Wizara ya Elimu: Mara ya mwisho mitihani kuvuja ni mwaka 2008

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,445
7,816
Naibu waziri wa elimu akiwa bungeni, amesema suala la kuvuja mitihani halipo na mara ya mwisho mitihani kuvuja ni mwaka 2008 na ulikuwa mtihani mmoja wa somo la hisabati wa kidato cha nne.

Naibu waziri amesema kutoka mwaka 2008 hakujawahi kutokea kuvuja mitihani bali kinachotokea ni udanganyifu katika mitihani kwenye baadhi ya maeneo ambapo wanafunzi wanaingia na nyaraka zisizotakiwa au udanganyifu baada ya mitihani kufunguliwa na sasa wanapambana nao.

Pia, naibu waziri alijibu swali la nyongeza kutoka kwa mbunge Yustina alilohoji matamuzi ya polisi katika mitihani yanavyoweza kuzua taharuki kwa watahiniwa ambapo alisema Polisi hawaendi kusimamia mitihani kwasababu hakuna polisi anayeingia katika chumba cha mitihani bali kuhakikisha usalama kwenye kituo cha mitihani.
 
Mfumo mbovu wa elimu, unampimaje mtu kwa siku moja kama siyo ujinga? kwanini kusiwe na continuous assessment kwa mwanafunzi?
 
Back
Top Bottom