Imani kumbe ni kitu cha ajabu sana. Tunaweza kuamini mambo mengi hata bila sababu ya msingi ya kuamini. Wakati mwingine muda ndio kitu pekee kinachohitajika kuweza kupima imani yetu. Sasa hivi nimejifunza kuamini tofauti; naamini kuwa bado kanuni za mabadiliko ya kimaumbile zinafanya kazi. Lakini bado kanuni hizo bado hazijaweza kutuonesha kwa uhakika kuwa kama kweli binadamu alitoka kwa sokwe kwanini sokwe bado wapo na binadamu bado wapo? Na hazijatudokeza ni vitu gani vinahitajika kwa kinyonga kugeuzwa na kuwa kambale?
Mag3
Hivi nyoka anapojivua gamba, kuna sehemu ya mwili inabaki ? mfano kichwa au Kikwete ! Halafu tunapoongelea makundi ndani ya CCM, Kikwete tunamweka kundi gani na hao tunaowatuhumu kwa Ufisadi ndani ya CCM, je Kikwete si moja wao ? Kwa mbali nakumbuka ile "first eleven" ya Mwembeyanga, kapteni na mabeki bado wametulia tuli ! Na sasa eti wanawarubuni waokota mpira vijana, kaazi kweli kweli !
Kwa siku kadhaa wengine tumekuwa tukiamini kuwa hiki ni kiini macho, tukiamini kuwa nyoka swila akijivua gamba habadiliki kuwa kifutu, au chatu akijivua gamba habadiliki kuwa mamba, wote watabaki na hulka zao kimaumbile au kwa sumu.
CCM ni wajuzi sana wa kuteka fikra za Watanzania na wamekuwa wanacheza karata yao vema wakijua sisi Watanzania huwa hatujiulizi: kwanini, nani, vipi au kwasababu gani. Ni watu wa kwenda na upepo hata kama unatupeleka baharini.
CCM wanajua kilio cha wanachama wao ni mafisadi waliokichafua chama na kubaki na nyadhifa zao. Kilichofanyika ni kubadilisha rangi na sasa tunaona watu wanashangalia. Hakika si nyadhifa za mafisadi ni zaidi ya hapo. Kujivua gamba na kuwaacha wakifanya mambo kwa 'remote control' ni kujidanganya.
Tathmini:
Ni ngumu sana kumuondoa RA& Co kutoka CC (EL alishaondoka kwa kupoteza wadhifa), lakini imebidi ili kujenga imani (cosmetic) kwa wanachama. Kwa nguvu zao kiutawala watahakikisha kuna watu wao ndani ya CC ili wawe kiungo na wale wa NEC kuweka mambo sawa. January angechaguliwa kuingia CC moja kwa moja ingeleta malalamiko ya 'urithi'. Ujanja ni kumteua kuwa mkuu wa oganazeisheni ambayo kwa mujibu wa Katiba ya CCM ni mjumbe wa CC(automatic) na pia anatakiwa aingie NEC (technically) na ndiyo maana amechaguliwa katika wajumbe wa heshima anaoruhusiwa kuteua mwenyekiti. January na baba yake ni marafiki wa RA na EL, kwahiyo kumuingiza pale ni kufanya 'replacement ya RA & Co. technically'. Huyu ni muhimu sana kama kiungo mchezaji kati ya CC, NEC na RA& Co.
Mara zote mkuu wa oganaizesheni ya mambo ya nje ni waziri wa mambo ya nje lakini utaratibu huo umesahaulika wakati huu!!!. Kumweka oganaizesheni ya uchumi hana sifa, ya propaganda na uenezi hana mvuto hasa kwa vijana, upenyo uliokuwa ni kwa Membe.
January na oganizesheni ya CCM mambo ya nje atakuwa karibu sana na EL ambaye ana wadhifa kama huo katika kamati ya bunge(1+1). Ni Jan huyu ambaye ni mwenyekaiti wa kamati ya nishati ambako huko ndiko masilahi makubwa ya wazee yalipo.
Kwa mchezo huu gamba gani limevuliwa? Haya ni kwa uchache tu, tukimchambua kila mmoja, tutajua mengi na kujiridhisha kuwa 'kinyonga amebadili rangi lakini hajawa kambale'
Ndani ya CC kuna wajumbe wanaoingia kwa nyadhifa zao, mmoja ni spika wa bunge. Rejea nyuma uone Sitta aliondokaje na kwa nguvu ya nani na Makinda aliingiaje na kwa nguvu ya nani. Spika ndiye mkuu wa shughuliza bunge na kamati ya utawala ambayo wakuu wa kamati zingine kama za mambo ya nje na ya nishati wapo chini yake. Hapo gamba gani litakuwa limevuliwa. Fikiria.
Hii ni sehemu tu ya kuonyesha karata zilivyochezwa, lakini ni zaidi ya hapo.