Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,817
- 4,566
Kamati ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imebainisha leo Jumanne Mei 16, 2023, kwamba kuna mgongano na mwingiliano wa majukumu katika uendeshaji wa elimu na uendeshaji wa shule kwa ngazi ya elimu ya awali, msingi na sekondari.
Kulingana na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Profesa Kitila Mkumbo, ambaye alikuwa akitoa maoni ya kamati kuhusu mapato na matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka 2023/24, anasema
"Mgongano na mwingiliano unajidhihirisha katika maeneo ya utawala wa elimu, ujenzi wa miundombinu, na utoaji wa miongozo mbalimbali ya uendeshaji wa elimu."
Profesa Mkumbo amehimiza Serikali kufanya tathmini ya kina kuhusu utekelezaji wa sera ya ugatuaji katika sekta ya elimu ili kubaini changamoto na mafanikio yake.
Aidha, kamati yake pamoja na ile ya TAMISEMI zimepanga kufanya kikao cha pamoja ili kutafakari changamoto hizo na kutoa ushauri wa pamoja ili kuleta ufanisi katika elimu.