Wilson Mukama awa katibu Mkuu mpya CCM na CC Mpya

Wilson Mukama awa katibu Mkuu mpya CCM na CC Mpya

Nionavyo mimi "Hapo awali hasa kipindi cha Baba wa Taifa,wananchi walikuwa na imani kubwa kwenu CCM, hii ilitokana na kutokuwa na watu wasomi wenye kupambanua mambo, kuwa na mfumo wa chama kimoja hivyo wananchi hawakuwa na pa kukimbilia, hata kipindi cha vyama vingi mlishinda kwa kishindo kutokana na kuotesha mizizi imara kwa wananchi, pia uoga wa wananchi wakidhani chama kingine kingeweza kuvuruga utulivu wa nchi uliopo. Kwa sasa mambo yamebadilika, tuna wasomi wengi wenye kupambanua mambo, na wananchi wengi kustuka na udhalimu wenu hasa katika kipindi hiki mlichozidisha ufisadi ndani ya chama na hata serikalini. Kimsingi CCM hamtaki mabadiliko na mnaendelea kuimba nyimbo zile zile tangu 'a so called Uhuru', mnapaswa kutambua kuwa, nyimbo hizi zimewachosha watanzania wengi mpaka kukosa imani na ninyi. Hata sasa mnachofanya ni kama danganya toto, 'KUVUA GAMBA' kwa uelewa wangu, ni kuachana na mambo mabaya ya kale, na kuendeleza mazuri yaani kama kitu kinazaliwa upya, mimi nadhani hamjajua kuwa kansa inakaa kwenye damu na sio kwenye gamba kama mnavyofikiri. Kumbukeni kuwa, hao watu mnaowatoa wana makundi yao, na wanaokuja wanayo pia, hivyo mtarudi palepale. Mlichopaswa ni kukaa pamoja na kuondoa tofauti zenu, harafu mkavua gamba, hiyo haitoshi, mngekuwa mstari wa mbele katika kupiga vita ufisadi ndani ya chama na serikalini na sio kuongoza nchi hii kirafiki kama ilivyo sasa. Kwanza jisafisheni wenyewe,bila hivyo mtakuwa mnafagia uchafu, mnarudisha uchafu. Viongozi sio wabaya, tatizo ni system ndio mbovu." Ni hayo tu, Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.
 
Wewe unataifa kweli sidhani. wewe kwako utaifa ni kikundi cha watu wachache wasio na idea yoyote ambao wamejikuta by chance wako kwenye madaraka na wanayang'ang'ania kwa nguvu yoyote ile. Kwangu mimi huu sio utaifa ila ni ufashisti kwa hiyo siwezi jadiriana na wewe hata kidogo
Mkuu kama huna point za kuweka hadharani si lazima kuchangia!
 
There are currently 397 users browsing this thread. (155 members and 242 guests)
Kiranga
huyu jamaa anatunga kitabu cha physics
 
Off course "mafisadi" sio watatu tu! But who should be blamed for cheapening the war on corruption? Ni Chadema na kundi la CCM la "Wapiganaji" ambao wametumia muda mwingi kujenga nadharia hawa watu watatu tu ndio tatizo la kila kitu! Mzee Mengi akaongezea mafisadi papa kwenye mdundo huu. Leo hii hawa watu watatu ambao mpaka jana wengi wenu mlikuwa mnang'aka waondolewe, sasa wametolewa kwenye CC mnageuza kibao! Huo ni unafiki tu, hakuna kingine. Mmegundua hoja yenu ya ufisadi imesinyaa. Kubalini tu kwamba jambo zuri limefanyika halafu tusonge mbele jamani!

Haya mabadiliko ya sasa ya CCM yanatoa nafasi mpya ya kupambana na ufisadi na rushwa kwa ujumla wake, kitaifa bila ya kujali chama wala itikadi, na bila ya kuwa ni vita dhidi ya watu wachache tuliyokuwa tunachezeshwa saa zote na Chadema, Sitta na Mwakyembe.

Ninakuonea huruma ndugu yangu kuamini kuwa hiki ambacho CCM imefanya kimelenga kuondokana na ufisadi. Mafisadi wa kweli na si wa kuzushiwa bado ni Mawaziri, Wabunge na watumishi wa serikali na hakuna cha maana walichofanyiwa bali kupigwa makofi ya pongezi mgongoni. Sijashangaa kuona hata CCM haina hata aibu na hata kumweka Dr. Hussein Mwinyi kwenye Kamati Kuu (KK) yake licha ya kuwa miezi miwili iliyopita alishindwa kuwajibika kutokana na mauaji ya Gongo la Mboto. CCM inaamini kuwa Watanzania hawana kumbukumbu kama maji ya mto. Aibu mbona aibu! Ukiangalia safu hii nzee-pya utaona kuwa watu wenye mawazo-pitwa na mawazo-zembe ndio wametawala ikiwa ni pamoja na kinara wake. Sasa hapo kusema eti kuna jipya litatokea hapo si ni kuota mchana? Ni kweli mtu kama Nape alifichua ufisadi wa Jengo la UVCCM ambalo kiweli ni jengo la Serikaili kwani liijengwa na Watanzania wote. Ni kweli kuwa licha ya ukweli wake kufahamika mafisadi waliokuwa vinara wa wizi huo bado wako CCM na wana kauli kubwa.

CCM na Kikwete wanafahamu ufisadi wa Meremeta, Kagoda, EPA, Richmond, na wizi wa noti mpya-bandia. Je kuna kuwajibishwa kwa maana kumefanyika? Je, suala la rada nani kawajibishwa kikweli. Je si ndio chama ambacho kimewakumbatia,kuwafumbata, kuwabusu, kulala na kula na hao mafisadi? Sasa hapo mtu hayo matumaini-hewa unayapata wapi? Je, kauli za Chiligati je zinakupa matumaini gani ya kupambana na ufisadi. Kauli ya Kikwete ya kujivua gamba ni ya kuchekesha sana kwani haigusi chanzo cha tatizo ambalo ni pamoja na udhaifu wa ajabu sana katika uwezo wake wa kuongoza. Gamba gani limevuliwa wakati sehemu ya watu ambao ni tatizo bado wamo katika Kamati yake kuu na wamejikita katika Halmashauri Kuu(HK) na wametawala bunge?

Kwa ufupi Watanzania wenye mapenzi mema na nchi yetu matumaini yao yaelekezwe kwenye vyama vya kweli shindani na vyenye hoja za kuangalia masilahi ya nchi yetu. Ni lazima tuwe na watu ambao wanakataa kwa nguvu, akili roho, na hisia zao zote hoja-maangamizi za udini, ukabila, ukanda na rangi. Kwa kulipatia taifa letu uongozi makini unatokana na ushindanishaji wa hoja katika jukwaa la kitaifa ndipo tutaibadilisha nchi yetu na kiurudisha katika njia ya kweli ya maendeleo. Kwa kufanya hivyo tutaweza kumuangali usoni Muumba wetu siku ya haki na ukweli itakapofika.
 
Mimi sio mtabiri,lakini kwa hali ilivyo sasa ccm ndo inakufa inachofanya sasa ni kupiga makelele ya mtu anaye kata roho! mwl alitwaa mwl anatwaa,jina la TANU lihimidiwe
 
Off course "mafisadi" sio watatu tu! But who should be blamed for cheapening the war on corruption? Ni Chadema na kundi la CCM la "Wapiganaji" ambao wametumia muda mwingi kujenga nadharia hawa watu watatu tu ndio tatizo la kila kitu! Mzee Mengi akaongezea mafisadi papa kwenye mdundo huu. Leo hii hawa watu watatu ambao mpaka jana wengi wenu mlikuwa mnang'aka waondolewe, sasa wametolewa kwenye CC mnageuza kibao! Huo ni unafiki tu, hakuna kingine. Mmegundua hoja yenu ya ufisadi imesinyaa. Kubalini tu kwamba jambo zuri limefanyika halafu tusonge mbele jamani!

Haya mabadiliko ya sasa ya CCM yanatoa nafasi mpya ya kupambana na ufisadi na rushwa kwa ujumla wake, kitaifa bila ya kujali chama wala itikadi, na bila ya kuwa ni vita dhidi ya watu wachache tuliyokuwa tunachezeshwa saa zote na Chadema, Sitta na Mwakyembe.

Sijui kama mzee mwenzangu umeona ulichosema; ulichosema ni kuwa Kamati Kuu ya CCM haikufanya utafiti wake yenyewe wala kujiridhisha pasipo shaka kuona kama hao "watatu" ni kweli wanahusika na ufisadi. Kwamba, CCM Taifa wamekaa chini na kuyachukua maneno ya Chadema na "wapiganaji" na kuyachukulia maamuzi ya kuwatimua watu ili kuridhisha walalamikaji. Yaani Kikwete na kundi lake wamewaondoa madarakani kina Lowassa, Chenge na RA miongoni mwa wanachama wake waaminifu na watiifu sana kwa maneno ya "wapiganaji" basi naweza kusema pasipo shaka kuwa yumkini CCM ina matatizo makubwa zaidi kuliko tunavyofikiria.

Kama hawakuwa na ajenda ya Katiba Mpya sasa wakaichukua
Na kuwa hawakuwa wanajua mafisadi ndani ya CCM hadi walipotajwa na Chadema na sasa imewachukulia hatua

Ni wazi kuwa CCM inahitaji kuwasikiliza sana Chadema! Lakini vyovyote vile ilivyo kama hatua zilizochukuliwa Dodoma zinatokana na maneno ya Chadema basi kilichotokea kwa kina EL, RA, na AC ni travesty of justice ambayo ukilinganisha na kamati ya mwakyembe hii ya Halmashauri Kuu ya Taifa haina mfano. Maana angalau Mwakyembe alijaribu kuonesha uhusiano wa ofisi ya waziri mkuu na Richmond! Ndio maana toka mwanzo wa sakata hli binafi nimekuwa nikiuliza ni "charges" gani zilimeletwa dhidi ya hao trio? Haiwezekani kusema kuwa "wanatajwa na Chadema au wananchi wanataja taja sana majina yao". I hope the burden of proof was higher than that.
 
Truest post I ve seen in this forum in a long long time.. Nikweli kina Slaa, Mwakyembe,6 wana cheap politics.. Corruption is only part of Tanzania's problem and making it even slimmer kuwa EL,RA, Karamagi , JK ,Chenge sijui nani..ndio shida.. Shida ni kubwa kuliko hivyo na wote wanajua... CDM and the so called CCM-wapiganaji ni wambea tuu... Kilango alikuwa anapiga kelele kisa Mtandao walimpoteza yeye na mumewe 2005, kwa mfano... Hakuna cha nini wala nini..6 ambae alihongwa hela na wabrazil wakati barabara ya moro-dom inajengwa.. leo eti msafi-mpiganaji... Unafiki mtupu. Washabiki wangapi wa humu JF wanaponda ufisadi kila siku wakati wenyewe katika level yao wanapokea rushwa ndogo ndogo ama la basi wanatoa ata kwa ma traffic... Tanzania hakuna innovation, hakuna striving for excellence in research and development, business and original enterprise.. Haya huleta uongozi mbovu, policies mbovu kwanzia kwenye elimu, siasa, haki za binadamu, uchumi nk.... Ndio maana hamna kitu... Tatizo sio ufisadi pekee... Na wapiga kelele asilimia 80% humu mnahonga ma traffic police au TRA magari yenu yatoke fasta....ndio system tunayoishinayo... Wanafunzi wa sekondari wanahangaika kununua mitiani aka 'feki' as much as wanahangaika kusoma tuition.... CCM sio tatizo pekee, ata ije serikali ya the 12 Apostles, bado rushwa na ukiukwaji wa haki utakuwepo Tanzania.. Infact ata Katiba mpya haiwezi kutusaidia.. Inabidi tufundishe taifa lijalo 2050 huko mambo ndio kidogo yanaweza kuwa mazuri... Tuamkeni jamani.. Kama mimi muongo wangapi hapa hamkutafuta ma 'feki' ya form 4 au form 6??? Leo JK ndio aje kusolve yote haya, na sio namtetea wala nini.. Ukweli ni kwamba tunamatatizo mengi... Tungekaa ata tukayajadili kwa undani na uhasilia wake basi...sio ufisadi wa watu wa 3 ambao eti wakifukuzwa CCM na bungeni basi ghafla Tanzania itakuwa middle income country. That is utter nonsense.
Katika woote hawa, wewe ndio umezungumza la maana!
 
Imani haiwezi kurejea kwa kubadilisha watu, bali imani itarejea kama hatua za kulinda mali zetu dhidi ya ufisadi wa ndani na nje zitachukuliwa na matunda yake kuonekana.Leo hii tz imekuwa shamba la bibi , wawekezaji wanatuibia hivihivi tunawaona, na wengi wao wakisaidiwa na viongozi wetu, sisi tunabaki maskini wa kutupwa. Kwa hiyo kubadilisha majina hakuna maana yoyote kama hatua za kuzuia wizi wa mali zetu hazitachukuliwa, ni lazima tufike sehemu tunaposema uchumi umekuwa iwe real kwamba unatufikia wananchi kupata unafuu wa maisha kuliko kuendelea kusema LEO AFADHALI YA JANA. Kama raslimali za nchi yetu zisipoibiwa hakuna mtu kufa kwa ugonjwa unaotibika, hakuna mtoto wa mtu kushindwa kusoma kwa kukosa ada, hakuna kufa na njaa nk. Kama Gadafi aliweza wakati nchi yake ni jangwa na railimali ni mafuta tu vipi tz yenye raslimali lukuki? na nasema walibya watamkumbuka gadafi muda mfupi tu baada ya gadafi kuondoka.
 
duh kweli akina dada hawapendani watu tunajadili mengine wewe unasubiri comment za Regia ndiyo u copy na ku edit acha mambo ya taraab
Huyo mbunge ni mchemkaji tu,hana la maana analoongea,mbona chama chake ni baba mkwe akmwachia mkwewe!! au hajui?
 
kama hii mifasadi mikubwa bado ipo ni sawa na kuwa na kanzu mpya lkn sheikh wa zamani
 
W. Malecela,

Hivi ndani ya CCM hakuna vijana wengine makini zaidi ya Makamba ambae ni mbunge na tena Mwenyekiti wa kamati ya bunge! na Nape ambaye ni DC , MI NADHANI WANA MAJUKUMU YA KUTOSHA KULITUMIKIA TAIFA, KWANINI CCM WASI IBUE VIPAJI VIPYA VYA UONGOZI? Hapa naona ni status quo inaendelezwa na hilo sisi watanzania hatupendi! watu wale wale kuendelea kujirundikia madaraka! ccm bado sana! Bora chadema chama cha kanda tatu, ziwa, nyanda za juu kusini, na kaskazini lakini ccm ni chama cha koo kadhaa!

- Kwa hiyo mkuu unasema kwamba Freeman tu mkwe wa Mzee Mtei ndiye aliyefaa kuongoza Chadema hakuna wengine huko? I mean hivi haya mengine si ni kufikiri japo one minute kabla hujaandika!


FMeS!
 
JK anastahili pongezi kidogo, lakini power aliyonayo Rais na Mwenyekiti wa CCM, ni kubwa mno, hana haja ya kucompromise. Sisi waafrica tunataka kuburuzwa, Kwa hiyo JK buruza tu, as long as unasimamia haki tutakupa support.

Big Moe, kwa hiyo kwa maneno mengine unachosema ni kwamba Kikwete yeye ni safi na hivyo ana mamlaka ya kimaadili ya kuongoza vita dhidi ya ufisadi?

Kama sikosei Mwanakijiji is on record saying something to this effect 'yes i said it, Kikwete naye si safi'. What do you make of that?
 
Truest post I ve seen in this forum in a long long time.. Nikweli kina Slaa, Mwakyembe,6 wana cheap politics.. Corruption is only part of Tanzania's problem and making it even slimmer kuwa EL,RA, Karamagi , JK ,Chenge sijui nani..ndio shida.. Shida ni kubwa kuliko hivyo na wote wanajua... CDM and the so called CCM-wapiganaji ni wambea tuu... Kilango alikuwa anapiga kelele kisa Mtandao walimpoteza yeye na mumewe 2005, kwa mfano... Hakuna cha nini wala nini..6 ambae alihongwa hela na wabrazil wakati barabara ya moro-dom inajengwa.. leo eti msafi-mpiganaji... Unafiki mtupu. Washabiki wangapi wa humu JF wanaponda ufisadi kila siku wakati wenyewe katika level yao wanapokea rushwa ndogo ndogo ama la basi wanatoa ata kwa ma traffic... Tanzania hakuna innovation, hakuna striving for excellence in research and development, business and original enterprise.. Haya huleta uongozi mbovu, policies mbovu kwanzia kwenye elimu, siasa, haki za binadamu, uchumi nk.... Ndio maana hamna kitu... Tatizo sio ufisadi pekee... Na wapiga kelele asilimia 80% humu mnahonga ma traffic police au TRA magari yenu yatoke fasta....ndio system tunayoishinayo... Wanafunzi wa sekondari wanahangaika kununua mitiani aka 'feki' as much as wanahangaika kusoma tuition.... CCM sio tatizo pekee, ata ije serikali ya the 12 Apostles, bado rushwa na ukiukwaji wa haki utakuwepo Tanzania.. Infact ata Katiba mpya haiwezi kutusaidia.. Inabidi tufundishe taifa lijalo 2050 huko mambo ndio kidogo yanaweza kuwa mazuri... Tuamkeni jamani.. Kama mimi muongo wangapi hapa hamkutafuta ma 'feki' ya form 4 au form 6??? Leo JK ndio aje kusolve yote haya, na sio namtetea wala nini.. Ukweli ni kwamba tunamatatizo mengi... Tungekaa ata tukayajadili kwa undani na uhasilia wake basi...sio ufisadi wa watu wa 3 ambao eti wakifukuzwa CCM na bungeni basi ghafla Tanzania itakuwa middle income country. That is utter nonsense.

- The point ni kwamba CCM wameanza somewhere Roma haikujengwa siku moja!, Chadema wamepiga kelele CCM wamesikia na pole pole ndio mwendo wakikosea Chadema wapo, watawamsha tena!

FMeS!
 
Big Moe, kwa hiyo kwa maneno mengine unachosema ni kwamba Kikwete yeye ni safi na hivyo ana mamlaka ya kimaadili ya kuongoza vita dhidi ya ufisadi?

Kama sikosei Mwanakijiji is on record saying something to this effect 'yes i said it, Kikwete naye si safi'. What do you make of that?

Sup my people!! Long time....

The war we are trying to stop is against Corruption Sharks that have hijacked the country. JK is not among them. Pamoja na mapungufu yote aliyonayo JK, sio fisadi papa. Sisi watanzania kwa ujumla wetu karibu wote kwa njia moja au nyingine tuna cut corners. Hili la kina RA, EL, Chenge, Karamagi, Manji, Tanil nk ni mbaya sana sababu wanacontrol mpaka decision making ya mwelekeo wa nchi. Unaona hata watu wengine ambao unajua kabisa ni smart, wakiongea unagundua kabisa akili si zao, wametekwa hiyo ndio problem TZ.

Nimesema siku zote, kama TISS ingekuwa ndio ile ya wakati wa Nyerere, Kwa vyovyote vile watu hawa wangekuwa jela, au wangefilisiwa, au wasingeruhusiwa kuwa na nguvu kiasi cha kucompromise nchi kiasi hiki.

Sorry for a long mumbling, lakini JK si FISADI in this context.
 
Mtoto akianza kusimama huwa tunamuimbia "simama dede"; mtu hawezi kulaumiwa kwa kujaribu kufanya kitu kizuri. Nadhani watu wengi ambao wamekuwa kama walioumwa na nyoga kuanzia kikao cha "Butiama" hadi hivi sasa wanawasiwasi kama hiki ni cha kweli au ni sehemu ya mazingaombwe yale yale. Nadhani yote inategemea kama CCM itawatimua uanachama au hata kuwapa "karipio kali". Ninavyoona kuna uwezekano wa suala zima kuwa muted kwamba yalifanyika mabadiliko bila ya kutaja majina wala kuonesha hatua za ziada.

Tusubiri wingu litue kwanza ndipo tutajua vizuri ni kitu gani kimetokea.
 
Kuna kitu nimeanza kujifunza hapa hasa kuhusiana na huu mkutano wa CCM. Watanzania ni wepesi sana wa kuzugika na ni wepesi wa kusahau.
 
Tathmini:
Ni ngumu sana kumuondoa RA& Co kutoka CC (EL alishaondoka kwa kupoteza wadhifa), lakini imebidi ili kujenga imani (cosmetic) kwa wanachama. Kwa nguvu zao kiutawala watahakikisha kuna watu wao ndani ya CC ili wawe kiungo na wale wa NEC kuweka mambo sawa. January angechaguliwa kuingia CC moja kwa moja ingeleta malalamiko ya 'urithi'. Ujanja ni kumteua kuwa mkuu wa oganazeisheni ambayo kwa mujibu wa Katiba ya CCM ni mjumbe wa CC(automatic) na pia anatakiwa aingie NEC (technically) na ndiyo maana amechaguliwa katika wajumbe wa heshima anaoruhusiwa kuteua mwenyekiti. January na baba yake ni marafiki wa RA na EL, kwahiyo kumuingiza pale ni kufanya 'replacement ya RA & Co. technically'. Huyu ni muhimu sana kama kiungo mchezaji kati ya CC, NEC na RA& Co.

Mara zote mkuu wa oganaizesheni ya mambo ya nje ni waziri wa mambo ya nje lakini utaratibu huo umesahaulika wakati huu!!!. Kumweka oganaizesheni ya uchumi hana sifa, ya propaganda na uenezi hana mvuto hasa kwa vijana, upenyo uliokuwa ni kwa Membe.
January na oganizesheni ya CCM mambo ya nje atakuwa karibu sana na EL ambaye ana wadhifa kama huo katika kamati ya bunge(1+1). Ni Jan huyu ambaye ni mwenyekaiti wa kamati ya nishati ambako huko ndiko masilahi makubwa ya wazee yalipo.
Kwa mchezo huu gamba gani limevuliwa? Haya ni kwa uchache tu, tukimchambua kila mmoja, tutajua mengi na kujiridhisha kuwa 'kinyonga amebadili rangi lakini hajawa kambale'

Ndani ya CC kuna wajumbe wanaoingia kwa nyadhifa zao, mmoja ni spika wa bunge. Rejea nyuma uone Sitta aliondokaje na kwa nguvu ya nani na Makinda aliingiaje na kwa nguvu ya nani. Spika ndiye mkuu wa shughuliza bunge na kamati ya utawala ambayo wakuu wa kamati zingine kama za mambo ya nje na ya nishati wapo chini yake. Hapo gamba gani litakuwa limevuliwa. Fikiria.

Hii ni sehemu tu ya kuonyesha karata zilivyochezwa, lakini ni zaidi ya hapo.

Duh! Yaani tathmini yako nzima ya muundo mpya wa uongozi wa CCM umemlenga Januari Makamba peke yake. Utadhani yeye pekee ndio Sekretarieti ya Chama! Hata Katibu Mkuu Mukama hujamtaja mwanawane. This young Makamba guy must be doing something good! :love:
 
Back
Top Bottom