WITO WA MWANAKIJIJI: Rais Magufuli Atumie Sheria ya Hali ya Dharura (1986) Kukabili COVID-19 (Corona Virus)

Coronavirus ishaingia na wazir wa afya kathibitisha Sasa tulipewa ushauri kuwa tunapocheza tusijibinue chupi zikaonekana ndo ushaur tuliopewa!
 
View attachment 1389304

(Picha toka US Centers for Disease Control rangi nyekundu ikionesha kusambaa kwa virusi vya corona nchi mbalimbali duniani hadi jana Jumamosi Machi 14, 2020).
Na. M. M. Mwanakijiji

Tukisubiri tupate mgonjwa wa kwanza wa virusi vya corona tutakuwa tumechelewa. Tukiendelea kuombea kuwa Mungu atuepushe na janga hili tutakuwa tumechelewa. Tukisema kuwa janga hili halitatufikia tutakuwa tunajidanganya. Njia bora ya kukabiliana na janga lililo mbali ni kujiandaa nalo. Nchi nyingi za Magharibi zimechelewa sana kuchukua hatua kali kabla ya ujio wa corona ndani ya mipaka yao kiasi kwamba sasa hivi wanachukua hatua ambazo zinaonekana ni kali kweli kweli.

Katika Jimbo la Michigan nchini Marekani ambako naishi tangu taarifa za Corona zilipoanza kuja uongozi wa kisiasa wa Jimbo na miji midogo na mikubwa mara moja ulianza taratibu za kujipanga. Waliunda kamati kazi kwa ajili ya kuchukua maamuzi mbalimbali ya kuwaandaa wananchi wao. Wiki iliyopita ndio tulipata wagonjwa 2 wa kwanza na hadi kufikia leo jimbo lina wagonjwa 25 wa Corona Virus Disease ya 2019 (COVID-19). Ijumaa iliyopita Gavana amefunga kufungwa kwa shule zote za msingi na za sekondari kwa muda wa wiki tatu (kuanzia kesho) na vyuo vikuu vyote vimefungwa. Jimbo Kuu Katoliki la Detroit limetangaza kusimamisha maadhimisho ya misa za hadhara kwa muda wa wiki tatu. Leo, kila mtu anaenda kujiombea nyumbani kwake na kuombea taifa sebuleni kwake. Hakuna kumjaribu Mungu au kucheza bahati nasibu na afya.

Nchi zote ambazo zinakabiliana na ugonjwa huu viongozi wake wameamua kutumia mojawapo ya zana za kiutawala zilizoko kwenye nchi zote – Sheria za Madaraka wakati wa Dharura. Nchi zote zimeweka sheria hizi zikijua kuwa kuna wakati kuna janga au dharura fulani inaweza kutokea ambayo taratibu, sheria, na mifumo iliyopo haiwezi kusaidia kukabiliana nalo. Sheria hizi zinaitwa “Emergency Powers laws”. Sheria hizi zina lengo la kumpa kiongozi wa nchi madaraka makubwa zaidi na kuondoa ukiritimba ambao watu wameuzoea katika kufikia maamuzi. Rais basi anakuwa ndiyo mtunga sheria, taratibu na kwa agizo lake anaweza kuamuru karibu jambo lolote.

Tanzania kama nchi nyingine inayo sheria ya aina hii; inaitwa sheria ya madaraka ya dharura ya mwaka 1986 (Emergency Powers Act – 1986)*(pamoja na mabadiliko yake). Sheria hii inatafsiri “dharura” kama jambo lolote lile ambalo linafanya taifa kuwa katika hali ya wasiwasi; hii ni pamoja na vita, uvamizi, uasi, kuvunjika kwa Amani, pamoja na jambo lolote linalotokana na asili au janga la asili. Magonjwa na vitu kama hivi yanaangukia katika haya majanga ya asili.

Kutangazwa kwa Hali ya Dharura/Hatari

Endapo Rais baada ya kupewa taarifa zote za kitalaam anaridhika kuwa kweli kuna janga linalotishia hali ya usalama wa taifa basi anatakiwa kwa mujibu wa Ibara ya 32 ya Katiba kutangaza hali hiyo kama ni katika eneo fulani la Jamhuri ya Muungano au sehemu yake. Atatangaza muda wa dharura hiyo na tangazo lake ni ushahidi tosha (kwa mujibu wa sheria hiyo) ya kuwepo kwa dharura hiyo. Sheria hiyo inahusu Jamhuri nzima ya Muungano (Bara na Visiwani).

Chini ya kifungu cha 6 cha sheria hiyo Rais anaweza kutoa maagizo, na kuweka taratibu za kukabiliana na janga hilo. Katika hali ya sasa, Rais akiona inafaa atatangaza nini kinatakiwa kufanyika kukabiliana na virusi vya corona. Hii ni tofauti na kutoa wito wa hiari kwa wananchi. Ina maana Rais haombi na kutegemea watu wafanye kwa hiari bali anatoa agizo au maagizo yenye nguvu za kisheria chini ya sheria hii.

Sheria hii inampa Rais hata madaraka ya kumfukuza kazi mtu yeyote ambaye anaweza kukwamisha kukabiliana na janga hilo – hata kamamtu huyo anafanya kazi kwenye kampuni binafsi. Na sheria hiyo inampa Rais madaraka ya kusitisha matumizi ya sheria au kanuni fulani. Haya ndiyo ambayo Donald Trump alifanya siku ya Ijumaa lengo ikiwa ni kurahisisha maamuzi mbalimbali. Rais wetu naye akiona inalazimisha anaweza kuweka hilo katika maagizo yake.

Kwa ufupi, sheria hii ndio njia ya haraka, sahihi, na inayopaswa kutumiwa kujiandaa kukabiliana na janga hili la corona. Tusisubiri ugonjwa uingie. Tuna faida (advantage) kuliko nchi za Magharibi na ninaamini ndio zimechangia kuchelewa kusambaa kwa ugonjwa huu. Nitataja faida hizo chache lakini siyo kinga.

  • Wagonjwa wengi kwenye za magharibi wamepatikana kwenye mikusanyiko mikubwa ya watu hasa watu wazima (kwenye nyumba za wazee, meli za starehe –cruise ships, na maeneo yenye watalii wengi wazee kama kule Italia).
  • Nchi zetu hazirundiki sana wazee kwenye eneo moja, hatuna nyumba nyingi za kutunzia wazee na hata zile zilizopo ni hasa kwa wazee ambao hawana watu wa karibu wa kuwatunza. Hata hivyo hadi jana (Jumamosi Machi 14) tayari nchi 16 za Afrika zilikuwa na angalau mgonjwa mmoja.
  • Kwa vile tumejifunza kuwa wagonjwa wengi hadi hivi sasa ni wazee, hili linaendana na hali ya ilivyo kuhusu demografia ya nchi za Magharibi. Nchi hizi nyingi (hata zile za Asia) zina watu wengi wazee kuliko vijana kulinganisha na Afrika. Ni kwa sababu hiyo ugonjwa huu unapokuja Afrika unakutana na vijana wengi wenye afya nzuri.
  • Kwa vile hii ni aina ya homa ya mafua; wapo wanaoaminikuwa hali ya hewa ya joto ambayo iko sehemu ya Afrika chini ya jangwa la Sahara inasaidia kuangamiza virusi hivi kuliko kwenye nchi za Magharibi ambako kuna majira ya baridi sasahivi. Hata hivyo hii ni nadharia ambayo haijathibitishwa kisayansi kwani baadhi ya nchi ambazo zina majira ya joto pia zinawagonjwa wa corona. Labda kipo kitu kingine (x-factor) ambacho bado hakijajulikana (binafsi ninayo nadharia yangu).
Hata hivyo, tayari tumeona kuwa tayari virusi hivi vimeshafika kwenye nchi mbalimbali za Afrika. Katika nchi hizi zote ni watu waliosafiri kutoka ng’ambo ndio wamekuja na virusi hivyo na bado hatujapata kile kinachoitwa “community spread” yaani kuanza kuambukizana kwenye jamii. Hili ndilo limetokea na linaendelea kutokea Marekani kwani watu sasa wanaanza kuambukizana wenyewe kwa wenyewe. Hili ndilo linalosababisha nchi kuchukua hatua za kufanya watu wakae mbalimbali (social distancing). Ndio sababu ya watu kutokusalimiana kwa mikono au kugusana kwa namna yoyote – hata kugongeana viatu inawafanya watu wakaribiane sana.

Maoni yangu ni kuwa Rais Magufuli amefanya vizuri hadi hivi sasa kwa kuwapa wananchi taarifa sahihi na za wakati na kuwasisitiza kuchukua hatua za kujikinga. Lakini naamini kwa kutumia sheria hii ya Madaraka ya Wakati wa Dharura anaweza kuliandaa taifa kwa haraka zaidi na kuhakikisha kuwa hata ugonjwa huu ukiingia hautaenea katika jamii au kwa wazee wetu. Binafsi ningependa kuona baadhi ya hatua kama hizi zikichukuliwa kwa haraka:

  • Kutangaza kusitisishwa kwa wasafiri kutoka Ulaya na Asia kuingia nchini kwa muda wa angalau siku 21. Hii itatoa nafasi kwa watu waliopo nchini kuweza kupimwa na kuweza kutengewa eneo maalum la uangalizi wa karantini.
  • Kutangaza kuwa katika kila mkoa (na ikiwezekana wilaya) kuna hospitali ambayo imeandaliwa kuchukua wagonjwa wa COVID-19.
  • Shughuli za mikusanyiko mikubwa ya michezo hasa kwenye miji mikubwa kusitishwa. Ni vizuri kusema ni idadi gani ya watu ambayo inaruhusiwa kukusanyika. Nchi mbalimbali zina idadi tofauti, kuanzia watu 100, 200, 500, na sehemu nyingine kama Israeli wao wameweka namba ya chini kabisa. Je, kwenye nchi yetu ni idadi gani ya watu iruhusiwe kwa muda wa wiki tatu zijazo?
  • Kutenga kiasi cha fedha za dharura kukabiliana na upimaji, kuweka karantini, na kutibu magonjwa mbalimbali. Hapa Marekani pamoja na vitu vingi wana Hifadhi ya Taifa ya Madawa ambayo unaweza kulinganisha na ile ya Mafuta na Nafaka. Lengo la hifadhi hiyo ni kuhakikisha kuna dawa na vifaa mbalimbali vya kitabibu vinavyohitajika wakati wa dharura. Tanzania ifikirie pia kuanzisha hifadhi ya namna hii ambayo uwepo wake na idadi yake iwe “classified” (yaani isijulikane kwa umma).
  • Endapo ugonjwa huu utaanza kusambaa nchini naamini mojawapo ya maeneo ambayo yatasambaza kwa haraka ni usafiri wa mabasi, sherehe mbalimbali (harusi ni mfano mmojawapo) na burudani mbalimbali. Ni muhimu kudhibiti kwa ukali idadi ya watu wanaosafiiri kwenye vyombo vya umma vya usafiri ili kuhakikisha kuwa hakuna msongamano mkubwa.
  • Tupunguze msongamano kwenye jela na mahubusu zetu haraka iwezekanavyo. Nchi za wenzetu zimefungulia wafungwa na mahubusu ambao si wa makosa ya hatari ili kuhakikisha kuwa kwenye jela na mahubusu zao hakuna msongamano mkubwa wa watu. Rais Magufuli tayari anajua na ameona msongamano huo. Naamini ikimpendeza anaweza kuona ulazima na sababu ya kupunguza wafungwa na mahubusu wakati huu; na wanaweza hata kupewa credit – endapo hawatajihusishwa na uhalifu au makosa yoyote wakati wa msamaha huu wa muda basi wanapunguziwa vifungo vyao au hata kufutiwa makosa yao (kwa wale mahubusu). Pamoja na hili ni muhimu kusitisha kutembelea wagonjwa na wafungwa (isipokuwa kama kuna ulazima fulani).
  • Mambo mengine ambayo Serikali itaona yanafaa kwani wakati huu ni wakati wa dharura na wakati wa dharura unahitaji mambo ya dharura.
Ndugu zangu, mara nyingi nimekuwa nikisema kuwa “Taifa Lisilojiandaa kwa Majanga, LImejiandaa kwa Maafa”. Sasa hivi Watanzania ni kama tumepewa muda wa kujiandaa. Tumeona wenzetu (tena wakubwa) wanavyopelekeshwa na gonjwa hili na sisi tukifuata msemo wa wahenga – mwenzako akinyolewa, wewe anza kutia kichwa maji – ni vizuri tukaanza kujiandaa kunyolewa. Mtu mmoja mmoja na kama taifa tunaweza kuchukua hatua mbalimbali. Jambo hili halitoshi kuombewa na kukemewa kama pepo; jambo hili linahitaji kuangaliwa kisayansi na kijamii katika kulinda afya ya jamii (public health).

Ni vizuri kukumbuka kuwa sheria hii ni chini tu kidogo ya tangazo la hali ya hatari ya kijeshi. Hilo pia linakuwa chini ya Ibara ya 32 ya Katiba lakini inakuwa na sehemu (component) ya kipekee ya matumizi ya jeshi. Hadi hivi sasa nchi kadhaa zimeweza kushirikisha majeshi yao lakini hakuna ambayo imetangaza Martial Law (Hali ya Utawala wa Kijeshi wa Kikatiba). Sidhani kama tutafika huko.

Rais Magufuli na serikali yake wameshatoa maelekezo na wito mbalimbali katika kuwataka Watanzania kuwa wangalifu. Tayari wametuonesha hata mifano ya nini tufanye. Lakini naamini – na mimi napenda sana tahadhari kabla ya shari – ipo haja ya kutumia sheria hii ili kulilinda taifa hadi baa hili litakapopita na kwa maoni ya wengi, angalau siku thelathini. Ni bora nusu shari, kuliko shari kamili.

Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com

NB: Kwa wenye kupenda rejea; nimeambatanisha sheria husika chini.
Laiti kama wangekusikiliza
 
Bado Kuna nafasi ya kuzuia kusambaa..huyo mama aliyekutwa anao..he amekutana na watu wangapi na wao wamekutana na kina Nani? Kama kweli hiini kesi moja Basi tusubiri kusikia community spread tokea Arusha.
 
Korona ije kwanza ili serikali isipoteze rasimali kupambana na chadema bora izo nguvu wazitumie kupambana na korona kukosa majanga ya kitaifa kunaifanya nchi kubweteka na viongozi kufanya mambo ya kipumbavu ugonjwa huu uje tuone investment yake.
Sijui wewe ni kabila gani?Watu unaokaa nao karibu wana shetani anayejiita mtu
 
Acha uongo na upotoshaji,Trump kutangaza hali ya dharura kupitia sheria ya hali ya dharura ni kufungulia rasilimali za serikali kuu ziweze kutumika kwa upana zaidi katika majimbo kukabiliana na ugonjwa sio hizo propoganda zako ndefu kama riwaya na ambazo mfu ulizoandika.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama umeona tofaut ungemkosoa kwa utaratibu lakn mengi ameandika kwa usahihi kabisa na s yakuyafanyia mzaha ni ushaur bora sana hope serikali inapita huku ya kuyafanyia kazi

Bandiko zuri sababu unajua kuandika na kuremba mwandiko ili tukija kwny technicality upo wrong kwny baadhi ya maeneo
1.Taifa bado alijafikia kutangaza hali ya hatari kwa kesi moja tu ambayo imelipotiwa
2.Sikweli kwamba nchi za Ulaya zina wazee wengi ndio maana Kesi nyingi zilizoreportiwa ni wazee the facts is immune system ndio sababu ya waanga wengi ni wazee ,watu wenye age 60-80 are highly vulnerable to Corona due to low immune ndio maana kuna vitu km vitamin C viashauriwa utumie Ku boost kinga yako ya mwili
3.Hatuwezi waachilia wafungwa wote nchi itakuwa pabaya zaidi ya hapa,nchi ambazo zimefanya hvyo kwa wale wenye kesi nyepesi nyepesi tu ili kupungza msongamano mheshimiwa juzi alipunguza wafungwa magerezani kupitia misamaha aliyotoa
4.Mkumbushe Mbowe kwamba huu sio mda wa siasa tupo busy kupambana na kuizibiti Corona maana nimesikia anataka aanze mikutano ya kisiasa nchi nzima,huu sio mda wa siasa kuna uzi niliandika miezi iliyopita kuomba serikali ihailishe uchaguzi maana budget ya uchaguzi ni kubwa na huu ugonjwa haushambulii tu watu bali unadhofisha uchumi wa nchi na dunia .
 
Bado Kuna nafasi ya kuzuia kusambaa..huyo mama aliyekutwa anao..he amekutana na watu wangapi na wao wamekutana na kina Nani? Kama kweli hiini kesi moja Basi tusubiri kusikia community spread tokea Arusha.

Bado kuna nafasi ya kutumia sheria hii na kufuatilia mapendekezo mengine; vinginevyo baada ya Pasaka mlipuko wa maambukizi utakuwa mkubwa zaidi; na hasa watu wanapoenda kwenye Ramadhani tutajikuta na mlipuko mwingine kabisa...
 
Back
Top Bottom