Wilson Mukama awa katibu Mkuu mpya CCM na CC Mpya

Wilson Mukama awa katibu Mkuu mpya CCM na CC Mpya

Invisible

Robot
Joined
Feb 26, 2006
Posts
16,285
Reaction score
8,467
Wilson Mukama kaukwaa ukatibu mkuu wa CCM, Makamba nje!

Ni kama ilivyotabiriwa na mwana JF mmoja January 12, 2011 hapa ~ https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...lson-mukama-anaandaliwa-kumpokea-makamba.html

ZAIDI ni kuwa, Lowassa, RA na wenzao (watuhumiwa wa ufisadi) wamepewa muda kufikia kikao kijacho wawe wameachia ngazi ama watoe sababu za kwanini wasivuliwe vyeo. Ni miezi mitatu ijayo.

Mengine zaidi ni kwa msaada wa Mugumu (kama inavyoonekana chini)


Wajumbe wapya wa NEC wa kuteuliwa na Mwenyekiti ni Nchimbi, Januari Makamba, Anna Abdallah, Ali Juma Shamhuna, Peter Kisumo, Wilson Mukama na Lameck Mwigulu.

Katibu Mkuu mpya wa CCM atakuwa ni Wilson Mukama, Naibu wake atakuwa ni John Chiligati, Fedha atakuwa ni Mwigulu, Nape atakuwa Uenezi, Mambo ya nje ni Januari Makamba.

Hussein Mwinyi, Mbarawa, Omar Yusuf, Seif Khatib, Samia, Maua Daftari, Meghji, Kinana, Lukuvi na Mwenyekiti wa Kagera wa CCM (Mama Buhie), Kigoda, Wassira na Pindi Chana - CC

NEC ya CCM ipo hivi:

(VIONGOZI WA TAIFA)
1. Jakaya Kikwete
2. Pius Msekwa
3. Ali Mohamed Shein


(KUTOKA BARA)
3. Abdulrahman Kinana
4. Zakia Meghji
5. Dr. Abdallah Kigoda
6. Steven Wassira
7. Constancia Buhiye
8. William Lukuvi


(KUTOKA ZANZIBAR)
9. Dr. Hussein Mwinyi
10. Maua Daftari
11. Samia Suluhu Hassan
12. Shamsi Vuai Nahodha
13. Omar Yusuf Mzee
14. Prof. Makame Mbarawa
15. Mohamed Seif Khatib


(KUTOKA SEKRETARIAT)
16. Wilson Mkama
17. Capt. John Chiligati
18. Vuai Ali Vuai
19. January Makamba
20. Mwigulu Nchemba
21. Asha Abdallah Juma
22. Nape Nnauye
 
Kinana kawa deputy Tz bara, Nape kapelekwa itikadi na Zakhia Meghji kaenda fedha wakati Rehema Nchimbi akienda Organisation

Bado majina haya yanaweza kubadilika kwani kikao kinaendelea. Katibu Mkuu sidhani kama watabadilisha!
 
Habari zinazoletwa na ka-nzi kutoka Dodoma baada ya kutulia na kufuatilia toka ndani kabisa zinadokeza kwa uhakika mkubwa ...

Katibu Mkuu mpya wa CCM ni W. Mukama kama ilivyoripotiwa awali
Naibu Katibu Mkuu (bara) - John Chiligati (mwanzoni ilitajwa ni Kinana)
Mambo ya Nje (kamati ya CCM) - January Makamba (akichukua nafasi ya Ben Membe)
Itikadi na Uenezi - Nape (kama ilivyoripotiwa)
Uchumi na Fedha - Mwigulu Mchemba (nadhani hii iliripotiwa kuwa ni Zakia Meghji).



... stay tuned... (I'll be updating as ka-nzi kanafanya kazi yake)..Press Conference itakuwa underway muda si mrefu... we are monitoring..
 
Sasa hizi habari toka jana zimevuja inaelekea mhshmiwa JK ana MOLES humo ndani ya CCM!
 
Nao CCM kwanini hawaweki mambo hadharani?? Au kwa kuchelewesha kutoa matokeo wanafikiria kutawasaidia kurudisha imaniya wananchi kwao??!
 
Nadhani watu wanakuwa na presha tu zisizo na sababu; as usual JF inakuwa ahead of the crowd.. nadhani baada ya habari kuvuja ilibidi wafanye mabadiliko kidogo as kutokana na reaction ya watu. Kudos!!

Hapo mi nadhani JF ndo imewatengenezea CC yao, bila aibu nao wanaitangaza! Another sign of gross leadership mismanagement
 
Thanks MM, tuko pamoja, and will continue watching this space, ... nategemea ka-inzi hatapuliziwa Expel huko ndani ya 'WHITE HOUSE'
 
Mkuu endelea kutujuza!

Hata kwenye chama ni chomoa chomeka...Makambaz!

Lol....!

 
CCM inapenda kuona matatizo makubwa kama vile ni madogo. Wakati tatizo lipo mahali pengine wao wanatibu kwingine. Mie nadhani sekretariat siyo tatizo la msingi.tatizo lipo kwa mwenyekiti mwenyewe ambaye anawabeba mafisadi na kuwanyima wanachama wa kawaida kuwa na sauti inayosikika.
 
Hilo lilikuwa swali la kipima joto la leo ITV... Kama ilivyo kawaida yao uanza kwa kuhoji wananchi mitaani kabla ya kurejea studio kutoa matokeo kamili ambayo ujumuisha na Maoni ya njia ya mtandao(SMS). Wananchi wengi wa mtaani walihojiwa wamesema hatua hiyo ya chama tawala haitarejesha imani kwa wananchi kwani watendaji wakuu wa serikali ambao ndio wamekithiri kwa ubadhilift nao walipaswa kujiuzulu.. Ghafla ITV walitisha habari na kuweka tangazo kabla ya kutupa matokeo jumla ambayo yana jumuisha SMS, na badala yake wakaleta habari za Afrika Mashariki.
 
Nadhani watu wanakuwa na presha tu zisizo na sababu; as usual JF inakuwa ahead of the crowd.. nadhani baada ya habari kuvuja ilibidi wafanye mabadiliko kidogo as kutokana na reaction ya watu. Kudos!!

wamebugi step kama wamesubstitute January kwa Nape. January hana uwezo kisiasa na amefika hapo alipo kwa mgongo wa baba yake. Ilitakiwa jina la Makamba lififie kabisa kwenye ngazi za juu za CCM.
 
Jamani wale wazee watoto (uvccm) waliokuwa bize na matamko hakuna hata mmoja aliyeambulia kitu?
 
wamebugi step kama wamesubstitute January kwa Nape. January hana uwezo kisiasa na amefika hapo alipo kwa mgongo wa baba yake. Ilitakiwa jina la Makamba lififie kabisa kwenye ngazi za juu za CCM.

Well said FA
 
Mkuu mbona sioni gamba walilovua? Au Gamba alikuwa Makamba? Mbona Makamba ametoka na kuingia? CCM hata wakivua gamba bado wanabaki na sumu tu kwani nyoka akivua gamba huwa haitoi sumu aliyonayo na CCM halikadhalika!!
 
Nilishaambiwa mwongo; nimeamua kutulia tu


Usitulie mkuu kwa kuogopa vitoto ambavyo havijui kuchanganua mambo vizuri......keep us informed

Thanks MMM kwa taarifa, JF speaks na inasikika.......
 
Mkuu mbona sioni gamba walilovua? Au Gamba alikuwa Makamba? Mbona Makamba ametoka na kuingia? CCM hata wakivua gamba bado wanabaki na sumu tu kwani nyoka akivua gamba huwa haitoi sumu aliyonayo na CCM halikadhalika!!

Mkuu umenena....

Cha kufahamu ni kwamba Kikwete ni mswahili na anajua sana kutumia misemo

Nyoka anapovua gamba habadiliki na kuwa kambale bali hubaki nyoka

Sana sana anaweza kuongeza makali kwa kuwa kijana zaidi na hivyo kuwa na kasi zaidi, nguvu zaidi na ari zaidi ya kung'ata

Nadhani CCM imejiongeza kasi ya kujitafuna yenyewe kwa yenyewe na kuivuruga Tanzania yangu
 
Back
Top Bottom