WORLD VISION ni shirika la wachaga??

WORLD VISION ni shirika la wachaga??

Status
Not open for further replies.
Mimi nimeanza kuijua World vision muda mrefu na walikuwa na miradi mingi sana mkoa wa Kagera na most of people na wengine nikiwa nawajua walikuwa ni Wahaya na Wanyambo na sikuwahi kuona Mchagga hata mmoja, kadri illivyoendelea nimeshuudia watu wengi wakiwemo marafiki zangu wakiwa wameajiliwa na hiyo World Vision na wote ninaowajua na wana nafasi kubwa si Wachagga. ni Mchanganyiko wa makabila ila Wakristo. Kwa hiyo ili uweze kuajiliwa lazima uwe Mkristo na hiyo siyo hoja maana waanzilishi wameweka sharti ilo. Kwa hiyo hoja ya kusema World Vision ni ya Wachagga kwa kweli inanipa ugumu kuamini. Mimi mwenyewe hapa siyo Mchagga kusema kwamba nawatetea bali naongelea kile ninachojua kuhusu World Vison

Mkuu, sijasema kuwa hakuna makabila mengine, kwani wapo hata baadhi ya 'vigogo' wa shirika wanatoka makabila mengine!!! Nimetoa mfano hapo juu, Zonal Manager wa Eastern Zone ni msukuma!!
Halafu hapo Kagera unapoongelea (lake zone) ni moja kati ya ADP chache ambapo kipindi wanafungua mradi kuna watu walipambana sana kubakikisha ni wazawa ndio wanapewa kipaumbele katika kuajiriwa!! La sivyo hali ingekuwa kama huku kwingine..
Kuhusu WVT kuajiri wakristu mimi binafsi sina shida na hilo, kwani naamimi wanasababu za msingi kuweka hiyo policy..
 
Na huyu mtu anatuambia na anataka kutwambia kwamba ni consultant. Kama kweli u-consultant uko hivyo nadhani kuna kasoro mahali. Maana kama kweli alitaka kufanya analysis ya kweli angeangalia sehemu nyingi za kazi na kutwambia Waruguru wako wangapi kila taasisi kulinganisha na Wachagga, Wahaya, Wanyakyusa na Wanyasa, kisa aende vyuo vikuu aangalie rate ya wanafunzi je wengi wanatoka katika makabila gani, na je kweli Waruguru, Wasambaa, wanashindana na makabila niliyotaja. Tuje hata walimu wa vyuo hivyo je ni Wasambaa, Wazigua, Wabondei na Wadigo, Wangulu, Wakagulu, Wasagala, Wapogolo, Wandamba wangapi katika vyuo hivyo. Watu wenyewe wa mikoa hiyo anayotaja wamekalia kupiga ngoma na kumtoa mwali shule saa ngapi ili wafanye kazi World vision? Penye ukweli lazima usemwe haya makabila ya Tanga na Morogoro si wote wana uwezo wa kufanya kazi world vision maana shule hawaendi.

Hili nimeshalisemea, labda nirudie tu!! Kabla ya octoba mosi 2013 ukiwa na cheti cha kidato cha nne unaajitrwa kama DA, na staff wengi wa WVT ni Hawaii (hii tittle ilibadilishwa august 2013 kwasasa wanaitwa SPF) Sasa huu usomi unaousema unaingiaje hapa..
 
nashindwa kuelewa kama PWC, KPMG, n.k nao wana ukabila

WVT na KPGM wako tofauti sana na mizizi yao ni tofauti sana!!
Sitegemei kama utalielewa bandiko langu kwasababu hauielewi vizuri WVT!!! Niambie uko mkoa gani nikuelekeze ofisi zao zilipo alafu jaribu kupiga stori za kawaida tu na staff wao, then chomekea hilo suala!! Majibu utakayopewa utaelewa naongelea nini!!! Kisha rudi hapa uendelee kunitukana..!
 
Huna tofauti na yule mnyama anaezaa na kula watoto nimesahau jina lake

Mnyama huyo ni...

summer-pigs-080.jpg
 
Nimeishi sana arusha na huku ndiko makao makuu yao na wana Projects nyingi sana wenyewe wanaziita ADP's cha ajabu kila ADP ofisini wote ni wachaga! Nilishtuka kidogo lakini nikapotezea nikajipa moyo labda 'mcheza kwao utunzwa' (wachaga>>arusha) baadae nikahamia tanga nako wana ADP nyingi sana wilaya tofauti tofauti nako pia hali ni ileile kila ofisi ya ADP unayoenda wachaga wamejaa!!! Ikaniuma kiduchu nikajipa moyo labda kwasababu tuko nao karibu (tanga na arusha).. sasa last week nimekuja Morogoro nikaenda pale ofisi yao kuu ya mkoa (MOROGORO CLUSTER OFISI) nikakuta ofisi wachaga 90%!!! Kesho yake nikaenda kwenye moja ya projects zao inaitwa MLALI ADP iko ndani ndani kabisa vijijini huko nako project manager mchaga, project accountant mchaga, zagazaga nyingine nao 80% wachaga!! Nikafadhaika sana ikabidi nimuulize swali mmoja ni Staff wa hapo mlali adp (sio mchaga) akanijibu kuwa hata yeye aelewi ila hali ni hiyo hiyo karibia tanzania nzima, yeye binafsi kabla ya kuja mlali alikuwa ofisi ya kigoma nako hali ni hiyo hiyo, wachaga wachaga wachaga!!!! Nikachoka..

------------------------

UPDATE

Sina shida yeyote na World Vision kuajiri wakrist kwasababu wao ni shirika la kikrust na hiyo ni policy yao na katika kusajiliwa imesajiliwa hivyo! Siko hapa kuongelea DINI.. Wapo wanaosema naendekeza ukabila kwa kuzungumzia wachaga, lakini mimi naamini kuwa kama kuna mahali tunakosea ni vizuri kusahihishana, na wanachofanya hawa wenzetu wa World Vision si sahihi hata kidogo...
Binafsi sinawahi kuomba kazi World Vision wala sijawahi kufikiria hilo lakini nimefanya nao kazi mara nyingi sana nikiwa kama consultant (kama ambavyo nafanya kazi na mashirika mengine mengi). Kwa mfano; mwaka 2006 nilishiriki kufanya evaluation ya mradi wa Mlali ADP na kuandika proposal ya kuomba extension ya miaka mitano ya mradi (mradi ulikuwa unatakiwa kuphase out mwaka huo) na 'wazungu' wakawapa extension! Mwaka 2008 nilihusika tena kuandaa proposal ya kuomba extension ya pili ya miaka mitatu na 'wazungu' walikubali.. ieleweke kuwa huu ndio mradi pekee toka kuanzishwa kwa World Vision Tanzania ambao ulifanikiwa kupata extension mara mbili.. mpaka leo hii watu wanashangaa tulifanya 'mazingaombwe' gani mpaka wale 'wazungu' wakakubali.. hivyo naomba ieleweke naifahamu vilivyo World vision na najua ninachokiongea..

Nirudi kwenye mada, kuna watu hapa wanadai kuwa shirika limejaa wachaga kwasababu wao ati wamesoma sana, huo ni UONGO wa hali ya juu.. nitaeleza.. katika shirika la world vision majority wa staff wake ni jamaa wanaitwa CRS (mwaka 2012 walibadilishwa jina na kuitwa DA, na kuanzia Oct 1, 2013 wameanza kuitwa SPF) hawa jamaa (CRS/DA) kabla ya octoba mwaka jana karibia wote walikuwa ni form VI leavers!!! Walikuwepo mmoja mmoja wa kuokoteza ndio walikuwa form six, na wengine wana certificate!! Waratibu wa miradi na baadhi ya PF ( project facilitator) ndio walikuwa na shahada! Lakini DA's/CRS karibia wote hawakuwa hata na diploma (hapa tunaongelea zaidi ya wafanyakazi 1500 tanzania nzima)! Ni mwaka jana tu hapa octoba ndio wamebadilisha hiyo tittle na kuiita SPF (sponsorship and project facilitator) na wakaweka sharti muombaji awe na angalau diploma! Lakini miaka yote hawa jamaa walikuwa ni form VI leavers tena wale waliokosa nafasi za kwenda advanced level!! Sasa ninyi wenzetu mnaopiga kelele kuwa wachaga ni wasomi ndio maana wamejaa World Vision, mnataka kutuambia kuwa hakuna WALUGURU waliomaliza form VI mpaka mchukue form VI wa arusha muwapeleke Morogoro, inamaana hakuna WAHA Waliomaliza form 4 mpaka mpeleke wachaga kigoma, hakuna wazigua wenye form 4 pale korogwe na lushoto na korogwe????
Cha kushangaza zaidi kuna ADP moja pale Morogoro cluster office, ambapo wameajiri Office attendant (mfagiaji) mchaga kutoka arusha huyu dada anaitwa Matilda! Inamaana waluguru na wapogoro hawajui kufagia!!! Unaweza kusema hii ni coincidence?????

Asavali ulalamike mdau,hata mimi napeleka malalamiko wizara ya kazi kwa nini bodaboda wote ni vijana wa kiume,kwani wanawake hawawezi!

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Hili nimeshalisemea, labda nirudie tu!! Kabla ya octoba mosi 2013 ukiwa na cheti cha kidato cha nne unaajitrwa kama DA, na staff wengi wa WVT ni Hawaii (hii tittle ilibadilishwa august 2013 kwasasa wanaitwa SPF) Sasa huu usomi unaousema unaingiaje hapa..

Kweli,na sasa hv SPF wenye Divisheni Faivu wanachukuliwa pia!

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Mzee Es,
Naona kati ya wote, wewe peke yako tumekuacha mataani!... ndio hivyo mzee usituone mtaani, wengine asili yetu bara - deep msituni.
Jasusi,
Sio tu nakimanya ndio lugha yangu ya kwanza! - Magamboki mozowe!
Kyomo,
Unajua mshikaji ktk kuleta tamu ya gumzo vitu hivi vipo. Na baya kuliko yote ingawa tunayachukulia juu juu mambo haya lakini tukumbuke kwamba mtaalam hapa ni mvuvi Mkerewe sio yule wa Marekani ama mbongo msomi aliyetumwa. Kwa sababu jibu la utafiti wote huo lilikuwepo Ukerewe kwa mvuvi na kilichofanyika hapa ni kutafsiri tu utafiti wa mvuvi.
Hivyo basi - efwi zyona zafilwe ndio utafitri wenyewe na jawabu isipokuwa lugha tu ndio imeondoa uzito wa elimu ya mvuvi, ikafuatia All fish dead huyo msomi m-swanglish, kisha wakamalizia na A hundred percent of biota exhibited mortality rate huko Ulaya na kuwa somo la elimu ya juu..huyo mwandishi wa kitabu atatajirika hali mkerewe mvuvi mtoa jibu, ataendelea kuwa maskini.
Ndio maana mimi husisitiza kuwa Wakulima wanbantu,, hao kina Mwanakijiji, sisi wavuvi na wafugaji ni utajiri wa elimu ambao tumejaaliwa na Mungu isipokuwa tumeshindwa kuutumia ktk mazingira haya mapya kutokana na uzembe wa viongozi wetu ambao wanaamini kabisa solution ya umaskini wa mtu mweusi ni misaada na wasomi toka nje!.
Hakuna dawa ya Umaskini isipokuwa kutambua vipaji hivi na -KUWAWEZESHA WATU WEUSI ku-invest ktk utajiri wao.

Tehe tehe tehe! Hatari sana
 
Ukianza kuongelea Nepotism usione aibu ingia tu moja kwa moja...
Anzia kwenye siasa,Nenda kwenye utawala, nenda kwenye masuala ya kijamii,dini,huduma na sehemu nyingine...
 
kwa nini world vision kwenye interview wanauliza maswali ya kwenye vifungu vya biblia mkuu..?

Unatia aibu, jifunze kusoma kwa kina na jitahidi kuelewa mambo. World Vision na Compassion International ni Mashirika ya Kikristo, yamesajiliwa hivyo, hii no pamoja na partners wao. Hata hivyo, beneficiaries ni watu wa imani tofauti; ukikuta nako wapo watu wa dini moja hapo utakuwa na haki ya kuhoji.
 
Kwenye huu mjadala kuna watu wawili wanatuvuruga sana, watu hao ni Abakoramo na Jibwa, Mods tuondoleeni post zao humu, zinashusha hadhi ya JF.
 
kwa nini world vision kwenye interview wanauliza maswali ya kwenye vifungu vya biblia mkuu..?

Jibu : Lile ni Christian organisation na msingi wao umejengwa katika biblia na mwajiriwa lazima awe Mkristo na ili kujua kama wewe ni Mkristo wa kweli lazima upimwe kwa Biblia. Au kupima kama mtu ni mkristo au la una shauri vipimo gani vitumike ili kuepuka wazee wa kuchakachua na magumashi
 
Hawa wachaga bas watakuwa ni wengi sana maana CDM mnasema ni wachaga, TRA nako wachaga, Wizara ya fedha wachaga, CRDB wachaga na sasa World Vision. Kuna siku mtasema Tanganyika ni ya wachaga

Hivi alivyopata hiyo Consultancy Mlali alikuwa Mchagga pia? Hivi hawa wachagga mnataka kuwafikisha wapi kwani inaonyesha hawatakiwi kuwa idara moja wawili au watatu. Mtazamo huu wa kikabila ukiruhusiwa kuna kila dalili za kuivuruga nchi
 
mkurugenzi mkuu-tim andrew-mmarekani.
nd-devocatus kamara -mhaya.
fd-moses uwoth-kenya.
james mathenge-kenya
alex malekia-mchaga.
yosh kasilima-mhaya.
greefing zakayo-mchaga.
amithay kuhanda-mnyamwezi.
ladislaus mganga-musoma
john parmar-india.
 
Nimejaribu kusoma and kutafiti kwa haraka na nimegundua kuwa huyu jamaa ana lake jambo ambalo ingekuwa vyema ajadili mwenyewe rohoni pengine lingeleta maana badala ya kuleta hapa jamvini.


Jambo amablo tungeweza kujadili kwa kina hapa kuhusu WV ingekuwa kama:

World Vision kama ni ya Kikristo kwa nini wamefukuzwa baadhi ya nchi Duniani???
Is World Vision a CIA front as it has access under cover as samaritans???
Is World Vision doing right???
Why does the highest ranking leaders of World Vision - CIA????

Haya ndiyo mambo ya msingi kujuzana na sio ukabila. Unaongelea ukabila wakati pengine janga ni la kidunia. Ukiweka mchagga katika ramani ya dunia ni tone katika bahari.

Lest discuss this way.

Nawasilisha
 
Tatizo nyie wachaga mko kila mahali- sasa hata wakitaka kupata watu wa eneo husika- ghafla anatokea mchaga.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom