Benki Kuu ya Tanzania (BoT) yatangaza riba ya Benki Kuu kwa robo ya kwanza ya mwaka 2024

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,565
Kamati ya Sera ya Fedha iliyokutana tarehe 18 Januari 2024 imetangaza Riba ya Benki Kuu kuwa asilimia 5.5 kwa robo ya kwanza ya mwaka huu ili kutimiza malengo ya kiuchumi katika kipindi hicho.

Kiwango cha Riba ya Benki Kuu kilichotangazwa kinaendana na malengo ya kuhakikisha kuwa mfumuko wa bei unabakia ndani ya lengo la asilimia 5 na kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi kufikia lengo la asilimia 5.5 au zaidi kwa mwaka 2024.

Aidha, riba hiyo imezingatia lengo lakuhakikisha thamani ya Shilingi dhidi ya fedha za kigeni inaendelea kuwa imara.Ili kuwezesha kufikiwa kwa malengo haya, Benki Kuu itatumia nyenzo mbalimbali za sera ya fedha kuhakikisha riba katika soko la fedha baina ya benki hapa nchini (interbank market) inakuwa tulivu.

“Hivyo, Benki Kuu itakuwa inafuatilia mwenendo wa riba ya mikopo ya siku 7 katika soko hilo na kuchukua hatua kuhakikisha mabadiliko ya riba yanakuwa ndani ya wigo usiozidi asilimia 2 chini au juu (+/-2%) ya Riba ya Benki Kuu, amesema Gavana wa Benki Kuu na Mwenyekiti waKamati ya Sera ya Fedha wakati akitangaza uamuzi wa Kamati hiyo.Tamko Kamati ya Sera ya Fedha ni la kwanza kutolewa tangu Benki Kuu ya Tanzania ilipoamua kubadili mfumo wa utekelezaji wa sera ya fedha kutoka kutumia ujazi wa fedha na kuanza kutumia mfumo wa riba kuanzia Januari mwaka huu.

Mfumo wa kutumia riba unatarajiwa kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa Sera ya Fedha. Aidha, mabadiliko haya yanaendana na makubaliano ya Itifaki ya Kuanzisha Umoja wa Fedha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ikiwa ni mojawapo ya hatua kuelekea kuwa na Sarafu Moja na Benki Kuu Moja ya Afrika Mashariki. Tanzania inakuwa nchi ya nne katika jumuiya kutumia mfumo wa riba, zingine ni Kenya, Uganda na Rwanda.

Riba ya Benki Kuu kwa robo ya pili ya mwaka 2024 itatangazwa mwezi Aprili mwaka huu. Hii ni kulingana na kalenda ya mikutano ya Kamati ya Sera ya Fedha itakayotolewa hivi karibuni.

1705706017571.jpeg

1705706032290.jpeg

1705706048701.jpeg

1705706066103.jpeg
 
Wametangaza leo, 6%..
Unaweza kufafanua kidogo?
 
Back
Top Bottom