WITO WA MWANAKIJIJI: Rais Magufuli Atumie Sheria ya Hali ya Dharura (1986) Kukabili COVID-19 (Corona Virus)

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
32,935
2,000
1584294208294.png

(Picha toka US Centers for Disease Control rangi nyekundu ikionesha kusambaa kwa virusi vya corona nchi mbalimbali duniani hadi jana Jumamosi Machi 14, 2020).
Na. M. M. Mwanakijiji

Tukisubiri tupate mgonjwa wa kwanza wa virusi vya corona tutakuwa tumechelewa. Tukiendelea kuombea kuwa Mungu atuepushe na janga hili tutakuwa tumechelewa. Tukisema kuwa janga hili halitatufikia tutakuwa tunajidanganya. Njia bora ya kukabiliana na janga lililo mbali ni kujiandaa nalo. Nchi nyingi za Magharibi zimechelewa sana kuchukua hatua kali kabla ya ujio wa corona ndani ya mipaka yao kiasi kwamba sasa hivi wanachukua hatua ambazo zinaonekana ni kali kweli kweli.

Katika Jimbo la Michigan nchini Marekani ambako naishi tangu taarifa za Corona zilipoanza kuja uongozi wa kisiasa wa Jimbo na miji midogo na mikubwa mara moja ulianza taratibu za kujipanga. Waliunda kamati kazi kwa ajili ya kuchukua maamuzi mbalimbali ya kuwaandaa wananchi wao. Wiki iliyopita ndio tulipata wagonjwa 2 wa kwanza na hadi kufikia leo jimbo lina wagonjwa 25 wa Corona Virus Disease ya 2019 (COVID-19). Ijumaa iliyopita Gavana amefunga kufungwa kwa shule zote za msingi na za sekondari kwa muda wa wiki tatu (kuanzia kesho) na vyuo vikuu vyote vimefungwa. Jimbo Kuu Katoliki la Detroit limetangaza kusimamisha maadhimisho ya misa za hadhara kwa muda wa wiki tatu. Leo, kila mtu anaenda kujiombea nyumbani kwake na kuombea taifa sebuleni kwake. Hakuna kumjaribu Mungu au kucheza bahati nasibu na afya.

Nchi zote ambazo zinakabiliana na ugonjwa huu viongozi wake wameamua kutumia mojawapo ya zana za kiutawala zilizoko kwenye nchi zote – Sheria za Madaraka wakati wa Dharura. Nchi zote zimeweka sheria hizi zikijua kuwa kuna wakati kuna janga au dharura fulani inaweza kutokea ambayo taratibu, sheria, na mifumo iliyopo haiwezi kusaidia kukabiliana nalo. Sheria hizi zinaitwa “Emergency Powers laws”. Sheria hizi zina lengo la kumpa kiongozi wa nchi madaraka makubwa zaidi na kuondoa ukiritimba ambao watu wameuzoea katika kufikia maamuzi. Rais basi anakuwa ndiyo mtunga sheria, taratibu na kwa agizo lake anaweza kuamuru karibu jambo lolote.

Tanzania kama nchi nyingine inayo sheria ya aina hii; inaitwa sheria ya madaraka ya dharura ya mwaka 1986 (Emergency Powers Act – 1986)*(pamoja na mabadiliko yake). Sheria hii inatafsiri “dharura” kama jambo lolote lile ambalo linafanya taifa kuwa katika hali ya wasiwasi; hii ni pamoja na vita, uvamizi, uasi, kuvunjika kwa Amani, pamoja na jambo lolote linalotokana na asili au janga la asili. Magonjwa na vitu kama hivi yanaangukia katika haya majanga ya asili.

Kutangazwa kwa Hali ya Dharura/Hatari

Endapo Rais baada ya kupewa taarifa zote za kitalaam anaridhika kuwa kweli kuna janga linalotishia hali ya usalama wa taifa basi anatakiwa kwa mujibu wa Ibara ya 32 ya Katiba kutangaza hali hiyo kama ni katika eneo fulani la Jamhuri ya Muungano au sehemu yake. Atatangaza muda wa dharura hiyo na tangazo lake ni ushahidi tosha (kwa mujibu wa sheria hiyo) ya kuwepo kwa dharura hiyo. Sheria hiyo inahusu Jamhuri nzima ya Muungano (Bara na Visiwani).

Chini ya kifungu cha 6 cha sheria hiyo Rais anaweza kutoa maagizo, na kuweka taratibu za kukabiliana na janga hilo. Katika hali ya sasa, Rais akiona inafaa atatangaza nini kinatakiwa kufanyika kukabiliana na virusi vya corona. Hii ni tofauti na kutoa wito wa hiari kwa wananchi. Ina maana Rais haombi na kutegemea watu wafanye kwa hiari bali anatoa agizo au maagizo yenye nguvu za kisheria chini ya sheria hii.

Sheria hii inampa Rais hata madaraka ya kumfukuza kazi mtu yeyote ambaye anaweza kukwamisha kukabiliana na janga hilo – hata kamamtu huyo anafanya kazi kwenye kampuni binafsi. Na sheria hiyo inampa Rais madaraka ya kusitisha matumizi ya sheria au kanuni fulani. Haya ndiyo ambayo Donald Trump alifanya siku ya Ijumaa lengo ikiwa ni kurahisisha maamuzi mbalimbali. Rais wetu naye akiona inalazimisha anaweza kuweka hilo katika maagizo yake.

Kwa ufupi, sheria hii ndio njia ya haraka, sahihi, na inayopaswa kutumiwa kujiandaa kukabiliana na janga hili la corona. Tusisubiri ugonjwa uingie. Tuna faida (advantage) kuliko nchi za Magharibi na ninaamini ndio zimechangia kuchelewa kusambaa kwa ugonjwa huu. Nitataja faida hizo chache lakini siyo kinga.

 • Wagonjwa wengi kwenye za magharibi wamepatikana kwenye mikusanyiko mikubwa ya watu hasa watu wazima (kwenye nyumba za wazee, meli za starehe –cruise ships, na maeneo yenye watalii wengi wazee kama kule Italia).
 • Nchi zetu hazirundiki sana wazee kwenye eneo moja, hatuna nyumba nyingi za kutunzia wazee na hata zile zilizopo ni hasa kwa wazee ambao hawana watu wa karibu wa kuwatunza. Hata hivyo hadi jana (Jumamosi Machi 14) tayari nchi 16 za Afrika zilikuwa na angalau mgonjwa mmoja.
 • Kwa vile tumejifunza kuwa wagonjwa wengi hadi hivi sasa ni wazee, hili linaendana na hali ya ilivyo kuhusu demografia ya nchi za Magharibi. Nchi hizi nyingi (hata zile za Asia) zina watu wengi wazee kuliko vijana kulinganisha na Afrika. Ni kwa sababu hiyo ugonjwa huu unapokuja Afrika unakutana na vijana wengi wenye afya nzuri.
 • Kwa vile hii ni aina ya homa ya mafua; wapo wanaoaminikuwa hali ya hewa ya joto ambayo iko sehemu ya Afrika chini ya jangwa la Sahara inasaidia kuangamiza virusi hivi kuliko kwenye nchi za Magharibi ambako kuna majira ya baridi sasahivi. Hata hivyo hii ni nadharia ambayo haijathibitishwa kisayansi kwani baadhi ya nchi ambazo zina majira ya joto pia zinawagonjwa wa corona. Labda kipo kitu kingine (x-factor) ambacho bado hakijajulikana (binafsi ninayo nadharia yangu).
Hata hivyo, tayari tumeona kuwa tayari virusi hivi vimeshafika kwenye nchi mbalimbali za Afrika. Katika nchi hizi zote ni watu waliosafiri kutoka ng’ambo ndio wamekuja na virusi hivyo na bado hatujapata kile kinachoitwa “community spread” yaani kuanza kuambukizana kwenye jamii. Hili ndilo limetokea na linaendelea kutokea Marekani kwani watu sasa wanaanza kuambukizana wenyewe kwa wenyewe. Hili ndilo linalosababisha nchi kuchukua hatua za kufanya watu wakae mbalimbali (social distancing). Ndio sababu ya watu kutokusalimiana kwa mikono au kugusana kwa namna yoyote – hata kugongeana viatu inawafanya watu wakaribiane sana.

Maoni yangu ni kuwa Rais Magufuli amefanya vizuri hadi hivi sasa kwa kuwapa wananchi taarifa sahihi na za wakati na kuwasisitiza kuchukua hatua za kujikinga. Lakini naamini kwa kutumia sheria hii ya Madaraka ya Wakati wa Dharura anaweza kuliandaa taifa kwa haraka zaidi na kuhakikisha kuwa hata ugonjwa huu ukiingia hautaenea katika jamii au kwa wazee wetu. Binafsi ningependa kuona baadhi ya hatua kama hizi zikichukuliwa kwa haraka:

 • Kutangaza kusitisishwa kwa wasafiri kutoka Ulaya na Asia kuingia nchini kwa muda wa angalau siku 21. Hii itatoa nafasi kwa watu waliopo nchini kuweza kupimwa na kuweza kutengewa eneo maalum la uangalizi wa karantini.
 • Kutangaza kuwa katika kila mkoa (na ikiwezekana wilaya) kuna hospitali ambayo imeandaliwa kuchukua wagonjwa wa COVID-19.
 • Shughuli za mikusanyiko mikubwa ya michezo hasa kwenye miji mikubwa kusitishwa. Ni vizuri kusema ni idadi gani ya watu ambayo inaruhusiwa kukusanyika. Nchi mbalimbali zina idadi tofauti, kuanzia watu 100, 200, 500, na sehemu nyingine kama Israeli wao wameweka namba ya chini kabisa. Je, kwenye nchi yetu ni idadi gani ya watu iruhusiwe kwa muda wa wiki tatu zijazo?
 • Kutenga kiasi cha fedha za dharura kukabiliana na upimaji, kuweka karantini, na kutibu magonjwa mbalimbali. Hapa Marekani pamoja na vitu vingi wana Hifadhi ya Taifa ya Madawa ambayo unaweza kulinganisha na ile ya Mafuta na Nafaka. Lengo la hifadhi hiyo ni kuhakikisha kuna dawa na vifaa mbalimbali vya kitabibu vinavyohitajika wakati wa dharura. Tanzania ifikirie pia kuanzisha hifadhi ya namna hii ambayo uwepo wake na idadi yake iwe “classified” (yaani isijulikane kwa umma).
 • Endapo ugonjwa huu utaanza kusambaa nchini naamini mojawapo ya maeneo ambayo yatasambaza kwa haraka ni usafiri wa mabasi, sherehe mbalimbali (harusi ni mfano mmojawapo) na burudani mbalimbali. Ni muhimu kudhibiti kwa ukali idadi ya watu wanaosafiiri kwenye vyombo vya umma vya usafiri ili kuhakikisha kuwa hakuna msongamano mkubwa.
 • Tupunguze msongamano kwenye jela na mahubusu zetu haraka iwezekanavyo. Nchi za wenzetu zimefungulia wafungwa na mahubusu ambao si wa makosa ya hatari ili kuhakikisha kuwa kwenye jela na mahubusu zao hakuna msongamano mkubwa wa watu. Rais Magufuli tayari anajua na ameona msongamano huo. Naamini ikimpendeza anaweza kuona ulazima na sababu ya kupunguza wafungwa na mahubusu wakati huu; na wanaweza hata kupewa credit – endapo hawatajihusishwa na uhalifu au makosa yoyote wakati wa msamaha huu wa muda basi wanapunguziwa vifungo vyao au hata kufutiwa makosa yao (kwa wale mahubusu). Pamoja na hili ni muhimu kusitisha kutembelea wagonjwa na wafungwa (isipokuwa kama kuna ulazima fulani).
 • Mambo mengine ambayo Serikali itaona yanafaa kwani wakati huu ni wakati wa dharura na wakati wa dharura unahitaji mambo ya dharura.
Ndugu zangu, mara nyingi nimekuwa nikisema kuwa “Taifa Lisilojiandaa kwa Majanga, LImejiandaa kwa Maafa”. Sasa hivi Watanzania ni kama tumepewa muda wa kujiandaa. Tumeona wenzetu (tena wakubwa) wanavyopelekeshwa na gonjwa hili na sisi tukifuata msemo wa wahenga – mwenzako akinyolewa, wewe anza kutia kichwa maji – ni vizuri tukaanza kujiandaa kunyolewa. Mtu mmoja mmoja na kama taifa tunaweza kuchukua hatua mbalimbali. Jambo hili halitoshi kuombewa na kukemewa kama pepo; jambo hili linahitaji kuangaliwa kisayansi na kijamii katika kulinda afya ya jamii (public health).

Ni vizuri kukumbuka kuwa sheria hii ni chini tu kidogo ya tangazo la hali ya hatari ya kijeshi. Hilo pia linakuwa chini ya Ibara ya 32 ya Katiba lakini inakuwa na sehemu (component) ya kipekee ya matumizi ya jeshi. Hadi hivi sasa nchi kadhaa zimeweza kushirikisha majeshi yao lakini hakuna ambayo imetangaza Martial Law (Hali ya Utawala wa Kijeshi wa Kikatiba). Sidhani kama tutafika huko.

Rais Magufuli na serikali yake wameshatoa maelekezo na wito mbalimbali katika kuwataka Watanzania kuwa wangalifu. Tayari wametuonesha hata mifano ya nini tufanye. Lakini naamini – na mimi napenda sana tahadhari kabla ya shari – ipo haja ya kutumia sheria hii ili kulilinda taifa hadi baa hili litakapopita na kwa maoni ya wengi, angalau siku thelathini. Ni bora nusu shari, kuliko shari kamili.

Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com

NB: Kwa wenye kupenda rejea; nimeambatanisha sheria husika chini.
 
Attachments

JFK wabongo

JF-Expert Member
Aug 11, 2015
3,698
2,000
Kweli kabisa, bora nusu shari kuliko Shari kamili. Leo nimeongea na kijana yuko UD. Kaniambia chuo cha UD wako likizo fupi na wanatarajia kufungua wiki ijayo. Sote tunajua UD ina wanafunzi kutoka mataifa mbalimbali. Kwa hiyo tunawaleta kutoka mataifa yao na kuja kuchangamana na wenyeji. Risk ni kubwa. Bila kuchukua hatua sitahiki mapema tunaweza kuishia pabaya.
 
chuma cha mjerumani

JF-Expert Member
Dec 4, 2013
7,990
2,000
Mkuu serekali inachukua tahadhari waziri wa afya alisema tunawe na maji yanayo tiririka.

Pia Raisi alisema wakati radio inapiga mziki wakiwa wanacheza na vichupi vyao akisikia corona ata vaa gunia.

Siumeona juhudi zipo mkuu???

UMENENA VYEMA SANA WASHAURI WA RAISI AU RAISI MWENYEWE AKIPITIA HUU USHAURI TUTAKUWA KWENYE NAFASI NZURI hakutatokea maafa makubwa. Tukianza kusema tumwachie Mungu tutakuwa tumepotea. Mungu Ni wa wote na sio mbaguzi, nadhani huko magereza washapata list watakao toka. Pia hosptal za wagonjwa pia ziko tayari.

Maisha ya Tanzania yalivyomagumu huyu COVID 19 akiingia maisha yatakuwa magumu sana. Asilimia kubwa kipato kidogo mno umwambie mtu akae ndani kwa week ndo akafanye manunuzi, njaa ndo itaua watu badala ya corona.
 
mwarobaini_

JF-Expert Member
Jan 26, 2020
384
1,000
Hatukutangaza dharura wakati wa milipuko SERS na MERS, hatuna haja ya kutangaza dharura sasa, corona itapita na hakutakua na madhara makubwa kwetu, it's science.
 
Watu8

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
53,135
2,000
Serikali inabidi ianze kufanya baadhi ya jitihada ikiwemo kuanza kusafisha vyombo na magari ya usafiri wa umma kwa kemikali maalumu...

Kuzuia ndege na meli zinazotoka maeneo/nchi fulani...

Waweke vituo vya upimaji vya hiyari ikiwepo na maeneo tengefu kwa wataobainika kuwa na maambukizi,badala ya kisubiri hadi isemekane mtu au watu fulani wanashukiwa kuwa na maambukizi...

Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Dar nq mingine yoyote ya mipakani inapaswa iwekwe chini ya programu ya ukaguzi wa hali ya juu pengine ikilihusisha jeshi ili ku screen kila mtu anayeingia...
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,643
2,000
Kwanza, napenda kukufahamisha kwamba huna uelewa wa nini kinaendelea duniani, ni busara ukasikiliza na kujifunza
"mkuuwakaya, post: 34672352, member: 132163"]
Huu ugonjwa ni wa kuuendea taratibu. Unaweza tengeneza panic za ajabu na kuharibu uchumi wa nchi.
Rais Trump alijaribu ku downplay, madhara ya uchumi ni makubwa sana. Sekta ya usafiri duniani imeathirika sana.
Huwezi kusema kuna Panic wakati nchi kama Italy ipo katika lockdown. Nchi kama China, uchumi wa pili dunia wame lockdown. Kusema kuna panic ni kutoelewa ukubwa wa tatizo. Unazungumzia uchumi gani wa Tz ikiwa chumi za dunia zinazoongoza uchumi wetu zipo katika wakati mgumu.
Kitu kingine,huu ugonjwa sio hatari kama inavyo chagizwa/kubebewa mabango na vyombo ya habari.
Huu ugonjwa hauko hata kwenye top 10 ya magonjwa hatari. Huu ugonjwa na mafua ya kawaida, mafua ya kawaida ni hatari na yanaua Zaidi kulinganisha na covid ya 2019.
Kuna kitu hukijui.
Watalaam wanasema virus hawa ni novel.
Maana yake ni kuwa hawajulikani tabia zao na hata kwanini wanashambulia wazee zaidi ya vijana inabaki kuwa swali.
Kila siku watalaam wa CDC na kwingine duniani wanabadilisha data ili kujua hawa virus ni wa aina gani .

Virus hawa wanaua mara 10 zaidi ya wale wa kawaida. Kitaalam wanasema Fatality rate yake ni kubwa, kwa maana kuwa ikiwa unaupata chances ya ku survive ni ndogo kuliko virus wa kawaida.
Italy watu 360 wamekufa katika masaa 24. Huwezi kusema hayo ni mafua ya kawaida.
Kusanya takwimu za mataifa kama Marekani, watu wanakufa pamoja na utaalam na wataalam walio nao.

Mafua ya kawaida yanaua zaidi katika season , usichoangalia ni fatality rate. Wangapi wanaugua mafua ya kawaida na ku survive ukilinganisha na Covid. Kuna Epidemiology,Biostat, pathology n.k katika haya mambo si kama unavyotazama wewe kwa uelewa finyu sana.
Pia usisahau wabongo tumesha zoea shida, kuumwa kichwa au mafua makali tumeshazoea. Wenzetu wa magharibi kidogo tu, tayari anapiga simu, na akikihoa kohoa tu tayari wanamcount kwenye covid-19.
Kwa maana wabongo wamezoea misiba! ndiyo maana nasema, kaa kimya !
 
WAKO WAPI WATU WAKO

JF-Expert Member
Sep 26, 2017
1,486
2,000
View attachment 1389304

(Picha toka US Centers for Disease Control rangi nyekundu ikionesha kusambaa kwa virusi vya corona nchi mbalimbali duniani hadi jana Jumamosi Machi 14, 2020).
Na. M. M. Mwanakijiji

Tukisubiri tupate mgonjwa wa kwanza wa virusi vya corona tutakuwa tumechelewa. Tukiendelea kuombea kuwa Mungu atuepushe na janga hili tutakuwa tumechelewa. Tukisema kuwa janga hili halitatufikia tutakuwa tunajidanganya. Njia bora ya kukabiliana na janga lililo mbali ni kujiandaa nalo. Nchi nyingi za Magharibi zimechelewa sana kuchukua hatua kali kabla ya ujio wa corona ndani ya mipaka yao kiasi kwamba sasa hivi wanachukua hatua ambazo zinaonekana ni kali kweli kweli.

Katika Jimbo la Michigan nchini Marekani ambako naishi tangu taarifa za Corona zilipoanza kuja uongozi wa kisiasa wa Jimbo na miji midogo na mikubwa mara moja ulianza taratibu za kujipanga. Waliunda kamati kazi kwa ajili ya kuchukua maamuzi mbalimbali ya kuwaandaa wananchi wao. Wiki iliyopita ndio tulipata wagonjwa 2 wa kwanza na hadi kufikia leo jimbo lina wagonjwa 25 wa Corona Virus Disease ya 2019 (COVID-19). Ijumaa iliyopita Gavana amefunga kufungwa kwa shule zote za msingi na za sekondari kwa muda wa wiki tatu (kuanzia kesho) na vyuo vikuu vyote vimefungwa. Jimbo Kuu Katoliki la Detroit limetangaza kusimamisha maadhimisho ya misa za hadhara kwa muda wa wiki tatu. Leo, kila mtu anaenda kujiombea nyumbani kwake na kuombea taifa sebuleni kwake. Hakuna kumjaribu Mungu au kucheza bahati nasibu na afya.

Nchi zote ambazo zinakabiliana na ugonjwa huu viongozi wake wameamua kutumia mojawapo ya zana za kiutawala zilizoko kwenye nchi zote – Sheria za Madaraka wakati wa Dharura. Nchi zote zimeweka sheria hizi zikijua kuwa kuna wakati kuna janga au dharura fulani inaweza kutokea ambayo taratibu, sheria, na mifumo iliyopo haiwezi kusaidia kukabiliana nalo. Sheria hizi zinaitwa “Emergency Powers laws”. Sheria hizi zina lengo la kumpa kiongozi wa nchi madaraka makubwa zaidi na kuondoa ukiritimba ambao watu wameuzoea katika kufikia maamuzi. Rais basi anakuwa ndiyo mtunga sheria, taratibu na kwa agizo lake anaweza kuamuru karibu jambo lolote.

Tanzania kama nchi nyingine inayo sheria ya aina hii; inaitwa sheria ya madaraka ya dharura ya mwaka 1986 (Emergency Powers Act – 1986) (pamoja na mabadiliko yake). Sheria hii inatafsiri “dharura” kama jambo lolote lile ambalo linafanya taifa kuwa katika hali ya wasiwasi; hii ni pamoja na vita, uvamizi, uasi, kuvunjika kwa Amani, pamoja na jambo lolote linalotokana na asili au janga la asili. Magonjwa na vitu kama hivi yanaangukia katika haya majanga ya asili.

Kutangazwa kwa Hali ya Dharura/Hatari

Endapo Rais baada ya kupewa taarifa zote za kitalaam anaridhika kuwa kweli kuna janga linalotishia hali ya usalama wa taifa basi anatakiwa kwa mujibu wa Ibara ya 32 ya Katiba kutangaza hali hiyo kama ni katika eneo fulani la Jamhuri ya Muungano au sehemu yake. Atatangaza muda wa dharura hiyo na tangazo lake ni ushahidi tosha (kwa mujibu wa sheria hiyo) ya kuwepo kwa dharura hiyo. Sheria hiyo inahusu Jamhuri nzima ya Muungano (Bara na Visiwani).

Chini ya kifungu cha 6 cha sheria hiyo Rais anaweza kutoa maagizo, na kuweka taratibu za kukabiliana na janga hilo. Katika hali ya sasa, Rais akiona inafaa atatangaza nini kinatakiwa kufanyika kukabiliana na virusi vya corona. Hii ni tofauti na kutoa wito wa hiari kwa wananchi. Ina maana Rais haombi na kutegemea watu wafanye kwa hiari bali anatoa agizo au maagizo yenye nguvu za kisheria chini ya sheria hii.

Sheria hii inampa Rais hata madaraka ya kumfukuza kazi mtu yeyote ambaye anaweza kukwamisha kukabiliana na janga hilo – hata kamamtu huyo anafanya kazi kwenye kampuni binafsi. Na sheria hiyo inampa Rais madaraka ya kusitisha matumizi ya sheria au kanuni fulani. Haya ndiyo ambayo Donald Trump alifanya siku ya Ijumaa lengo ikiwa ni kurahisisha maamuzi mbalimbali. Rais wetu naye akiona inalazimisha anaweza kuweka hilo katika maagizo yake.

Kwa ufupi, sheria hii ndio njia ya haraka, sahihi, na inayopaswa kutumiwa kujiandaa kukabiliana na janga hili la corona. Tusisubiri ugonjwa uingie. Tuna faida (advantage) kuliko nchi za Magharibi na ninaamini ndio zimechangia kuchelewa kusambaa kwa ugonjwa huu. Nitataja faida hizo chache lakini siyo kinga.

 • Wagonjwa wengi kwenye za magharibi wamepatikana kwenye mikusanyiko mikubwa ya watu hasa watu wazima (kwenye nyumba za wazee, meli za starehe –cruise ships, na maeneo yenye watalii wengi wazee kama kule Italia).
 • Nchi zetu hazirundiki sana wazee kwenye eneo moja, hatuna nyumba nyingi za kutunzia wazee na hata zile zilizopo ni hasa kwa wazee ambao hawana watu wa karibu wa kuwatunza. Hata hivyo hadi jana (Jumamosi Machi 14) tayari nchi 16 za Afrika zilikuwa na angalau mgonjwa mmoja.
 • Kwa vile tumejifunza kuwa wagonjwa wengi hadi hivi sasa ni wazee, hili linaendana na hali ya ilivyo kuhusu demografia ya nchi za Magharibi. Nchi hizi nyingi (hata zile za Asia) zina watu wengi wazee kuliko vijana kulinganisha na Afrika. Ni kwa sababu hiyo ugonjwa huu unapokuja Afrika unakutana na vijana wengi wenye afya nzuri.
 • Kwa vile hii ni aina ya homa ya mafua; wapo wanaoaminikuwa hali ya hewa ya joto ambayo iko sehemu ya Afrika chini ya jangwa la Sahara inasaidia kuangamiza virusi hivi kuliko kwenye nchi za Magharibi ambako kuna majira ya baridi sasahivi. Hata hivyo hii ni nadharia ambayo haijathibitishwa kisayansi kwani baadhi ya nchi ambazo zina majira ya joto pia zinawagonjwa wa corona. Labda kipo kitu kingine (x-factor) ambacho bado hakijajulikana (binafsi ninayo nadharia yangu).
Hata hivyo, tayari tumeona kuwa tayari virusi hivi vimeshafika kwenye nchi mbalimbali za Afrika. Katika nchi hizi zote ni watu waliosafiri kutoka ng’ambo ndio wamekuja na virusi hivyo na bado hatujapata kile kinachoitwa “community spread” yaani kuanza kuambukizana kwenye jamii. Hili ndilo limetokea na linaendelea kutokea Marekani kwani watu sasa wanaanza kuambukizana wenyewe kwa wenyewe. Hili ndilo linalosababisha nchi kuchukua hatua za kufanya watu wakae mbalimbali (social distancing). Ndio sababu ya watu kutokusalimiana kwa mikono au kugusana kwa namna yoyote – hata kugongeana viatu inawafanya watu wakaribiane sana.

Maoni yangu ni kuwa Rais Magufuli amefanya vizuri hadi hivi sasa kwa kuwapa wananchi taarifa sahihi na za wakati na kuwasisitiza kuchukua hatua za kujikinga. Lakini naamini kwa kutumia sheria hii ya Madaraka ya Wakati wa Dharura anaweza kuliandaa taifa kwa haraka zaidi na kuhakikisha kuwa hata ugonjwa huu ukiingia hautaenea katika jamii au kwa wazee wetu. Binafsi ningependa kuona baadhi ya hatua kama hizi zikichukuliwa kwa haraka:

 • Kutangaza kusitisishwa kwa wasafiri kutoka Ulaya na Asia kuingia nchini kwa muda wa angalau siku 21. Hii itatoa nafasi kwa watu waliopo nchini kuweza kupimwa na kuweza kutengewa eneo maalum la uangalizi wa karantini.
 • Kutangaza kuwa katika kila mkoa (na ikiwezekana wilaya) kuna hospitali ambayo imeandaliwa kuchukua wagonjwa wa COVID-19.
 • Shughuli za mikusanyiko mikubwa ya michezo hasa kwenye miji mikubwa kusitishwa. Ni vizuri kusema ni idadi gani ya watu ambayo inaruhusiwa kukusanyika. Nchi mbalimbali zina idadi tofauti, kuanzia watu 100, 200, 500, na sehemu nyingine kama Israeli wao wameweka namba ya chini kabisa. Je, kwenye nchi yetu ni idadi gani ya watu iruhusiwe kwa muda wa wiki tatu zijazo?
 • Kutenga kiasi cha fedha za dharura kukabiliana na upimaji, kuweka karantini, na kutibu magonjwa mbalimbali. Hapa Marekani pamoja na vitu vingi wana Hifadhi ya Taifa ya Madawa ambayo unaweza kulinganisha na ile ya Mafuta na Nafaka. Lengo la hifadhi hiyo ni kuhakikisha kuna dawa na vifaa mbalimbali vya kitabibu vinavyohitajika wakati wa dharura. Tanzania ifikirie pia kuanzisha hifadhi ya namna hii ambayo uwepo wake na idadi yake iwe “classified” (yaani isijulikane kwa umma).
 • Endapo ugonjwa huu utaanza kusambaa nchini naamini mojawapo ya maeneo ambayo yatasambaza kwa haraka ni usafiri wa mabasi, sherehe mbalimbali (harusi ni mfano mmojawapo) na burudani mbalimbali. Ni muhimu kudhibiti kwa ukali idadi ya watu wanaosafiiri kwenye vyombo vya umma vya usafiri ili kuhakikisha kuwa hakuna msongamano mkubwa.
 • Tupunguze msongamano kwenye jela na mahubusu zetu haraka iwezekanavyo. Nchi za wenzetu zimefungulia wafungwa na mahubusu ambao si wa makosa ya hatari ili kuhakikisha kuwa kwenye jela na mahubusu zao hakuna msongamano mkubwa wa watu. Rais Magufuli tayari anajua na ameona msongamano huo. Naamini ikimpendeza anaweza kuona ulazima na sababu ya kupunguza wafungwa na mahubusu wakati huu; na wanaweza hata kupewa credit – endapo hawatajihusishwa na uhalifu au makosa yoyote wakati wa msamaha huu wa muda basi wanapunguziwa vifungo vyao au hata kufutiwa makosa yao (kwa wale mahubusu). Pamoja na hili ni muhimu kusitisha kutembelea wagonjwa na wafungwa (isipokuwa kama kuna ulazima fulani).
 • Mambo mengine ambayo Serikali itaona yanafaa kwani wakati huu ni wakati wa dharura na wakati wa dharura unahitaji mambo ya dharura.
Ndugu zangu, mara nyingi nimekuwa nikisema kuwa “Taifa Lisilojiandaa kwa Majanga, LImejiandaa kwa Maafa”. Sasa hivi Watanzania ni kama tumepewa muda wa kujiandaa. Tumeona wenzetu (tena wakubwa) wanavyopelekeshwa na gonjwa hili na sisi tukifuata msemo wa wahenga – mwenzako akinyolewa, wewe anza kutia kichwa maji – ni vizuri tukaanza kujiandaa kunyolewa. Mtu mmoja mmoja na kama taifa tunaweza kuchukua hatua mbalimbali. Jambo hili halitoshi kuombewa na kukemewa kama pepo; jambo hili linahitaji kuangaliwa kisayansi na kijamii katika kulinda afya ya jamii (public health).

Ni vizuri kukumbuka kuwa sheria hii ni chini tu kidogo ya tangazo la hali ya hatari ya kijeshi. Hilo pia linakuwa chini ya Ibara ya 32 ya Katiba lakini inakuwa na sehemu (component) ya kipekee ya matumizi ya jeshi. Hadi hivi sasa nchi kadhaa zimeweza kushirikisha majeshi yao lakini hakuna ambayo imetangaza Martial Law (Hali ya Utawala wa Kijeshi wa Kikatiba). Sidhani kama tutafika huko.

Rais Magufuli na serikali yake wameshatoa maelekezo na wito mbalimbali katika kuwataka Watanzania kuwa wangalifu. Tayari wametuonesha hata mifano ya nini tufanye. Lakini naamini – na mimi napenda sana tahadhari kabla ya shari – ipo haja ya kutumia sheria hii ili kulilinda taifa hadi baa hili litakapopita na kwa maoni ya wengi, angalau siku thelathini. Ni bora nusu shari, kuliko shari kamili.

Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com
Muandikie Jiwe......yuko bize kuua Demokrasia...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Top Bottom