WITO WA MWANAKIJIJI: Rais Magufuli Atumie Sheria ya Hali ya Dharura (1986) Kukabili COVID-19 (Corona Virus)

View attachment 1389304

(Picha toka US Centers for Disease Control rangi nyekundu ikionesha kusambaa kwa virusi vya corona nchi mbalimbali duniani hadi jana Jumamosi Machi 14, 2020).
Na. M. M. Mwanakijiji

Tukisubiri tupate mgonjwa wa kwanza wa virusi vya corona tutakuwa tumechelewa. Tukiendelea kuombea kuwa Mungu atuepushe na janga hili tutakuwa tumechelewa. Tukisema kuwa janga hili halitatufikia tutakuwa tunajidanganya. Njia bora ya kukabiliana na janga lililo mbali ni kujiandaa nalo. Nchi nyingi za Magharibi zimechelewa sana kuchukua hatua kali kabla ya ujio wa corona ndani ya mipaka yao kiasi kwamba sasa hivi wanachukua hatua ambazo zinaonekana ni kali kweli kweli.

Katika Jimbo la Michigan nchini Marekani ambako naishi tangu taarifa za Corona zilipoanza kuja uongozi wa kisiasa wa Jimbo na miji midogo na mikubwa mara moja ulianza taratibu za kujipanga. Waliunda kamati kazi kwa ajili ya kuchukua maamuzi mbalimbali ya kuwaandaa wananchi wao. Wiki iliyopita ndio tulipata wagonjwa 2 wa kwanza na hadi kufikia leo jimbo lina wagonjwa 25 wa Corona Virus Disease ya 2019 (COVID-19). Ijumaa iliyopita Gavana amefunga kufungwa kwa shule zote za msingi na za sekondari kwa muda wa wiki tatu (kuanzia kesho) na vyuo vikuu vyote vimefungwa. Jimbo Kuu Katoliki la Detroit limetangaza kusimamisha maadhimisho ya misa za hadhara kwa muda wa wiki tatu. Leo, kila mtu anaenda kujiombea nyumbani kwake na kuombea taifa sebuleni kwake. Hakuna kumjaribu Mungu au kucheza bahati nasibu na afya.

Nchi zote ambazo zinakabiliana na ugonjwa huu viongozi wake wameamua kutumia mojawapo ya zana za kiutawala zilizoko kwenye nchi zote – Sheria za Madaraka wakati wa Dharura. Nchi zote zimeweka sheria hizi zikijua kuwa kuna wakati kuna janga au dharura fulani inaweza kutokea ambayo taratibu, sheria, na mifumo iliyopo haiwezi kusaidia kukabiliana nalo. Sheria hizi zinaitwa “Emergency Powers laws”. Sheria hizi zina lengo la kumpa kiongozi wa nchi madaraka makubwa zaidi na kuondoa ukiritimba ambao watu wameuzoea katika kufikia maamuzi. Rais basi anakuwa ndiyo mtunga sheria, taratibu na kwa agizo lake anaweza kuamuru karibu jambo lolote.

Tanzania kama nchi nyingine inayo sheria ya aina hii; inaitwa sheria ya madaraka ya dharura ya mwaka 1986 (Emergency Powers Act – 1986) (pamoja na mabadiliko yake). Sheria hii inatafsiri “dharura” kama jambo lolote lile ambalo linafanya taifa kuwa katika hali ya wasiwasi; hii ni pamoja na vita, uvamizi, uasi, kuvunjika kwa Amani, pamoja na jambo lolote linalotokana na asili au janga la asili. Magonjwa na vitu kama hivi yanaangukia katika haya majanga ya asili.

Kutangazwa kwa Hali ya Dharura/Hatari

Endapo Rais baada ya kupewa taarifa zote za kitalaam anaridhika kuwa kweli kuna janga linalotishia hali ya usalama wa taifa basi anatakiwa kwa mujibu wa Ibara ya 32 ya Katiba kutangaza hali hiyo kama ni katika eneo fulani la Jamhuri ya Muungano au sehemu yake. Atatangaza muda wa dharura hiyo na tangazo lake ni ushahidi tosha (kwa mujibu wa sheria hiyo) ya kuwepo kwa dharura hiyo. Sheria hiyo inahusu Jamhuri nzima ya Muungano (Bara na Visiwani).

Chini ya kifungu cha 6 cha sheria hiyo Rais anaweza kutoa maagizo, na kuweka taratibu za kukabiliana na janga hilo. Katika hali ya sasa, Rais akiona inafaa atatangaza nini kinatakiwa kufanyika kukabiliana na virusi vya corona. Hii ni tofauti na kutoa wito wa hiari kwa wananchi. Ina maana Rais haombi na kutegemea watu wafanye kwa hiari bali anatoa agizo au maagizo yenye nguvu za kisheria chini ya sheria hii.

Sheria hii inampa Rais hata madaraka ya kumfukuza kazi mtu yeyote ambaye anaweza kukwamisha kukabiliana na janga hilo – hata kamamtu huyo anafanya kazi kwenye kampuni binafsi. Na sheria hiyo inampa Rais madaraka ya kusitisha matumizi ya sheria au kanuni fulani. Haya ndiyo ambayo Donald Trump alifanya siku ya Ijumaa lengo ikiwa ni kurahisisha maamuzi mbalimbali. Rais wetu naye akiona inalazimisha anaweza kuweka hilo katika maagizo yake.

Kwa ufupi, sheria hii ndio njia ya haraka, sahihi, na inayopaswa kutumiwa kujiandaa kukabiliana na janga hili la corona. Tusisubiri ugonjwa uingie. Tuna faida (advantage) kuliko nchi za Magharibi na ninaamini ndio zimechangia kuchelewa kusambaa kwa ugonjwa huu. Nitataja faida hizo chache lakini siyo kinga.

  • Wagonjwa wengi kwenye za magharibi wamepatikana kwenye mikusanyiko mikubwa ya watu hasa watu wazima (kwenye nyumba za wazee, meli za starehe –cruise ships, na maeneo yenye watalii wengi wazee kama kule Italia).
  • Nchi zetu hazirundiki sana wazee kwenye eneo moja, hatuna nyumba nyingi za kutunzia wazee na hata zile zilizopo ni hasa kwa wazee ambao hawana watu wa karibu wa kuwatunza. Hata hivyo hadi jana (Jumamosi Machi 14) tayari nchi 16 za Afrika zilikuwa na angalau mgonjwa mmoja.
  • Kwa vile tumejifunza kuwa wagonjwa wengi hadi hivi sasa ni wazee, hili linaendana na hali ya ilivyo kuhusu demografia ya nchi za Magharibi. Nchi hizi nyingi (hata zile za Asia) zina watu wengi wazee kuliko vijana kulinganisha na Afrika. Ni kwa sababu hiyo ugonjwa huu unapokuja Afrika unakutana na vijana wengi wenye afya nzuri.
  • Kwa vile hii ni aina ya homa ya mafua; wapo wanaoaminikuwa hali ya hewa ya joto ambayo iko sehemu ya Afrika chini ya jangwa la Sahara inasaidia kuangamiza virusi hivi kuliko kwenye nchi za Magharibi ambako kuna majira ya baridi sasahivi. Hata hivyo hii ni nadharia ambayo haijathibitishwa kisayansi kwani baadhi ya nchi ambazo zina majira ya joto pia zinawagonjwa wa corona. Labda kipo kitu kingine (x-factor) ambacho bado hakijajulikana (binafsi ninayo nadharia yangu).
Hata hivyo, tayari tumeona kuwa tayari virusi hivi vimeshafika kwenye nchi mbalimbali za Afrika. Katika nchi hizi zote ni watu waliosafiri kutoka ng’ambo ndio wamekuja na virusi hivyo na bado hatujapata kile kinachoitwa “community spread” yaani kuanza kuambukizana kwenye jamii. Hili ndilo limetokea na linaendelea kutokea Marekani kwani watu sasa wanaanza kuambukizana wenyewe kwa wenyewe. Hili ndilo linalosababisha nchi kuchukua hatua za kufanya watu wakae mbalimbali (social distancing). Ndio sababu ya watu kutokusalimiana kwa mikono au kugusana kwa namna yoyote – hata kugongeana viatu inawafanya watu wakaribiane sana.

Maoni yangu ni kuwa Rais Magufuli amefanya vizuri hadi hivi sasa kwa kuwapa wananchi taarifa sahihi na za wakati na kuwasisitiza kuchukua hatua za kujikinga. Lakini naamini kwa kutumia sheria hii ya Madaraka ya Wakati wa Dharura anaweza kuliandaa taifa kwa haraka zaidi na kuhakikisha kuwa hata ugonjwa huu ukiingia hautaenea katika jamii au kwa wazee wetu. Binafsi ningependa kuona baadhi ya hatua kama hizi zikichukuliwa kwa haraka:

  • Kutangaza kusitisishwa kwa wasafiri kutoka Ulaya na Asia kuingia nchini kwa muda wa angalau siku 21. Hii itatoa nafasi kwa watu waliopo nchini kuweza kupimwa na kuweza kutengewa eneo maalum la uangalizi wa karantini.
  • Kutangaza kuwa katika kila mkoa (na ikiwezekana wilaya) kuna hospitali ambayo imeandaliwa kuchukua wagonjwa wa COVID-19.
  • Shughuli za mikusanyiko mikubwa ya michezo hasa kwenye miji mikubwa kusitishwa. Ni vizuri kusema ni idadi gani ya watu ambayo inaruhusiwa kukusanyika. Nchi mbalimbali zina idadi tofauti, kuanzia watu 100, 200, 500, na sehemu nyingine kama Israeli wao wameweka namba ya chini kabisa. Je, kwenye nchi yetu ni idadi gani ya watu iruhusiwe kwa muda wa wiki tatu zijazo?
  • Kutenga kiasi cha fedha za dharura kukabiliana na upimaji, kuweka karantini, na kutibu magonjwa mbalimbali. Hapa Marekani pamoja na vitu vingi wana Hifadhi ya Taifa ya Madawa ambayo unaweza kulinganisha na ile ya Mafuta na Nafaka. Lengo la hifadhi hiyo ni kuhakikisha kuna dawa na vifaa mbalimbali vya kitabibu vinavyohitajika wakati wa dharura. Tanzania ifikirie pia kuanzisha hifadhi ya namna hii ambayo uwepo wake na idadi yake iwe “classified” (yaani isijulikane kwa umma).
  • Endapo ugonjwa huu utaanza kusambaa nchini naamini mojawapo ya maeneo ambayo yatasambaza kwa haraka ni usafiri wa mabasi, sherehe mbalimbali (harusi ni mfano mmojawapo) na burudani mbalimbali. Ni muhimu kudhibiti kwa ukali idadi ya watu wanaosafiiri kwenye vyombo vya umma vya usafiri ili kuhakikisha kuwa hakuna msongamano mkubwa.
  • Tupunguze msongamano kwenye jela na mahubusu zetu haraka iwezekanavyo. Nchi za wenzetu zimefungulia wafungwa na mahubusu ambao si wa makosa ya hatari ili kuhakikisha kuwa kwenye jela na mahubusu zao hakuna msongamano mkubwa wa watu. Rais Magufuli tayari anajua na ameona msongamano huo. Naamini ikimpendeza anaweza kuona ulazima na sababu ya kupunguza wafungwa na mahubusu wakati huu; na wanaweza hata kupewa credit – endapo hawatajihusishwa na uhalifu au makosa yoyote wakati wa msamaha huu wa muda basi wanapunguziwa vifungo vyao au hata kufutiwa makosa yao (kwa wale mahubusu). Pamoja na hili ni muhimu kusitisha kutembelea wagonjwa na wafungwa (isipokuwa kama kuna ulazima fulani).
  • Mambo mengine ambayo Serikali itaona yanafaa kwani wakati huu ni wakati wa dharura na wakati wa dharura unahitaji mambo ya dharura.
Ndugu zangu, mara nyingi nimekuwa nikisema kuwa “Taifa Lisilojiandaa kwa Majanga, LImejiandaa kwa Maafa”. Sasa hivi Watanzania ni kama tumepewa muda wa kujiandaa. Tumeona wenzetu (tena wakubwa) wanavyopelekeshwa na gonjwa hili na sisi tukifuata msemo wa wahenga – mwenzako akinyolewa, wewe anza kutia kichwa maji – ni vizuri tukaanza kujiandaa kunyolewa. Mtu mmoja mmoja na kama taifa tunaweza kuchukua hatua mbalimbali. Jambo hili halitoshi kuombewa na kukemewa kama pepo; jambo hili linahitaji kuangaliwa kisayansi na kijamii katika kulinda afya ya jamii (public health).

Ni vizuri kukumbuka kuwa sheria hii ni chini tu kidogo ya tangazo la hali ya hatari ya kijeshi. Hilo pia linakuwa chini ya Ibara ya 32 ya Katiba lakini inakuwa na sehemu (component) ya kipekee ya matumizi ya jeshi. Hadi hivi sasa nchi kadhaa zimeweza kushirikisha majeshi yao lakini hakuna ambayo imetangaza Martial Law (Hali ya Utawala wa Kijeshi wa Kikatiba). Sidhani kama tutafika huko.

Rais Magufuli na serikali yake wameshatoa maelekezo na wito mbalimbali katika kuwataka Watanzania kuwa wangalifu. Tayari wametuonesha hata mifano ya nini tufanye. Lakini naamini – na mimi napenda sana tahadhari kabla ya shari – ipo haja ya kutumia sheria hii ili kulilinda taifa hadi baa hili litakapopita na kwa maoni ya wengi, angalau siku thelathini. Ni bora nusu shari, kuliko shari kamili.

Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com
Unamfahamu jeipiemu unamsikia?
 
Jambo ambalo hamna anayesema ni kuwa sehemu nyingi za Africa kama mnazoona kwenye ramani huwa hazina muingiliano sana na wageni kutoka nje na wakija huwa wanajitenga sana.

Kwa Tanzania kwa kuwa bado haijaingia, huu ugonjwa unaweza mtu ukaupata sehemu za starehe ambazo wageni wanapenda kutembelea ambazo asilimia ndogo sana ya Watanzania huwa wanakwenda.

Ila kinachotuumiza kichwa kufanya maamuzi magumu ni mapato tutakayopoteza na kauchumi hetu haka tulikokuwa tunatoa data ambazo hata CAG aliyepita alikuwa anafungwa mdomo asizikosoe. Ndiyo maana tunadai kusitisha visafari vya ATCL vya India huku tukiendelea kuruhusu mashirika mengine yaingize abiria as if Corona inaweza kuletwa na ATCL pekee!

Miradi yote mikubwa itabidi isimame na itakuwa ngumu sana kuianza upya pale uchumi utakapokuwa uko shimoni.

Ila kwa sababu za kisiasa, uamuzi wako unaweza kufanyiwa kazi haraka kwa sababu wote tunajua upeo wa wafanya maamuzi.

Yaani mnampa jamaa mamlaka ya kisheria kuamuru lolote katika maisha ya watu binafsi na biashara zao, mbona tayari yamekuwa yanafanyika kwa miaka 5 sasa?
 
Bado haijafikia hatua Serikali kutangaza hali ya hatari kumpa Magufuli power za kususpend Katiba na kujitwalia madaraka makubwa yaliyo nje ya mfumo rasmi.

Jambo la msingi na la awali kabisa kwa sasa ni kwamba:

Kwa kuwa hakuna mgonjwa hata mmoja wa Korona mpaka sasa nchini, serikali inachopaswa kufanya ni kusitisha uingiaji wa wageni kutoka Ulaya, Asia na Marekani.

Kwa sasa serikali kutumia mamlaka ya hali ya hatari wakati hatuna case hata moja ni kufanya mambo kwa fasheni, eti kwa kuwa wengine wanafanya basi nasi tufanye

ila huko mbeleni pindi ikihitajika basi kama ikibidi kutangaza hali ya hatari basi ihakikishe supplies muhimu za chakula masokoni na magengeni kinapatikana.

Na pia kama ikibidi kuchukua hatua hiyo basi iliandae hilo zeoezi vyema na ifahamu kwamba wananchi wetu waliowengi uwezo wao ni kupata hela ya kula tu kwa siku, sasa serikali iwe na plan maalum, kwa kipindi chote wananchi hawa hawaingizi hela mfukoni ya kula kutokana na shughuli zao kuwa disturbed je itafanya nini kulinda miji dhidi ya vibaka na majambazi watakaotokana na watu waliosimamishiwa shughuli zao?.

Kwa sasa hili jambo la kuthibiti Corona linawezekana kwa kufuata hatua za kawaida tu na sheria zetu za kawaida bila kulazimika kumpa magufuli maguvu ya kidikiteta yatokanayo na udharura.

1. Serikali ihakikishe madawa na vifaa vya kupambana na corona vipo

2. Zuia watu wa ulaya, Asia na marekani wasije nchini kwa miezi mitatu

3. Tenga maeneo ya karantini yawe standby incase kama ugonjwa ukiingia

4. Kamwe usidisrupt supply ya mahitaji muhimu ya watu ya kila siku kwa kigezo cha Corona

5. Serikali iwe wazi na iwashirikishe wananchi kwa kila hatua inayofanya, isiwasurprize
 
Tufunge mashule na vyuo kwa muda wa cku 21.

Sent using Jamii Forums mobile app

Hili inaweza kufanyika bila kulazimika kutangaza hali ya hatari ya kumfanya Magufuli kuwa Dikteta rasmi!

Hatujapata Mgonjwa hata mmoja halafu eti Tutangaze hali ya hatari?

Labda watu wanadhani hali ya hatari ni kitu cha mchezomchezo!. Hali ya hatari maana yake Nchi iko mikononi mwa jeshi, check point kila mahali, haki zako za kikatiba nyingi zinakuwa suspended, Hakuna free movement ya watu.

Kwa sasa ambapo hatuna case hata moja hakuna justification yoyote ya kutangaza hali ya hatari ya kumpa Ngosha mamlaka za kuwa juu ya sheria, ataumiza wengi kwa kigezo cha kupambana na Corona.

Serikali iendelee kufanya juhudi kuhakikisha hicho kirusi hakiingii nchini kwa kuzuia waasia, watu wa ulaya na America kuingia nchini.

Na kwa jinsi kiongozi wetu anavyojua kuyatumia madaraka kisawasawa, ni nani wa kumthibiti kipindi hiki atakapoamua kuyatumia kwelikweli to the extreme?
 
Acha uongo na upotoshaji,Trump kutangaza hali ya dharura kupitia sheria ya hali ya dharura ni kufungulia rasilimali za serikali kuu ziweze kutumika kwa upana zaidi katika majimbo kukabiliana na ugonjwa sio hizo propoganda zako ndefu kama riwaya na ambazo mfu ulizoandika.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mueleze ukweli huyu jamaa sijui vipi? Kwanza kwa marekani ulivyoelezea wewe ndo sahihi kuhusu hatua aliyoichukua Trump. Hatua atakayoichukua Trump itakayofanana na anachosema ni “martial law”, ambapo bado ulazima huo haujafikia. Japokuwa kuna tetesi hizo.
 
Nadhani upo sahihi.

Sababu kuu ya Trump kutangaza ile hali ni ku free up federal government resources.

Ila yawezekana nikawa nimekosea....
 
View attachment 1389304

(Picha toka US Centers for Disease Control rangi nyekundu ikionesha kusambaa kwa virusi vya corona nchi mbalimbali duniani hadi jana Jumamosi Machi 14, 2020).
Na. M. M. Mwanakijiji

Tukisubiri tupate mgonjwa wa kwanza wa virusi vya corona tutakuwa tumechelewa. Tukiendelea kuombea kuwa Mungu atuepushe na janga hili tutakuwa tumechelewa. Tukisema kuwa janga hili halitatufikia tutakuwa tunajidanganya. Njia bora ya kukabiliana na janga lililo mbali ni kujiandaa nalo. Nchi nyingi za Magharibi zimechelewa sana kuchukua hatua kali kabla ya ujio wa corona ndani ya mipaka yao kiasi kwamba sasa hivi wanachukua hatua ambazo zinaonekana ni kali kweli kweli.

Katika Jimbo la Michigan nchini Marekani ambako naishi tangu taarifa za Corona zilipoanza kuja uongozi wa kisiasa wa Jimbo na miji midogo na mikubwa mara moja ulianza taratibu za kujipanga. Waliunda kamati kazi kwa ajili ya kuchukua maamuzi mbalimbali ya kuwaandaa wananchi wao. Wiki iliyopita ndio tulipata wagonjwa 2 wa kwanza na hadi kufikia leo jimbo lina wagonjwa 25 wa Corona Virus Disease ya 2019 (COVID-19). Ijumaa iliyopita Gavana amefunga kufungwa kwa shule zote za msingi na za sekondari kwa muda wa wiki tatu (kuanzia kesho) na vyuo vikuu vyote vimefungwa. Jimbo Kuu Katoliki la Detroit limetangaza kusimamisha maadhimisho ya misa za hadhara kwa muda wa wiki tatu. Leo, kila mtu anaenda kujiombea nyumbani kwake na kuombea taifa sebuleni kwake. Hakuna kumjaribu Mungu au kucheza bahati nasibu na afya.

Nchi zote ambazo zinakabiliana na ugonjwa huu viongozi wake wameamua kutumia mojawapo ya zana za kiutawala zilizoko kwenye nchi zote – Sheria za Madaraka wakati wa Dharura. Nchi zote zimeweka sheria hizi zikijua kuwa kuna wakati kuna janga au dharura fulani inaweza kutokea ambayo taratibu, sheria, na mifumo iliyopo haiwezi kusaidia kukabiliana nalo. Sheria hizi zinaitwa “Emergency Powers laws”. Sheria hizi zina lengo la kumpa kiongozi wa nchi madaraka makubwa zaidi na kuondoa ukiritimba ambao watu wameuzoea katika kufikia maamuzi. Rais basi anakuwa ndiyo mtunga sheria, taratibu na kwa agizo lake anaweza kuamuru karibu jambo lolote.

Tanzania kama nchi nyingine inayo sheria ya aina hii; inaitwa sheria ya madaraka ya dharura ya mwaka 1986 (Emergency Powers Act – 1986) (pamoja na mabadiliko yake). Sheria hii inatafsiri “dharura” kama jambo lolote lile ambalo linafanya taifa kuwa katika hali ya wasiwasi; hii ni pamoja na vita, uvamizi, uasi, kuvunjika kwa Amani, pamoja na jambo lolote linalotokana na asili au janga la asili. Magonjwa na vitu kama hivi yanaangukia katika haya majanga ya asili.

Kutangazwa kwa Hali ya Dharura/Hatari

Endapo Rais baada ya kupewa taarifa zote za kitalaam anaridhika kuwa kweli kuna janga linalotishia hali ya usalama wa taifa basi anatakiwa kwa mujibu wa Ibara ya 32 ya Katiba kutangaza hali hiyo kama ni katika eneo fulani la Jamhuri ya Muungano au sehemu yake. Atatangaza muda wa dharura hiyo na tangazo lake ni ushahidi tosha (kwa mujibu wa sheria hiyo) ya kuwepo kwa dharura hiyo. Sheria hiyo inahusu Jamhuri nzima ya Muungano (Bara na Visiwani).

Chini ya kifungu cha 6 cha sheria hiyo Rais anaweza kutoa maagizo, na kuweka taratibu za kukabiliana na janga hilo. Katika hali ya sasa, Rais akiona inafaa atatangaza nini kinatakiwa kufanyika kukabiliana na virusi vya corona. Hii ni tofauti na kutoa wito wa hiari kwa wananchi. Ina maana Rais haombi na kutegemea watu wafanye kwa hiari bali anatoa agizo au maagizo yenye nguvu za kisheria chini ya sheria hii.

Sheria hii inampa Rais hata madaraka ya kumfukuza kazi mtu yeyote ambaye anaweza kukwamisha kukabiliana na janga hilo – hata kamamtu huyo anafanya kazi kwenye kampuni binafsi. Na sheria hiyo inampa Rais madaraka ya kusitisha matumizi ya sheria au kanuni fulani. Haya ndiyo ambayo Donald Trump alifanya siku ya Ijumaa lengo ikiwa ni kurahisisha maamuzi mbalimbali. Rais wetu naye akiona inalazimisha anaweza kuweka hilo katika maagizo yake.

Kwa ufupi, sheria hii ndio njia ya haraka, sahihi, na inayopaswa kutumiwa kujiandaa kukabiliana na janga hili la corona. Tusisubiri ugonjwa uingie. Tuna faida (advantage) kuliko nchi za Magharibi na ninaamini ndio zimechangia kuchelewa kusambaa kwa ugonjwa huu. Nitataja faida hizo chache lakini siyo kinga.

  • Wagonjwa wengi kwenye za magharibi wamepatikana kwenye mikusanyiko mikubwa ya watu hasa watu wazima (kwenye nyumba za wazee, meli za starehe –cruise ships, na maeneo yenye watalii wengi wazee kama kule Italia).
  • Nchi zetu hazirundiki sana wazee kwenye eneo moja, hatuna nyumba nyingi za kutunzia wazee na hata zile zilizopo ni hasa kwa wazee ambao hawana watu wa karibu wa kuwatunza. Hata hivyo hadi jana (Jumamosi Machi 14) tayari nchi 16 za Afrika zilikuwa na angalau mgonjwa mmoja.
  • Kwa vile tumejifunza kuwa wagonjwa wengi hadi hivi sasa ni wazee, hili linaendana na hali ya ilivyo kuhusu demografia ya nchi za Magharibi. Nchi hizi nyingi (hata zile za Asia) zina watu wengi wazee kuliko vijana kulinganisha na Afrika. Ni kwa sababu hiyo ugonjwa huu unapokuja Afrika unakutana na vijana wengi wenye afya nzuri.
  • Kwa vile hii ni aina ya homa ya mafua; wapo wanaoaminikuwa hali ya hewa ya joto ambayo iko sehemu ya Afrika chini ya jangwa la Sahara inasaidia kuangamiza virusi hivi kuliko kwenye nchi za Magharibi ambako kuna majira ya baridi sasahivi. Hata hivyo hii ni nadharia ambayo haijathibitishwa kisayansi kwani baadhi ya nchi ambazo zina majira ya joto pia zinawagonjwa wa corona. Labda kipo kitu kingine (x-factor) ambacho bado hakijajulikana (binafsi ninayo nadharia yangu).
Hata hivyo, tayari tumeona kuwa tayari virusi hivi vimeshafika kwenye nchi mbalimbali za Afrika. Katika nchi hizi zote ni watu waliosafiri kutoka ng’ambo ndio wamekuja na virusi hivyo na bado hatujapata kile kinachoitwa “community spread” yaani kuanza kuambukizana kwenye jamii. Hili ndilo limetokea na linaendelea kutokea Marekani kwani watu sasa wanaanza kuambukizana wenyewe kwa wenyewe. Hili ndilo linalosababisha nchi kuchukua hatua za kufanya watu wakae mbalimbali (social distancing). Ndio sababu ya watu kutokusalimiana kwa mikono au kugusana kwa namna yoyote – hata kugongeana viatu inawafanya watu wakaribiane sana.

Maoni yangu ni kuwa Rais Magufuli amefanya vizuri hadi hivi sasa kwa kuwapa wananchi taarifa sahihi na za wakati na kuwasisitiza kuchukua hatua za kujikinga. Lakini naamini kwa kutumia sheria hii ya Madaraka ya Wakati wa Dharura anaweza kuliandaa taifa kwa haraka zaidi na kuhakikisha kuwa hata ugonjwa huu ukiingia hautaenea katika jamii au kwa wazee wetu. Binafsi ningependa kuona baadhi ya hatua kama hizi zikichukuliwa kwa haraka:

  • Kutangaza kusitisishwa kwa wasafiri kutoka Ulaya na Asia kuingia nchini kwa muda wa angalau siku 21. Hii itatoa nafasi kwa watu waliopo nchini kuweza kupimwa na kuweza kutengewa eneo maalum la uangalizi wa karantini.
  • Kutangaza kuwa katika kila mkoa (na ikiwezekana wilaya) kuna hospitali ambayo imeandaliwa kuchukua wagonjwa wa COVID-19.
  • Shughuli za mikusanyiko mikubwa ya michezo hasa kwenye miji mikubwa kusitishwa. Ni vizuri kusema ni idadi gani ya watu ambayo inaruhusiwa kukusanyika. Nchi mbalimbali zina idadi tofauti, kuanzia watu 100, 200, 500, na sehemu nyingine kama Israeli wao wameweka namba ya chini kabisa. Je, kwenye nchi yetu ni idadi gani ya watu iruhusiwe kwa muda wa wiki tatu zijazo?
  • Kutenga kiasi cha fedha za dharura kukabiliana na upimaji, kuweka karantini, na kutibu magonjwa mbalimbali. Hapa Marekani pamoja na vitu vingi wana Hifadhi ya Taifa ya Madawa ambayo unaweza kulinganisha na ile ya Mafuta na Nafaka. Lengo la hifadhi hiyo ni kuhakikisha kuna dawa na vifaa mbalimbali vya kitabibu vinavyohitajika wakati wa dharura. Tanzania ifikirie pia kuanzisha hifadhi ya namna hii ambayo uwepo wake na idadi yake iwe “classified” (yaani isijulikane kwa umma).
  • Endapo ugonjwa huu utaanza kusambaa nchini naamini mojawapo ya maeneo ambayo yatasambaza kwa haraka ni usafiri wa mabasi, sherehe mbalimbali (harusi ni mfano mmojawapo) na burudani mbalimbali. Ni muhimu kudhibiti kwa ukali idadi ya watu wanaosafiiri kwenye vyombo vya umma vya usafiri ili kuhakikisha kuwa hakuna msongamano mkubwa.
  • Tupunguze msongamano kwenye jela na mahubusu zetu haraka iwezekanavyo. Nchi za wenzetu zimefungulia wafungwa na mahubusu ambao si wa makosa ya hatari ili kuhakikisha kuwa kwenye jela na mahubusu zao hakuna msongamano mkubwa wa watu. Rais Magufuli tayari anajua na ameona msongamano huo. Naamini ikimpendeza anaweza kuona ulazima na sababu ya kupunguza wafungwa na mahubusu wakati huu; na wanaweza hata kupewa credit – endapo hawatajihusishwa na uhalifu au makosa yoyote wakati wa msamaha huu wa muda basi wanapunguziwa vifungo vyao au hata kufutiwa makosa yao (kwa wale mahubusu). Pamoja na hili ni muhimu kusitisha kutembelea wagonjwa na wafungwa (isipokuwa kama kuna ulazima fulani).
  • Mambo mengine ambayo Serikali itaona yanafaa kwani wakati huu ni wakati wa dharura na wakati wa dharura unahitaji mambo ya dharura.
Ndugu zangu, mara nyingi nimekuwa nikisema kuwa “Taifa Lisilojiandaa kwa Majanga, LImejiandaa kwa Maafa”. Sasa hivi Watanzania ni kama tumepewa muda wa kujiandaa. Tumeona wenzetu (tena wakubwa) wanavyopelekeshwa na gonjwa hili na sisi tukifuata msemo wa wahenga – mwenzako akinyolewa, wewe anza kutia kichwa maji – ni vizuri tukaanza kujiandaa kunyolewa. Mtu mmoja mmoja na kama taifa tunaweza kuchukua hatua mbalimbali. Jambo hili halitoshi kuombewa na kukemewa kama pepo; jambo hili linahitaji kuangaliwa kisayansi na kijamii katika kulinda afya ya jamii (public health).

Ni vizuri kukumbuka kuwa sheria hii ni chini tu kidogo ya tangazo la hali ya hatari ya kijeshi. Hilo pia linakuwa chini ya Ibara ya 32 ya Katiba lakini inakuwa na sehemu (component) ya kipekee ya matumizi ya jeshi. Hadi hivi sasa nchi kadhaa zimeweza kushirikisha majeshi yao lakini hakuna ambayo imetangaza Martial Law (Hali ya Utawala wa Kijeshi wa Kikatiba). Sidhani kama tutafika huko.

Rais Magufuli na serikali yake wameshatoa maelekezo na wito mbalimbali katika kuwataka Watanzania kuwa wangalifu. Tayari wametuonesha hata mifano ya nini tufanye. Lakini naamini – na mimi napenda sana tahadhari kabla ya shari – ipo haja ya kutumia sheria hii ili kulilinda taifa hadi baa hili litakapopita na kwa maoni ya wengi, angalau siku thelathini. Ni bora nusu shari, kuliko shari kamili.

Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com

Wito mzuri sana huo Mzee Mwanakijiji.

Kwa kuongezea tu, sijaona ulipozungumzia test kits [kama umezungumzia basi niwie radhi].

Tumeona jinsi ambavyo imekuwa changamoto kwa nchi kama Marekani kuzisambaza hizo kits. Nadhani kuanzia kesho ndo zitaanza kusambazwa kwa wingi nchi nzima.

Kwa Tanzania, hiyo changamoto unakabilianaje nayo? Unahakikishaje hizo kits zinafika kwa wakati huku kwetu Bariadi?

81BF5E67-F19A-4B57-8B9B-B4FC1731A636.jpeg

Jingine nililoliona Marekani ni kuhusu public-private partnership na makampuni makubwa kama Target, Walmart, Quest Diagnostics, Labcorp, Walgreens, nk., ili kuongeza na kurahisisha uwezo wa watu kupima/ pimwa hiyo Corona.

Kwa mazingira ya Tanzania, hilo unalionaje? Linawezekana kweli?

Jingine ambalo nimeliona na ambalo limenikera sana na linaendelea kunikera ni hili la ‘panic buying’.

Nadhani hata wewe utakuwa umeliona huko ulipo kijijini. Ukienda kwenye grocery stores sasa hivi kukuta baadhi ya bidhaa ni mbinde.

Paper products kama toilet paper na paper towels watu wamekuwa wakizinunua kwa wingi kupita kiasi.

Ona hizi shelves

15FC895D-B975-452A-85BA-BC2A38E5C656.jpeg
EA14B76A-9E13-4CC1-ACD6-B810646641C3.jpeg

Hawa toilet paper na paper towel hoarders wanakera sana.

Na hili si suala la Wamarekani tu. Naamini ni suala la kibinadamu zaidi. Binadamu wakabiliwapo na sintofahamu ya mustakabali wao, mambo kama hayo ya hoarding hutokea tu naturally.

Naamini uongozi wa nchi una wajibu wa kuwatuliza hofu wananchi na kuwa discourage wasinunue vitu kwa wingi na kuvihodhi majumbani mwao.

Trump leo katoa wito watu waache kufanya hivyo.

And check this out. Kabla sijamaliza kuandika hapa nimepata notification kuwa Mayor Keisha Lance-Bottoms kapiga marufuku mikusanyiko ya watu 250 na zaidi!!

FC52AD88-FA92-4150-AA83-324B068FDBF8.jpeg
 
Stafford Act was declared by Trump on Friday. Na hiyo ni kuwezesha federal funds kwenda kwenye states kukabiliana na hii pandemic.Hadi usawa huu, Illinois na Ohio wamepiga marufuku ufunguzi wa Bar and Restaurants.
 
Naunga mkono hoja, this is the Mwanakijiji we used to know and admired.
Asante Mkuu Mzee Mwanakijiji.

P
Paskali tuwe wa kweli wakati mwingine
Huyu anayeshauriwa ni leo ndio amesikia swala la corona virus?
Juzi amezungumza upupu eti sijui kubinuka sijui skirt nk do you think the guy knows what's happening around the world?! He is not serious analeta mzaha kwenye vitu vya msingi kutwa kukimbizana na Chadema na kutwa kuongelea mambo machafu utafikiri kijana wa form one kumbe mtu mzima. Mwambieni ajiheshimu kwanza ndio watu watamuelewa so far ni kama kituko cha Simpson show!

Mtoa mada asiwafanye WaTz mabwege
Corona Tz ipo mnaficha tu mwisho wake ni mbaya
Mmeambiwa wachina wanaingia toka Zambia KIA Namanga huko ndio usiseme

Kuweni serious na maisha ya Watanzania
 
Porojo tu hizo MM hata wafanye nini ugonjwa utawafikia tu watake wasitake!
Hapa Gerten, Minnesota wanafunzi wa Africa tunapata tabu sana hatuna fedha za kutosha kufanya manunuzi mbalimbali na authorities zimetuzuia kutoka kwenda kutafuta pesa
Poleni!.
P
 
Kwa wale wenye kupenda kusoma sheria yenyewe; nimeiambatanisha hapo juu kwenye posti ya kwanza. Siyo ndefu sana wala ngumu sana kuielewa.
 
Paskali tuwe wa kweli wakati mwingine
Huyu anayeshauriwa ni leo ndio amesikia swala la corona virus?
Juzi amezungumza upupu eti sijui kubinuka sijui skirt nk do you think the guy knows what's happening around the world?! He is not serious analeta mzaha kwenye vitu vya msingi kutwa kukimbizana na Chadema na kutwa kuongelea mambo machafu utafikiri kijana wa form one kumbe mtu mzima. Mwambieni ajiheshimu kwanza ndio watu watamuelewa so far ni kama kituko cha Simpson show!

Mtoa mada asiwafanye WaTz mabwege
Corona Tz ipo mnaficha tu mwisho wake ni mbaya
Mmeambiwa wachina wanaingia toka Zambia KIA Namanga huko ndio usiseme

Kuweni serious na maisha ya Watanzania

Nafikiri faida ingekuwepo endapo ingetangazwa hali ya hatari katika democrasia yetu ili Tume huru iundwe kabla ya uchaguzi wa mwaka huu, hii ya Covid-19 ni panic responce ya kibinaadamu tu kama vile Polio ilivyoanza dunia mzima ilipanic na mwisho wa siku leo hakuna anayetetemeka anaposikia neno Polio, halafu jambo jingine kimahesabu haiwezekani kutangaza hali ya hatari wakati chungu chako kiko empty..utawapa au kuwalisha nini watu wako? leo hii dawa za mafua tu kupatikana kwake ni mpaka mbinde, mask za kawaida tu hazipo na zikiwepo bei ni ya kuruka pia kuna diagnostic kits sidhani kama tuna uwezo wa kuwa nazo za kutosha kwani chungu chetu hatukijui kama kinapumua ama laa
 
Back
Top Bottom