Se Busca
Member
- Dec 11, 2023
- 88
- 306
Mtu Aliyetawala Biashara ya Dawa za Kulevya...
Alilelewa huko Mombasa na wazazi wa kiPakistani, akianza kama mjasiriamali halali, akiendesha kampuni ya usafirishaji Akasha Transporters, ikiingiza mizigo ndani na nje ya Kenya kupitia bandari ya Mombasa.
Je, umewahi kufikiria jinsi Bandari ya Mombasa ilivyokua kuwa kitovu muhimu cha ulimwengu kwa biashara ya dawa za kulevya, ikifanya kazi kama hatua muhimu ya kusafirisha mihadarati kutoka Mashariki ya Kati hadi masoko ya Ulaya?
Ikiwa wewe ni mpenda hip-hop, unaweza kuwa umewahi kukutana na mstari huu kutoka kwa Octopizzo,"I spit fire and let it burn like Usher, A corrupt game, I chase cash like the Akasha..." ikiwa na tafsiri ya
"Natapika moto na kuacha uendelee kuwaka kama Usher, Mchezo ushaharibika, nitafuta pesa kama Akasha..."
Akasha ambayo Octopizzo amemtaja si mwingine ila Ibrahim Abdalla Akasha, mfanyabiashara mashuhuri ambaye alikuwa muhimu katika kugeuza bandari ya Mombasa kuwa lango la kufanya biashara na watawala wa dawa za kulevya kutoka Mashariki ya Kati.
Tamaa ya utajiri wa haraka ilimzidi na kumvuta Akasha katika biashara haramu ya dawa za kulevya aina ya heroini na hashish kutoka Pakistan, zilizokua zinasafirishwa kwenda Ulaya hasa Yugoslavia na Uholanzi. Kutokana na sheria kali za mihadarati ilibidi dawa hizi za kulevya zisafiri kutoka pakistan zifike Kenya ndio zisafirishwe kwenda mataifa ya Ulaya. Dili hili la kutengeneza ruti mpya ya madawa kupitia Kenya lilimpata Akasha kama mtoa huduma wa kuaminika wa usafirishaji wa mizigo hii kutoka na kwamba alikua tayari anamiundombinu na connection za kufanya mizigo hii ipite bila kupingwa. Njia hii ya kupitia Kenya ilijulikana kama Njia ya Kusini.
Ruti hii ilimpatia Akasha jina la "Don" wa Afrika Masharik ingawa alikua mtu kati tu. Mtu yoyote aliyekua akitaka kupitisha cargo yake haramu kupitia bandari ya Mombasa mtu wa kufanikisha akawa ni Akasha na angehakikisha inafanyika kwa urahisi.
Akasha alikua akifanikiwa kufanya haya yote kwa sababu hapo awali aliwahi kuwa mkurugenzi wa KENATCO, kampuni ya uchukuzi iliyokua inamilikiwa na serikali ambayo ilikua ikisafirisha mafuta hadi Zambia na kurudi na shaba hadi Mombasa kwa ajili ya kuuza nje. Kabla ya KENATCO kufungwa mwaka 1983, Akasha alikuwa amejua njia muhimu za kutumia kwenye madili yake na wakati wa kuzitumia.
Njia hizi zilimwinua Akasha hadi hadhi ya VIP kati ya wafanyabiashara wa dawa za kulevya wa nchi za Kusini mwa jangwa la sahara na haya yalitokea kimya kimya bila serikali wala vyombo vya habari kujua kuhusu shughuli zake.
Biashara za Akasha ziliingia kwenye target za serikali baada ya mtoto wa Akasha, Nurdin Akasha, kukamatwa na kufungwa nchini Tanzania, mwaka 1997 akiwa na dawa za kulevya aina ya Mandrax yenye thamani ya $8,994,000 zilizofichwa katika malori ya Akasha Transport Ltd, ambazo zilikuwa zikisafirishwa kuelekea Zambia. Nurdin alijaribu kuhonga polisi wa Tanzania kiasi kinachokadiriwa kua Ksh 910,000 (kama Tsh 5,230,000 kwa wakati huo ambayo ni kama 22,000,000 kwa sasa), lakini maafisa wa polisi wa Tanzania waligoma kuchukua rushwa hiyo.
Mwaka mmoja baadae mwanae mwingine Yusuph Abdalla alikamatwa akiwa na kontena la mandrax na akidanganya kua kabeba mirija ya kunywea vinyaji na mataulo
Huu ukawa mwanzo wa matatizo kwa Akasha, kwan baada ya hapa alifunguliwa kesi na licha ya kwamba alikua na mawakili wazoefu na wagharama alishindwa dhidi ya wakali mdogo na asiye na uzoefu kama mawakili wake.
Akikabiliwa na changamoto hizi,liamua kutafuta namna ya kujilinda na Alitambua kwamba "kila mtu ana bei," na alikuwa tayari kuilipa.
Kutokana na rushwa iliyokikithiri nchini Kenya, kupata ulinzi ilikuwa kwa mtu mwenye nafasi kama Akasha ilikua rahisi.
Alianza kwa kuhonga wakuu wa Polisi katika Mkoa wa Pwani, majaji na mawakili wa mahakama kuu mpaka mwanasheria mkuu wa serikali nae alihongwa.
Aliwahonga viongozi hawa kwa kuwajengea nyumba kuwalipia watoto wao ada na kuwapa pesa taslimu. Lengo lilikua kuhakikisha malori yake hayakaguliwi wakati yakisafirisha mihadarati. Alienda mbali sana hadi kuwaajiri maafisa wa polisi ili wasindikize malori yake.
Licha ya ulinzi huu aliopata kwa kuhonga sana lakini biashara za Akasha zilkua zinaangaliwa. Akikabiliwa na kesi nyingi na alikua akifatiliwa na wapelelezi na waandishi wa habari ambao hakua akiwalipa. Mbali na kua alikua akifatilia lakini hata washirika wake wa kibiashara walikua wakimletea shida wakiona nguvu yake kupungua.
Mwaka 1999 mmoja ya washirika wake wa biashara ya madawa, Drug lord Sam Klepper kutoka Hells Angels, Amsterdam Uholanzi, alikataa kulipa baada ya kupokea mzigo wa madawa kutoka kwa Akasha, hii ilimkasirisha sana Akasha.
Mwaka 2000, Akasha kupitia watu wake anaowalipa alipata taarifa kua kunahati ya kukamatwa kwake imetolewa kwa polisi wa Kenya. Aliamua kutoroka na mkewe hadi Amsterdam kwa kutumia pasipoti bandia. Ingawaje Mbali na kukimbia polisi alienda Amsterdam kufatilia malipo yake kwa Klepper pamoja na kutibiwa.
Wakati yupo huko polisi wa Kenya walifanya uvamizi katika nyumba yake na waligundua hashish yenye thamani ya shilingi milioni 940 za Kenya. Walichukua magari ya kifahari kumi, kilo 60 za dhahabu, na boti ya kifahari kutoka nyumba yake ya huko Mombasa.
Baada ya uvamizi huu, walitoa hati za kukamatwa kwa Akasha huko Amsterdam na kwa mtoto wake, ambaye alikimbia na kiasi kibubwa cha madawa hayo kabla ya uvamizi.
Kabla ya kwenda Amsterdam Akasha alipitia Yugoslavia na kumteka jamaa aliyewaunganisha na Sam Klepper na kudai dola 2.5million kama malipo ya mzigo aliotuma ili amwachie huyu mateka wake. Lakini Baada ya kupokea mzigo kutoka kwa Akasha, Klepper alimpa Munir Barsoum. Huyu Munir alikua drug lord mwingine jijini Amsterdam. Hivyo Akasha alitakiwa kulipwa na Munir na sio Klepper. Kaka yake Munir, Magdi aliomba wakutane ili wasolve hii ishu. Walipanga wakutane kwenye moja ya mgahawa wa Magdi. Magdi akiwa kama mpatanishi kati ya Akasha na Munir.
Akiwa anaenda kwenye kikao hiki cha usuluhishi alipigwa risasi na muuaji aliekua akiendesha pikipiki. Muuaji huyu ambae inasemekana alitumewa na Munir hajawahi kutambulika mpaka leo.
Biashara za Akasha zikabaki mikononi mwa wanae Baktash na Ibrahim Akasha Abdalla. Hawa waliipanua biashara kua kubwa zaidi ya baba yao wakati baba yao alikua akideal zaidi na Hashish wao waliuza karibu kila aina ya dawa za kulevya ikiwapo heroin, methamphetamine (meth) na dawa zingine waliipanua pia biashara kimipaka wakati baba yao alideal na Ulaya peke yake wao walikua wakiuza mpaka marrkani n nchi zingine .
Mbali na kuikuza biashara hawa walikua mafia kweli kweli kwani walikua wakiua, kuteka na uhalifu wa kutumia silaha.
Mwaka 2014 Baktash na Ibrahim walikamatwa na baadae kusafirishwa kupelekwa Marekani (Extradited) kusomewa mashtaka yao. Mwaka 2019 walipatikana na hatia na hukumu zao zilisomwa na Baktash alihukumiwa miaka 25 gerezani na Ibrahim akihukumiwa kifungo miaka 23.
Story ya Akasha na familia yake imekuwa ni moja ya stories za kusisimua kuhusu uhalifu na namna magenge ya dawa za kulevya yanavyoweza kuwa ngumu kuyaondoa. Nguvu wanayokuwa nayo na sapoti wanayopata kutokana na rushwa sio rahisi kuondolewa.
Unadhani kwa sasa Tanzania tuna “Akasha” wetu anaesababisha kuongezeka kwa mateja mtaani?