William Malecela - Mbunge Mtarajiwa Afrika Mashariki

William Malecela - Mbunge Mtarajiwa Afrika Mashariki

Status
Not open for further replies.

Suzie

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2010
Posts
1,267
Reaction score
422
Nimekuwa nikisikia kuwa kuna watu wamepita kwenye mchujo wa kwanza wa CCM katika kupata mwakilishi wao kwenye Bunge letu la EA na mmoja wao ni huyu W.J. Malechela, swali langu hivi huyu mtu ni kweli anastahili japo hata kugombea? Au ni kweli ndo walewale wanaotumia kofia za wazee wao kutaka kuteka akili za vilaza wengi tuliopo Tanzania?
 
Wewe ndio tuambie kwanini unaona hafai, pengine una rekodi yake
 
Kichwa cha habari kimenileta fastaaaaaa, acha presha hizoo

Mbwembwe zako tu kwani nimesema kawa mbunge? Si nimeweka dash kumaanisha topic ni W. J. Malechela na subject ni Mbunge EA
 
Wewe ndio tuambie kwanini unaona hafai, pengine una rekodi yake

Hapana sijasema hafai nimeuliza je anastahili hata kugombea hicho kiti na kuleta huo upinzani mpaka akawashinda watu ambao wako kwenye siasa za bongo kwa muda mrefu na walikua wanashiriki kisawasawa sio kama yeye miaka mingi yuko nje ya nchi
 
jifunze skills za kuandika poor presentation@suzie

You might be right lakini kumbuka sio kila anayetakiwa kutoa mawazo ni lazima awe na skills za kufanya hiyo presentation, kama kwako ni kazi sisi wengine ni jamvi tu la kutolea mawazo yetu. Uandishi na Udereva hauhitaji kuupatia ajira maana kila mtu anaweza akiamua
 
mara nje ya nchi,mara wazaziwe,therefore@Suzie

Nafikiri ujumbe umeupata je wewe unafikiri anafaaa? Kakutuma uipotezee post nini usiogope kuwa mwepesi na jiamini critics zitakuimarisha
 
Huyu bwana ni vyema akajipanga vyema kupambana na yule mbwatukaji kule Mtera. Afrika Mashariki si stahili yake!

Kwanini si stahili EA ikawa ni stahili Mtera. What so spesho alichonacho kwa matatizo ya mtera
 
Nafikiri ili wengine tuchangie kwa haki tunaomba CV yake hapa jamvini na kama ilishawekwa tuelekezwe hiyo link ili tuchangie with evidence
 
Kwanini si stahili EA ikawa ni stahili Mtera. What so spesho alichonacho kwa matatizo ya mtera

Kwenda kumtoa yule mvuta bange DEADSTONE LUSHINDWE kwani kachemka mbaya. Anastahili coz Dodoma huko ni Magamba wametawala then wote ni wagogo so mchuano utakuwa poa!
 
CV yake ni kwamba alikuwa baharia ameishi nje ya nchi kwa miaka kama 30 hivi na amerudi nchini rasmi kama mwezi mmoja uliopita.
 
W.J. Malechela ni zero..
Ndo wale wale na vitambi vyao kwa vile tu
wamekaa njee ya nchi basi wanajiona wao ndo wao funny enough watapewa kiti cha mbele ..
baadaye wanajitundikia PHD fake na kujiita DR W.J Malechele . Ushauri wangu wa kwanza punguza kitambi bado u mdogo utajiletea matatizo ya kiafya.
 
Suzie umeuliza swali technical. Maoni yangu naona swala kwamba anafaa au hafai litajibiwa na wapiga kura wake mjengoni. Ila ni vema tukubali kuwa Huyu bwana anatumia haki yake ya kikatiba kama mtanzania yeyote kugombea ubunge wa Afrika mashariki. Na kama anatumia kofia ya mzee wake, sidhani kama hilo ni tatizo. Naturally, hauwezi kutenganisha jina la baba yake na mgombea. Kwamba Masanja ni mtoto wa mkulima, William baba yake ni kiongozi mkubwa....well..its an accident of nature...beyond our making....In fact mi nadhani hapa tuhoji sera na uwezo wake. Tumuulize anataka kutufanyia nini akiwa bunge la EAC. Atupe manifesto yake.

Swali kwamba ni mtoto wa kigogo wa W/M mstaafu wala lisikutishe..maana si umeona kijana mdogo wa miaka 26 Nassari alivyowagaragaza kwa hoja 'top brass' wa taifa hili akina Mkapa, Lowassa etc? So hilo siyo shida kabisa. Tanzania ya leo inabadilika na sidhani kama huyu bwana anagombea kwa sababu ilmradi tuu. If thats the case...then he is wrong. Ila nadhani at some point hili bunge la Afrika mashariki tutahitaji kulibadirisha..hakuna democrasia ya kuchaguliwa viongozi.....

I personally, huyu mkuu mimi namheshimu. Tumekuwa naye jamvini humu na namuelewa nini mtizamo wake kuhusu taifa. Sana sana namuuliza..ni kitu gani anataka kutufanyia akiingia mjengoni Arusha?? Anadhani tatizo kubwa linaloikabili Tanzania kule EAC ni lipi na anategemea kulitatua/kuyatatua vipi?
 
mara nje ya nchi,mara wazaziwe,therefore@Suzie

Usiogope kaka ni kwamba watu wamechoka mara Malima, Mwinyi, Mnauye, Makamba, Malechela, Sioi na sasa kuna Bilali. Hatukatai kugombea bali je mnakidhi vigezo? Wacha wakuchambue wajiridhishe wenyewe na wakusahau usitumie nguvu kupinga ndo vikwazo kaka ulifikiri mteremko
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom