Iringa: Afungwa Jela Maisha na Faini ya Tsh. Milioni 5 kwa Kubaka Mtoto

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa imemuhukumu Mkude Nziku kifungo cha maisha jela na fidia ya Tsh. milioni tano baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka Mtoto wa Kaka yake mwenye umri wa miaka 11 na kumuondolea usichana wake.

Kesi hii ilikuwa na Mashahidi wanne akiwemo Mtoto mwenyewe aliyebakwa, Mama Mzazi, Daktari pamoja na Polisi aliyechukua maelezo ya awali.

Inaelezwa siku ya tukio Mtuhumiwa aliingia chumbani kwa Binti huyo kupitia njia ya dirisha akamchukua Mtoto huyo kwa nguvu kutoka kitandani akamuweka chini na kumvua nguo zake za ndani kisha kutenda unyama huo “Alinivua sketi akaivuta nguo yangu ya ndani akaniingiza ‘LIDUDE’ lake sehemu ya kukojolea nilihisi maumivu makali nikapiga kelele Mama akaja chumbani kwangu lakini Mkude akakimbia”

Shahidi wa pili ambaye ni Mama mzazi wa Mtoto huyo amesema baada ya kusikia kelele za Mwanae alitoka haraka hadi chumbani kwa Mwanae akapishana na Mtuhumiwa sebuleni na alianza kumkumbiza, Mkude akaanguka chini na Mama akammulika na taa yake ya Solar na kumtambua kuwa ni yeye na akamuuliza ulikuwa unafanya nini chumbani kwa Binti yako (Mtoto wa Kaka yako) Mkude akadai kuwa alikosea nyumba kisha akakimbia na Mama alivyorudi chumbani akamkuta Mtoto wake akilia kwa maumivu makali na alivyomkagua akaona akitokwa na damu sehemu za siri.

Kesi hii imesimamiwa na Waendesha mashtaka watatu upande wa Jamuhuri ambao mi Nashon Simoni, Simon Masinga pamoja Batton Mayage ambao waliomba itolewe adhabu kali ili iwe fundisho kwake na wengine wanaotarajia kufanya kosa la namna hiyo kutokana na ongezeko la makosa ya ubakaji na ulawiti Mkoani humo.
 
So sad nyege zinafanya kijana akaozee jela, akizubaa na huko jela anaweza akabakwa na yeye
 
Back
Top Bottom