Wilson Mukama awa katibu Mkuu mpya CCM na CC Mpya

Wilson Mukama awa katibu Mkuu mpya CCM na CC Mpya

Labda mlivujiwa habari nusu nusu tu bwana. Watu walikuwa na additional info tangu jana ambazo nyie JF hamkuweka.

Na wewe humo humu JF na hao wengine nao wamo humu humu. So kama hawakuweka au haikuwekwa sidhani kama kuna mtu wa kubeba lawama. Kwani JF ni "wao" na siyo "sisi"?
 
Kinyozi hajinyoi.

Hili lilikuwa zoezi la KUMSHIKISHA ADABU MAKAMBA na limefanikiwa.

kwa kuwa mtu mwenyewe ni mtata, imebidi waume na kupuliza maana angeambiwa ajiuzulu peke yake pangechimbika.

Na katika jitihada ya kumpoza zaidi wakamwingiza MAKAMBA-TOTO.

Hii ni sawa na kutumia KARATASI ku*******mbia huwezi maliza M******v:hug:
 
Nyie watu bwana! Siku zote mmedai kwamba "mafisadi" watolewe (EL, RA na Chege). Sasa wametoka, bado tu hamridhiki? Vile vile mmedai nidhamu irudi, kwahiyo wenye makundi nao wawekwe kando (ongeza Sitta, Membe, Sumaye). Na yenyewe imefanyika. Nini zaidi? Au mnaogopa sasa kwamba hamtakuwa na sababu ya kujijenga?

Kumbe "mafisadi" ni watatu tu? Na kumbe "adhabu" yao ni kutolewa tu? Ama kweli......
 
Watanzania tuna moyo sana... alipotokea Babu na Kikombe chake macho yetu yote yalielekezwa kule. Tuliamini na bado tunaamini katika uponyajio wa ajabu kule. Imani kumbe ni kitu cha ajabu sana. Tunaweza kuamini mambo mengi hata bila sababu ya msingi ya kuamini. Wakati mwingine muda ndio kitu pekee kinachohitajika kuweza kupima imani yetu. Nilikuwa naamini hivi zamani; CCM wakifanya kitu moyo wangu unashtuka kwa matamanio kuwa labda "this is it".

Sasa hivi nimejifunza kuamini tofauti; naamini kuwa bado kanuni za mabadiliko ya kimaumbile zinafanya kazi. Lakini bado kanuni hizo bado hazijaweza kutuonesha kwa uhakika kuwa kama kweli binadamu alitoka kwa sokwe kwanini sokwe bado wapo na binadamu bado wapo? Na hazijatudokeza ni vitu gani vinahitajika kwa kinyonga kugeuzwa na kuwa kambale?
 
nilidhani labda CCM italeta mabadiliko makubwa na kuleta tija ktk ushindani wa kisiasa Tz na pia kuandaa mazingira ya 2015 lakini hakuna walichokifanya kabisaaa! Hatudanganyiki....
 
Viongozi wasio na maadili wamepewa option mbili
1) wajiwajibishe, wakichelewa
2) chama kitawawajibisha

Source : Kikwete TBC1

UPDATE:

Chiligati ameongelea viongozi wanaotajwa twajwa akasema "Kagoda, Dowans etc, hata kama chama ushahidi hauna, lakini jamii ina hisia hizo, tumewaambia wao wenyewe wapime na wachukue hatua za kuwajibika kwa kujiuzuru kwenye NEC, la pili wasipo tekeleza haya chama chenyewe kitawawajibisha, RUSHWA NI ADUI WA HAKI SITAPOKEA WALA KUTOA RUSHWA, hatuhitaji ushahidi "..jamii ikikuhukumu basi lazima ujiwajibishe !
 
nadhani hii ndiyo CCM niijuayo na kudhani jinsi inavyotakiwa kuwa.....!
 
naamini Jk si kiongozi mbaya bali ana washauri wabaya. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni yapo mambo amefanya nchini ikiwemo kuwapeleka mafisadi mahakamani ambapo marais wote walishindwa na chuo kikuu Dodoma si mchezo! Big up Jk.
Thanks.
 
This "boy" is so confused...yaani, wajiwajibishe then wasipojiwajibisha ndio chama kiwawajibishe?....

Chama hakina mfumo na utaratibu wa kuwajibisha? Hakika ushkaji kwenye kazi ni tatizo......
 
Thread litafungwa sasa hivi kumuokoa bondia mmoja ambae yuko kwenye kamba mpaka hivi sasa.

Duu, kweli watu wamechoka na koo tawala.
 
Viongozi wasio na maadili wamepewa option mbili
1) wajiwajibishe, wakichelewa
2) chama kitawawajibisha

Source : Kikwete LIVE TBC1

Wajiwajibishe au chama kitawawajibisha maana yake ndiyo nini?

Na ni kina nani hao wasio na maadili? Na ni nani huyo anayeamua kuwa fulani na fulani hawana maadili? Kikwete yeye ana maadili?
 
CCM inachofanya sasa ni kuwahadaha wananchi kwani baada ya viongozi kujiuzulu na kuanza mchakato wa kuweka uongozi mpya ila hawa viongozi wanaotajwa kuchukua uongozi je walikuwa wapi wakati chama kikienda mrama?

My take:
CCM haina jipya zaidi ya kupeana nafasi waendelee kuwanyonya watanzania.

Nawasilisha
 
- Ndio Demokrasia wengine tunawapenda so!

William @ New York City, USA.

Wewe ndiyo kweli pamoja na kumtenda tinga tinga wewe mapenzi yako pale pale du nakueshimu mzee. Kweli wewe unampenda sana na akija NYC sijui utampeleka wapi mzee!
 
JK bwana, kama katuni vile

He real remind me of my favorite cartoon, Tomie and Jerry......

Mkuu fang hebu tujuze je amewataja? Kama hajawataja basi huu ni upuuzi mwingine wa kuwekwa kwenye kumbuykumbu kutoka kwa mkuu wa nchi

Ni yale yale ya walioiba nawajua warudishe pesa kimyakimya, wauzaji wa madawa ya kulevya nawajua wajisalimishe...wapi, nani kasema na tayari imezoeleka Kikwete akisema watu wanafanya kinyume...

Ni kama matangazo ya usikojoe hapa kwenye kuta maeneo ya miji.....ni bora hata zile ambazo hazikuandikwa usikojoe hapa..........

sometimes its better angekaa kimya kuliko kujitokeza na kuongea utumbo kama huu

Lakini pia wanaposema wajipime na kujivua NEC wanamaanisha nini? kwani NEC situnaambiwa walishajiuzulu? Au alikuwa anataka kumaanisha kujivua uanachama? Thubutu, uone kama EL hajapelekea Monduli PPT-Maendeleo

Lakini jamani hakuna mwandishi wa habari hapo amuulize mbona wakati wa kampeni walisema hawana ushahidi wa kuwatia nguvuni na kuwatimua chamani, vipi leo tena wanajidai kugeukia nguvu ya umma kuwa umma ukisema hata kama hujatiwa nguvuni ujipime?Ndo leo wanajua kuna umma...au ndio kwenda na mapigo ya CDM
 
Watanzania tuna moyo sana... alipotokea Babu na Kikombe chake macho yetu yote yalielekezwa kule. Tuliamini na bado tunaamini katika uponyajio wa ajabu kule. Imani kumbe ni kitu cha ajabu sana. Tunaweza kuamini mambo mengi hata bila sababu ya msingi ya kuamini. Wakati mwingine muda ndio kitu pekee kinachohitajika kuweza kupima imani yetu. Nilikuwa naamini hivi zamani; CCM wakifanya kitu moyo wangu unashtuka kwa matamanio kuwa labda "this is it".

Sasa hivi nimejifunza kuamini tofauti; naamini kuwa bado kanuni za mabadiliko ya kimaumbile zinafanya kazi. Lakini bado kanuni hizo bado hazijaweza kutuonesha kwa uhakika kuwa kama kweli binadamu alitoka kwa sokwe kwanini sokwe bado wapo na binadamu bado wapo? Na hazijatudokeza ni vitu gani vinahitajika kwa kinyonga kugeuzwa na kuwa kambale?

- Maneno mazito sana mkuu wangu!, Hope wanaohusika watayasikia au ikibidi tutawafikishia!

William @ New York City, USA.
 
ccm haina mvutooo mizee ile ile ya mwaka arobaini na saba mpaka leooo inatutapeli tuuu ondokeni madarakani mmetutia umaskini mkubwaaaaa
 
Back
Top Bottom