William J. Malecela kugombea ubunge wa EAC

- Bob Siamini kwamba tumepotea na EAC, ninaamini kwamba tupo sawa ila marekebisho tu yanatakiwa na ni lazima tupelekea Strong MPs huko, wanaoweza kusimamia interest ya Taifa letu, badala ya siasa zaidi. Nina tatizo na Sarafu Moja na Free Movemment ya wananchi wa Members States kwenye hayo mawili ninasema we need to be very carefull ama sivyo tutaumia sana na pia la Ajira kwa maoni yangu halijakaa sawa linahitaji marekebisha, lakini yote yanajadilika!

FMeS!
Hakika hatujapotea ikiwa tulichoanya ni kuunda nguvu ya nchi tano kuwa na msimamo mmoja ktk maswala ya kimataifa iwe hata kuunda msimamo mmoja ktk biashara na mali zetu ktk soko huria, lakini I doubt kama tunaweza kuwa na uwezo huo maana viongozi wetu wenyewe wana fungamana wanapoona kuna maslahi yao.. Na kama tunafanya jumuiya hii ikiwa ni hatua ya Pan Africanism waliyotaka kina Nkurumah na Nyerere - safi kabisa! lakini sii kufikiria kuboresha Uchumi wa nchi yetu hili tumeliwa sisi -hatuwezi kufaidika na hilo..

Mfumo wetu wa kodi ndani ni mbovu sana inahitaji marekebisho makubwa, Policies zetu ktk uwekezaji wa viwanda mbovu au wananchi wenyewe wanapenda biashara za kuzungusha fedha haraka (money laundry) ambayo imehalalishwa Bongo na ndio maana hatuna viwanda, less than 2% wana account bank, wanalipa kodi au wana TIN number tofauti na Kenya ambao mfumo wao umejengwa kibiashara zaidi na wapo tayari kuingia jumuiya hii kwa faida yao..Kwao it's all blessing lakini sisi hatuna zaidi ya Ujirani mwema.
 
Heshima FMES,

Mkuu ulikuwa wapi siku nyingi sijasikia nondo zako za uhakika.Back to topic ni kweli suala la EAC linatakiwa kutazamwa kwa umakini mkubwa sana kuanzia uwakilishi namuundo wake.Mkataba wa EAC itifaki zote zinazojadiliwa na zilizopitishwa hazifahamiki kwa wananchi wengi actually sehemu kubwa ya mikataba inafahamika kwa viongozi na wananchi wachache sana.

Ukiangalia EU baadhi ya mikataba haioperate kwa baadhi ya nchi mfano UK bado wanatumia sarafu yao ingawa ni mwananchama kamili wa EU.Kwa mfano huo Tanzania inaweza pia kujiondoa katika kipengele cha ajira,ardhi,usalama,fedha na nk.Hili litawezekana kama tutakuwa na wawakilishi imara na makini katika kutetea na kujenga hoja.

Nakubaliana na wewe lakini nina walakini na LE MUTUZ🙁Nothing personal here IDs and anything else set aside)

Mosi: Hajawa nasi kimaisha ya kila siku kwa kitambo kidogo na anaweza kuwa na mtazamo usio sawa na uhalisia

Pili: Hicho chama anachogombelea

Tatu: Yeye akama yeye anajiamimni kupita kiasi nza sidhani kama ameshawahi kujifanyia personal SWOT analysis kama ipo

Nne: Ni dhamira yake. Je anagombea ikiwa ni kuatfuta palatform ya kupata jimbo baadae kama alivyofanya Masaburi? Au ni kweli anadhamira na shida zetu EAC?

Tano: Kuwa katika kundi la watoto wa yester-politicians wa CCM
 
Mkuu FmEs,sio kila mwana jf anaweza kuwa kiongozi bora wa taifa letu.Jf iendelee kuwa sehemu ya kuwakomaza na kuwachallenge wale wanaotaka kuwa viongozi.Nakubaliana nawewe kuwa personalities ziwekwe kando na watu wakate hoja.Ila sikubaliani na mtazamo kwamba akitokea mwanajf kutaka nafasi ya uongozi basi apewe 'go ahead' na wanajf wote eti kwakuwa tu ni mwanajf!Hapa jf itakuwa haitimizi wajibu wake kwa taifa hili.

Back to topic mkuu FmES nakubali hoja zako za EAC as far as Tanzania is concerned.Natamani kama Willy ajifunze vitu flani hivi kutoka kwa Fmes kama kweli anataka kuwa kiongozi.
 
Japo kuna watu wana lalamika kuwa William Malecela anaonewa na wale wanaosema asigombee bado sija sikia sababu muhimu za kwa nini he is the man for the job.
 
Mkuu wangu huyu awe ndio MUTUZ au sio nadhani sio hoja bali nachoweza kushukuru ni kwamba mmoja wa wana JF anagombea nafasi kubwa ktk Ubalozi wa nchi yetu na sisi kama wanajanvi inatakiwa kumjaza mavitu na mitazamo tofauti. Yeye atakuwa na silaha ya kuweza kwenda vitani akiwa na tahadhali hizi. Maadam maji ya EAC tumeshayavulia nguo nina hakika Willy is a good candidate bila kujali chama. Ila tumwelezee pale tunapoona hatukubaliani na viongozi wetu kimtazamo, hivyo ataweza chukua yako, yangu, ya Field Marshal na kadhalika.
 
I will be MORE THAN happy akija live na kutuambia nia yake......insofar tunaambiwa ni nyepesi nyepesi......watu tutaumiza vichwa only yeye aje kukanusha hajasema anagombea......au akagombea halafu 2015 huyoooo Mtera
 
Nakubaliana na wewe lakini nina walakini na LE MUTUZ🙁Nothing personal here IDs and anything else set aside)

Mosi: Hajawa nasi kimaisha ya kila siku kwa kitambo kidogo na anaweza kuwa na mtazamo usio sawa na uhalisia

Wewe unamjua Willie na awe na wewe kimaisha kivipi?..hajawa NASI?..wewe na nani?

Pili: Hicho chama anachogombelea

Sasa hapa hueleweki kabisa, una tatizo na mtu au chama, na je unajua ni Chama gani, mkuu hapa maslahi ya taifa kwanza, vyama ni vitu vidogo sana kwenya issues zenye maslahi ya Taifa

Tatu: Yeye akama yeye anajiamimni kupita kiasi nza sidhani kama ameshawahi kujifanyia personal SWOT analysis kama ipo

Kujiamini ni kitu positive sana kwa mwanadamu kamili, kama wewe unadhani tunataka viongozi laini laini wasiojiamini, then uko jukwaa tofauti

Nne: Ni dhamira yake. Je anagombea ikiwa ni kuatfuta palatform ya kupata jimbo baadae kama alivyofanya Masaburi? Au ni kweli anadhamira na shida zetu EAC?

Ni haki yake kama mtanzania kikatiba, na wewe kagombee

Tano: Kuwa katika kundi la watoto wa yester-politicians wa CCM

Hoja za hovyo hovyo huwa hazijibiwi hapa, kama vipi kaanzishe thread ya yester-politician tutakuja kukutana huko
 
- Safari Safari, kama majina ndio kipimo cha uwezo wa binadam kufikiri basi JF tusingekwua tulipo kwenye chati ya juu kwenye Taifa, maana siamini kwamba majina mengi humu yana maana, lakini muhimu ni hoja kwanza sio jina!

- Na by the way vipi umeshapita ofisi za bongo ukaona Wa-Kenya walivyojaaa? Je unaamini na kule Kenya tukienda tutakuta Wabongo wamejaa kwenye maofisi yao?

Respect!

FMES!

...haya mambo yanishangaza sana, kama Wakenya wameamka na kuweza kuja kutafuta fursa ndani ya Tanzania ilhali Watanzania hawana haja ya kutafuta fursa Kenya, then tatizo sio la Wakenya bali ni la Watanzania..

..kwenye ardhi temporarily tupo pamoja, lakini hiyo sio solution ya kudumu, as long as waTanzania hawajaweza kuujenga uchumi endelevu kupitia ardhi,na kama tukiwa wakweli na nafsi yetu, tulikubali hilo, na atleast kwa wakati huu tujiandae na tuwaandae watu wetu kwa hilo...
 
Japo kuna watu wana lalamika kuwa William Malecela anaonewa na wale wanaosema asigombee bado sija sikia sababu muhimu za kwa nini he is the man for the job.
William anapingwa na wanaomjua kuwa jamaa ni kilaza fulani hivi , wanasema ni Bomu katika uelewa na ufahamu ! hana weledi wala hadhi ya kustahili kuwa kiongozi wa umma wala wa familia yake ! wanaomjua wanasema Hafai , Hafai , na wala hafanani na uongozi wa ngazi ya taifa.

wanaomjua wanasema , William ni Muhuni mmoja hivi , anaeshinda katika madisco , tangu amerudi Dar amekua akishinda kwenye macasino, akitumbua maisha na kujisahaulisha mikasa yake ya maisha kule kwenye Maroli New York.

AMESHINDWA KUJISIMAMIA MWENYEWE KIMAISHA ATAWEZAJE KUWA KIONGOZI WA NGAZI YA TAIFA !
 
Kwa maoni yangu kila mwana JF ana haki ya kimsingi kugombea uongozi, na wakati ufike wakuitambua na kuheshimu haki hii kama kweli sisi ni greater thinkers.

That said, ningependa kuongea machache kwenye dukuduku za FMES juu ya EAC. Suala la EAC sio rahisi kama tunavyojaribu kuliangalia. Kwanza linatakiwa lifanyiwe objective analysis kwa maana kwamba researcher husitafute points za ku justify position yako au imani yako juu ya EAC. Ukiitazama EAC kwa kuanza na imani kwamba haifai kwasababu italeta wakenya Tz disproportionately na waTz watakao kwenda Kenya, labda ningekushauri ufikirie mara mbili lengo la kutaka uongozi kwa sababu faida za economic integration ni zaidi ya equal inflow and outflow of labour among country members.

Vile vile ukienda na mtazamo kama wa mzee mwenzangu, Bob Makandara (my regards and salute to him), kwamba Tz tutakuwa soko la bidhaa za Kenya na hivyo kuwa loser-maxim ningekushauri pia kufikiria mara mbili nia ya kugombea maana faida za EAC go beyond that to include such things a trade creation and deviation, cheap imports, improved comparative advantages, compesantions etc. Vile vile EAC haijaanza leo kwa hiyo unaweza kuchecki trade volumes among state members.

Angalizo ni kwamba utafiti wa kina unatakiwa ufanyike ili kujuwa madhara ya kuingia kwenye EAC. Serikali ilishafanya utafiti huu 1998 kama sikosei ukiongozwa na Francis Muthaura na utafiti ukahitimisha kwamba kuna faida ya Tz kujiunga na EAC. Ni utafiti Wa kiuchumi uliongalia mambo yote ya msingi, binafsi niliukubali.

Kwa hiyo kimsingi Tz itanufaika na EAC kwa maana kwamba Haifa USA worse off kwa kuwa ndani ya EAC. Sasa kwenye regional integration yeyote suala la equal distribution ya faida za umoja hazina tija sana kwa wachumi wa economic integration, kwani linakuwa la kisiasa zaidi bila kuwa na support ya nadharia ya uchumi.

Suala la safaru moja ni zuri tu kiuchumi lakini sio kisiasa. Nchi inapounganisha sarafu yake na nchi nyingine inapoteza muhimili mkubwa wa meno ya serikali yake. Mfano Tz itatulazimu tuwasiliane na central bank ya EAC kuomba ela zichapishwe ili tukapigane na nchi isiyo mwanachama, uwezo wetu kwa ku-raise funds for emergency expenditure over night unakuwa haupo pasipo kuishauri central bank ya EAC. Kadhalika control ya inflation na development projects unakuwa limited kwa kiasi fulani. Wana siasa na baadhi ya wachumi wanaamini meno ya serikali ya nchi ni uwezo wake wakudhibiti fedha bila kutegemea taasisi nyingine.

All in all unatakiwa ufanye uchunguzi makini ili ukatetee EAC kwa ufahamu mpana. Kujisomea juu ya faida na hasara za economic integration kutakupa uelewa mwingi. Nakutakia kila mafanikio katika maamuzi yako na namini JF watajivunia endapo utafanikiwa.
 
Mkuu FmEs,sio kila mwana jf anaweza kuwa kiongozi bora wa taifa letu.Jf iendelee kuwa sehemu ya kuwakomaza na kuwachallenge wale wanaotaka kuwa viongozi.Nakubaliana nawewe kuwa personalities ziwekwe kando na watu wakate hoja.Ila sikubaliani na mtazamo kwamba akitokea mwanajf kutaka nafasi ya uongozi basi apewe 'go ahead' na wanajf wote eti kwakuwa tu ni mwanajf!Hapa jf itakuwa haitimizi wajibu wake kwa taifa hili.

Back to topic mkuu FmES nakubali hoja zako za EAC as far as Tanzania is concerned.Natamani kama Willy ajifunze vitu flani hivi kutoka kwa Fmes kama kweli anataka kuwa kiongozi.

- Na pia si kila mwana JF hawezi kuwa Kiongozi, lakini point taken bro na heshima mbele sana!

FMeS!
 
The best he can do to utilize what he was doing in USA is to contest for Parliamentary seat? Let give him General Tyre or Kilimanjaro machine tools to prove his elite instead of member of parliament.

Huyu asifikilie sie tuliokuwa hapa bongo ni wajinga aje kutoka huko New York akafikiri kuwa yeye anajua zaidi kuliko sisi na kumtumia mama yake wa kambo kumpigia debe kuwa mbunge wa Afrika Mashariki!! Safari hii lazima tupeleke watu wasomi mahili ambao watatuletea heshima iliyopotea ya nchi yetu; tunahitaji watu wenye kisomo cha hali ya juu na sio mabahalia!! Mambo ya kutumia majina ya baba zao umepitwa na wakati , watanzania wanataka mabadiliko ya kweli na sio ulaghai!
 
Japo kuna watu wana lalamika kuwa William Malecela anaonewa na wale wanaosema asigombee bado sija sikia sababu muhimu za kwa nini he is the man for the job.

- Vipi sababu za msingi kwamba he is not the man for the job, au unaridhika na hizi za Social life yake kule Facebook? I mean naona kama tunacheza lotto hapa kwa sababu is it true kua anagombea? Na what authority we have here kuamua asigombee au agombee?

Otherwise heshima mbele sana bro!

FMes!
 
Huyu asifikilie sie tuliokuwa hapa bongo ni wajinga aje kutoka huko New York akafikiri kuwa yeye anajua zaidi kuliko sisi na kumtumia mama yake wa kambo kumpigia debe kuwa mbunge wa Afrika Mashariki!! Safari hii lazima tupeleke watu wasomi mahili ambao watatuletea heshima iliyopotea ya nchi yetu; tunahitaji watu wenye kisomo cha hali ya juu na sio mabahalia!! Mambo ya kutumia majina ya baba zao umepitwa na wakati , watanzania wanataka mabadiliko ya kweli na sio ulaghai!

- Alipokuwa Baharia, alikuwa Assistant Engineer, ambao aliusomea DMTU DSM, na baadaye akafanya Field kwenye MV. Bukoba Mwanza, na kuhamia MV. Liemba na MV. Mwongozo Kigoma kwa mwaka mmoja, ndio akaenda kusoma zaidi Antwerpen, Belgium, ambako alilifanyia kazi Shirika la Meli la CMB Belgian line!

- Baadaye akahamia New York akasoma Associate Degree ya Criminology na Police Science, na pia BA ya Political Science, amesoma Mahenge morogoro Secondary, ameshiriki JKT Oljoro mwaka mmoja wka mujibu wa Sheria, sijaona tatizo la elimu yake!

Es1

v.
 
William anapingwa na wanaomjua kuwa jamaa ni kilaza fulani hivi , wanasema ni Bomu katika uelewa na ufahamu ! hana weledi wala hadhi ya kustahili kuwa kiongozi wa umma wala wa familia yake ! wanaomjua wanasema Hafai , Hafai , na wala hafanani na uongozi wa ngazi ya taifa.

wanaomjua wanasema , William ni Muhuni mmoja hivi , anaeshinda katika madisco , tangu amerudi Dar amekua akishinda kwenye macasino, akitumbua maisha na kujisahaulisha mikasa yake ya maisha kule kwenye Maroli New York.

AMESHINDWA KUJISIMAMIA MWENYEWE KIMAISHA ATAWEZAJE KUWA KIONGOZI WA NGAZI YA TAIFA !

- Well, ni yale yale tu majitaka, William hajawahi kunywa pombe wala kuvuta sigara maishani mwake, amefanya kazi Belgium, China, na USA hatimaye ameamua kurudi nhyumbani, ni kweli anaenda kwenye mipira, anaenda kwenye miziki na pia alikuwa bungeni, hay ya macasino ndio majitaka, ya kwamba mtu aliyekwenda Ulaya na USA akajisomesha na kujenga nyumba yake hapa bongo Kinyerezi akiwa na shamba kubwa la mazao, kumsingizia hayo ni siasa za majitaka maana unahitaji kujiul;iza ni Watanzania wangapi wameweza kufanya hayo on thier own?

- Eti bosi unasema owners wa macasino au bendi za miziki ni wahuni na hawafai kuwa viongozi? ha! ha! ha! ha! unatisha bro!

- Heshima mbele bro1 na karibu sana!

FMeS!
 
...haya mambo yanishangaza sana, kama Wakenya wameamka na kuweza kuja kutafuta fursa ndani ya Tanzania ilhali Watanzania hawana haja ya kutafuta fursa Kenya, then tatizo sio la Wakenya bali ni la Watanzania..

..kwenye ardhi temporarily tupo pamoja, lakini hiyo sio solution ya kudumu, as long as waTanzania hawajaweza kuujenga uchumi endelevu kupitia ardhi,na kama tukiwa wakweli na nafsi yetu, tulikubali hilo, na atleast kwa wakati huu tujiandae na tuwaandae watu wetu kwa hilo...

- Wa-Kenya wamekuja under guidance ya mkataba wa Jumuiya, sasa swali je na sisi tumeenda Kenya under hizo guidance, na it has nothing na kuchanhamkia isipokuwa ni the guidance kama na sisi as Taifa tupo samba samba nalo!

Otherwise heshima mbele sana!

ES!
 
Kwa maoni yangu kila mwana JF ana haki ya kimsingi kugombea uongozi, na wakati ufike wakuitambua na kuheshimu haki hii kama kweli sisi ni greater thinkers.

That said, ningependa kuongea machache kwenye dukuduku za FMES juu ya EAC. Suala la EAC sio rahisi kama tunavyojaribu kuliangalia. Kwanza linatakiwa lifanyiwe objective analysis kwa maana kwamba researcher husitafute points za ku justify position yako au imani yako juu ya EAC. Ukiitazama EAC kwa kuanza na imani kwamba haifai kwasababu italeta wakenya Tz disproportionately na waTz watakao kwenda Kenya, labda ningekushauri ufikirie mara mbili lengo la kutaka uongozi kwa sababu faida za economic integration ni zaidi ya equal inflow and outflow of labour among country members.

Vile vile ukienda na mtazamo kama wa mzee mwenzangu, Bob Makandara (my regards and salute to him), kwamba Tz tutakuwa soko la bidhaa za Kenya na hivyo kuwa loser-maxim ningekushauri pia kufikiria mara mbili nia ya kugombea maana faida za EAC go beyond that to include such things a trade creation and deviation, cheap imports, improved comparative advantages, compesantions etc. Vile vile EAC haijaanza leo kwa hiyo unaweza kuchecki trade volumes among state members.

Angalizo ni kwamba utafiti wa kina unatakiwa ufanyike ili kujuwa madhara ya kuingia kwenye EAC. Serikali ilishafanya utafiti huu 1998 kama sikosei ukiongozwa na Francis Muthaura na utafiti ukahitimisha kwamba kuna faida ya Tz kujiunga na EAC. Ni utafiti Wa kiuchumi uliongalia mambo yote ya msingi, binafsi niliukubali.

Kwa hiyo kimsingi Tz itanufaika na EAC kwa maana kwamba Haifa USA worse off kwa kuwa ndani ya EAC. Sasa kwenye regional integration yeyote suala la equal distribution ya faida za umoja hazina tija sana kwa wachumi wa economic integration, kwani linakuwa la kisiasa zaidi bila kuwa na support ya nadharia ya uchumi.

Suala la safaru moja ni zuri tu kiuchumi lakini sio kisiasa. Nchi inapounganisha sarafu yake na nchi nyingine inapoteza muhimili mkubwa wa meno ya serikali yake. Mfano Tz itatulazimu tuwasiliane na central bank ya EAC kuomba ela zichapishwe ili tukapigane na nchi isiyo mwanachama, uwezo wetu kwa ku-raise funds for emergency expenditure over night unakuwa haupo pasipo kuishauri central bank ya EAC. Kadhalika control ya inflation na development projects unakuwa limited kwa kiasi fulani. Wana siasa na baadhi ya wachumi wanaamini meno ya serikali ya nchi ni uwezo wake wakudhibiti fedha bila kutegemea taasisi nyingine.

All in all unatakiwa ufanye uchunguzi makini ili ukatetee EAC kwa ufahamu mpana. Kujisomea juu ya faida na hasara za economic integration kutakupa uelewa mwingi. Nakutakia kila mafanikio katika maamuzi yako na namini JF watajivunia endapo utafanikiwa.

- Sawa sawa Bro, we are raising our fears na ni kutokana na Jumuiya ya kwanza kushindwa na sisi as a nation tukapata hasara sana sasa next time arround tunatakwia kuwa waangalifu, lakini katika hoja zangu I am not guided with fear hapana, nimesema tunahitaji kuwa waaanngalifu na kuuliza maswali serious kabla ya kuingia an anything!

Heshima mbele lakini!

ES!
 
Rev Fr Masanilo leo amenisaidia kujuwa kwamba Pasco ndiye yeye huyohuyo Pascal Mayala, twende taratibu tu na hapa kuna mtu atajisahau tu na atajitaja jina lake bila kukusudia.
 
- Majina ya members sio muhimu sana, muhimu ni hoja muhimu kwa taifa na wananchi!

heshima mbele sana bro!

Es!

Es

lakini
 
Mkuu FMES salute sana

Personally sina tatizo na Mkuu Willie @NYC..

Hawa watu tumekuwa nao sana hapa JF,tumekuwa tunapiga kelele kuwa wana JF hawajitokezi kugombea ili tuone kama wanaweza kuonesha utofauti..

Yes its time..Bado Mzee Mwanakijiji tu...

I am done.
 
Back
Top Bottom