Wizi wa vipuri vya magari umeanza upya, Serikali mpo wapi?

ruukada

Member
Feb 24, 2014
67
117
Niliandika kuhusu wizi wa vipuli vya magari ulivyoshamiri hapo zamani kidogo, serikali kama ikasiliza kilio cha wananchi wake sana sana wa Dar es salaam, kupitia mkuu wa mkoa wa Dar es salaam serikali ikafanya kampeni ndogo (siwezi kusema kubwa kwa kuwa wote tunajua) wakatishwa watu wanao uuza vipuli za magari Ilala na maeneo mengine, wengine mpaka maduka wakafunga, lakini kwenye ‘kitovu’ cha uwovu pale Kariakoo maeneo ya gerezani wala hapakuguswa.

Wakati leo hii mtu yeyote akiibiwa akienda Police ama akiuliza kwa watu, kabla ya chochote ataelekezwa aende Gerezani atavikuta vitu vyake na watu wengi wamefanya hivyo na wakavikuta vitu vyao vilevile, (ukisema maeneo ulioibiwa watu wanazama ndani wanaangalia kiroba kinachokuusu unaletewa mali yako baada ya kutoa hela).

Sasa Serikali yetu kama kawaida inafanya jambo inaposikia kelele za wananchi, wakiona dalili za utulivu nao wanatulia, kumbe wenzao hawatulii wanawasubiria wakijuwa nguvu zao ni za soda.

Sasa vijana wamerudi tena kwa kasi na njaa ya hatari, kwa mfano maeneo ya Tegeta kwenda ndani ya wiki moja yamepigwa magari kadhaa na hayo ni ya watu ninao wajuwa na wengine kuadisiwa na watu wakaribu.

Na sasa hawachagui gari kama hapo mwanzo, lolote watakalopata nafasi, liwe hata ford zile za Marekani za zamani ama Landrover, wanavunja kioo wanafungua boneti wanaiba hata betri, ilimradi wapate hata kitu cha 50,000.

Ninavyojua mie na kusikia mara kwa mara kwenye radio/tv - kazi ya askari ni kulinda rahia na………………
 
Hii hali sasa imekuwa ngumu mzee,kwa njia yoyote watu wanatafuta chakula.
 
Back
Top Bottom