Wolper 'amsapraiz' baba mtoto wake kwa dhahabu ya Tsh. Milioni 25! Leo Birthday ya Rich Mitindo

Ambakucha

JF-Expert Member
Aug 16, 2019
277
445
Nyota wa Sinema za Bongo, mjasiriamali na mwanamitindo anayepanda kwa kasi nchini, Jacqueline Wolper 'amevunja kibubu' kwa kumnunulia baba wa mtoto wake, Richi Mitindo zawadi ya cheni mbili, pete moja, vyote vya madini ya dhahabu (gold) kwa thamani ya Shilingi Milioni 25 ikiwa ni 'sapraizi' katika siku ya kuzaliwa ya mfanyabiashara huyo maarufu jijini Dar.

Rafiki mmoja wa Wolper amesema kuwa, leo Juni 18, 2022, Richi Mitindo anagonga miaka kadhaa ya kuwepo kwake chini ya jua (kuzaliwa) ambapo Wolper au mama P akaamua kumfanyia 'shoping' baba wa mtoto wake huyo bila kujali gharama kubwa.

Rafiki huyo alisema: "Yeye (Wolper) alitamani ampe zawadi kubwa zaidi ya hizo cheni na pete. Lakini kwa vile aliamua kumfanyia 'mshtuko' huo kwenye 'bethdei' yake ya leo, ndipo jana akaamua kumnunulia gold hizo zenye thamani ya Shilingi milioni 25."

Cheni hizo; moja ina mzunguko wa kawaida, ya pili ina mzunguko wenye kidani cha Msalaba, pia cha gold, kama ishara ya imani ya kiroho ya baba mtoto wake huyo.

Zote mbili, kila moja ipo ndani ya mkebe wake kama ilivyo kwa pete. Na mikebe hiyo inafunguka kama kompyuta mpakato (lap top).

Wolper mwenyewe alipopatikana asubuhi hii, amekiri kumfanyia shoping baba mtoto wake huyo huku akisema: "Bethdei yake nyingine huenda nikamjengea nyumba kabisa."

Richi Mitindo ni mfanyabiashara anayemiliki duka la kuuza T-shirt za jumla (Kariakoo), pia ana duka la kuuza suti na viatu vya kuvalia suti na mikanda ya kisasa (Makumbusho) na ni mwanamitindo maarufu.

Ameendelea kuzoa sifa kuwa mwanaume aliyeibuka kidedea kwa kumpa ujauzito Wolper na kujifungua baada ya kitambo cha kusaka mtoto bila mafanikio.

Itakumbukwa mwaka jana, mitandao ya kijamii ilizua gumzo kufuatia kauli ya Wolper aliyosema; 'mwanaume atakayenizalisha mtoto nitamjengea nyumba.'

Ndipo alipozaliwa Paschal maarufu kama P na Rich Mitindo kutajwa kuwa ndiye baba wa mtoto huuo ambaye tayari ametimiza mwaka mmoja huku akiwa ni balozi wa Duka la nguo la Moni Baby Diper ambalo linauza nguo, viatu na bidhaa nyingine mbalimbali.

Screenshot_20220617-192541~2.jpg
Inside-Jackline-Wolper-and-Rich-Mitindo-Engagement-Party.jpg
 
View attachment 2264433View attachment 2264434
Wanamitindo!
 
To each his/their own...

Anyway pesa ni nyenzo ya kufanya kile roho inapenda na kupanga ni kuchagua (na hapo huenda amenunua front page kwenye magazeti ya udaku na kutupotezea muda wajenga nchi kujadili non issues

Well that's a second Wasted which I will never get back...., ngoja nisiendelee isije kuwa dakika....
 
Harmonizer si alisema ana kaharufu,akapiga chini!
Dem star ivo hivi anaweza kua na kaharufu kweli?
Ila dem mwenye kaharufu ni changamoto sio siri aisee, japo huwa wanatumia perfume na spray kichizi ila bado huwa kanakuwemo tuu.

Au labda jamaa ndo kalikua kasababu ka kumtema demu kimazebe.
 
Back
Top Bottom