Mabibi na mabwana afya tokeni ofisini na mpite mitaani, hali ya mazingira hairidhishi

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,116
Mabibi na mabwana afya tokeni ofisini mlikojificha, piteni mitaani, masokoni nk hali ya mazingira ni mbaya hairidhishi, kwa Jiji la Dar ndio kimbembe hasa kipindi hiki cha mvua, watu wasio wastaarabu wanafungulia chemba za vyoo vyao zinatirirsha maji machafu yanajichaganya na maji ya mvua yanasambaa barabarani na kusababisha vinyesi kuzagaa mitaani, Kipindupindu kinaweza kulipuka.

Mitaa mingi Dar ina watu wa aina hii, mitaa inanuka harufu mbaya kutokana na maji hayo machafu mbaya zaidi hakuna hata hatua zinazochukuliwa dhidi ya tabia hii na inaonekana ni ya kawaida kwani imekuwepo miaka mingi.

Hata kwenye maeneo yenye mikusanyiko mikubwa ya watu kama Kariakoo nako kuna watu hufanya huu ufedhuli na sijawahi kusikia hata mtu kapelekwa mahakamani kwa kuhatarisha afya za watu kwa kufungulia maji machafu.

Mbali na hilo kuna hawa wanaozoa taka, kazi wanayoimudu vyema ni kukusanya hela zao na si kuzoa taka, unakuta taka zinakaa mpaka zinaoza hazijachukuliwa nazo zinauka na kusababisha uzalishwa wa wadudu, kiafya ni hatari sana huku mitaani.

Watu wenye majukumu ya kuchukua hatua sijui mmejifugia wapi wakati mnahitajika sana hasa wakati huu wa mvua, hebu tokeni huko mliko mpite muone wenyewe mchukue hatua.
 
Makampuni ya uzoaji wa taka ni ya kipumbavu sana, taka hawazoi, pesa zetu wanazipenda na kuzilazimisha hata kama hawajazoa taka zozote!, ni makampuni ya kihuni haya.

Tunaomba kuwepo na utaratibu maalumu, anapokuja kuzoa taka, nyumba husika iwe inasaini pahala kuonyesha tarehe fulani saa fulani siku fulani taka zilizolewa then saini za pande zote mbili.
 
Makampuni ya uzoaji wa taka ni ya kipumbavu sana, taka hawazoi, pesa zetu wanazipenda na kuzilazimisha hata kama hawajazoa taka zozote!, ni makampuni ya kihuni haya,
Tunaomba kuwepo na utaratibu maalumu, anapokuja kuzoa taka, nyumba husika iwe inasaini pahala kuonyesha tarehe fulani saa fulani siku fulani taka zilizolewa then saini za pande zote mbili.
Hii ingesaidia sana.
 
Badala ya kuitwa bwana/bibi afya siku hizi wanaitwa afisa afya (health officer).
 
Back
Top Bottom