Wife wangu ananiibia, ushauri unahitajika

Mambo ya ndoa nayo sometimes ni pasua kichwa
miss chaga, hebu ueleze why wadada wa huko migombani wanakumbwa na kashfa kama hizi, mbona kesi za wanawake wa migombani zimekuwa nyingi sana
 
Last edited by a moderator:

hapo kwenye red kaka hapana, uchukulie kama mzigo wako we ndo umewaleta apa duniani? ulivyoooa uliambiwa utakua na zigo kama hilo? tena wengine wamezalishwa uko na wanaume wengine c wakawatafute hao waliowazalisha? kuongea nae sawa mkatafuta suluhu lakini si kuchukulia kwamba ni zigo lako, hawana ndugu zao wengine kwan mkeo kwao amezaliwa peke yake au ndo kutegemea slope tu kwa sababu jamaa alianza kujilegeza mwazoni?

dawa ni hii,
kaa chini mueleze iyo tabia ikome na hao watu wajitegemee, acha kununua vitu in bulky kila cku jion unarud na vitu vya kupika kesho tu mtaenda sawa amani mwenyewe ataitafuta!!!
 

Mangi asante...
1- Familia zetu zimekuwa vema for so long, alifariki babake,,, then babangu..... but kiukweli nimekuwa mchango mkubwa sana kwao,,, kuna kipindi nlitengwa kwetu coz niliangalia sana ukweni.
2- Baada ya kuwaondoa kulianza vijineno,, sikuvikiliza sbb i have my rite to control my teritorry...walikuwa 3,,,, wa 1 nilimfungulia duka,,,, mauzo yakanunua mimba,,,,,akatoroka mwenyewe,,, the remaing 2,,,nimewasomesha from form 1 to 6, mmoja alienda chuo kabisa....
3- Sikuwahi kuishi na ndugu kabisa, zaidi ya baba yangu,,, ambaye by now kapumzika mbele ya haki.
4- Nimemzidi kielimu
5- hakika nimemzidi, coz nimeweza kumiliki a lots of things, kutunza nyumba yangu, mashamba na nina miradi kiasi cha kuniweka salama kimapato na akiba pia.....yeye nna hakika ana akiba kubwa sana kama anaweka bank, nilimfungulia akaunti,,, akawa anasomba zote,,, hata akaunti ya pamoja ambayo tulikubaliana kuweka for kids,,, hakuweka kabisa tukiifunga kwa ugomvi usio kifani...
6- tumetoka kwenye familia za kawaida sana - standard life.....labda niseme hapa.. babake alikuwa na 2 wife,,, so alikuwa na watoto 14....
7- kwao yy ndo kinara wa mafanikio,,, akipitia mgongo wangu...kwetu wote tuko poa and am the lastborn...

karibu kwa ushauri
 
kwanza pole sana huyo mkeo yupo hapo kwa maslahi binafsi hakupendi hata hawezi kuiba vitu vya ndani na kuwapa wadogo zake. kama kweli anawapenda angekuwa anatoa mshahara wake awape. sasa cha kufanya usiende mahakamani akirudi ita ndugu zake na zako hafu mpe likizo ya muda aende kwao mpaka atakapojirekebisha tena uwe mkali balaaa usitake majadiliano na mwambie atakaporudi awe yeye anatoa hela ya chakula au mtoe nusu kwa nusu. hiyo likizo fanya hata iwe ya miezi kadhaa
 
Acha akili za utegemezi mtoto wa kiume,...angalia ucje...
 
Sina hakika mara baada ya hili tukio kama huyu mama wa Kimarangu atarudi tena hapo home? Hakika sina HAKIKA!
 
Mimi siyo mchaga,ila wanawake wengi wa kitanzania wako ivyo,..ndio maana ikitokea umefulia mwanamke anakukimbia,..kama huamini angalia coment nyingi za watoto wa kike zinazohusu pesa humu JF!
 
Mkuu kabla sijasema neno naomba unijubu maswali haya
(1)Wakwe zako wapo hai?wako wapi na wanashughulika na nini?
(2)Mkeo ni wangapi kuzaliwa kwao?
(3)Ukiangalia uwezo wa kiuchumi mkeo kwao anaweza kuwa namba ngapi
(4)Mkeo kwao wanamtegemea kwa namna gani kuitegemeza familiya yao?
(5)Chanzo cha kuwatimua kwao ni kipi? je walikua na tabia mbaya au ni familiya kuwa kubwa?
(6)Shemejio mjini wanafanya nini?
(7)Unao wadogo zako?
(8)nduguzo wanaweza kuishi kwako?
(9)Nini chanzo cha kufanya shoping ya vitu vya jikoni?
 

Mkuu shemejio wanafanya nini hapo mjini?.Mamamkwe anafanya shughuli gani?
Tofauti na mkeo kuna shemeji yako wa tumbo moja na mkeo mwenye kauwezo?
Wazazi wako wako hai?
Wanafanya nini?
Una wadogo zako ambao hawajitegemea bado?
Kaka zako na dada zako kiuchumi wakoje?
kuna ndugu yako akiyewahi kuishi kwako?
UKIJIBU HAY VEMA NITAWRZA KUTOA COMMENT YA USHAURI MKUU
 

Mimi siyo mchaga,ila wanawake wengi wa kitanzania wako ivyo,..ndio maana ikitokea umefulia mwanamke anakukimbia,..kama huamini angalia coment nyingi za watoto wa kike zinazohusu pesa humu JF!

Pole sana
 
Achana na kesi; italeta athari za muda mrefu baina ya familia zenu; cha kufanya ni mazungumzo juu ya meza; hebu jaribu hatua hizi moja baada ya nyingine; na kila baada ya hatua moja fanya tathmini ya kina; kama bado ugonjwa upo sogea hatua ifuatayo:
Step 1: Mshirikishe mshenga; myazungumze bayana wote pamoja na mkeo akiwapo;
Step 2: Washirikishe viongozi wa kiroho
Step 3: Ni mguu kwa mguu hadi kwa wazazi wa pande zote; nyote wawili
Step 4: Kama hajajirekebisha ina maana anawadharau hata wazazi wenu; ni mgonjwa hana daktari; ni kunguru hafugiki; atafikia kiasi cha kutaka kukudhuru wewe mwenyewe au watoto wenu; anza maandalizi ya kutenganishwa kwa muda; say 2 years uone kama ana dalili za kujirekebisha au talaka moja kwa moja.

Kila la kheri na pole sana, Ndoa ni taasisi ngumu sana; kwani waliomo wanataka kutoka wakati wlioko nje wanataka kuingia!!
 

Pole ndugu yangu. Naona kwa kiasi kikubwa tuna matatizo yanayofanana. Naamini ushauri unaopewa utanisaidia hata mimi. MUNGU atuepushie majaribu haya.
 

Kaka nilichoona hapa ambacho pia mimi binafsi nimepitia ni kuwa. Huyu mama, hana tatizo, the problem ni kuwa kwao hali si nzuri , kwa ukubwa huo wa familia naamini pia ndugu zake hawakwenda shule sana, hivyo kujitegemea imekuwa ni issue.Sasa dada wanamuona ndio kila kitu, kitendo cha wewe kuwatimua kwako ndio kimeleta hili tatizo la sasa.

Kikubwa cha kufanya hapa, kama bado unampenda mkeo na yeye anakupenda, kaaeni chini mueleze tatizo liko wapi na kuwa sasa yeye ana familia yake, na hao ndugu wamekuwa wakubwa na mlisha wasaidia vya kutosha.

Aina ya msaada anayowapa kamwe haiwezi kuwa suluhisho. Fanya hivi waite hao ndugu waulize kila mtu anataka kufanya nini na kuwa hiyo ndio chance ya mwisho wewe kusaidia. Wakupe idea zao, toa msaada wako wa mwisho unaoweza na waambie wasikusumbue tena, na dada yao alielewe hilo na muwe pamoja kwenye hilo. Kama mkukubaliana hilo mtamaliza hili tatizo.
 
tuwapige vita kwa mikono na miguu jamaa kagharamia miaka 10 na bado anaendelea kuiba
bado aliwagombanisha na ndugu zake au limbwata

Mmezidi lol! Kutwa kucha kunanga wanawake wasomi, kwani miongoni mwao si ndo wapo dada zako! Utawapiga vita hao wasomi hadi lini/wapi? Kwa kizazi cha sasa wazazi wengi wameamka kielimu wanapeleka watoto wao shule na elimu inapatikana hivyo tegemea kizazi cha wanawake waliomaliza vyuo kutokwisha.

Na hao waloishia form IV tena wengi shule za kata ni majanga zaidi kwa hali iliyopo huko shule za kata, vicheche mno! Hata umpeleke binti wa vipi huko wanaharibika kitabia. Wasichana wanaoishia drs la 7 wachache mno siku hizi, maana hata wasiojua kusoma na kuandika wapo sekondari.

Hamna kwa kukwepea, mtaoa haohao mnaowabeza kila uchwao. Usipo oa wewe basi kaka ako ataoa. Wacheni kulalama tafuteni jinsi ya kuishi nao vema. Watu wanakimbiwa na wachumba kisa perceptions mnazowajengea kila siku. Kha! Ingawa mi form IV lakini mmezidi jamani.
 
Hapo sasa...anapoteza sifa zote za kuwa mwanamke shemeji ujue?
ni shida shemeji! yaani ni tatizo! kila nikitafakari najikuta vinakuja vya kirumi! nahotaji google translation asap shemeji Kaizer! ni shida ujue ........
 
Last edited by a moderator:
mkuu yote haya nimeshatolea maelezo ukifuatilia hii thread yote utayaona....asante na karibu
 

Safi sana. Wewe ni wa kupigiwa mfano na mpo wachache sana wa aina yako wlio wengi ni kama huyo anayelalamikiwa na huyo ndugu yetu.
 

8 na 9 ndo sijatolea ufafanuzi..

8-Kama ntakosea nisahihishe,,,,,aliyeishi kwa ni only baba yangu wakati akimalizia siku zake alizopewa na Muumba...only
hata wakati namuuguza baba wanakuja wanashinda na jioni wanasepa,,, labda on wkend waje walale till sunday.
9-labda nimeiga kutoka kwa baba yangu na ikawa ni tabia....but kuna wakati nilikuwa nikiacha pesa ya mwezi ,,, inaisha tarehe 10, nikiuliza huo ugomvi hautamaniki,,,,, so nikaona isiwe shida.... naenda mwenyewe na sioni shida kabisa,,, nina ratiba yangu iko sawa ........
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…