Mwadilifu Mdhulumiwa
JF-Expert Member
- Jul 22, 2021
- 418
- 630
Salam ndugu wana JF!
Moja kwa moja kwenye maada, ndugu zangu kwa muda mrefu kumekuwapo na wito na maagizo mengi ya serikali kuzitaka taasisi za fedha kushusha riba wanazotoza katika mikopo wanayotoa kwa wanananchi.
Kila linapojitokeza tukio linalomkutanisha ama Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu au Waziri wa fedha katika hotuba wanazotoa ni lazima tu moja ya mambo huwa ni kuzungumzia kuzitaka taasisi hizo za fedha kushusha riba zao za mikopo ili kuleta nafuu kwa wanaoomba mikopo hiyo.
Hata hivyo utekelezaji wake umekuwa ni wa kusuasua sana kwani mpaka sasa bado viwango vya riba za mikopo kwenye taasisi zote za fedha viko juu sana!
Hivyo wananchi tunajiuliza je nini sababu ya taasisi hizi kupuuzia au kukaidi wito unaotolewa kwao na serikali? Serikali ndiyo inayosajili na kutoa vibali na leseni za biashara hizo, Je inashindwa wapi kuweka viwango vya riba elekezi kwa mabenki yote?
Wananchi tunaitaka serikali ikazie na kufanya ufuatiliaji wa wito na maagizo inayoyatoa kwenye taasisi za fedha ikiwa ni pamoja na kuzitaka benki kupunguza masharti na vikwazo wanavyoweka katika utoaji wa mikopo hiyo. Mathalani inafahamika vijana wengi hawana hata viwanja vya kujenga nyumba , ajabu kijana akienda benki kuomba mkopo mdogo tu wa milioni 2.5, anaambiwa mpaka uwe na hati ya nyumba.
Tunaiomba serikali iwe serious na suala hili, kwani vijana wengi wamejiajiri kupitia shughuli binafsi, Hivyo ni wajibu wa serikali kutanua na kuboresha mazingira ya uwezeshaji kiuchumi.