Wife wangu ananiibia, ushauri unahitajika

nosspass

JF-Expert Member
Mar 7, 2013
5,798
4,752
Wandugu

Hili janga ni kubwa sana kwangu, nimekuwa na kawaida ya kununua mahitaji yote ya nyumbani kama baba na kiongozi wa familia kuna kipindi kulitokea mtafaruku kisa kikiwa shemeji zangu wamejaa kwangu, nikatangaza la mgambo sitaki cha shemeji wa wala wifi kwangu......wote wakatawanyika.

Bi mkubwa ilimuuma sana hakuwa na jinsi, kwani kama ni msaada niliwapa ikiwa ni kusoma na mambo mengine ya kuwasaidia, but aliwadekeza bila kujali kuwa niliyemuoa ni yeye pekee wamekaa kwangu kwa muda mrefu tuu.

Kwa hasira akawapangishia chumba, hata sijui ni wapi.

Bi mkubwa ana kazi yake nzuri tuu, but hachangiii chochote ndani ya nyumba, na wala kwangu sio tatizo kabisa, namshukuru Mola wanetu 2 wana afya njema sana na wana furaha.

Tatizo linalonisukuma kutaka ushauri hapa ni hii tabia aliyoanzisha bi mkubwa, anabeba vyakula ndani mwetu anapeleka kwa wadogo zake, niligundua kipindi fulani nikamkanya, akataharuki kwanza nimejuaje, akahamishia ugomvi kwa dada na kaka (wasaidizi wetu pale home), mpaka kaka aka resign.

Safari ikaendelea hakuacha hiyo tabia, tena imeota mizizi. Kila j3 hua anakuja na mdogo wake mmoja, anamfungashia furushi la mchele, sukari, mafuta ya kula, matunda na kila aina ya kitu apendacho.

Nikaweka mtego, kijana wangu mmoja ndo jasusi langu pale home, nimelifundisha likakomaa, kama zoba hivi, so bi mkubwa wala hana hofu nae ya kunitonya mie.

Siku ya siku nikajipanga na kijana wa kova, coz yule anaetoka na furushi kwangu namshuku ni mwizi, ile ametoka kwa gate, nilimwambia kijana afunge fasta ili bi mkubwa asijue nini kimetokea nje, ilikuwa mida ya saa nne usiku. Kabaaang, kanaswa binti, polisi fasta chini ya ulinzi, mie huyo nikaingia ndani kama sijui kunani.

Muda si mrefu akapigiwa simu aende kituoni, huko binti keshanaswa vitasa vya haja kasema kila kitu, aliogopa kuniomba nimsindikize, so akaenda na kaka, ile kafika na yeye chini ya ulinzi, walilala selo jana.

Asubuhi nikapitia, pale wakawa weshamumbia mie ndo niliwapa taarifa ya mchezo mzima, nikaomba waendelee kukaa pale, mchana kakayake akaenda kumtoa.

Ndugu zangu huyu mwanamke kalivuruga, kwa maelezo ya mdogo wake wameiba vitu vingi sana, hasa vya watoto, coz ana mdogo wake ana mtoto analingana na wa kwetu wa 1.

Kubwa nafikiria ni watoto wetu, najua wanaraha hata wakiwa na mimi, ila mama yao ni muhimu katika makuzi.

Hebu nipeni ushauri kidogo kabla sijaamua wa kwangu.

Hii kesi niipeleke mahakamani?
Kweli ni mdokozi, tena anakwiba vyakula vya wanawe, nitengane nae?
Anakazi yake nzuri, nikamshtaki kwa bosi wake?

Ongezeeni yatakayo nitoa hapa nilipo.

Karibuni
 
dah, nashawishika kukuuliza huyo mkeo ni mtu wa wapi? asijekuwa wa mgombani! hii ishu ngumu asee, sawa ni vitu vidogo lakini si jambo jema hata kidogo, ni mkeo, ana mshahara, hachangii chochote nyumbani, anaiba vitu vya nyumbani kussuport ndugu zake, wewe si utanyonyoka kama kuchi nduguyangu!! kadri wanavyokuwa ndiyo mahitaji yaoyanaongezeka, huyo mwanamke pesa yake chungu ya kwako tamu kwa sababu wewe ni atm, kunamapenzi kweli hapo? nahofia kusema mengi,lakini kwenye mahusiano kuna mitihani mikubwa sana!
 
Poleni sana mkuu!kumshitaki kwa boss haina maana kwa sababu haya ni mambo ya nyumbani,mna muda gani katika ndoa?me kuna vitu hapa naona kama na wewe umevijenga mwenyewe mpaka vikakufanya mmefika hapa,kwanza kumuzoesha kutochangia hela yake kwa chochote kwa huduma za nyumbani,umemlemaza,deal naye kwanza yeye kama yeye,kumpeleka police itakua imeshamchangamsha,kaa naye achangie na yeye gharama ndani ya nyumba nusu nusu,si wanwake wa sasa wanataka usawa,sina maana mbaya wewe umejitahidi sana kama baba,weka misingi sasa kwanza humo ndani ya nyumba yako na sheria,nadhani utaona mambo yataenda kwa mstari
 
Kwanza unaonekana unafatilia sana mambo ya jikoni!Una moyo mgumu sana duu Mimi nisingeweza kumuweka ndani shemeji Yangu tena sababu ya chakulaaaa ....hapo tatizo ni njaaa .mmh we kweli jasusi!
Ni wazi unatatizo kubwa na mkeo.

Unacho takiwa kufanya ni kukaa na mkeo chini na kumueleza ukweli kuwa na yeye aanze kuchangia na swala la kuwasaidia ndugu zake mnaweza kukaa chini na kuangalia jinsi ya kuwasaidia bila kuingia kwenye mikwaruzano.

Kama ndugu zake hawana kazi basi jitahidi muwatafutie kibarua na ni vyema mka kaa na mkeo mkajua jinsi ya kufanya!

Halafu ni wazi hili swala umeligeuza kama uadui ndio maana mkeo anafanya hivyo bila kukushirikisha!

Hebu jaribu kukaa na mkeo muongee kuhusu hili swala na uchukulie kama huo ni mzigo wako pia!
 
Mkuu jaribu kuwa na moyo wq kutoa, yote hayo ni kuifanya dunia sehemu nzuri ya kuishi...

Hao shemeji zako wana hali mbaya, kama wangekua wanajitosheleza kamwe usingewaona kwako, zaidi sana wangekuja kusalimia tu...

Usiwe na roho ya chuki, it's a world where we know nothing even the next second, hujui kesho yatakukuta nini, they so say "kufa kufaana"...

Watoe lock up hao wapendwa, sambaza upendo mkuu...
 
dah, nashawishika kukuuliza huyo mkeo ni mtu wa wapi? asijekuwa wa mgombani! hii ishu ngumu asee, sawa ni vitu vidogo lakini si jambo jema hata kidogo, ni mkeo, ana mshahara, hachangii chochote nyumbani, anaiba vitu vya nyumbani kussuport ndugu zake, wewe si utanyonyoka kama kuchi nduguyangu!! kadri wanavyokuwa ndiyo mahitaji yaoyanaongezeka, huyo mwanamke pesa yake chungu ya kwako tamu kwa sababu wewe ni atm, kunamapenzi kweli hapo? nahofia kusema mengi,lakini kwenye mahusiano kuna mitihani mikubwa sana!

mule mule kaka,,,, maranguuu....kaka mtihani mkubwa sana....sema tuu kaka,,, naweza pona...
 
Itategemea, kama atashuka chini na ku regret alichofanya akatubu makosa yake msameehe.... Mlee watoto wenu ila kama analeta ununda fukuza huko ataambukiza udokozi wanao
 
Ruttashobolwa

Mkuu,,, wadogo zake nimewasomesha mie kwa fedha zangu mwenyewe,,,, kuanzia form 1 mpaka 6, mwingine mpaka chuo,,,, hivi ni msaada gani tena mie natakiwa kuwapa, sio kufuatilia mambo ya jikoni, ni wajibu wangu kujua everything around my corner meku....nimemkanya sio once or twice,,, kigezo sina ushahidi......
 
Last edited by a moderator:
Poleni sana mkuu!kumshitaki kwa boss haina maana kwa sababu haya ni mambo ya nyumbani,mna muda gani katika ndoa?me kuna vitu hapa naona kama na wewe umevijenga mwenyewe mpaka vikakufanya mmefika hapa,kwanza kumuzoesha kutochangia hela yake kwa chochote kwa huduma za nyumbani,umemlemaza,deal naye kwanza yeye kama yeye,kumpeleka police itakua imeshamchangamsha,kaa naye achangie na yeye gharama ndani ya nyumba nusu nusu,si wanwake wa sasa wanataka usawa,sina maana mbaya wewe umejitahidi sana kama baba,weka misingi sasa kwanza humo ndani ya nyumba yako na sheria,nadhani utaona mambo yataenda kwa mstari

we got 10yrs bro,,, nimefanya mengi sana kwa upande wao, mpaka nilitengwa kwetu....nilipogutuka ndo nikaanza kuyanyoosha mpaka yakapinda tena......
 
mule mule kaka,,,, maranguuu....kaka mtihani mkubwa sana....sema tuu kaka,,, naweza pona...

pole sana kaka, tena pole hasaa! yanayokufika wewe ni madogo sana, kuna ndugu yangu mmoja yalimfika mazito, MAZITO!
 
Back
Top Bottom