Ukubwa wa maumbile ya mume wangu umesababisha vifo vya waganga 7

Fatma Pazi

Member
May 5, 2018
20
45
Mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 43. Ni mfanyabiashara na mkaazi wa jijini Dar Es Salaam. Mwaka 2011 nikiwa na umri wa miaka 36 nilianzisha uhusiano wa kimapenzi na kijana alie kuwa na umri wa miaka 26 kwa wakati huo, so nilikuwa namzidi miaka kumi.

Kijana huyu alikuwa ndio kwanza amemaliza Chuo Kikuu so hakuwa na kazi wala shughuli yoyote ile ya maana. Mimi ndio nilikuwa namtunza na kumuhudumia kwa kila kitu.

Mwaka 2014 tulifunga ndoa ya bomani na kuanza kuishi pamoja kama mke na mume kwenye nyumba ya urithi niliyo achiwa na marehemu baba yangu.

Kusema ukweli nilitokea kumpenda sana mume wangu na kama mnavyo jua upendo wa ukweli huwa unaendana na wivu.

Nilikuwa na wivu mkali sana kwa mume wangu. Wivu na gubu langu kwa mume wangu ulibadilika na kuwa manyanyaso na masimango pamoja na ugomvi wa mara kwa mara.

Nilikuwa namsimanga na kumtukana sana kila mara nilipo muhisi ana ni cheat na mwanamke mwingine.

Kwa sababu ya ugomvi wa mara kwa mara, mume wangu alikuwa mara kwa mara anaondoka kwenye nyumba tuliyo kuwa tunaishi wote na kwenda kwa dada yake au rafiki zake na kisha baadae tukielewana anarudi tena nyumbani. Hali hii iliendelea kwa muda mrefu sana hadi mwaka 2016 mwezi wa kumi na mbili.

Siku hiyo mida ya saa kumi za jioni nikiwa narudi nyumbani kwa taxi ya kukodi kutoka kwenye shughuli zangu nilimuona mume wangu barabarani akiwa anakatiana mhindi na dada mmoja wa mtaani kwetu huku wakiwa wanatembea taratibu. Kwa bahati mbaya au nzuri yeye hakuniona

Kutokana na wivu mkubwa nilio kuwa nao kwa mume wangu picha hiyo kusema ukweli sikuielewa kabisa. Moja kwa moja nikahisi kama watakuwa hawatongozani basi watakuwa na uhusiano wa kimapenzi. Hasa ikizingatiwa kuwa dada huyo alikuwa mrembo haswa na mdogo kiumri kwa mume wangu.

Nilifika nyumbani nikiwa natetemeka kwa hasira. Bila kupoteza muda nikampigia simu mume wangu simu ikawa inaita bila kupokelewa. Nilifanya hivyo zaidi ya mara kumi na hali ikawa hiyo hiyo.

Baadae simu ikawa haipatikani tena… Hali hii ilinichanganya sana na kunifanya moja kwa moja niamini mume wangu alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Yule dada na kwamba walikuwa wameenda wote kufanya zinaa. Niliumia sana moyoni. Siwezi kuelezea hasira nilizo kuwa nazo. Ni Mungu tu ndio alinizuia nisiue siku hiyo vinginevyo ingekuwa habari nyingine tena.

Saa 4 usiku mume wangu ndio akaingia nyumbani. Sikumpa hata muda wa kupumzika nikamuuliza Yule mwanamke walio kuwa wanakatiana nae muhindi barabarani ni nani na ni kwanini hakuwa akipokea simu zangu na kunizimia simu.. Kabla hata hajaanza kunijibu nikamrukia nikamkaba. Tukaanza purukushani, Ulitokea ugomvi mkubwa sana .

Baadae nikachukua vitu vyake vyote na kumtupia nje huku nikimtukana matusi makubwa ya kumdhalilisha na kumwambia aondoke zake na asirudi tena kwangu na kwamba mimi na yeye ndio basi tena nitatafuta mwanaume mwingine anae jitambua.

Mume wangu hakuwa na jinsi zaidi ya kutii amri yangu na kuondoka zake.

Kama nilivyo kuwa nimezoea nilitegemea kesho yake ningepokea simu kutoka kwa dada yake ambae alikuwa msuluhishi wetu mkubwa kila mara tulipo gombana lakini haikuwa hivyo.

Mwezi mmoja baadae nikapewa taarifa kuwa mume wangu anaishi na mwanamke mwingine.. Niliingiwa na wivu sana na baada ya kufanya upelelezi wangu binafsi nikagundua kuwa huyo mwanamke anaeishi kinyumba na mume wangu ni tajiri sana na anapenda sana viserengeti boy na amekwisha vunja mahusiano mengi kwa kutumia pesa zake.

Niliumia sana moyoni nikaamua kumtafuta mume wangu ili turudishe uhusiano wetu lakini akakataa kata kata . Nikaenda kwa dada yake ili kumuomba aongee na mdogo wake tuyamalize lakini haikufua dafu.

Kwa muda wa zaidi ya miezi minne nikawa najaribu kutafuta suluhu na mume wangu lakini bila mafanikio yoyote.


Sikuwa tayari kumuona mume wangu akiwa anaishi kwa furaha na mwanamke mwingine mbele ya macho yangu hasa ikizingatiwa nilipo mtoa ni mbali sana na gharama nilizo tumia kwake ni kubwa sana.

Kwa uchungu mkubwa nikaamua bora tukose wote tu. Nilijua kinacho mtia jeuri mume wangu ni kwa sababu amebarikiwa na ana jua vizuri sana namna ya kumfurahisha mwanamke kunako faragha na hicho ndicho kimemtia wazimu huyo Bi. Mkubwa.

KUSEMA UKWELI WANGU KUTOKA MOYONI MWANGU. MIMI LENGO LANGU HALIKUWA KURUDIANA NA HUYO MWANAUME ISIPOKUWA SIKUTAKA KUMUONA MWANAUME HUYO AKIWA ANAISHI KWA FURAHA NA MWANAMKE MWINGINE. NILITAKA NIMUONE AKITESEKA BAADA YA KUACHANA NA MIMI NA KURUDIA MAISHA YAKE YA KIFUKARA. I WANTED HIM TO FEEL MY ABSENCE. SASA KUTOKEA KWA MWANAMKE HUYU TENA MWENYE PESA NA MAISHA MAZURI KULIKO MIMI KULIZUIA LENGO LANGU. NIKACHANGANYIKIWA SANA!

Nikapata wazo ovu kwamba niende kwa mganga afanye dawa ya kumtia ukhanithi mume wangu ili akimbiwe na huyo mwanamke wake. Nilijua silaha na mtaji wake pekee ni maumbile yake na uwezo wake mkubwa pindi anapokuwa faragha so nikawaza, endapo uwezo huo utaondolewa basi itakuwa kwisha janja yake.Mwanamke atakimbia na atarudia maisha yake ya kifukara na hapawezi kutokea mwanamke mwingine yoyote Yule wa kumshika mkono.

Shoga yangu mmoja akanipeleka kwa mganga mmoja. Mganga akasema suala la kumtia huyo mwanaume ukhanithi linawezekana lakini lazima tupate mbegu zake za kiume kwanza. Hizo mbegu zake ndio tutazitumia kutengeneza dawa ya kumtia ukhanithi.

Nikamjibu mganga kuwa kupata mbegu zake itakuwa vigumu sana kwa sababu sasa hivi huyo mwanaume anaishi na mwanamke mwingine kwa zaidi ya miezi mitatu.Hataki kabisa kuwasiliana na mimi. Simu zangu hapokei wala meseji hajibu na ikitokea amepokea basi hunitukana sana na kuniambia nisimsumbue.

Mganga akaniambia hiyo ni kazi ndogo sana. Akanielekeza sehemu kwenye duka la kuuza dawa za asili nikanunue mita nne za kipande cha sanda iliyo tumika kukafinia maiti.

Nilivyo peleka hicho kipande cha sanda, mganga akakipokea kisha akaanza kufanya dawa zake kwa kuchoma kile kitambaa huku akitamka maneno yake ya kiganga na kutaja majina ya mume wangu na la mama ake huku akinielekeza na mimi kutamka maneno Fulani ya kiganga.

Baada ya takribani lisaa limoja hivi kazi ya mganga ikawa imekamilika akanipa dawa za kuoga na kuniambia nirudi nyumbani.

Nikiwa ndani ya bus kurudi nyumbani nikashangaa sana kuona mume wangu anapiga simu. Kwa kuwa nilikuwa kwenye bus nikamwambia anipigie baada ya masaa matatu nitakuwa sehemu nzuri.

Baada ya masaa matatu mume wangu akanipigia na kuniomba nimsamehe sana shetani alimpitia na kwamba amenimiss sana anataka aje kulala nyumbani leo. Baada ya kumsikiliza nikamwambia anipigie tena baada ya kama nusu saa tuongee vizuri kuna kazi namalizia.

Alivyo kata simu nikampigia tena mganga na kumwambia kilicho tokea, kwa sababu mganga aliniambia atakacho niambia mume wangu baada ya kunipigia simu nimjulishe haraka sana ili anielekeze kitu gani cha kufanya.

Nilivyo mpigia mganga akaniambia, sawa mruhusu aje alale na hakikisha unapata hizo manii zake zikiwa zenyewe kwenye mpira wa kufanyia mapenzi na kesho alfajiri udamkie nazo kilingeni.

Mume alivyo kuja kweli tukafanya tendo la ndoa kwa kutumia kondomu na alfajiri nikadamkia kwa mganga nikiwa na kondomu zenye mbegu za mume wangu.

Kabla ya kuanza kufanya uchawi wa kumtia mume wangu ukhanithi, mganga alinisisitizia tena na tena kama nina uhakika na ninacho kitaka. “ Ni kweli umeamua kuwa unataka kumtia mumeo ukhanithi ili asiwe na uwezo wa kusimamisha katika maisha yake yote au ni hasira zako tu ?”. Ninakuuliza hivi kwa sababu uchawi huu ni mbaya sana na unawatesa sana wanaume.. Kwa sababu kama ni mume tayari amesharudi ni bora tu tufanye uchawi wa kumfunga kwako na kumtenganisha na huyo mwanamke wake kuliko kumtia ukhanithi ”

Mimi nikamwambia nipo tayari nimedhamiria kutoka moyoni na sihitaji tena kuishi na mwanaume huyo kwa sababu amenidhalilisha sana kwenda kuishi na mwanamke mwingine na kunifanya nionekane mpumbavu..

Akajibu sawa halafu akanielekeza niende sehemu kununua kasuku , jogoo, bata dume na maksai ama dume la n’gombe lililo hasiwa.

Baada ya kupeleka vitu hivyo tukaenda porini kasuku akachinjwa damu ikawekwa kwenye chungu chuesi, tulikuta kuna kenge pale ameuwawa pia, akakatwa ulimi ukawekwa kwenye chungu pamoja na damu yake, halafu zikachukuliwa zile manii za mume wangu zikachanganywa kwenye chungu na madawa ya kiganga huku mganga akizungumza maneno yake ya kiganga.

Baada ya hapo Yule n’gombe maksai akapigwa mshale wa mbavuni, damu yake kiasi ikakingwa na kuchanganywa kwenye chungu halafu alipo kufa, akapasuliwa kichwa ubongo na moyo vikachukuliwa vikatiwa kwenye chungu , kisha uume wake ukachukuliwa ukatiwa kwenye chungu halafu zikaongezwa dawa huku mganga akitamka maneno yake ya kiganga

Zoezi lili fanyika kwa kama masaa matatu hivi. Baada ya hapo ukaletwa mti na kijana mmoja alie onekana kama msaidizi wa mganga pamoja na bibi kizee mwenye umri wa miaka kama sabini hivi na ushee. Huo mti ulikua umechongwa mfano wa uume na kuandikwa maandishi ambayo sikuelewa maana yake ni nini.

Mti ulivyo fika mganga akachukua vitu mfano wa miiba na kuanza kuandika herufi kwenye mti huyo ambazo siku zijua maana yake nini. Alitumia damu ya kwenye chungu kama wino.

Baadae Yule bibi kizee alijifunua matiti yake na kuchovya damu kwenye kile chungu kisha kwa maelekezo ya mganga akauchukua ule mti na kuupaka kwa damu kwa kutumia matiti yake huku akisema maneno ya kichawi/kiganga sambamba na mganga.

Alikuwa anazungumza lugha nisiyo ifahamu na baadae akawa anazungumza maneno ya Kiswahili. Baadhi ya maneno ninayo yakumbuka vizuri ni pamoja na “ ( Jina la mume wangu Bin Mama ake ) Uume wako ulale doro kama yalivyo lala haya maziwa yangu, kama maziwa yangu haya yatasimama basi uume wako pia utasimama ..n.k )

Baadae Yule bibi akamkabidhi mganga ule mti halafu akachukuliwa nyoka ambae ameuwawa akachanganywa kwenye ile damu ilyo kuwa kwenye chungu pamoja na dawa kisha vikachemshwa mpaka vikawa jivu.

Vilipo kuwa jivu, vikafungwa pamoja kwenye kitambaa cheusi pamoja na ule mti, halafu akachukuliwa Yule jogoo mwekundu akapelekwa kulishwa mchele kaburini kisha akaletwa jirani na kilingeni kwa mganga.

Mganga akaniambia kwa kuwa kazi yangu itafanyika alfajiri basi natakiwa nilale kilingeni. Ilipofika saa sita usiku mganga akaniamsha tukaenda hadi mahali alipokuwa amekaa Yule kuku, halafu kikachukuliwa kipande cha ile sanda akafungwa kuku kwenye mguu kwa upande mmoja wa sanda na upande wa pili ukafungwa ule mti.

Baada ya hapo mganga akaniambia nirudi kulala ila niwe macho saa kumi alfajiri ndo tunamalizia zoezi la mwisho.

Hata sikuweza kupata usingizi. Ilipo fika saa kumi nikawa nimeamka. Mganga na yeye akawa ame amka . Tukaenda kukaa karibu na kuku. Mganga alikuwa ameshika panga kali sana.

Ilipofika saa kumi na moja na nusu Yule jogoo akawika. Alivyo wika kwa mara ya kwanza tu Yule mganga akamuwahi akamkaba. Yani hakutoa sauti nyingine tena. Alitoa sauti moja tu. Alivyo mkaba akachukua kile kipande cha mti akakiweka kwenye shingo yake na kukifunga kwa kutumia sanda kisha akamlaza Yule kuku kwenye jiwe na kupiga panga moja tu ambalo lilikata shingo ya Yule jogoo pamoja na ule mti…

Baada ya hapo mganga akaniambia kazi yangu imekamilika sasa ninaweza kwenda nyumbani kujithibitishia mwenyewe kwa kulala tena na mume wangu.

Nili pofika nyumbani nilimkuta mume wangu yupo sebuleni anatazama tv. Nilipo fika moja kwa moja nikazama chumbani na kumwambia aje anipe haki yangu .

Kwa kuwa alikuwa anapenda sana kufanya tendo la ndoa mume wangu alikuja haraka haraka.. Hadi baada ya lisaa lizima, tulikuwa tunachezeana tu na jogoo wa mume wangu hakuwa amepanda mtungi.

Ghafla mume wangu akazuga kama tumbo limemshika vile akaomba kwenda chooni. Alikaa chooni kama dk ishirini vile alipo toka akaniambia anajisikia vibaya ghafla anaomba kwenda hospitali nikamwambia nikusindikize akaniambia haina haja nisisumbuke.

Akaoga huyo akaondoka zake. Alipo ondoka nikampigia mganga simu na kumueleza kilicho tokea. Mganga akaniambia nisimuulize chochote mimi nisubiri ataniambia nini akitoka hospitali.

Alivyo toka hospitali akaniambia amekutwa na malaria na kwamba kesho yake anatakiwa kwenda Morogoro ambako atakaa kwa wiki tatu.

Nikamwambia mganga akaniambia huyo anaenda kujaribu kulala na wanawake wengine ili aone kama hali itakuwa hivyo hivyo. Akaniambia usimwambie chochote wewe kaa kimya kana kwamba hujui kinacho endelea..

Umepita mwaka na kama miezi mwili tangu mume wangu awe Khanithi. Hali hii imemchanganya sana na sasa amekuwa mlevi wa kutupwa na ninavyo andika hapa mume wangu anaweza kujiua wakati wowote .

Mwaka jana mwezi Agosti alirudi nyumbani akiwa amelewa sana. Nikachukua simu yake kuona watu anao wasiliana nao. Meseji zake zinaonyesha kuwa Alisha zunguka kwa waganga zaidi ya ishirini bila mafanikio. Na kati ya waganga hao 20 waganga watatu tayari wamepoteza maisha yao wakiwa kwenye process ya kujaribu kumsaidia arudie katika hali yake ya kawaida. Nili ogopa sana!

Hayo alikuwa anaongea na mganga wake mwingine ambae alikuwa anajaribu kumtibia. Mume wangu alimuandikia meseji kuwa haoni raha ya kuishi duniani na anaweza kujiua.

Katika meseji hizo mume wangu anasema hata Yule mwanamke wake mchepuko amemkimbia baada ya kuona hawezi tena kufanya tendo la ndoa na mimi mkewe nitajua siri yake muda wowote na nikijua siri yake nikamtmua sijui ataenda kuishi wapi?.

Niliingiwa na huruma sana kuona namna wivu wangu wa kimapenzi ulivyo fanya nimsababishie kijana wa watu mateso makubwa kiasi hiki.

Roho ya huruma ikaniingia nikaamua kwenda kwa mganga alie fanya uchawi huu ili amzindue. Mganga alikuwa mkali sana na kunifukuza kama mbwa. Aliniambia kabla sijafanya huo uchawi nilikuuliza mara kumi kumi ukasema unataka tu mume wako awe khanithi sasa hivi unakuja kuniambia upuuzi gani tena huu.

Akasema yeye anaweza kumfungua mtu aliefungwa kichawi na mganga au mchawi yoyote Yule duniani lakini kwake ni mwiko mkubwa sana kumfungua kichawi mtu ambae amemfunga mwenyewe na kwamba akimfunga mtu hawezi kufunguliwa sehemu yoyote ile na atakae jaribu kufanya hivyo atakufa .

Nilichanganyikiwa sana na kujilaumu kwanini nimemuingiza mume wangu kwenye majanga makubwa namna hii. Wazo likanijia niongee na mume wangu ili wote mimi na yeye tuanze kutafuta tiba lakini bila kumueleza ukweli kwamba mimi ndio nilisababisha.

Niliongea na mume wangu kwa upole na utaratibu sana kwamba kwanini ananificha kuhusu maradhi yanayo msumbua . Akajifanya kama hajui vile. Nikamwambia asinifiche nimeona kila kitu kwenye meseji zake. Nikamuelewesha kuwa ni jambo la kawaida kutokea na kwamba tiba yake ipo inabidi tuhangaike kuitafuta. Maneno yangu yalimpa faraja sana.

Tumetembea kwa kila aina ya mganga , tumetembea kwa masheikh na wachungaji lakini hakuna mafanikio yoyote.

Kibaya zaidi kuna waganga wengine wanne wamekufa wakijaribu kumtolea mume wangu huo uchawi alio tolewa.

Mganga wa mwisho amefariki mwezi wa 2 mwaka huu. Mganga mwingine alinusurika kufa akatutimua nyumbani kwake usiku wa manane. Huyu ni mganga alie sifika kuwa na nguvu kubwa sana yupo magharibi mwa Tanzania. Alitupokea vizuri tukaanza tiba, ila usiku hakulala. Anasema alitokewa na mauzauza mazito sana na usiku huo huo akatutimua. Hii ni mwezi wa tatu mwaka huu huu.

Nilirudi tena kwa mganga alie mfunga mume wangu na kumwambia nipo tayari kumpa kiasi chochote cha pesa anacho kihitaji. Nipo tayari kumpa hata nyumba yangu ili amrudishe mume wangu katika hali yake ya kawaida lakini bado akashikilia msimamo wake na kuniambia kuwa yeye shida yake sio pesa bali anasimamia miiko na maagano na majini/mizimu wake. Funguo iliyo tumika kumfunga mume wangu imemezwa kwenye tumbo la hewa. Haiwezi kupatikana na wala mume wangu hawezi kurudia katika hali yake ya kawaida.

Nimekata tamaa na hapa ninapo zungumza mume wangu amekuwa kama chizi kabisa. Anashinda nyumbani analia kama mtoto na kuongea peke yake.

Nimeandika barua hii ili kuomba msaada wa haraka. Please kama unamjua mtu yoyote Yule anaeweza kumsaidia mume wangu na kumrudisha katika hali yake ya kawaida mimi nipo tayari kulipa gharama yoyote ile.

Mume wangu anapata mateso makubwa sana jamani na mpaka sasa tayari wamefariki waganga 7 wakiwa katika process ya kujaribu kumtibia mume wangu na yote hiyo ni kwa sababu ya maumbile yake makubwa na uhodari wake awapo faraghani ambavyo vilinitia wivu na husda na kunifanya niende kumroga ukhanithi. Kinacho niuma zaidi ni pale ninapo gundua kuwa mimi ndio chanzo cha yote hayo.
 

dafity

JF-Expert Member
Aug 16, 2008
1,738
2,000
Hata ukisaidiwa akarudia URIJALI WAKE bado mawivu yako ya kijinga yatafanya umfunge tena kwa uhanithi. Ni tamaa na wivu wa kijinga tu. Vumilia mama kwani miaka yote mliyotiana haitoshi? Bakini kama kaka na Dada na umweleze ukweli kwamba wewe ndio ulimloga, maana hata pepo imefungwa kwako usipoomba msamaha.
 

Fatma Pazi

Member
May 5, 2018
20
45
Mmh. Kama ni kweli nikupe tu pole.

Ungekuwa umekumbuka ule usemi akiwa kwako ni wako akitoka nje sio wako, hata kama hana mtu nje wala usingepata dhambi kwa kumuharibu kiasi hiki mtoto wa mwanamke mwenzio.

Ndio basi tena hapo we mfute machozi tu mwaya sababu hukuwa mwanamke mwenye kuwaza mbele hivyo akili yako ikaishia hapo ilipoishia kumfanya mumeo hivyo.

Pole kwako na kwa huyo Mumeo.
asante kwa ushauri wako dada . Naona watu wananikejeli tu humu ndani
 

Fatma Pazi

Member
May 5, 2018
20
45
Hata ukisaidiwa akarudia URIJALI WAKE bado mawivu yako ya kijinga yatafanya umfunge tena kwa uhanithi. Ni tamaa na wivu wa kijinga tu. Vumilia mama kwani miaka yote mliyotiana haitoshi? Bakini kama kaka na Dada na umweleze ukweli kwamba wewe ndio ulimloga, maana hata pepo imefungwa kwako usipoomba msamaha.
Kumwambia ukweli hapana.. Mimi nataka nipate msaada arudi katika hali yake ya kawaida. Ila nashukuru sana kwa ushauri wako
 

Fatma Pazi

Member
May 5, 2018
20
45
Nenda congo
Congo sehemu gani mkuu ? Tulienda hadi sehemu inaitwa Moba ambayo inasifika Congo nzima kwa kuwa na uganga na uchawi mkubwa. Ilikuwa ni safari ya mateso sana. Tulipanda meli kutoka Kigoma hadi sehemu inaitwa Kalemie upande wa Congo, huko tukachukua gari za kuunga unga hadi Moba. Ni Congo ipi mkuu? Tafadhali. Lakini kote huko hatujafanikiwa. Tumetumia pesa nyingi sana
 
Top Bottom