Wizi wa Airtel kwenye vifurushi na huduma mbovu za TCRA

ngungwangungwa

JF-Expert Member
Jul 23, 2013
642
554
Wakuu,

Nilijiunga kifurushi cha Airtel cha Uniofa ambacho unapata dakika 40, sms 10 na mb 350 kwa muda wa siku 7. Kilichonishangaza leo asbh nilipoangalia salio, ikaonyesha kifurushi changu zile dakika 40 na sms zinaisha tar 04 June. Lkn zile mb zinaisha leo tarehe 31 May saa 2 asbh.

Nikashangaa kwa sababu gani mb ziishe Leo na dakika ziishe tar.04!? Nikawapigia simu Airtel nikaambiwa eti hicho kifurushi ni cha ofa, kwa hiyo ofa inaweza kuisha wakati wowote. Nikamuuliza mbona dakika zinaendelea na kwa nini mpaka Sasa kwenye menu inaonyesha ni siku 7!?

Nimejaribu ku-up load mazungumzo yangu na Airtel ili mjionee wenyewe km ntakuwa nimefanikiwa ku-up load maana hapa kupandisha audio ni shughuli pevu. Nimeambatanisha na pia na majibu ya tcra baada ya kulalamika kwao.

Majibu ya tcra ndiyo kichefuchefu zaidi..hii nchi wizi hauwezi kuisha! Najua waziri nape ni member hapa apitie hapa aone huu uozo wa watu wao wa tcra. Nawasilisha.

Screenshot_20230531-094633.png
Screenshot_20230531-101517.png
 
Pole sana mkuu kwa changamoto hiyo

Kingine Mkuu hizo voice attachments ulizoweka zina uhusiano wowote na mada?
 
Back
Top Bottom