Wito kwa CAF na FIFA wafuatilie kwa karibu sakata Yanga na Simba, lazima adhabu itolewe iwe fundisho

Tunzo

JF-Expert Member
Feb 1, 2013
4,021
2,296
Wito kwa CAF na FIFA wafwatilie kwa karibu sakata Yanga na Simba, lazima adhabu itolewe iwe Fundisho, kama kweli ratiba ilibadilishwa kwa sababu za itifaki ya kitabu kuwa kuna huduma zingine hii halikubaliki, kwani kabla ya hayo masaa 24 ratiba hiyo ya kiserekal ilikuwa haitambuliki?

Yani habari ya kitabu nimeanza kuisikua muda sana kabla hata wiki kabla ya mechi, huwezi umiza mashabiki na wapenzi wa mpira wakati ulikua unajua kuna mechi kubwa na unajua watu wako uwanjani timu kubwa wanasubiria mtanange, swali la kujiuliza ni je hili swala lililoamua mechi ipelekwe mbele ratiba ilikua haijulikani kabla ya masaa 24?
 
Yule Walace Karia ni bure kabisa! Ifikie wakati hivi vyama vya michezo viongozwe na watu wa michezo. Badala ya kuruhusu takataka kutoka nje kwa kigezo cha shahada!

Angekuwa Karia siyo kada wa CCM na angekuwa ni mtu kutoka jumuiya ya wanamichezo, naamini angekuwa muwazi kuwajulisha akina Bashungwa ya kwamba kuahirisha hiyo mechi hata kwa nusu saa tu bila ya sababu za msingi, ni kinyume na kanuni za mpira wa miguu.
 
Unataka CAF au FIFA wafanye nini? Kama Yanga busara yao iliwatuma kususia mechi kisa mida kusogezwa, sawa. Sisi Simba tupo tayari kuwapa pointi tatu na magoli mawili. Ila swali, watachukua ubingwa?
 
Unataka CAF au FIFA wafanye nini? Kama Yanga busara yao iliwatuma kususia mechi kisa mida kusogezwa, sawa. Sisi Simba tupo tayari kuwapa pointi tatu na magoli mawili. Ila swali, watachukua ubingwa?
Hapa umetoa hoja gani ndugu?
 
Wito kwa CAF na FIFA wafwatilie kwa karibu sakata Yanga na Simba, lazima adhabu itolewe iwe Fundisho, kama kweli ratiba ilibadilishwa kwa sababu za itifaki ya kitabu kua kuna huduma zingine hii halikubaliki, kwani kabla ya hayo masaa 24 ratiba hiyo ya kiserekal ilikua haitambuliki? Yani habari ya kitabu nimeanza kuisikua muda sana kabla hata wiki kabla ya mechi, huwezi umiza mashabiki na wapenzi wa mpira wakati ulikua unajua kuna mechi kubwa na unajua watu wako uwanjani timu kubwa wanasubiria mtanange, swali la kujiuliza ni je hili swala lililoamua mechi ipelekwe mbele ratiba ilikua haijulikani kabla ya masaa 24?
Hili swala likifika FIFA ,TFF inapigwa faini na nchi ya Tanzania haitoruhusiwa kushiriki mashindano yoyote yale,tutabika humu humu hamna kuchekana.
 
Back
Top Bottom