Kesho natumai Secretariat mpya itawaeleza watanzania nani ni mmiliki wa Kagoda, dowans, ni nani alirejesha fedha za EPA, kwa nini ccm ilitaka kuilipa dowans Shs 94 billions nk.
Tofauti na hapo ni paukwa pakawa, hapo zamani paliondokea baba mmoja akawa katibu mkuu wa chama cha wala maskini, akawa anasema ovyo kila alipokuwa akikutana na hao maskini. Maskini wakachachamaa wakaahidi kutokichagua chama hicho asilani. Mwenyekiti alipogundua akaanzisha giliba; akaamua kumweka pembeni kisha akamweka mwanaye. Wananchi maskini wakaitisha maandamano ya kumsifu mwenyekiti wa chama cha wala maskini. Yeye mwenyewe akajisahau akawaambia wale maskini, mnahitaji wakati mwingine kuchanganya na akili zenu angalau kidogo; yaani mmesahau kuwa jasiri haachi asili; mi nimemundoa katibu na katika madaraka nikamweka mwanaye kwenye kapu sasa mnanipongeza kwa lipi. Wananchi masikini wakaguna ooooh! Hiyo ilikuwa ni mwaka wake wa 10 ktk madaraka yake, naye alikuwa tayari kuondoka madarakani kwa mujibu wa taratabu.
Tehe teheheeeeeeeeee