Pengine kunahitajika sasa kuunda Wizara itakayoshughulikia Maafa na Mazingira

Robert S Gulenga

JF-Expert Member
Jan 3, 2013
2,161
1,493
Ni kipindi kigumu kwa kila Mtanzania kwa kilichotokea kwa ndugu zetu wa Hanang, Watanzania tumeungana kuwaombea ndugu zetu waliotangulia mbele za haki na tunaendelea kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu manusura wote wapate kupona haraka.

Kutoka na maafa haya na utayari wetu, Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ikikupendeza ni vyema ukaunda Wizara itakayoshughulikia Maafa na mazingira, Wizara itakayokuwa na Waziri na Katibu mkuu wanaoweza kuwajibika, Wizara itakayokuwa na bajeti ya vifaa na utayari wa kupambana na majanga yanayoanza kidogo kidogo kutokana na uhalibifu wa mazingira na majanga kama haya ya Katesh.

Natambua uwepo wa Taasisi kama NEMC na Kitengo cha Maafa kilicho chini ya OWM, yawezekana Vinafanya kazi nzuri lakini uwepo kwa Wizara itakayokuwa inaomba Bajeti kuwalipa nguvu na utayari wa kukabiliana na Majanga kuliko hivi vitengo vinavyosubiri kuombewa Bajeti.

Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, leo hii kuna nyumba zinadondoka hapa tu Dar Es Salaam kutoka na kupanuka kwa mito lakini hakuna jitihada za kusaidia watu hawa kwa kuwa tatizo linamkuta mtu mmoja mmoja.

Naomba nitoe mfano wa mto Tegeta maeneo ya kwa Magereza, mtaa wa Mtimizi na kuendelea, miaka kumi 15 iliyopita mto huu ulikuwa ni kama mfereji tu, lakini Leo hii ni mto mkubwa umepanuka na ushadondosha nyuma za watu, sina hakika kama NEMC au kitengo cha maafa kama wanachukulia hili kama ni janga, Mto huu unatishia ustawi wa maisha ya Wananchi wako Mh Rais.

Natambua na kupongeza juhudi za mto Msimbazi kupata ufumbuzi, Mh. Rais, ombi langu ni kuwa tatizo la mito kwa hapa Dar Es Salaam kuendelea kuharibu Makazi ya Wananchi wako linaendelea kukua siku hadi siku, pengine ni muda sahihi ukatusaidia kwa kuwa na Wizara itakayoweza kushughulikia na hili, kilio hakisikiki law sababu tatizo linaanza kwa Mwananchi mmoja na kufuata mwingine.

Naomba wanaohusika watembelee mto Tegeta wapate tathimini ya namna mto huo unavyotanuka law kasi na kuharibu makazi ya Watu.

Mwenyezi Mungu ibariki Tanzania.

Mwenyezi Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan.
 
Muungano na Mazingira.
Sina tatizo na Jafo wala Wizara hii, hoja yangu ni kuwa Kuwepo na Wizara ambayo kazi yake sio kulinda tu Mazingira, lakini inasaidiaje watu pale ambapo mali zao ziko hatarini?
Kwa utendaji wa Serikali yetu, hata tungekuwa na Wizara ya majanga pekee yake, siamini kama itabadilisha chochote. Kwa sababu, kwa serikali yetu, kila nafasi inayoundwa inakuwa ni nafasi ya kujinufaisha wale waliopewa hizo nafasi na wala siyo kutatua matatizo yanayoangukia kwenye nafasi iliyoundwa.

Kwa Serikali na watu makini, hata kwa muundo wa sasa, wala hakuna kinachoshindikana kufanya kama tungekuwa na watu makini. Tena majanga yapo chini ya Waziri mkuu, na Waziri mkuu ana access ya Rais masaa 24.
 
Yes watu ni walewale na tabia zao
 
Upigaji loading, waafrika kujiongoza ni shida,

Sasa hao viongozi kuanzia ngazi ya wilaya wanakazo gani?
 
Hiyo wizara italeta jambo gani jipya ambalo ofisi ya waziri mkuu haiwezi kufanya?.Tatizo sio kuongeza wizara bali tatizo ni serikali yenyewe kuchoka.Unawaza tu kuongeza mzigo kwa wananchi.
 
Muungano na Mazingira.
Sina tatizo na Jafo wala Wizara hii, hoja yangu ni kuwa Kuwepo na Wizara ambayo kazi yake sio kulinda tu Mazingira, lakini inasaidiaje watu pale ambapo mali zao ziko hatarini?
Naona unatafutia tu watu ulaji.
 
Back
Top Bottom