Wizi wa magari Dodoma

Hizi majuzi nimesikia watu watatu ninao wafahamu wameibiwa magari Dodoma. Na jhuu wizi unafanyika kibabe sana, wanakuja nyumbani wanafunga grill zenu kwa kufuli hata mkiamka wakato wanawasha gari msiweze kutoka.

Tena naskia kama una geti la ku slide wanaruka ukuta wanaingia ndani kisha wanavunja kufuli na kifungua gari...

hawa jamaa inaelekea ni wajuzi sana kiasi kwamba wanaweza washa gari lolote na hata kama lina alarm zinakuwa disabled.

Magari wanayopenda mpaka sasa ni Run X, Toyota Allex, Kluger, IST, n.k

Ushauri
Tufunge car tracking, japo sijui kama wanaweza.kuzi.disable au kujua kama ipo

Funga kamera nyumbani au motion detector

Kama kuna mwenye ujuzi zaid tujuzane maana hii hali ni hatar kw mkoa wa DODOMA kwa sasa... Polisi naona ni kama wameanza mishe za kuyasaka.. Mungu atusaidie.

Sent using Jamii Forums mobile app
Bado kuna wezi wa magari na hawakamatwi! Tupo na technolojia ndogo sana nimeamini.
 
Jaribuni kuwa wabunifu. Ukiachana na njia official kama za kuweka alarm, tracking devices etc fanya ujanja wa kuzaliwa. Sehemu unapolaza gari isiwe mbali na dirisha la chumba unacholala, halafu tafuta nguzo ya chuma ndefu eg taruma la reli. Ichimbie chini kama unavyosimika nguzo za umeme , lakini iingie ardhini karibu yote na uache ichomoze kwa juu kama futi moja tu. Imarisha na sementi ikiwezekana. Kwa juu ya nguzo chomelea sehemu ya kuweka mnyororo. Wakati wa kuilaza gari isogeze gari mpaka isimame juu ya nguzo (nguzo iwe imechomoza kwenye uvungu wa gari). Kisha tumia mnyororo wa chuma imara, ingia uvunguni wa gari na kufunga eg diff ya gari kwenye nguzo kwa kofuli kubwa na imara. Wezi watakapokuja hawatajua kuwa kuna kikwazo cha aina hiyo. Wakiwasha gari na kujaribu kuliondoa halitasogea. Fanya ubunifu zaidi kwa kuunganisha huo mnyororo na taa na spika zilizofichwa sehemu. Spika unganisha na kinasa sauti utakachorekodi sauti. Wezi watakaposogeza gari likivuta ule mnyororo taa ziwake ziwamulike huku spika ikipiga kelele ''ua, washenzi hawa'' ua wezi hawa''
aiseee..kazi ipo. 🙇‍♂️ 🙇‍♂️
 
Wee jamaa ni nyoko nimecheka sn aisee, kasajili wazo uanze kula mpunga mkuu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wee jamaa ni nyoko nimecheka sn aisee, kasajili wazo uanze kula mpunga mkuu!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbinu local ziko nyingi sana mkuu. Haya nyingine: Unachimba mifereji miwili sambamba. wakati wa kupaki gari unalengesha tairi kwenye mifeji. Yaani tairi za kushoto zinaingia kwenye mfereji wa kushoto na tairi zote za kulia zinaingia kwenye mfereji wa kulia. gari itakaposimama iache nafasi ndogo sana uvunguni, yaani iwe kama imetolewa matairi ikakaa chini. Halafu kwa chini, chimba shimo uweke bomba liende chini kiasi halafu likate liende upande upande halafu likate tena kona litokeze juu. Yaani iwe kama bomba la maji machafu. Sasa ndani ya bomba weka mnyororo imara unaoanzia pale unapopaki gari unaingia ndani ya bomba halafu unafuata bomba moja kwa moja mpaka linapotokeza juu. Wakati wa kupaki gari kabla hujaliingiza kwenye vile vimfereji funga ule mnyororo kwenye diff ya gari. (unatakiwa mnyororo uwe mrefu kufikia sehemu gari liliposimama kabla ya kuingia kwenye mfereji) Ukishafunga lisogeze liingie kwenye vile vimfereji. Likishaingia nenda upande wa pili unapotokea ule mnyororo uvute mpaka uwe taiti kabisa halafu ufunge. Sasa mwizi atakapokuja kwanza atashangaa gari liko chini kabisa na hawezi kuona uvungu wa gari kwa chini kwani hakuna nafasi. Akiliwasha na kutaka kulisogeza ule mnyororo unazuia (kumbuka umefungwa sehemu imara na hajui) Hata akijua chini kuna kizuizi hawezi kukitoa kwani hawezi kuingia uvunguni mwa gari. Kesho yake wewe ukitaka kuliondoa unafungua ule mnyororo upande wa pili unalisogeza gari na likishasogea unaufungua!
 
Insurance inakava wizi mkuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Motor insurance ziko hivi
1.third party cover inalipa yule uliemgonga wewe utajijua.
2.third party,fire and theft cover hii inalipa yule uliemgonga,gari ikiungua au ikiibiwa.
3.comprehensive cover hii inakulipa ukigonga,ukigongwa,ikiibiwa,ikiungua moto,ikiangukiwa na mti etc ndio tunaita bima kubwa.
 
Unapolala toa battery ya gari weka ndani.
Ukilala toa upepo tairi zote.

Hakikisha unakicompressor kidogo cha kujazia upepo kinachotumia 12VDC.
hahaha siku utakayotembea uchi(kusahau kufanya hayo) ndio utakayokutana na mama mkwe(majambazi)
 
Unamjua RRONDO vizuri linapokuja suala la Magari au unamsikia tu? Maana naona unaanzisha ligi ambayo sidhani kama utaiweza.......in short RRONDO yupo vizuri sana kwenye Magari.
Mimi mwenyewe nimeona ila nikampotezea. Anaongelea yenye Distrubutor, yale mambo ya condenser na point😂😂😂 sitaisahau gari ya mzee Hilux 12R, tuliisukuma ili tustue almost the whole day bila kitu kuwaka. Kumbe distributor imecheza kidogo sana. Ile condenser ikiingiliwa tone la maji kidogo sana(ambalo haliwezi kubeba hata corona vurus) inatengeneza kutu on the post so haiwezi kutengeneza sparks. Yaani ukiangalia magari ya leo, dah! Technology imekua sana. Magari yetu enzi hizo unatembea na spana za kufungua nati na bolt zote, Msasa na takataka zote.

Kiufupi nadhani tuanzishe uzi wa kujadili kero za magari ya zamani. Eti leo gari unaipaki kwa Handbrake, zamani ni lazima uweke mawe taili angalau mbili.
 
Back
Top Bottom