Wito wa mpito kwa DPP: Wakili aliyemwandaa ACP Kingai aondolewe jopo la Mashtaka la akina Mbowe

CROSS EXAMINATION OF WITNESS SIO MCHEZO MCHEZO UONGO NA UKWELI HUWA MAJI NA MAFUTA.
 
Jana nilikuwepo Mahakama Kuu, Divisheni ya Uhujumu Uchumi. Sikwenda pale kwa minajiri ya kuhudhuria kesi ya akina Mbowe. Nilikwenda kufuatilia mambo ya mwanangu anayesoma pale Law School of Tanzania. Kwakuwa nilimaliza kilichonipeleka mapema na niliwaona hata marafiki zangu wakijumuika kuhudhuria kesi ya akina Mbowe, niliamua kujumuika nao. Ni katika viunga hivyohivyo vya Law School of Tanzania.

Jana, upande wa Mashtaka (Jamhuri) ilianza kuleta mashahidi. Shahidi wa kwanza, na nilishajua na kumtegemea, akawa ni ACP Ramadhani Kingai ambaye kwasasa ni RPC wa Kinondoni. Kama shahidi wa kwanza na wa muhimu wa Jamhuri, Kingai alieleza mengi kwenye kesi ya msingi na hata kwenye kesi ndogo iliyoibuka baada ya mapingamizi yaliyotolewa na upande wa Utetezi uliokuwa ukiongozwa na Wakili Msomi Kibatala.

Katika uga wa kisheria, shahidi yeyote huandaliwa na Wakili anayemleta mahakamani. Kuandaliwa si kufundishwa cha kusema ila ni kuunda mtiririko na mueleweko wa ushahidi wa shahidi husika. Pia, maadalizi hujumuisha upembuzi wa kipi cha kuanza; kipi cha kumalizia; kipi cha kusemwa na kipi cha kutokusema mahakamani kwenye kesi husika. Hata ACP Kingai aliandaliwa na Wakili au Mawakili wa Jopo la Mashtaka.

Kuna mambo ya wazi kabisa ambayo yameleta mkanganyiko badala ya muunganiko kwenye ushahidi wa Kingai. Mkanganyiko usio na tija. Kuhusu mtiririko wa matukio; kilichotokea na kilichofanyika na polisi. Nitatoa mifano michache kwakuwa mambo yenye mkanganyiko yalikuwa mengi mno. Kwanza, Kingai hakutaja kwenye ushahidi wake kuhusu watuhumiwa kufikishwa kituo cha Polisi Mbweni. Aliishia kusema walifikishwa Central Dar. Kwanini hakuandaliwa kuhusu hilo?

Pili, Kingai amesema kuwa watuhumiwa walikutwa na bastola moja na risasi tatu. Ni tofauti na Hati ya Mashtaka inayotaja risasi moja. Tatu, amezungumzia watuhumiwa kukutwa na madawa ya kulevya. Kwanini hakuandaliwa kuacha kuzungumzia kitu kisicho sehemu ya mashtaka ya akina Mbowe? Nne, Kingai amesema kuwa alipokuwa akiongoza timu ya upelelezi na ukamataji alikuwa Regional Criminal Officer (RCO) wa Arusha. Hakuandaliwa kueleza kwanini alifanyia kazi mikoa ya wengine kwenye ma-RCO na askari wengine?

Au Kingai naye alikuwa Sabaya wa pili? Tena, Kingai ameeleza kuwa kuna mashahidi walichukuliwa maelezo yao Moshi. Hapohapo akasema watuhumiwa walichukuliwa maelezo yao Dar es Salaam kwakuwa ndiko jalada lilipokuwa limefunguliwa. Kwanini wahusika wa jambo moja watofautishwe mahali pa kuchukuliwa maelezo yao? Hapa pia hakuandaliwa vyema. Kingai amefanya kadiri ya uwezo wake kuelezea. Lakini, hakuandaliwa vyema.

Halafu, kama mkamataji hakupaswa kushiriki kwenye kuwachukua maelezo washtakiwa. Hivi Wakili aliyemwandaa hakulijua hata hilo? Maana Kingai amekuwa akirudiarudia mahakamani kuwa aliwachukua maelezo washtakiwa ambao yeye mwenyewe ndiye aliyewakamata. Kufanya hivyo si kuandika stori yake mwenyewe anayetaka wengine waiamini na kumpongeza kwa uandishi wa stori tamu kuwahusu washtakiwa?

DPP Mwakitalu, chukua hatua mapema. Ondoa Wakili au Mawakili waliomuandaa Kingai. Kama Kingai amejikanyaga vile, watakaofuata wataanika madudu mapya na yakutisha zaidi.

Chief Hangaya, nasi tuanze kampeni chamani?

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Mkuu; usiwashitue. Mungu kawatia upofu. Waache wajikaange kwa mafuta yao. Inapendeza na kufurahisha.
 
Hv unadhan yanaelewa haya???
Ni wazi kuwa huielewi logic ya hoja na swali la Behaviourist au unaamua kupotezea kwa makusudi badala ya kujibu...

Ukitaka kuwa honest na kuufanya mjadala huu uwe wa manufaa kwa wote ktk kujengeana ufahamu wa hili jambo wekeni mapenzi yenu binafsi pembeni kisha tambueni nafasi ya Rais katika hili na nafasi yangu, yako na raia wengine wa kawaida...

Kiukweli kabisa ndugu Jumbe Brown Rais alipohojiwa na BBC, alisema mambo mawili very controversial yanayotafsiriwa kama "mhimili wa serikali kupitia Rais kuingilia mahakama" kuhusu kesi hii;

1. Kwamba, kuna "wenzake na Mbowe" waliokwisha hukumiwa tayari kwa makosa hayohayo. Huu ulikuwa uongo wa mchana kweupe...!

2. Kwamba, kuna ushahidi wa kutosha kuthibitisha "makosa ya Mbowe" na ndiyo maana alikimbilia Nairobi Kenya akijua ana kesi. Hii direct kuingilia mahakama...

KUMBUKA: Jambo moja kuwa, mtu aliye katika nafasi ya U Rais wa nchi kama Samia Hassan huyu, kwake anapopanua mdomo wake kuzungumza mambo ya nchi, welfare za watu anaowaongoza, hakuna kitu kinaitwa "maoni ya Rais". Kwake anapozungumza juu ya jambo lililo halisi, anakuwa anaelekeza...

Hayo sijui hupewa daily briefing na mengine ni ya kwao huko ndani. Kama hudanganywa au vipi is not our business. Sisi tuna - consume na ku - analyse kinachokuwa kimetoka tayari nje...
 
Mkitaka kutunga uongo ni lazima waongo wote mkusanyike pamoja sehemu moja, hamuwezi kutunga uongo kwa kutumia simu ambazo nazo zimechanganyikiwa kwa uongo wa kila aina na ni kila siku.
Madawa ya kulevya yameingizwa ili kukazia uwezo wa kukata miti kuanzia Dar mpaka Mbeya, kwani bila bangi hauwezi hata kufika Kimara.
Hata mkikaa pamoja bado mtapitiwa tu. Iliwahi kujitokea hii na jamaa angu . Tuliaibika mbele ya mkuu wa kituo sitakaa nisahau.
 
Hivi ni lini mahakama zetu zitaanza kufanya live streaming ya mwenendo wa kesi hasa zile zenye hisia na maslahi mapana ya jamii.
 
Jana nilikuwepo Mahakama Kuu, Divisheni ya Uhujumu Uchumi. Sikwenda pale kwa minajiri ya kuhudhuria kesi ya akina Mbowe. Nilikwenda kufuatilia mambo ya mwanangu anayesoma pale Law School of Tanzania. Kwakuwa nilimaliza kilichonipeleka mapema na niliwaona hata marafiki zangu wakijumuika kuhudhuria kesi ya akina Mbowe, niliamua kujumuika nao. Ni katika viunga hivyohivyo vya Law School of Tanzania.

Jana, upande wa Mashtaka (Jamhuri) ilianza kuleta mashahidi. Shahidi wa kwanza, na nilishajua na kumtegemea, akawa ni ACP Ramadhani Kingai ambaye kwasasa ni RPC wa Kinondoni. Kama shahidi wa kwanza na wa muhimu wa Jamhuri, Kingai alieleza mengi kwenye kesi ya msingi na hata kwenye kesi ndogo iliyoibuka baada ya mapingamizi yaliyotolewa na upande wa Utetezi uliokuwa ukiongozwa na Wakili Msomi Kibatala.

Katika uga wa kisheria, shahidi yeyote huandaliwa na Wakili anayemleta mahakamani. Kuandaliwa si kufundishwa cha kusema ila ni kuunda mtiririko na mueleweko wa ushahidi wa shahidi husika. Pia, maadalizi hujumuisha upembuzi wa kipi cha kuanza; kipi cha kumalizia; kipi cha kusemwa na kipi cha kutokusema mahakamani kwenye kesi husika. Hata ACP Kingai aliandaliwa na Wakili au Mawakili wa Jopo la Mashtaka.

Kuna mambo ya wazi kabisa ambayo yameleta mkanganyiko badala ya muunganiko kwenye ushahidi wa Kingai. Mkanganyiko usio na tija. Kuhusu mtiririko wa matukio; kilichotokea na kilichofanyika na polisi. Nitatoa mifano michache kwakuwa mambo yenye mkanganyiko yalikuwa mengi mno. Kwanza, Kingai hakutaja kwenye ushahidi wake kuhusu watuhumiwa kufikishwa kituo cha Polisi Mbweni. Aliishia kusema walifikishwa Central Dar. Kwanini hakuandaliwa kuhusu hilo?

Pili, Kingai amesema kuwa watuhumiwa walikutwa na bastola moja na risasi tatu. Ni tofauti na Hati ya Mashtaka inayotaja risasi moja. Tatu, amezungumzia watuhumiwa kukutwa na madawa ya kulevya. Kwanini hakuandaliwa kuacha kuzungumzia kitu kisicho sehemu ya mashtaka ya akina Mbowe? Nne, Kingai amesema kuwa alipokuwa akiongoza timu ya upelelezi na ukamataji alikuwa Regional Criminal Officer (RCO) wa Arusha. Hakuandaliwa kueleza kwanini alifanyia kazi mikoa ya wengine kwenye ma-RCO na askari wengine?

Au Kingai naye alikuwa Sabaya wa pili? Tena, Kingai ameeleza kuwa kuna mashahidi walichukuliwa maelezo yao Moshi. Hapohapo akasema watuhumiwa walichukuliwa maelezo yao Dar es Salaam kwakuwa ndiko jalada lilipokuwa limefunguliwa. Kwanini wahusika wa jambo moja watofautishwe mahali pa kuchukuliwa maelezo yao? Hapa pia hakuandaliwa vyema. Kingai amefanya kadiri ya uwezo wake kuelezea. Lakini, hakuandaliwa vyema.

Halafu, kama mkamataji hakupaswa kushiriki kwenye kuwachukua maelezo washtakiwa. Hivi Wakili aliyemwandaa hakulijua hata hilo? Maana Kingai amekuwa akirudiarudia mahakamani kuwa aliwachukua maelezo washtakiwa ambao yeye mwenyewe ndiye aliyewakamata. Kufanya hivyo si kuandika stori yake mwenyewe anayetaka wengine waiamini na kumpongeza kwa uandishi wa stori tamu kuwahusu washtakiwa?

DPP Mwakitalu, chukua hatua mapema. Ondoa Wakili au Mawakili waliomuandaa Kingai. Kama Kingai amejikanyaga vile, watakaofuata wataanika madudu mapya na yakutisha zaidi.

Chief Hangaya, nasi tuanze kampeni chamani?

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Sasa hii ni kuandaliwa au kufundishwa kudanganya!!
 
Mashahidi wameamua kukimbia wakajipange upya, Kingai alijikojolea wengine watakata gogo kizimbani…. dadadeeki.
 
MWENENDO MZIMA WA KESI YA MH. FREEMAN MBOWE MAHAKAMANI LEO.
PART 7.

Wakili Peter Kibatala anaendelea..

Sehemu ya kwanza ya pingamizi letu kuhusu ushahidi wetu ni kuhusu jambo la sheria na sehemu ya pili ni namna ushahidi ulivyopatikana

Naiomba mahakama ifanye kesi Ndogo katika kesi Kubwa..

Wakili Kibatala anaendelea

Jaji kwa maana hiyo tutoe hukumu sehemu ya 1 Au tufanye hukumu kwa zote mbili?

Kibatala; tutoe hukumu sehemu ya 1 kisha tufanye kesi ndani ya kesi

JAJI; unafikiri inawezekana utaratibu zote na uchukuaji wa ushahidi unaweza kuwa sehemu ya kesi ndogo?

Wakili Kibatala; ndiyo inawezekana kwa sababu sisi tunataka tuzingatie kifungu 169 CPA

Wakili Mtobesya; ukisoma kifungu cha 151 kinaruhusu kuondoa muda pale mtuhumiwa anakuwa anaendelea na upelelezi, lakini kwa ushahidi wa shahidi wa 1 waliwakamata tarehe 05 na waliwaweka lockup

Maelezo labda kama pangelikuwa na ushahidi Mbele yako unaonyesha pana sababu iliyosababisha wasichukue maelezo

Ukisoma hukumu mbalimbalimbali za Mahakama Kuu, zinaeleza kuwa labda kama palikuwa na mazingira yaliyopeleka msichukue maelezo wakati wanafanya Maelezo

Tarehe 06 walikuwa nao wote na akasafiri kuja DSM na wakafika tarehe 07 Alfajiri

Mheshimiwa Jaji Kuna muda hapa haujaelezewa, Ukisoma ushahidi wa Shahidi wa kwanza anasema hawa watu walihifadhiwa majira ya saa 4 Usiku, Ukiangalia sioni sababu kuna nini kiliwazuia wasichukue

JAJI: je unaona unahitaji kesi ndogo Nlndani ya kesi hii kama Wakili Kibatala alivyosema kwa Kifungu cha 169 cha CPA?

Wakili Mtobesya: Vifungu vya ushahidi vinamtaka shahidi yeye ndiyo aeleze, tukienda upande wa pili wa kesi ndogo inampa shahidi kuelewa ambayo hajayaleza,

Jaji; Je, Mshtakiwa wa pili alitoa hayo maelezo au hajayatoa? Je, washtakiwa walitoa maelezo au hawajatoa iwe kwa mateso au lah?

Wakili Mtobesya; Maelezo yaliyochukuliwa kinyume na Sheria hayawezi kuwa maelezo halal

Wakili Mtobesya; Mheshimiwa Jaji baada ya kujiridhisha kama walifuatisha vifungu vya sheria ndiyo twende Kwenye kesi ndani ya kesi ya msingi.

Wakili wa Serikali wanasimama na kusema tumesikia mapingamizi yote...

Kwa maoni yetu, Mapingamizi hayo yaliyowasilishwa na Upande wa Utetezi, yanaweza kuteuliwa baada ya mahakama hii kufanya kesi ndogo ndani ya kesi..

Ni baada ya Wakili Kibatala sehemu ya Pili Kulalamikia ukiukwaji wa taratibu za kisheria wakati wa kuchukua maelezo

Jambo lingine hata wakati Wakili Mtobesya alikuwa anaelezea anashindwa kujitenganisha na ushahidi.

Wakili wa pili wa serikali; Mheshimiwa jaji ni msimamo wetu kuwa mapingamizi haya yasikilizwe kupitia kesi ndogo, Baada ya ushahidi kuwa umepokelewa mahakama ituruhusu kuwasilisha

Na hata sehemu ya Kwanza ya maelezo ya kwanza ya wakili Kibatala pia ina uhusiano na kesi kubwa

Sasa sisi tunaona pingamizi la kwanza lina uhusiano na Pingamizi la Pili, Mahakama ijielekeze kwenye kesi ndogo katika Kesi ya msingi

Kibatala alisema shahidi na maafisa wengine wa polisi waliwatesa washtakiwa, atusaidie kuwataja pasipo kutuacha, je ni akina nani?

Wakili Kibatala; tunaomba tupate ruhusa ya mahakama twende kwenye kesi ndogo katika kesi ya Msingi (Trial within a trial)

Ukimya unatawala kidogo

Tunasubiri Maamuzi ya Jaji juu ya mapingamizi 2 ya kupokelewa ushahidi wa ACP kingai ambao Umewekewa mapingamizi mawili na upande wa mawakili wa utetezi

1. Maelezo ya watuhumiwa kuchukuliwa nje ya muda.

2.Maelezo ya watuhumiwa kutolewa kwa mateso kwa watuhumiwa.

Lakini kwa Pingamizi la pili linataka mahakama ihairishe kusikiliza kesi ya msingi, tusikilize Kwanza kesi kuhusu pingamizi la pili kuhusiana na watuhumiwa kama waliteswa au sivyo..

BAADA YA DAKIKA 10

Jaji anasema kama ambavyo mawakili wasomi wamebainisha kuhusu maelezo yanayosadikiwa kuwa ni maelezo ya Onyo, Kimsingi pingamizi la kwanza lilikuwa linaweza kutatuliwa bila kuwa na kesi ndogo katika kesi ya Msingi.

Jaji anasema, nakubaliana na mawakili wasomi kusimamisha kesi kuu ya msingi kwanza na kuanza kusikiliza kesi ndogo, hivyo, nahairisha kesi hii ya msingi hadi saa nane mchana, tuanze kesi kusikiliza kesi ndogo..

Kesi imehairishwa hadi sasa nane mchana. Jaji ameondoka mahakamani

TUKUTANE SAA NANE......
 
yake ndiyo si likuwa anamhoji mtuhumiwa anaandika na mtuhumiwa anasaini kwamba kilichoandikwa ni sawa sasa hapo kosa liko wapi? mbowe anaenda kula mvua za kutosha gaidi mkubwa mbwa huyu
Hii mada siyo size yako. Ficha aibu kidogo waachie waelewa watoe mtiririko wa kisheria na sio wa kiudaku kama ulivyojaza kichwani mwako.
 
Jana nilikuwepo Mahakama Kuu, Divisheni ya Uhujumu Uchumi. Sikwenda pale kwa minajiri ya kuhudhuria kesi ya akina Mbowe. Nilikwenda kufuatilia mambo ya mwanangu anayesoma pale Law School of Tanzania. Kwakuwa nilimaliza kilichonipeleka mapema na niliwaona hata marafiki zangu wakijumuika kuhudhuria kesi ya akina Mbowe, niliamua kujumuika nao. Ni katika viunga hivyohivyo vya Law School of Tanzania.

Jana, upande wa Mashtaka (Jamhuri) ilianza kuleta mashahidi. Shahidi wa kwanza, na nilishajua na kumtegemea, akawa ni ACP Ramadhani Kingai ambaye kwasasa ni RPC wa Kinondoni. Kama shahidi wa kwanza na wa muhimu wa Jamhuri, Kingai alieleza mengi kwenye kesi ya msingi na hata kwenye kesi ndogo iliyoibuka baada ya mapingamizi yaliyotolewa na upande wa Utetezi uliokuwa ukiongozwa na Wakili Msomi Kibatala.

Katika uga wa kisheria, shahidi yeyote huandaliwa na Wakili anayemleta mahakamani. Kuandaliwa si kufundishwa cha kusema ila ni kuunda mtiririko na mueleweko wa ushahidi wa shahidi husika. Pia, maadalizi hujumuisha upembuzi wa kipi cha kuanza; kipi cha kumalizia; kipi cha kusemwa na kipi cha kutokusema mahakamani kwenye kesi husika. Hata ACP Kingai aliandaliwa na Wakili au Mawakili wa Jopo la Mashtaka.

Kuna mambo ya wazi kabisa ambayo yameleta mkanganyiko badala ya muunganiko kwenye ushahidi wa Kingai. Mkanganyiko usio na tija. Kuhusu mtiririko wa matukio; kilichotokea na kilichofanyika na polisi. Nitatoa mifano michache kwakuwa mambo yenye mkanganyiko yalikuwa mengi mno. Kwanza, Kingai hakutaja kwenye ushahidi wake kuhusu watuhumiwa kufikishwa kituo cha Polisi Mbweni. Aliishia kusema walifikishwa Central Dar. Kwanini hakuandaliwa kuhusu hilo?

Pili, Kingai amesema kuwa watuhumiwa walikutwa na bastola moja na risasi tatu. Ni tofauti na Hati ya Mashtaka inayotaja risasi moja. Tatu, amezungumzia watuhumiwa kukutwa na madawa ya kulevya. Kwanini hakuandaliwa kuacha kuzungumzia kitu kisicho sehemu ya mashtaka ya akina Mbowe? Nne, Kingai amesema kuwa alipokuwa akiongoza timu ya upelelezi na ukamataji alikuwa Regional Criminal Officer (RCO) wa Arusha. Hakuandaliwa kueleza kwanini alifanyia kazi mikoa ya wengine kwenye ma-RCO na askari wengine?

Au Kingai naye alikuwa Sabaya wa pili? Tena, Kingai ameeleza kuwa kuna mashahidi walichukuliwa maelezo yao Moshi. Hapohapo akasema watuhumiwa walichukuliwa maelezo yao Dar es Salaam kwakuwa ndiko jalada lilipokuwa limefunguliwa. Kwanini wahusika wa jambo moja watofautishwe mahali pa kuchukuliwa maelezo yao? Hapa pia hakuandaliwa vyema. Kingai amefanya kadiri ya uwezo wake kuelezea. Lakini, hakuandaliwa vyema.

Halafu, kama mkamataji hakupaswa kushiriki kwenye kuwachukua maelezo washtakiwa. Hivi Wakili aliyemwandaa hakulijua hata hilo? Maana Kingai amekuwa akirudiarudia mahakamani kuwa aliwachukua maelezo washtakiwa ambao yeye mwenyewe ndiye aliyewakamata. Kufanya hivyo si kuandika stori yake mwenyewe anayetaka wengine waiamini na kumpongeza kwa uandishi wa stori tamu kuwahusu washtakiwa?

DPP Mwakitalu, chukua hatua mapema. Ondoa Wakili au Mawakili waliomuandaa Kingai. Kama Kingai amejikanyaga vile, watakaofuata wataanika madudu mapya na yakutisha zaidi.

Chief Hangaya, nasi tuanze kampeni chamani?

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Mungu ndie alieumba ubongo unaotunza kumbukumbu ivyo anajua namna ya kuuchezea ubongo ili uaibike unapopotosha ukweli kwa kuumiza viumbe wengine.

Mungu hashindwi kurekebisha screw kwenye ubongo ili kumuaibisha mtu muovu
 
Sometimes stories dont have a clear beggining, middle and end-- fiction stranger than truth. Mapolisi wajipange upya. Attention ! -Fall out.
 
Back
Top Bottom