuwashusha watu munkari ili wapate kujitazama wenyewe kwanz akabla ya kuzungumzia matokeo ya Kijana kukojolea Kuruan na uchomaji moto wa makanisa. Nawaomba jitazameni nyie wenyewe wala sio matukio na mtakuta ya kwamba mna CHUKI baina yenu...Maneno mnayoandika humu aidha kwa kuegemea upande mmoja au kukosoa upande mwingine ni dalali ya kuitaka haki upande unao kuhusu - WHY?..

Hadithi ya Mjengwa inaonyesha hekima kubwa ya mtume na mfano bora kwetu wa kuigwa lakini ukweli ni kwamba sisi sote sio MITUME wala hatuna hekima walopewa mitume hata kwa Ukaribu mdogo. Mantiki ya hadithi ile ni kuonyesha Uongozi bora, busara inayoweza kutumiwa na viongozi wetu pale wananchi wanapotaka kutumia hasira zao ktk swala ambalo wanaliona ni kinyume cha mila na tamaduni zao..Na kama hadithi ile inavyosema wale waumini wote wa Uislaam walitaka kumpiga yule mlevi, wao hawakuona Ulevi wake wala kutokujua kwake kuwa sababu isipokuwa kitendo cha kukojolea msikiti kilikuwa dharau kubwa na sio ustaarabu. Na kikubwa zaidi eleweni yule mtu aliitwa Bedui kwa maana asili yao hawa Mabadui walikuwa hawana ustaarabu na kawaida yao kukojoa, kuchuma dawa mahala popote wanapoona kama Baniani na kujamba au kutema makohozi.

Udini nchini kwetu umepandikizwa mbegu mbaya wala sio magugu yanayoota yenyewe na yanahitaji kupaliliwa. Ukipanda mbigiri bila shaka tutavuna Mbigiri na ndicho kilichotokea hivyo watoto wetu wanapokuja zikanyaga na kulia kwa maumivu hapo ndipo tunaanza kunyoosheana vidole. lakini UDINI nchini umetokana na nini haswa - Jibu lake rahisi sana - SIASA na UTAWALA. Toka siku tuloruhusu Dini kuwa sehemu ya Siasa za nchi yetu tukahalalisha waraka, mihadhara na mafundisho ya dini na hata viongozi kuongoza ufunguzi wa ibada, sala na mikutano ya dini kuwa sehemu ya ujenzi wa mandeleo nchini ndipo tulipokuwa tukipanda mbegu za UDINI.

Mwalimu Nyerere alipambana na UDINI kwa kuhakikisha hakuna mahusiano baina ya serikali na dini. Kwa waislaam waliona wanakwazwa kwa sababu haikuwa kawaida serikali kutoshirikiana na viongozi wa dini. Kweli waliomba mambo mengi sana na yakapigwa chini lakini vile vile hakuruhusu Upande wa imani yake wafaidike kwa lolote. Serikali yake ikachukua jukumu kubwa la kupambana na maadui wetu watatu yaani UMASIKINI, UJINGA na MARADHI na kuifanya haki ya kila Mtanzania bila kujali dini zao. Alipambana na Ukoloni mamboleo kwa kutowapa nafasi wageni kututawala kiuchumi. Nyerer aliwajuwa maadui wetu na hivyo kuweka misingi imara ya kulinda umoja wetu.. Huu ndio ulikuwa Uongozi wenye DIRA wenye mwongozo ambao hata mtume aliufuata kwa sababu alikuwa na mission, malengo na azma ya kuufikisha ujumbe kwa hawa mabedui wasioamini, sio viongozi wetu leo hii.

Toka Mageuzi ya Kiuchumi mwaka 1985 tanzania tumekuwa tunajiendesha kama gari bovu.. Umaskini, Ujinga na Maradhi haikuwa tena sababu ya vita ya kitaifa kuwakomboa wananchi hivyo mwenye uwezo aliweza kujipenyeza na kukamata nguzo hizo kibiashara. Na toka mwaka huo Ukoloni Mamboleo haukuwa tena maadui wetu wa nje isipokuwa tegemezi letu. Kwa hiyo Unapoutazama UDINI nchini nawaomba pia mtazame jinsi Ubeberu ulivyorudi nchini. Na wala msije walalamikia kina Barricks au Richmond isipokuwa sisi wenyewe ndio tumeruhusu mambo haya yafikie hapa tulipo. Tumewaruhusu wawekeze tukalegeza masharti yetu ili wapate kukamata njia za uchumi sasa leo tunawalalamikia nini?

Tanzania imepoteza SIASA SAFI na UONGOZI BORA, hivyo ni nchi inasokuwa na DIRA..Hao WATU na ARDHI vitabakia kuwa watumishi na shamba la utawala ulokosa ubunifu tukapanda mbegu hizi na hakika tutavuna tulichopanda..
 
Maggid,

As much as I agree na unachokizungumza pia uelewa yule Bedui alikuwa amelewa. Hivyo basi hujaelezea uhalisia wa jambo lilivyokuwa. Binafsi yangu I do not believe in violence but rather busara na hekima. Ndio maana nasema hivi suala la waislamu na wakristo ni vema likaangaliwa kwa macho mawili na uangalifu mkubwa. Niliwahi kushauri zamani kuwa iwepo TRUTH AND RECONCILIATION COMMITTEE. Watu wakanibeza but ukweli wa mambo ni kwamba waislamu wana joto lao moyoni linawauma. Waislamu wengi wanaamini Nyerere alitumika kuukandamiza uislamu (refer to Mohamed Said books). Vile vile baadhi ya mambo yanayofanywa na wakristo kukandamiza waislamu mfano wanapokejeli ati wao wamepeleka mwanzo MOU wakati sio kweli waislamu walipeleka mwanzo MOU ikapigwa chini (refer to Mohamed Said books), kunapelekea kuona waislamu wanaonewa.

Tukirejea suala la huyu kijana nadhani maggid you are misleading kwa sababu huyu ni kijana wa miaka 14 (inamaana ana fahamu zake na akili timamu kwasababu umri huo mara nyingi vijana wa kiume wanabelehe) hivyo basi anajua fika kitu anachokifanya na kwanini anafanya. Usimfananishe na mtoto wa miaka 7 ambaye hata kuoga hajui. Hapo Maggid unakosea. Vile vile mtume alitumia busara kuwaambia masahaba wamuachie yule bedui kwasababu alikuwa kwanza amelewa na pili hajui anafanya nini. Kisheria tunasema he is in the state of unsound mind. Hata kwenye macho ya kisheria ukiuwa katika hali hiyo unakuwa unapewa punishment pungufu kwasababu wanachukulia hukuwa unafahamu unachokifanya. Sasa huyu kijana alikuwa anajua fika analolifanya na sio kuwa alikuwa amelewa au hafahamu.

Hivyo nakushauri siku nyengine unapogusa suala la waislamu kuwa na ufahamu kidogo wa kitu unachokizungumzia. Yes hekima na busara ni muhimu katika jambo hili but GET YOUR FACTS RIGHT !!!!!

Nilikuwapo!!!!
Ndugu hebu punguza za uso kwa mjengwa na tafakari aliyoyaandika kwa mapana .la kwanza mtovu wa adabu ni mtoto -hajui atendalo tena ni mkristo wala umuhimu wa Qurani hajui,la pili walioshiriki fujo ni vijana wa kihuni maana haiwezekani waislam wakaingia bar na kuiba 'haramu' na kukimbia nayo la tatu kuliadhibu kanisa kwa kuliibia kwani uislamu unapinga ulevi na wizi.mjengwa hajapinga kuwa lililotokea kwa waislam ni ovu,tatizo liko kwa reaction ya tukio zima, hata kama mama wa 'bedui' alipoamua kuwa bedui kwa kujibu upumbavu walipom consult,labda utuambie kuwa scenerio hii ingerudi enzi za mtume(SAW)matokeo yangekuwa kama ya mbagala?
 
Ndugu zangu,

Moja ya hadithi za Mtume Muhammad S.A. W ni pale Mtume Muhammad alipokuwa msikitini na maswahaba wake. Mara akaingia msikitini mtu wa kabila la Mabedui na kuanza kukojoa. Maswahaba wa Mtume wakasimama kwa hamaki kutaka kumwadhibu Bedui yule.

Mtume akawasihi maswahaba wake wasifanye jambo lolote litakalomdhuru Bedui yule. Hapo ikavutwa subira. Bedui yule akakojoa na akamaliza. Mtume Muhammad alipomuhoji Bedui yule ikabainika kuwa alikuwa ni mtu wa hovyo na wala hakujua kuwa alimokuwa ni msikitini. Bedui yule akaelimishwa, akaelewa. Akarudi kwenye ustaarabu.

Ndio mkojo ule ulifutwa kwa maji na amani ikawepo. Wahenga walinena; Subira yavuta heri. Siku zote, hamaki si jambo jema. Kwa kutanguliza subira na kutumia hekima Mtume Muhammad aliivuta heri na kuepusha shari.

Maana, kama Mtume alisingewaasa maswahaba wake kuvuta subira, basi, makubwa matatu yangetokea ndani ya msikiti ule; Mosi, zingezuka vurugu na watu kuumizana na hata kutoana roho. Pili, mkojo wa Bedui yule ungesambaa msikitini kwa vile alishaanza kukojoa na isingekuwa rahisi kwake kukatisha mkojo wake. Tatu, Mkojo una madhara ya kiafya pia.

Naam, kwa mwanadamu, ni muhimu kuwa na subra na kutafakari kabla ya kufanya maamuzi. Kwa ndugu zangu Waislamu, tunaona Mtume Muhammad ameweza kuonyesha hilo. Na kwa ndugu zangu Wakristo, kuna mifano pia ya Yesu Kristo kuonyesha subra.

Ndio, Uislamu, kama ilivyo kwa Ukristo na dini nyingi za humu duniani, msingi wake ni amani na upendo. Kitendo cha mtoto yule wa Mbagala kukojolea korani kitazamwe kwa sura ya kitendo kilichofanywa na mtoto .

Na kama ilivyokuwa kwa Bedui yule, kama pale Mbagala subira na hekima vingetangulizwa, basi, yumkini tungebaini kuwa mtoto yule hakujua madhara ya kitendo chake. Naye angekanywa kama tuwakanyavyo watoto wetu. Na hata kitendo hicho kingefanywa na mtu mzima, bado tulikuwa na haja ya kutanguliza subira na hekima kumhoji aliyetenda, yaweza akawa kama Bedui yule kwenye msikiti alimosali Mtume na maswahaba wake.

Na kwa kuangalia picha zile za Mbagala naiona hatari iliyopo sasa, kuwa tuna vijana wengi wasio na kazi; Wakristo kwa Waislamu. Vijana wasio na dogo. Ni kama moto uliofifia. Akipatikana kwa kuchochea kuni wanalipuka.

Ni vijana wanaopatikana wakati wowote na mahali popote. Hata jambo likianza saa tatu asubuhi wao wapo. Hawana ofisi wala bosi wa kumwomba ruhusa ya kwenda kuandamana na kurusha mawe. Ndio hawa wanaonekana wamevaa ' Kata kiuno' na wengi wao hawajahi hata kuingia misikitini au makanisani.

Inakuawaje kijana wa kweli wa Kiislamu achome kanisa na kuiba kompyuta. Inakuawaje kijana na muumini wa kweli wa Kiislamu aonekane saa mchana wa jua kali akivamia baa na kukimbia na kreti za bia? Ni maswali yanayotutaka tutafakari kwa makini.

Maana, ninavyoamini mimi, uchumi na elimu duni ndio hasa vinavyochochea vurugu za kijamii, iwe za kidini au kisiasa, na hususan inapohusisha vijana. Vijana wetu hawana misingi mizuri ya elimu, na wengi hawana ajira pia. Haya ni sawa na makombora yasiyo na gharama kubwa kuweza kutumiwa na wanasiasa wasio waadilifu na hata viongozi wa kidini wenye mitazamo mikali. Ni makombora yaliyoanza kutulipukia. Tuliziona ishara, tukazipuuzia.

Leo Kuna vijana watakaotumiwa au kutumia fursa hiyo kutenda maovu kwa kisingizio cha dini. Ni hawa wataoshiriki kuchafua taswira za dini husika pia. Tujiadhari, kabla ya hatari kubwa inayotujia. Hatujachelewa.

Na hilo ni Neno La Leo.

Maggid Mjengwa,

Iringa.

0788 111 765

Kudos Mjengwa! Wengi wanabeba hoja zisizo na uzito wowote na kutaka kuliharibu Taifa.Umesema ukweli mtupu kwenye hii thread yako. Tufike mahala tusihukumu bila kujua kwa uhalisi jinsi mambo yalivyo.
 
mkojo wa bedui.
Mtume alikosea kumsamehe bedui. Alifanya hukumu ya zamani.
Leo kosa hilo linahukumiwa kwa mujibu wa maendeleo ya sayansi na technologia.
Kama suala la dini lilikuwa halihusiki basi ingefaa biblia itafutwe na yule kijana wa kiislam ainyee basi mambo yaishe.
Ila mimi biblia ikiharibiwa si jambo kuu, ila matendo yangu ndiyo jambo linalofaa zaidi iwapo ni mema na yenye kuwasaidia wengine wamtumikie Mungu wa kweli.
 
mkojo wa bedui.
Mtume alikosea kumsamehe bedui. Alifanya hukumu ya zamani.
Leo kosa hilo linahukumiwa kwa mujibu ya maendeleo ya sayansi na technologia.
Kama suala la dini lilikuwa halihusiki basi ingefaa biblia itafutwe na yule kijana wa kiislam ainyee basi mambo yaishe.
Ila mimi biblia ikiharibiwa si jambo kuu, ila matendo yangu ndiyo jambo linalofaa zaidi iwapo ni mema na yenye kuwasaidia wengine wamtumikie Mungu wa kweli.
Hapana mkuu wangu pengine hukuelewa vizuri mantiki ya hadithi ile kutokana na watu wamechapia chapia tafsiri zao..

Ukweli ni kwamba yule Bedui alikuwa ni mtu ambaye hajastaarabika wala kuamini. Mabedui walikuwa watu wasioamini Mungu hivyo asili zao ndizo ziliongoza maisha yao ktk kuamini miungu wao. Kwa hiyo, Umuhimu wa hadithi (tukio) lile ni kwamba wewe unapokuwa umestaarabika, umepata mafundisho ya dini na kuamini utaona ubaya wa kila jambo baya slisilo na usraatabu lakini haina maana kila mtu anajua maana hata wewe ulikuwa hujui vile vile ukaelemishwa.

Hivyo mwache akojoe kisha mfahamishe ubaya wa jambo lile akikuelewa naye atastaarabika na kesho hatakojoa msikitini maana lengo la dini ni kumvuta yule asiye elewa ktk UTU abadilike awe kama nyie ili naye kesho atamkanya mwingine na mwingine na watu wote watakapo kuwa wastaarabu basi hakuna atakayeweza kukojolea msikiti.. Haya ndio mafunzo na hekima ilokuwa nyuma ya tukio (hadith) lile..
 
Ndugu zangu,

Moja ya hadithi za Mtume Muhammad S.A. W ni pale Mtume Muhammad alipokuwa msikitini na maswahaba wake. Mara akaingia msikitini mtu wa kabila la Mabedui na kuanza kukojoa. Maswahaba wa Mtume wakasimama kwa hamaki kutaka kumwadhibu Bedui yule.

Mtume akawasihi maswahaba wake wasifanye jambo lolote litakalomdhuru Bedui yule. Hapo ikavutwa subira. Bedui yule akakojoa na akamaliza. Mtume Muhammad alipomuhoji Bedui yule ikabainika kuwa alikuwa ni mtu wa hovyo na wala hakujua kuwa alimokuwa ni msikitini. Bedui yule akaelimishwa, akaelewa. Akarudi kwenye ustaarabu.

Ndio mkojo ule ulifutwa kwa maji na amani ikawepo. Wahenga walinena; Subira yavuta heri. Siku zote, hamaki si jambo jema. Kwa kutanguliza subira na kutumia hekima Mtume Muhammad aliivuta heri na kuepusha shari.

Maana, kama Mtume alisingewaasa maswahaba wake kuvuta subira, basi, makubwa matatu yangetokea ndani ya msikiti ule; Mosi, zingezuka vurugu na watu kuumizana na hata kutoana roho. Pili, mkojo wa Bedui yule ungesambaa msikitini kwa vile alishaanza kukojoa na isingekuwa rahisi kwake kukatisha mkojo wake. Tatu, Mkojo una madhara ya kiafya pia.

Naam, kwa mwanadamu, ni muhimu kuwa na subra na kutafakari kabla ya kufanya maamuzi. Kwa ndugu zangu Waislamu, tunaona Mtume Muhammad ameweza kuonyesha hilo. Na kwa ndugu zangu Wakristo, kuna mifano pia ya Yesu Kristo kuonyesha subra.

Ndio, Uislamu, kama ilivyo kwa Ukristo na dini nyingi za humu duniani, msingi wake ni amani na upendo. Kitendo cha mtoto yule wa Mbagala kukojolea korani kitazamwe kwa sura ya kitendo kilichofanywa na mtoto .

Na kama ilivyokuwa kwa Bedui yule, kama pale Mbagala subira na hekima vingetangulizwa, basi, yumkini tungebaini kuwa mtoto yule hakujua madhara ya kitendo chake. Naye angekanywa kama tuwakanyavyo watoto wetu. Na hata kitendo hicho kingefanywa na mtu mzima, bado tulikuwa na haja ya kutanguliza subira na hekima kumhoji aliyetenda, yaweza akawa kama Bedui yule kwenye msikiti alimosali Mtume na maswahaba wake.

Na kwa kuangalia picha zile za Mbagala naiona hatari iliyopo sasa, kuwa tuna vijana wengi wasio na kazi; Wakristo kwa Waislamu. Vijana wasio na dogo. Ni kama moto uliofifia. Akipatikana kwa kuchochea kuni wanalipuka.

Ni vijana wanaopatikana wakati wowote na mahali popote. Hata jambo likianza saa tatu asubuhi wao wapo. Hawana ofisi wala bosi wa kumwomba ruhusa ya kwenda kuandamana na kurusha mawe. Ndio hawa wanaonekana wamevaa ' Kata kiuno' na wengi wao hawajahi hata kuingia misikitini au makanisani.

Inakuawaje kijana wa kweli wa Kiislamu achome kanisa na kuiba kompyuta. Inakuawaje kijana na muumini wa kweli wa Kiislamu aonekane saa mchana wa jua kali akivamia baa na kukimbia na kreti za bia? Ni maswali yanayotutaka tutafakari kwa makini.

Maana, ninavyoamini mimi, uchumi na elimu duni ndio hasa vinavyochochea vurugu za kijamii, iwe za kidini au kisiasa, na hususan inapohusisha vijana. Vijana wetu hawana misingi mizuri ya elimu, na wengi hawana ajira pia. Haya ni sawa na makombora yasiyo na gharama kubwa kuweza kutumiwa na wanasiasa wasio waadilifu na hata viongozi wa kidini wenye mitazamo mikali. Ni makombora yaliyoanza kutulipukia. Tuliziona ishara, tukazipuuzia.

Leo Kuna vijana watakaotumiwa au kutumia fursa hiyo kutenda maovu kwa kisingizio cha dini. Ni hawa wataoshiriki kuchafua taswira za dini husika pia. Tujiadhari, kabla ya hatari kubwa inayotujia. Hatujachelewa.

Na hilo ni Neno La Leo.

Maggid Mjengwa,

Iringa.

0788 111 765

Mjengwa uko sahihi kwa upande mmoja. Uko sahihi kwamba ni rahisi kwa vijana wasiokuwa na kazi kufanya fujo pasipo kuuliza sababu ya tukio husika au kuwa na subira.

Kwa upande wa pili hili tu haliwezi kuwa sababu hasa ya vijana kuibuka na kuchoma makanisa na kukojolea kuruhani. Lawama hasa za kukurupuka zinaenda kwa wale waliochoma makanisa. Je, hakuna vitendo ambavyo wakristo wametendewa kubwa kuliko kukojolea Qoran na hawakufikia hatua ya kuharibu mali yoyote kwa wale waliowakosea?

Tukisema kuwa hawa wanafanya hivi kwa kuwa ni vijana wasiokuwa na ajira tutakuwa tumepata tu immediate cause lakini si basic au the main cause of this incidence.
Ni mara ngapi tumewaona watu wazima wameandamana kwenye TV, wakifanya fujo, kuharibu majengo ya serikali, kuharibu mali za hasa watu wa magharibi pindi linapotokea tukio kama hili lilotokea Mbagala?

Sasa nikuulize swali; uvumilivu unaonekana kukosekana tu kwa vijana wa kiislamu au waislamu wengi? Kama jibu ni kwa vijana wa kiislamu hapo kuna tatizo manake hatuoni vijana wa kikristo wakikosa uvumilivu kwa kiwango hicho. Na kama visa hivi vinatokana na vijana kukosa kazi, tusingeona vijana wa kikristo nao wakikosa huo uvumilivu? Je, tusingewaona wakiandamana kwenda kulipiza kisasi kwa kuchoma misikiti?

Ninachokisema Mjengwa ni kuwa waislamu hawawezi kukwepa lawama kwenye vurugu hizi na kusema ni vijana wasiokuwa na kazi na kukosa elimu tu. Kitendo cha Qoran kuruhusu muumini kupigania dini yake ndio chanzo cha haya yote. Wewe umemfundisha kijana asiyekuwa na elimu wala uelewa wa kutosha apiganie dini yake, na anaona wenzake kwenye TV wakaipigania dini yao hiyo pindi inapochokozwa. Unategemea atakuwa na maswali ya kuuliza tena wakati makanisa yako karibu? Pili kafundishwa kuwa hao ni makafiri, ndio wanaofanya maisha yao yawe magumu, nchi yao inayonywa na mfumo ukristo, atafanya nini? Hao wanaoeneza chuki za mfumo ukristo na kuleta chuki kati ya jamii nao ni vijana wasio kuwa na elimu na kazi pia?

Nakubaliana nawe kuwa elimu na uchumi ambao utamfanya mtu ajiskie ana kitu cha kupoteza akipatikana na kosa inaweza kupunguza fujo hizi lakini hiyo itakuwa ni ndoto ikiwa kila tofauti iliyokuwako kati ya waislamu na wakristo au fursa yoyote iliyotolewa na serkali na ikatumiwa na wakristo au dhehebu lolote litakuwa mada ya kujenga chuki dhidi ya watu wengine kwenye jamii kuwa wanapendelewa na serikali tofauti na dini yao.
Tuwaangalie viongozi wetu wa dini, tuwakazie macho na kuwaambia wahubiri amani kati ya watu badala ya chuki kama zinavyohubiriwa kwenye mihadhara. Tusitafute sababu za kuwakwepesha na lawama.
 
Mkuu wangu ni wewe unayethamisha vitu hivi lakini kwao wao hawalitazami swala hili kwa picha yako.. Nitakufahamisha na nawaomba Wakristu wengine mnisikie kwa makini sana..

Kuna sinema moja inaonyesha jamaa mmoja millionea mwanamme aliweza kuwashawishi vijana wapendanao wawili ili atembee na mpenzi wake kwa siku moja atawapa millioni moja. Hawa vijana walikaa na kutafakari wakaamua kukubali ombi hilo na hivyo binti akaenda kwa tajiri kwa mapenzi ya siku moja wakitegemea ni jambo dogo sana kwa mavuno makubwa.. Lakini haikuwa hivyo kabisa, Fedha iliweza kushinda sawia na mapenzi ya dhati na hivyo kuvuruga mahusiano baina ya wapendanao. Ukawa mtihani mkubwa tofauti kabisa na vile walivyofikiria. Sinema ile inatufundisha nini?..

Kwa hiyo mkuu wangu, kwako wewe na mimi tunaweza sana kuthamini majengo ya makanisa na tukaiona hasara ya fedha lakini kwa hawa vijana Waislaam hiyo Kuruan kwao ina thamani kuliko hata maisha yao wenyewe. Na huwezi kuithamisha Kuruan kwa fedha au mali ndivyo wanavyoitazama dini yao..Hivyo basi wewe unapohesabu hasara ya majengo wao wanahesabu thamani ya imani yao kudharauliwa na matokeo ya mgongano huu ndio mavuno tunayoyaona.

nachowaomba ndugu zangu watanzania, UPENDO, kuthamini ya watu wengine na kuogopa majaribio ya Udini, kuheshimiana ndio njia pekee inayoweza kututoa hapa tulipo na kuanza mwanzo mpya. Dini usiyo iamini kwa nini watu wanapenda sana kuijaribu? iwe masheikh Misikitini kuwaita Wakristu majafir au Wakristu kujiaminisha Uislaam ni dini ya mashetani na kumkashifu mtume na vitabu vyao..Hawa watu huwa wanapata nini haswa? waacheni watu waabudu kiole wanachoabudu na hulazimishwi nawe kuabudu kile wanacho abudu, kila mmoja wetu atakwenda kaburini peke yake na amali yake pekee ndio itamwokoa yeye..
 
Mtume alijaaliwa hekima na busara! hawa wenzetu elimu dunia imewapita kando!

Hii ndio akili yako wewe unayejiona kama umesoma sana. Hebu nikuulize swali ni wakristo asilimia ngapi wana shahada ya chuo kikuu? Na je shahada hizo zinawasaidia kuufahamu ukweli wa mambo? mbona wewe mwenye elimu dunia nzuri mpaka leo hii unaamini kwamba Mungu alijidhirisha kama mwanadamu kupitia kwa Yesu, hivi Mungu alikuwa na shida hiyo ya kufanya hivyo wakati vyote vilivyomo mbinguni na ardhini ni kazi yake? Elimu dunia kama hii hata siihitaji kwani hainisaidii hata kidogo. Lakini cha msingi ni hiki inawezekana wewe umepata tu kishahada chako kilichotakana na uchakachuaji wa Ndalichako aliyekupa Division One wakati hustahili, ukaenda chuo kikuu ukapata kidigrii chako cha pass ambacho kimechangiwa na mambo fulani, ndio maana leo hii unaona watu wote hawajasoma. Hizo ndizo fikra mgando.
 
Ebu tuamini kuwa huyu mtoto amekosea sana kuliko watu wote duniani,-------- naomba kuuliza kwa nini makanisa yanacomwa? Kuna kanisa lolote ambalo laweza kutuma mtoto kukojolea kitabu kitakatifu cha waisilamu? Hao wanaowalea watawalea mpaka lini? Huhitaji busara ya kukopa kama mwenyewe huna' kujua kuwa kuna tatizo kubwa la kuelewa dini vibaya.
 
Nimechoka kusoma hoja za kutetea dhambi maana baadhi ya majibu yananirudisha kwenye huzuni. Sikutegemea kama waislam wangepinga busara za mtume wao, eti huyo alikuwa mtupe uwezo ambao wengi wa waislam hawana, sasa nani role model wenu kiimani??

Ngoja nisome threads za mambo mengine.
 
Ndugu Phillipo Kidwanga nadhani unakosea unapolinganisha Jazba ya Maswahaba wa Mtume Muhammad (S.A.W) na Waislam wote....Si kweli kwamba Waislam hawana Subra kama Maswahaba. Mbona Wafuasi wa YESU walitumia Panga hadi kumkata sikio Askari mmoja wakati wa kukamatwa kwa YESU? Inamaana Wakristo wote hawana Subra pia? Sitaki kuamini...siku nyingine tafakari kabla ya kuandika.
 
Mkuu wangu ni wewe unayethamisha vitu hivi lakini kwao wao hawalitazami swala hili kwa picha yako.. Nitakufahamisha na nawaomba Wakristu wengine mnisikie kwa makini sana..

Kuna sinema moja inaonyesha jamaa mmoja millionea mwanamme aliweza kuwashawishi vijana wapendanao wawili ili atembee na mpenzi wake kwa siku moja atawapa millioni moja. Hawa vijana walikaa na kutafakari wakaamua kukubali ombi hilo na hivyo binti akaenda kwa tajiri kwa mapenzi ya siku moja wakitegemea ni jambo dogo sana kwa mavuno makubwa.. Lakini haikuwa hivyo kabisa, Fedha iliweza kushinda sawia na mapenzi ya dhati na hivyo kuvuruga mahusiano baina ya wapendanao. Ukawa mtihani mkubwa tofauti kabisa na vile walivyofikiria. Sinema ile inatufundisha nini?..

Kwa hiyo mkuu wangu, kwako wewe na mimi tunaweza sana kuthamini majengo ya makanisa na tukaiona hasara ya fedha lakini kwa hawa vijana Waislaam hiyo Kuruan kwao ina thamani kuliko hata maisha yao wenyewe. Na huwezi kuithamisha Kuruan kwa fedha au mali ndivyo wanavyoitazama dini yao..Hivyo basi wewe unapohesabu hasara ya majengo wao wanahesabu thamani ya imani yao kudharauliwa na matokeo ya mgongano huu ndio mavuno tunayoyaona.

nachowaomba ndugu zangu watanzania, UPENDO, kuthamini ya watu wengine na kuogopa majaribio ya Udini, kuheshimiana ndio njia pekee inayoweza kututoa hapa tulipo na kuanza mwanzo mpya. Dini usiyo iamini kwa nini watu wanapenda sana kuijaribu? iwe masheikh Misikitini kuwaita Wakristu majafir au Wakristu kujiaminisha Uislaam ni dini ya mashetani na kumkashifu mtume na vitabu vyao..Hawa watu huwa wanapata nini haswa? waacheni watu waabudu kiole wanachoabudu na hulazimishwi nawe kuabudu kile wanacho abudu, kila mmoja wetu atakwenda kaburini peke yake na amali yake pekee ndio itamwokoa yeye..

Mkuu,

Hapo ndipo kuna tatizo. Kutoheshimu wala si kuthamini. Kuthamini si rahisi mpaka uwe umejua faida yake. lakini ni muhimu kuheshimu kwa kuwa ni imani ya mtu mwingine. Kati ya dini hizi mbili kinacholeta kuvurugana ni kutoheshimu imani ya dini nyingine.
Kinacholeta uislamu kwenye spolite na hapo ndipo watu wanaporeact kokote wanapokutana na waislamu na kuita dini ya shetani ni kule kufanya vurugu. Watu wanaofanya vurugu hakuna mtu ambaye utamwambia eti huyo anayefanya vurugu, kulaani kwa ukali, aliyeko tayari kuua ( walikuwa tayari kumuua kijana aliyekojolea Qoran), kuhubiri chuki waziwazi nk kuwa ni mtu wa Mungu. Wanadamu wanamwelewa Mungu ni mstaarabu, mpole, mwenye uvumilivu usiokuwa na kikomo (ndio maana hata jambazi sugu bado anamwacha anapumua). Kinyume cha hizi sifa za Mungu ni sifa zinazoonyeshwa na waislamu hata kutamkwa kwenye Qoran waziwazi. Sasa binadamu wamepewa uwezo wa kuchunguza na kutafakari. Wakiona vitendo vya waislamu, wasome kitabu chao pamoja na kwamba kina vifungu vinvi vinavyosisitiza utengamano wanakuta pia kuna vifungu vinavyosisitiza uvunjifu wa amani. Watu wanajua Mungu ni mwenye upendo lakini neno hilo halipo au halina maana kabisa kwenye Qoran. Mwisho wa siku watu wanalebo uislamu na kitabu chao kama ushetani.
Mimi nadhani waislamu na uislamu ungekuwa dini ya thamani sana mbele ya macho ya wanadamu kama wangekuwa watu wapole, wavumilivu, wenye kuheshimu imani nyingine ( hata ukristo basi wauheshimu manake Qoran inakiri Uyahudi na Ukristo ulikuwepo kabla ya Qoran).
Sasa nnachotaka kukuambia Mkandara ni hard pill ambayo pengine hutaikubali na wala hutaiamini lakini mimi nafikiri ndio kitu kitakachotokea japo itachukua muda. Dunia inabadilika. Sasa dini aidha zitabadilishwa na dunia kama hazitaki kubadilika na kufuata mfumo wa kawaida wa binadamu wa kuishi pamoja na kupendana au zitaanza kukosa thamani yake kama dini. Hii ni kwa dini zote. Sikuambii kuwa ukristo ni utakatifu. Mimi ni mkristo lakini kuna mengi ya upuuzi yaliyokuwa kwenye ukristo ambayo hata ndani ya hicho kitabu chao kinachoitwa Biblia hayapo. Kwa hiyo na wenyewe kama hawaendi na upendo, haki za binadamu na kuthamini maisha watawekwa kwenye kapu.
Kilichokuza dini kwa karne nyingi ni ujinga na kukosa elimu kwa watu. Sasa elimu dunia ndiyo iko njiani. Yaani dunia yote inawasiliana na kujua kinachoendelea. Yale yaliyotokea kwenye nchi za kiarabu siyo tu ni mfumo wa utawala lakini hata dini zinaguswa. Itafika wakati ukifanya vurugu au kama mtu ataondoka akakojolee kuruani au kuchoma kanisa kwa kufanya vurugu, kuaharibu mali ya serikali na watu hiyo dini inayohusika itaanza kupoteza hadhi yake. Sasa Mkandara lazima ukubali kuwa dini zina mawazo mengi ya watu yaliyobatizwa maneno ya mwenyezi Mungu. Ukiwa kama great thinker lazima uanze kuwashauri ndugu zako waislamu waache dini ya binadamu wafuate dini ya mwenyezi Mungu ambayo ni upendo na uvumilivu. Ukiniambia kuwa wathamini Qoran kiasi kwamba wako tayari kumpiga aliyekojoa msikitini pasipo kuuliza, au kumpiga aliyekojolea Qoran pasipo kujali kufuata sheria lazima ujue hiyo ni dini ya binadamu inayotakiwa kukemewa kwa nguvu zote ili kuleta dini ya mwenyezi Mungu inayosisitiza kufuata sheria, kuwa wavumilivu na kupendana pasipo kujali dini.
 
Kwahiyo maswahaba huwa hawana subra!
Siyo kweli hawakuwa na subira, bali ni hali ya kawaida kuna wanaotaaruki. Muhimu ni kiongozi kudhibiti nidhamu ya kundi lake kama Mtume (SAW) alivyofanya. Maswahaba ni wafuasi ambao wapo walitaka kuhamaki na wapo waliotulia kuona hukumu itakayotolewa
 
Mkuu wangu sasa unaenda kusiko faa kabisa tunatoka ktk Mada. Hivi unataka kunambia Wakristu hawauwi?.. Mpaka mtu aue kwa jina la dini yake na ukatangaziwa ktk vyombo vya habari ndio unajua mtu mbaya lakini yule anayeua pasipo kuitumia dini wakati ni muumini wa dini hana hatia siyo.. What make the difference ikiwa leo Marekani ndio nchi iloshambulia nchi nyingine na kuua watu wengi ili kusimika serikali wanayoipenda..lakini wao wazuri sana, Huko Marekani kuna vifo vya risasi kila siku kuliko sehemu yoyote duniani lakini wao ndio wazuri kuliko watu wote duniani..mbona mnataka kutuaminisha uongo jamani.. Hivi kweli unaweza kunipa hesabu ya mauaji ya Crusade ukilinganisha na vita yoyote ya kiimani?..

Mkuu wangu tulipofika leo hii hatuna sababu ya ku provoke watu ili wa react na mseme hii ndio dini ya shetani isipokuwa ushetani ni wa roho, unapopanga kufanya, yale ulokusudia rohoni ndio shetani hivyo kifo pekee sio dhambi maana hata Mungu mwenyewe katuandikia watu wote tutakufa...Na huwezi kusema Mungu ni Shetani kwa sababu katuandikia kifo..
 
IM SORY BUT LET ME SAY THIS

All Muslims are terrorists.

So kill them one by one.

Eliminate this terrorist breed from earth.

They are most uncivilised animals.

Even a Dog is better than a muslim
Unakichokisema ni ujinga uliopitiliza. Si waislamu wote ni magaidi ingawa waislamu wenye siasa kali ni magaidi. Pili hata kama hao wenye siasa kali ni maghaidi bado si turufu ya kuwaua. Kuna sheria za kuwashughulikia. Labda hujitambui lakini ulichokiandika kinakuonyesha "you are the most uncivilized animal in the word".
 
Maggid,

As much as I agree na unachokizungumza pia uelewa yule Bedui alikuwa amelewa. Hivyo basi hujaelezea uhalisia wa jambo lilivyokuwa. Binafsi yangu I do not believe in violence but rather busara na hekima. Ndio maana nasema hivi suala la waislamu na wakristo ni vema likaangaliwa kwa macho mawili na uangalifu mkubwa. Niliwahi kushauri zamani kuwa iwepo TRUTH AND RECONCILIATION COMMITTEE. Watu wakanibeza but ukweli wa mambo ni kwamba waislamu wana joto lao moyoni linawauma. Waislamu wengi wanaamini Nyerere alitumika kuukandamiza uislamu (refer to Mohamed Said books). Vile vile baadhi ya mambo yanayofanywa na wakristo kukandamiza waislamu mfano wanapokejeli ati wao wamepeleka mwanzo MOU wakati sio kweli waislamu walipeleka mwanzo MOU ikapigwa chini (refer to Mohamed Said books), kunapelekea kuona waislamu wanaonewa.

Tukirejea suala la huyu kijana nadhani maggid you are misleading kwa sababu huyu ni kijana wa miaka 14 (inamaana ana fahamu zake na akili timamu kwasababu umri huo mara nyingi vijana wa kiume wanabelehe) hivyo basi anajua fika kitu anachokifanya na kwanini anafanya. Usimfananishe na mtoto wa miaka 7 ambaye hata kuoga hajui. Hapo Maggid unakosea. Vile vile mtume alitumia busara kuwaambia masahaba wamuachie yule bedui kwasababu alikuwa kwanza amelewa na pili hajui anafanya nini. Kisheria tunasema he is in the state of unsound mind. Hata kwenye macho ya kisheria ukiuwa katika hali hiyo unakuwa unapewa punishment pungufu kwasababu wanachukulia hukuwa unafahamu unachokifanya. Sasa huyu kijana alikuwa anajua fika analolifanya na sio kuwa alikuwa amelewa au hafahamu.

Hivyo nakushauri siku nyengine unapogusa suala la waislamu kuwa na ufahamu kidogo wa kitu unachokizungumzia. Yes hekima na busara ni muhimu katika jambo hili but GET YOUR FACTS RIGHT !!!!!

Nilikuwapo!!!!
Mkuu ulichosema ni kweli, lakini kwa tukio la Mbagala, mimi nakubaliana na Majjid na Mtoi. Haikuwa busala kuhamaki kama kulivyotokea. Tatizo letu waislam ni migawanyiko tuliyonayo na sio wakristo kama wengi wanavyodhani.
Quran inasema zaidi ya mara moja
"shikamaneni katika kamba moja ya Mwenyezi Mungu na msifarikiane" then inasema
"pindi mnapofarikiana basi rudini kwa Allah na Mtume (SAW)" .
Hatutafanikiwa hata siku moja kama hatutafuata mafunzo na hadithi za Mtume (SAW) kama Quran inavyosemwa "Mwenyezi Mungu habadili hali/kitu kwa watu, mpaka hao watu wajibadili wenyewe"
 
Matokeo ya machafuko huwaathiri wote bila ya kujali dini zao.Wanaoshabikia fujo hawawezi kuthibitisha kuwa baada ya uharibifu wote na kejeli na matusi uliofanywa na waislamu sasa watakuwa wamerizika kwa lolote lile.Maswali ya msingi bado kujibiwa na ndugu zetu hawa.Kwanini wasimwadhibu na yule aliyetoa kurani ikojolewe?Je ni wakristo wa madhehebu yote na watu wa dini zingine walistahili kutendwa hivi kwasababu ya mtu au familia moja?

Madai yao ya kuonewa popote pia yanaweza kuwa ya dhana tu au ya ukweli kama itathibitishwa.Je wanajua madai ya watu wa dini zingine pia?Wapo tayari kuona nao wanajichukulia sheria mikononi kupata watakalo?Ni vema waislamu wote wajue kuwa si wote ni mbumbumbu kama watudhanivyo.Wengine tunajua kuwa tangu ukoloni hai uhuru na hata leo nchu hii inaongozwa kiislamu na kuwapendelea katika mambo mengi.Bahati mbaya kila tukijitahidi kuuueleza tunaishia kuzimwa na mfumo uliopo unaowapendelea waislamu kwa dhahiri shahili.
Hii nchi watu wengine wasizime haki za wenzao kwa kujiona wao ni bora sana kulio kama vile wao wana damu ya kijani wakati wenzao ni nyekundu.Kweli itadumu hata milele
 
Tukirejea suala la huyu kijana nadhani maggid you are misleading kwa sababu huyu ni kijana wa miaka 14 (inamaana ana fahamu zake na akili timamu kwasababu umri huo mara nyingi vijana wa kiume wanabelehe

hata kama angekuwa ni wa miaka 100, je msahafu unahalalisha kuchoma makanisa na kuiba mali za kanisa, je hilo ni suluhisho? kwani aliyefanya kitendo hicho ametumwa na makanisa yaliyovamiwa?
 
Maggid,

As much as I agree na unachokizungumza pia uelewa yule Bedui alikuwa amelewa. Hivyo basi hujaelezea uhalisia wa jambo lilivyokuwa. Binafsi yangu I do not believe in violence but rather busara na hekima. Ndio maana nasema hivi suala la waislamu na wakristo ni vema likaangaliwa kwa macho mawili na uangalifu mkubwa. Niliwahi kushauri zamani kuwa iwepo TRUTH AND RECONCILIATION COMMITTEE. Watu wakanibeza but ukweli wa mambo ni kwamba waislamu wana joto lao moyoni linawauma. Waislamu wengi wanaamini Nyerere alitumika kuukandamiza uislamu (refer to Mohamed Said books). Vile vile baadhi ya mambo yanayofanywa na wakristo kukandamiza waislamu mfano wanapokejeli ati wao wamepeleka mwanzo MOU wakati sio kweli waislamu walipeleka mwanzo MOU ikapigwa chini (refer to Mohamed Said books), kunapelekea kuona waislamu wanaonewa.

Tukirejea suala la huyu kijana nadhani maggid you are misleading kwa sababu huyu ni kijana wa miaka 14 (inamaana ana fahamu zake na akili timamu kwasababu umri huo mara nyingi vijana wa kiume wanabelehe) hivyo basi anajua fika kitu anachokifanya na kwanini anafanya. Usimfananishe na mtoto wa miaka 7 ambaye hata kuoga hajui. Hapo Maggid unakosea. Vile vile mtume alitumia busara kuwaambia masahaba wamuachie yule bedui kwasababu alikuwa kwanza amelewa na pili hajui anafanya nini. Kisheria tunasema he is in the state of unsound mind. Hata kwenye macho ya kisheria ukiuwa katika hali hiyo unakuwa unapewa punishment pungufu kwasababu wanachukulia hukuwa unafahamu unachokifanya. Sasa huyu kijana alikuwa anajua fika analolifanya na sio kuwa alikuwa amelewa au hafahamu.

Hivyo nakushauri siku nyengine unapogusa suala la waislamu kuwa na ufahamu kidogo wa kitu unachokizungumzia. Yes hekima na busara ni muhimu katika jambo hili but GET YOUR FACTS RIGHT !!!!!

Nilikuwapo!!!!

ndg. Mdondoaji, kwa kufuata jina inawezekana ndg.Maggid ni muislam, na kama ni muislam, basi kama angekuwepo katika kundi la waislam wa Mbagala basi ninaamini tukio lile la aibu lilofanyika kule Mbagala lisingefanyika, maana yeye (Maggid kwa thread hii amekuwa kama mtume - ameleta ujumbe wenye mantiki "polite" wa kufanya tutafakari na tusimpige "bedui" kuliko waislaamu wengine waliyochangia katika thread mbalimbali zinahusiana na tukio hilo la aibu). Inawezekana ametafakari sana na amerudisha upanga wake kwenye ala ili usilete madhala makubwa humu JF isije ikawa kama wale walioshiriki kule Mbagala.

Maggid, ameleta hoja ambayo naweza sema kama ina ujumbe ambao yeyote anayeongelea habari za Tume ya Maridhiano (ambayo wewe ni muumini) angeusema.
Nadhani na ninaamini unashangaa kumuona Maggid muislaam mwenzio anawasaliti kwa kuwa tofauti na waislaam wenzake (na wewe ukiwemo)kwa kuleta thread yenye mantinki kama hii, na hata ametoa baadhi ya mafundisho ya Mtume humu JF? Kitu ambacho waislaam wengi huwa hawapendi mambo ya imani yenu yawekwe hadharani.

Sijakuelewa, unapodai kuwa yule mtoto aliyekojolea kile kitabu ni mkubwa na hakuwa na sababu ya kufanya vile kwa sababu anafahamu na akiri zake timamu, napenda kukuuliza yafuatayo:-
(a)Je yule mtoto mwenzake aliyeleta kile kitabu na kufanya dhihaka ile kubwa alikuwa na umri gani?
(b)Je huoni yule mtoto (muislaam) aliyekuwa na kile kitabu hakuwa mzembe na mpumbuvu kwa kudhurura na kitabu kitakatifu mitaani na kukifanyia dhihaka?
(c) Huoni yule mtoto alikuwa ni "bedui" ambaye alikojoa msikitini na kwa sasa ameishaelewa makosa aliyofanya kwa kufanya dhihaka ile na kile kitabu?
Mwisho nadhani uache kuendelea kutetea ujinga na hamasa ambazo hazipo kwa masilahi ya uislam (unauamini, siasa, dini,utaifa,na mahusiano mengine katika jamii yetu?
ASANTE SANA MAGGID kwa hoja yako yenye mantiki
 
Back
Top Bottom