Akili za kuambiwa changanya na zako.
1. Siyo wote humu ndani wana ndoa, lakini lazima watachangia; ushauri wao mara nyingi umebase kwenye theory zaidi,
2. Kuna ambao hawana ndoa kwa sababu wamezitafuta hawajazipata na wanawaonea wivu wenye ndoa, so ukija na matatizo yako ya ndoa unawapa faraja; watakupa ushauri wa kinafiki,
3. Humu kuna watu wana ndoa zenye matatizo pia, so wakiona mwingine anaelezea matatizo yake wanafurahi kuwa na wenzao; hawa pia watakupa ushauri wa kinafiki,
4. Kuna wale wa roho ya wengine waendelee kuwa na maisha mabaya tu, wanafurahi kuona wenzao wakiwa kwenye magumu bila kujali kwamba na wao wako kwenye neema au ugumu; hawa pia watakupa ushauri wakinafiki,
5. Mwisho kabisa kuna wenye nia njema na wenzao, watakupa ushauri mzuri na ukiufanyia kazi unafanikiwa, hawa ni wachache sana JF, ukiangalia vizuri katika kila posts 5 au 6 unapata ushauri mmoja, yanayobaki ni matani.
Kazi inabaki kwako kufanya uchambuzi wa uliyoshauriwa.
Hawa wenye nia nzuri wanaweza kuwa hata hawana ndoa, au ndoa zao zina matatizo, ila ni watu wenye nia nzuri kwa wenzao; hawa ni wachache sana.
NB: Kuna thread yako nyingine humu, vipi jamaa karudi?
Ushauri: Nakinai kufanya mapenzi