Wilson Mukama awa katibu Mkuu mpya CCM na CC Mpya

Wilson Mukama awa katibu Mkuu mpya CCM na CC Mpya

Ngoja tuone utendaji wake kwanza bana........

Btw...........Wewe ulitaka nani na nani wawemo kwenye Secretariat na CC ili CCM isife?......Tupe alternative basi


kwana wewe huoni wamejaza MACOBRA NA WATOTO WAKE?


WALICHOFANYA NI KUPIGA PERFUME CHOONI
 
Muziki umenoga, Dj kaweka single wanayoipenda wachezaji -sijui ni ya Mbaraka Mwishehe, Babu Seya, 20%, au Twanga pepeta mi sijui; lakini kwa uhakika kabisa tutegemee zaidi ya miezi miwili - macho na masikio yetu kushuhudia pongezi kwa hatua hii ya kujivua gamba (kinamna). Tutakaposhutuka mswada wa kuhuhisha katiba iliyopo utakuwa umekwisha pitishwa na dowans imekwisha lipwa.
 
Habari ndio hiyo, gamba la nyoka likivika hurejea siku hiyo hiyo
 
hivi nyoka anapojivua gamba, kuna sehemu ya mwili inabaki ? Mfano kichwa au kikwete ! Halafu tunapoongelea makundi ndani ya ccm, kikwete tunamweka kundi gani na hao tunaowatuhumu kwa ufisadi ndani ya ccm, je kikwete si moja wao ? Kwa mbali nakumbuka ile "first eleven" ya mwembeyanga, kapteni na mabeki bado wametulia tuli ! Na sasa eti wanawarubuni wakokota mpira vijana, kaazi kweli kweli !

wajivue govi ndio lenye heshima sio gamba
 
Nadhani watu wanakuwa na presha tu zisizo na sababu; as usual JF inakuwa ahead of the crowd.. nadhani baada ya habari kuvuja ilibidi wafanye mabadiliko kidogo as kutokana na reaction ya watu. Kudos!!
Ya ukatibu mkuu nilijua kubadilisha ingekuwa kazi sana. Option iliyokuwepo ilikuwa ni SS, hapo ingeleta mtafaruku mkubwa (kwa wanaoelewa namaaanisha nini)
 
January na Nape bado sijawaelewa hawa wazeee wamewaweka hapo ili iweje kuna jambo behind the darkness? Why them now kuna woga gani ndani ya CCM kuwaweka hao vijana mapemaaa?

Pili hao wakina Bashe na Ridwani, Beno, Shigella wako wapi walikuwa wanajishepetua this time itakula kwao live wale wote waliko kwa mkondo wa kuwafanyia kazi wakina EL na RA ndio mwisho wao hamto amini nayo waambieni subirini mtayashuhudia mengi hao UVCCM, Mwakumbuka wali mtosa sana Nape sasa yako wapi mwenzao anachana Mbuga vibaya sasa
 
Tunasubiri tuone kazi, kwani kama kama ni majina Tanzania tunayo ya aina tofauti wasi wasi wangu ni kwamba watakuwa wamebadilisha MSITU manyani ni wale wale. Kwa kuzingatia kwamba msitu hauna tabia wenye tabia ni viumbe waishio humo! Tusubiri tuone kama kutakuwa na chochote kipya hasa suala la nidhamu ya chama chao.
 
Wakuu: kuna upotoshwaji unaofanywa na CCM, kupitia wanahabari pia hadi ndani na nje ya JF, kuhusu aliekuwa katibu mkuu wa ccm, "Mwalimu" Makamba. Issue hapa ni kastaafu, kajiudhuru ama kafukuzwa? Maneno haya yana tofauti kubwa, Tusipotoshe umma bana.
 
Kesho natumai Secretariat mpya itawaeleza watanzania nani ni mmiliki wa Kagoda, dowans, ni nani alirejesha fedha za EPA, kwa nini ccm ilitaka kuilipa dowans Shs 94 billions nk.
Tofauti na hapo ni paukwa pakawa,

Ugonvi wetu mkubwa ni watanzania kuendelea kuwa maskini wakutupwa ili hali Mali zetu na hasa Madini yetu nanachotwa bure na wageni na pia nchi kufilisiwa na mafisa wachache kwenye Chama cha SISIEME na Serikali yake. Mapambano yataendelea hadi wale wote wanaolindwa na sisieme kama Mzee wa Vijisente na akina Rostam wamefikishwa mahakamani na kulipa senti ya mwisho waliyoiyowaibia Walalahoi Tanzania
 
hahaaa kajiuzuru ndo maana soon ataanza kuitwa KATIBU MKUU MSTAAFU
 
Mbona Ridhiwani kakosekana - jamaa anaona noma kumweka mwanae - anaishia kuwaweka watoto wa maswahiba! Au ndio ahadi ya uwaziri aliyoitoa kwa Januari! Kweli gamba limevuka (makambo mkubwa to makamba mdogo) - lakini mtoto wa nyoka ni nyoka mbona?

Kwani na wewe una mawazo sawa na ya baba yako?
 
Koo nne bado zinakamata ulingo.Umenipata?

hivi mzazi kama aliwahi kutawala nchi/kampuni nk. watoto hawaruhusiwi kutawala?? hili suala la koo lina maana gani?
mtu kama anasifa za kufanya kazi vizuri - apewe madaraka.
nafikiri ni vizuri tuzungumzie individuals vs uwezo binafsi unless kama kuna ushahidi kuwa wanabebwa ndiyo sasa tujadili
 
Eti kuvugua gamba ni kumuondoa makamba! Ni herufi tu ndo ziko tofauti, Gamba,Makamba! Safu yao haitalingana hata robo ya ile ya cdm,akisimama Lissu au marando kutoa hoja,hawa walioteuliwa/si kuchaguliwa,wanaweza toroka kwa taksi.
 
ni msomi na mtu makini sana! Ukiacha itikadi mimi namkubali sana na huenda akakisaidia chama! Safari njema ccm ndani ya gamba jipya!
 
January alikuwa mlevi wa kupindukia enzi zake morogoro hadi alikuwa analala kwenye mabaa bahati ikikuangukia ushukuru. Hongera kaka mkubwa ila usifuate mfano wa baba yako mzee makamba.
 
Kama ilivyo ada, ina maana kwamba mgombea urais mwaka 2015 atatokana na wajumbe wa CC. Swali linakuja, je ni nani katika hawa atapeperusha kibendera:

Hussein Mwinyi, Mbarawa, Omar Yusuf, Seif Khatib, Samia, Maua Daftari, Meghji, Kinana, Lukuvi na Mwenyekiti wa Kagera wa CCM (Mama Buhie), Kigoda, Wassira na Pindi Chana - CC
 
Nadhani watu wanakuwa na presha tu zisizo na sababu; as usual JF inakuwa ahead of the crowd.. nadhani baada ya habari kuvuja ilibidi wafanye mabadiliko kidogo as kutokana na reaction ya watu. Kudos!!

Labda mlivujiwa habari nusu nusu tu bwana. Watu walikuwa na additional info tangu jana ambazo nyie JF hamkuweka.
 
Huku kuuma na kupuliza ndio kunakoiharibu CCM. January makamba anapaa kwa kasi ya rocket? Kafanya muujiza gani? ataweza haya majukumu yote? au ndio kumuachia ajikaange kwa mafuta yake mwenyewe? au kumpoza mzee anayeondoka? Chama kinapokuwa namna hii lazima uulize maswali! Akiondoka baba, mtoto anachukua nafasi, akiingia anatengeneza nafasi za watoto wake! Any way, wote tuna haki, ila naona haki za wengine kama zimezidi. CCM haina vijana wengine wenye uwezo? au ndio mtindo wa chiefdom. Son of chief, grandson of chief, chief chief!

CHADEMA kuna undugu wa kila aina...mke mume, baba watoto, kaka dada nk... mbona hamlalamikii chiefdom ndani ya CHADEMA? Acheni unafiki.
 
Back
Top Bottom